Pages

KAPIPI TV

Sunday, October 4, 2015

IT BRIDGE YAWAFIKIA WANAFUNZI 60,000

IMG_3000
Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Na mwandishi wetu
JUMLA ya wanafunzi 60,000 katika shule 150 nchini wamepitiwa na mafunzo ya programu ya Bridge IT yenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kidijiti (digital technology) katika ufundishaji na ujifunzaji wa Hisabati,Sayansi na Stadi za Maisha.
Hayo yamsemwa na Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama.
Alisema kutokana na mafanikio yaliyotokea sasa wanatanua wigo baada ya kuwezeshwa kifedha na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya elimu (Global Partnership For Education) kwa ajili ya kuendeleza teknolojia hiyo katika kujifunza na kufundisha katika shule za msingi na hasa darasa la awali la kwanza hadi la nne.
Aidha maonesho hayo yanayofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere yana lengo la kuonesha ubunifu ambao upo tayari kutumika kufanikisha mafunzo hayo.
Pia maonesho hayo yanatarajia kujadili na kuangalia mbinu za kielektroniki zitakazoweza kuendana na mazingira ya Tanzania katika ufundishaji na kujifunza kwa gharama nafuu.
Pia wanatarajia kuangalia utayari wa walimu na namna ya kuwabadilisha mtazamo ili waweze kufundisha na kufundishika.
“Lengo la serikali kupitia Wizara ya Elimu ni kupanua wigo wa elimu hasa elimu ya awali kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo itabadilisha ufundishaji kutoka kutumia vitabu vilivyopo katika mfumo wa ‘hard copy’ na kuwa katika mfumo wa sauti na picha au ‘soft copy’,” alisema Profesa Bhalalusesa.
IMG_3089
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifuatilia kwa makini risala Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa (hayupo pichani).
Alisema hadi kufikia wakati huu serikali imeshapiga hatua kubwa katika matumizi ya Tehama ambayo katika majaribio yake yameonesha kufanikiwa na wadau mbalimbali wa elimu wameyapongeza na kuyaunga mkono.
Profesa Bhalalusesa alisema kwa sasa wagunduzi mbalimbali wa mifumo ya Kompyuta inayoweza kutumika kufundishia ndio watakoonesha kazi zao na kutoa ufafanuzi wa kina kwa majaji wataochagua kazi chache na kuzifanyia majaribio kabla ya kuanza kutumika kufundishia.
Kwa Upande wake Mratibu wa Mpango wa Kukuza stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kutoka Wizara ya Elimu, Agripina Habichi alisema mpