Pages

KAPIPI TV

Wednesday, October 21, 2015

CHAGULIWA KUSHIRIKI KATIKA SHINDANO LA BONGO STYLE COMPETITION

Kipande cha Video ya mahojiano
 Majaji kwa Upande wa wabunifu wa Mitindo-Mavazi na Upigaji wa Picha wakiwa wanaendelea na kazi za uhakiki wa Majina ya kuwapata washiriki 20 ambao wataingia katika Shindano hilo.
Mbunifu na Mwanamitindo wa Mavazi ambaye pia ni Balozi wa Fasdo Martin kadinda akiongea kwa niaba ya Majaji upande Majaji wa Mitindo akielezea jinsi mchakato ulivyo kwenda.
 Majaji upande Ubunifu wa Mavazi wakiwa wanaendelea na kazi 
 Jaji katika upande wa kupiga Picha Sameer Kermalli akizungumzia mchakato mzima walioufanya kuwapata washiriki ambao wataingia katika shindano kwa upande wa upigaji picha
Majaji upande wa kupiga picha wakiendelea na Mchakato wa kuwapata washiriki 10 ambao wataingia katika ushiriki wa kumpata mshindi wa upande wa kupiga picha.
Mratibu wa FASDO Tanzania Joyce Msigwa akizungumzia mchakato mzima wa shindano la Bongo style Competition 
Kulia ni Philipo Florian kutoka kitengo ya Mitandao ya Kijamii Fasdo akiendelea na Kazi.

Kuelekea Shindano la Bongo Style  Competition , Ambalo linatarajiwa kufanyika Mwishoni mwa mwezi wa Kumi na moja mwaka huu, Majaji wamefanikiwa kuwapata washiriki ambao wataingia katika Kinyang'anyiro hicho

Akizungumzia Shindano hilo Mratibu wa FASDO Tanzania Joyce Msigwa alisema shindano hilo linalengo la kuibua vipaji vya vijana wenye kati ya umri wa miaka 18-25 katika nyanja za ubunifu mitindo na upigaji picha ili kuwahamasisha kutumia vipaji vyao kujiajili wenyewe. Aliongeza kuwa idadi ya Fomu zilizotumwa kwa njia ya mtandao zilikuwa 310 kati ya hizo zilizo pitiwa na Majaji pande zote ili kupata washiriki 20 zilikuwa fomu 285.

Aliwataja waliopita kushiriki katika upande wa picha ni pamoja na hao kwa upande wa  ni pamoja na Daniel Msirikale, Anneth Mgowano, Travis Gaudence, Victor Mpalile,Ebenezer Mmasi, Hassan Mohammed Ally, Rasheed Hamis, Erick Mwan'gonda, Nicetas Mtey na Nicetas Mtey

kwa upande wa Ubunifu wa mavazi na mitindo aliwataja washiriki hao ni pamoja na Anna Ben Paul,Eva Mary Sospeter,  Jocktan mwakeke
Lilian Ndanshau, Cecilia lyakulwa,Milly's Fenary Collection,Mamaland,Shahbaaz Sayed Yusuf,Salome Sebastian, na  Andrew Kalema

Nae Jaji wa Eneo la Mitindo Ambaye pia ni Balozi wa FASDO Martin Kadinda alizungumzia shindano hilo kuwa ni zuri na lipo kwa ajili ya kuibua vipaji vipya vya wanamitindo na kuongeza pia wale wote walioshiriki katika Shindano hili hasa walioleta fomu zao walikuwa wanauwezo lakini kwa kuwa ni shindano wachache ndio walikuwa wanatakiwa kulingana na vigezo na Masharti walivyoweka.

Akiongezea Jaji upande wa Picha Sameer Kermalli kwa niaba ya majaji wengine  amesema kuwa wamepokea na kupitia picha za washiriki wengi walioleta picha wamepitia na kugundua baadhi yao wamepiga picha nzuri ambazo zipo kitaalam na wengine wamepiga picha ka kuzi 'edit' sana jambo ambalo limesababisha kupunguza alama zao na pia wengine wametumia picha ambazo sio zao, pia aliongeza kwa kusema baadhi yao ambao wamechukuliwa pia wamefanya vizuri kutokana na ubunifu wao. 

Philipo Florian ambao wapo katika mitandao ya kijamii na waliokuwa wakipokea fomu hizo alisema kuwa fomu fomu nyingi zilikuja kwa kurudiwa rudiwa kitu ambacho kilichanganya kidogo mchanganuo, pia watu wengi  walipaa shida wakati wa kuweka Picha lakini hata hivyo wengi walifanikiwa na kushiriki kikamilifu. Pia Anna Semiono aliongeza kuwa zoezi lilienda kikamilifu na idadi ya wanawake na wanaume ambao walileta fomu zilikuwa sahihi ingawa baadhi yao walikosea kwa namna moja au nyengine kutokana na kuto elewa vizuri ni namna gani wangeweza wasilisha kazi zao, hata hivyo alisema changamoto hiyo haitakuwepo katika shindano lijalo kwa kuwa kutakuwa kuna elimu mbadala kupitia VIDEO CLIP itakayo onesha namna ya kutuma kazi zao.


UN, SMZ KUSHIRIKIANA KUKOMESHA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA

IMG_9939
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda wakati wa ziara fupi ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa visiwani humo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja huo tangu kuanzishwa.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amesema Umoja huo utaendelea kushirikiana na Serikali ya mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika kukomesha vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.
Akizungumza katika ziara ya kutembelea Dawati la jinsia la Wanawake na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda alisema umoja huo umelenga kusaidia uwepo wa utawala wa sheria na wenye kujali haki na utu wa binadamu kupitia mpango mkakati wake uliomo katika malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kuanzia mwaka 2016 utakosaidia kuondoa vitendo hivyo.
Alieleza kuwa tatizo la udhalilishaji wa kijinsia sio kwa Zanzibar pekee bali ni la kidunia, hivyo umoja wa mataifa(UN) unawajibu kusaidia juhudi za serikali kupambana na tatizo hilo.
“Tushirikiane kwa kila hatua ili kuondosha vitendo hivi kwani ni tatizo na kero kwa jamii ya Zanzibar pia ni miongoni mwa ishara tosha zinazoashiria uvunjifu wa haki za binadamu.”, alisema Rodriguez na kusisitiza kuwa ili kukomesha vitendo hivyo ni kuwepo na utawala wa kisheria utakaotenda haki kwa wale wanaoozalilishwa utu wao.
IMG_9951
Aidha Bw. Rodriguez aliyataka madawati ya jinsia kutumia vyombo vya habari kuwaelimisha wananchi kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ili kuhakikisha vinapungua ama kuisha kabisa kwa lengo la kujenga jamii yenye uadilifu.
Naye Mtendaji wa Dawati hilo, kutoka Jeshi la Polisi Koplo, Fatma Juma alifafanua kuwa kesi za ubakaji kwa wanawake na watoto zimepungua ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Alisema kwa sasa kuna changamoto ya utoroshwaji na utelekezaji wa watoto kesi ambazo kwa sasa ni nyingi lakini wanaendelea kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ili kuhakikisha zinapungua.
Akizitaja changamoto zilizopo katika dawati hilo kuwa ni pamoja na kukosekana kwa ushahidi wa kina kwa baadhi ya kesi hivyo kupelekea kuharibu mwenendo mzima wa kesi kutokana na kukosekana uthibitisho.
IMG_9928
Mtendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda, kutoka Jeshi la Polisi Koplo, Fatma Juma akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya kituo hicho tangu kufunguliwa ikiwa ni mwaka mmoja sasa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) ikiwa ni awamu yake ya pili kutembelea Dawati hilo. Kulia ni Mtaalamu wa masuala ya ulinzi kwa watoto wa UNICEF Zanzibar, Bw. Ahmed Ali.
Alifahamisha kuwa changamoto nyingine ni jamii ya wazanzibar kuwa na tabia ya mukhari (kuoneana haya) hivyo kumaliza kesi kwa njia ya kifamilia bila ya kufuata utaratibu wa kisheria, hali inayokuwa kikwazo cha kuwafikisha katika vyombo vya kisheria wahalifu wa kesi za ubakaji.
“Bado nasisitiza ni lazima Wazanzibar tubadilike na kuondokana na masuala ya muhari kwani unawaumiza watoto wetu na tujenge utamaduni wa kujiamini kwa kutoa ushahidi ili tutokomeze janga hili.,” alisisitiza Fatma.
Pamoja na hayo alishukru msaada unaoendelea kutolewa na Umoja wa mataifa (UN) kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwawezesha katika mambo mbali mbali kwa lengo la kupunguza vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.
Mwakilishi huyo Mkazi katika ziara hiyo alitembelea miradi mbali mbali ya umoja huo ikiwa ni moja ya sherehe za kutimiza miaka 70 ya kuanzishwa kwa umoja huo.
IMG_9935
Baadhi ya waandishi wa habari wa visiwani Zanzibar na maofisa wa Umoja wa Mataifa waliombatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) katika ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa visiwani humo.
IMG_9969
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipitia kitabu cha orodha za kesi katika Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda. Kulia ni Mtendaji wa Dawati hilo, kutoka Jeshi la Polisi Koplo, Fatma Juma na kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya ulinzi kwa watoto wa UNICEF Zanzibar, Bw. Ahmed Ali.
IMG_9963
IMG_9983
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa ndani ya chumba cha dawati la Jinsia.
IMG_0009  
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiagana na Mkuu wa Upelelezi wa Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kombo Khamis Kombo (kulia) alipofanya ziara ya kutembelea Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa. Kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya ulinzi kwa watoto wa UNICEF Zanzibar, Bw. Ahmed Ali.
IMG_9904
Mradi huu ulifadhiliwa kwa pamoja kati ya Jumuiya ya Ulaya (EU) na Shirika linalohudumia watoto duniani, UNICEF.
IMG_0023
Muonekano wa jengo la Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Kaskazini Unguja.

SHINE WITH SHINA ANNUAL GALA 2015 YAFANA GREENBELT, MARYLAND

Meza kuu kutoka kushoto ni Bi. Jennifer Jones ambaye ni ni mkuu wa Kamisheni ya wanawake kaunti ya Prince George, Afisa Suleiman Saleh ambaye alimwakilisha Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi. Kulia ni Dr. El Senzengakulu Zulu ambaye ndio mwanzilishi na mmiliki wa shule ya Ujamaa inayofundisha tamaduni za bara la Afrika. PICHA NA KWANZA PRODUCTION/VIJIMAMBO BLOG.
Kutoka kushoto ni Dr. John Rutayuga ambaye ni mwanzilish wa Ukwimwi Orphans akiwa meza kuu na Mr and Mrs William.
Mshereheshaji Tuma akifungua pazia ya kuashiria SHINA Gala imefunguliwa rasmi siku ya Jumamosi Octoba 17, 2015 ndani ya Hotel ya Hilton iliyopo Greenbelt, Maryland na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali Watanzania na marafiki zao wakiwemo wawakilishi wa makampuni yanayoshirikiana na SHINA kwa ajili ya kusaidia misaada mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule nchini Tanzania. 
 Kikundi cha sanaa cha Taratibu Youth Association kikifungua pazia la burudani hku wakishangilia muda wote kwa umahiri wao wa kucheza ngoma za asili kutoka Tanzania. Kundi hili hupata mialiko mabara mbalimbali kujifunza na kufanya maonesho ya ngoma za asili ambazo hua kivutia kwa watazamaji.
 Wapiga ngoma wa Taratibu Youth Association.
Mwanzilishi na mmiliki wa SHINA kwa heshima na taadhima akiwashukuru watu waliofika kwenye SHINA Gala Dinner na kusaidia kuchangisha pesa za kusaidia misaada mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule nchini Tanzania.
 Afisa Suleiman Saleh akimwakilisha Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi ambaye ndiye aliyekua awe mgeni rasmi kwenye SHINA Gala iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 17, 2015 katika hoteli ya Hilton, Greenbelt, Maryland nchini Marekani.
Afisa wa Ubalozi Bwn. Suleiman Saleh akimzawadia Bi. Jessica Mushala zawadi kutoka Zanzibar ambayo baadae ilifanyiwa mnada ili fadha zisaidie kumalizia ujenzi wa shule nchini Tanzania.
Bi. Jennifer Jones Kamisheni ya wanawake kaunti ya Prince George's ambaye ndiye aliyekua msemaji mkuu huku akishangiliwa muda wote kwa ujumbe mzito aliokua akiutoa mara kwa mara kwenye hotuba yake.
Bi. Jessica Mushala akimzawadia Bi. Jennifer Jones zawadi maalum.
Bwn. Amos Mushala akimzawadia Dr. John Rutayuga zawadi maalum kutambua mchango wake katika kuendelea kupambana ikiwemo kuwasaidia waathirika wa Ukimwi nchini Tanzania.
Dr. John Rutayuga akitoa shukurani zake kwa SHINA.
Mwimbaji wa nyimbo za injili DMV Bi. Rose Kachuchuru akiimba moja ya nyimbo zake.

Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Colonel Adroph Mutta katika picha na mkewe walipohudhuria SHINA Gala Dinner hiyo. 
Kwa picha zaidi bofya HAPA

Tuesday, October 20, 2015

WARIDHISHWA NA HUDUMA ZA KITUO CHA AFYA KIVUNGE, UNGUJA

IMG_20151016_175545
Pichani juu na chini ni muonekano wa Jengo la kituo cha afya Kivunge Wilaya ya Kaskazini "A" visiwani Unguja kilichojengwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi wetu
BAADHI ya Wananchi wa Kijiji cha Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” wameelezea kuridhishwa kwao na huduma za afya zinazotolewa katika kituo kipya cha afya cha Kivunge.
Kituo hicho kimejengwa chini ya mradi wa Umoja wa Mataifa(UN) wa kuviwezesha vituo vya afya mbali mbali nchi ambapo kituo hicho kinatoa huduma mbali mbali za akina mama na watoto pamoja na masuala ya kutibu vidonda na majeraha mbali mbali.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkazi wa kijiji hicho, Kassim Haji Simai alisema kituo hicho kimekuwa mkombozi wa wananchi kwani pindi panapotokea mgonjwa wa ghafla ufika katika kituo hicho na kupewa matibabu ya haraka.
Alizitaja changamoto kubwa iliyopo kituoni hapo kuwa ni pamoja na upungufu wa madakta na wauguzi jambo ambalo baadhi ya wananchi ukaa muda mrefu wakisubiri huduma kwani wagonjwa wanakuwa wengi kuliko watoa huduma.
IMG_9525
“Tunawashukru sana wafadhili waliojenga kituo hiki na serikali kwa ujumla kwani wametusaidia sana huduma hizi tulikuwa tunazifuata mbali sana”, alisema Haji.
Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alifika katika kituo hicho na kutembelea maeneo mbali mbali ya kituo hicho na kuona ni jinsi gani kinatoa huduma kwa wananchi.
Alisema kuwa ufanisi wa mradi huo unaongeza ushawishi kwa Umoja wa Mataifa kuongeza zaidi msaada hasa vifaa vya kisasa vya huduma za afya pamoja na wataalamu wa afya ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma za afya kwa ufanisi zaidi.
“ Kituo hiki kinatoa huduma kwa wananchi wengi hivyo nitapeleka salamu makao makuu ili tujadiliane na kuona ni jinsi gani tunaendelea kusaidia kituo hiki hasa katika suala la vifaa vya kisasa na madaktari.”, alifafanua Bw.Rodriguez.
IMG_9533
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitazama jengo la kituo cha afya Kivunge alipofanya ziara fupi ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa visiwani Unguja ikiwa ni sehemu ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuaznishwa. Kulia ni Daktari wa kujitolea wa kituo cha afya Kivunge, Alexander Vogt.
Naye Mratibu wa Mradi wa Health Improvement Project (HIP), Jabir James alisema kituo hicho kinatoa huduma bora na zenye kukidhi mahitaji kwa wananchi ambapo kwa siku wanapokea zaidi ya wagonjwa 100 hadi 200 hali ambayo kitathimini ni kubwa kutokana na uwezo wa kituo hicho kimatibabu.
Alisema kuwa bado wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa kuongeza vifaa na madaktari ili kuhakikisha wanaongeza ufanisi katika utoaji wa huduma bora ili kufikia dhana ya umoja wa mataifa katika masuala ya afya ya kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uhakika wa kupata huduma bora za afya na endelevu.
IMG_9557
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akikagua maeneo mbalimbali ya kituo hicho huku akiwa ameambatana na Mkuu wa ofisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar, Anna Senga (nyuma ya Alvaro) pamoja na Mtaalamu wa Mawasiliano na Mahusiano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu. Kulia ni Daktari wa kujitolea anayehudumia wangonjwa katika kituo hicho Alexander Vogt.
IMG_9564
Daktari wa kujitolea wa kituo cha afya Kivunge, Alexander Vogt akimwonyesha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez baadhi ya ripoti za magonjwa yanayowasumbua watoto chini ya umri wa miaka 5 wanaopatiwa matibabu katika kituo hicho.
IMG_9574
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akizungumza na Dr. Mohamed Abdallah (kulia) aliyekuwa akitoa huduma kwa mtoto Salma Shamis mwenye siku 10 ambaye anasumbuliwa na masikio wakati Bw. Rodriguez alipofanya ziara fupi ya kukagua kituo cha afya Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” visiwani Unguja kilichojengwa na Umoja wa Mataifa ikiwa ni sehemu ya sherehe za miaka 70 ya Umoja huo tangu kuanzishwa.
IMG_9591
Pichani juu na chini ni baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” wakiwa kwenye foleni ya kuingia kwenye vyumba vya madaktari kama walivyokutwa na kamera yetu.
IMG_20151016_175753 IMG_9612
Mratibu wa Mradi wa Health Improvement Project (HIP), Jabir James akizungumza na waandishi wa habari waliombatana kwenye ziara hiyo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
IMG_9621
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa amembeba mtoto Shekha Khamis (3) mkazi wa Kijiji cha Kivunge Wilaya ya Kaskazini “A” aliyefika kituoni hapo kupatiwa matibabu.

KIPINDI CHA JUKWAA LANGU OKTOBA 19/ 2015

Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Ni kipindi cha mwisho kabla ya uchaguzi, na washiriki wengi walishiriki kutoa mchango wao kuhusu mchakato ulivyokuwa, na neno ama wosia wao kwa waTanzania wote
KARIBU

Saturday, October 10, 2015

BENKI KUU YA TANZANIA YAANZISHA MFUMO MPYA WA MALIPO KWA MASAA 24 UTAJULIKANA KAMA TISS.

 Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bernard Dadi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu benki hiyo kuanza kutumia mfumo wa malipo baina ya benki na benki kwa masaa 24 kwa siku saba za wiki kwa mwaka utakajulikana kama TISS. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki, Marcian Kobello.
 Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki, Marcian Kobello (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea. Walioipa kamera mgongo kutoka kushoto ni Meneja Msaidizi wa Idara ya  Uhusiano wa benki hiyo, Vicky Msima na kulia ni Kaimu Meneja Huduma za Kibenki, John Kayombo.

Na Dotto Mwaibale

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imesema kuanzia mwakawa fedha ujao itaanza kutumia mfumo wa malipo baina ya benki na benki kwa masaa 24 kwa siku saba za wiki kwa mwaka ambapo utakuwa ukijulikana kama TISS.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo  mchana na Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo BoT, Bernard Dadi na kuongeza mfumo huo utaweza kufanya kazi kwa ufanisi iwapo wafanyabiasha na wananchi kwa ujumla watauchangamkia kwani kwa sasa inapatikana kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa mbili usiku kwa benki za kibiashara zilizojiunga.

"Kwa sasa kuna mfumo huu wa TISS ambao umekuwa ukifanya kazi siku za kazi hadi saa mbili usiku na siku za mapumziko na sikukuu unafanya kazi kuanzia saa tatu hadi saa nane, ila tunatarajia mwaka wa fedha ujao utakuwa unafanya kazi kwa masaa 24," alisema.

Alisema kimsingi mfumo huo una lengo la kuondoa mfumo wa kutumia hundi ambao unatumia muda mrefu na wakati mwingine kuna makosa ambayo yanatokea ya mtu anavyoandaa hivyo kuchelewa.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki wa BoT, Marcian Kobello alisema uhaba wa sarafu ya shilingi 500 mitaani unachangiwa na wananchi wenyewe ambao wakienda benki hawachukui fedha hizo hivyo kusababisha zibakie huko kwenye mabenki.

Alisema sarafu za shilingi 500 zipo zaidi ya milioni 100 BoT lakini hadi sasa ni milioni 20 ndizo zipo katika mzunguko hali ambayo inachangia kuadimika kwa fedha hizo.

Alitoa mwito kwa wananchi na wafanyabiashara kuchukua sarafu hizo katika mabenki ili ziweze kufika katika mizunguko na dhana kuwa sarafu hiyo ina madini ya fedha ni uongo kwani asilimia 94 ni chuma na asilimia 6 ni nikoni.

Aliwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kupeleka fedha ambazo zimechakaa katika mabenki ili waweze kubadilishiwa kwani utaratibu wa kuuza fedha haupo kisheria pamoja na ukweli kuwa hakuna sheria inayokataza.


OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU (NBS) YASEMA PATO LA TAIFA LIMEONGEZA KWA ASILIMIA 7.9

 Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa za pato la taifa robo ya pili ya mwaka kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2015. Kushoto ni Meneja Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa.
 Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
 Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Wapiga picha wakichukua picha katika mkutano huo.


Na Dotto Mwaibale

OFISI ya Taifa ya Takwimu imesema pato la taifa limeongezeka kwa asilimia 7.9 huku sekta ya madini na uzalishaji umeme ikifanya kuongezeka kwa pato katika kipindi cha robo mwaka 2015 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2014.

Akizungumza  Dar es Salaam leo asubuhi wakati wakati akitoa taarifa za pato la taifa robo ya pili ya mwaka kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2015, Mkerugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Morrice Oyuke alisema ongezeko hilo la takwimu ni la miezi mitatu ya mwaka huu.

Oyuke alisema ongezeko hilo la pato la taifa linaenda sanjari na matokeo ya thamani ya pato la taifa kwa mwaka huu ambalo lilikuwa ni trilioni 89.0 ambapo  katika robo ya mwaka ni trilioni 45.5 ikilinganishwa na trilioni 39.0 katika mwaka 2014.

Alisema thamani ya pato la taifa ya robo mwaka ya trilioni 45.5 ni kubwa hivyo kusababisha  pato la taifa la mwaka mzima linaweza kukuwa kama uchumi hautotetereka.

"Kama uchumi hautaweza kuguswaguswa na matatizo mingene inaweza ikasababisha pato la taifa la mwaka huu likaongezeka badala ya ile iliyotegemewa hapo mwanzo,"alisema.

Alisema ongezeko hilo la pato la taifa limechangiwa na sekta mbalimbali kufanya vizuri katika kipindi cha robo mwaka.

Alisema sekta ambazo zimeongoza katika kipindi cha robo mwaka ni sekta ya madini,umeme,kilimo na mifugo,viwanda na ujenzi na huduma za kitaalamu.

Alisema sekta ya uzalishaji umemere imekuwa kwa asilimia 18.5 huku bidhaa za viwandani ni asilimia 6.9 madini mawe na kokoto  zimeongezeka asimilia 8.3 limeongezeka kutokana na shghuli za kiuchumi.

"Kutokana na taarifa hii ya pato la taifa kwa robo mwaka taarifa hizi zitumike katika kupanga na kurekebisha sera mbalimbali za maendeleo ya nchi," alisema.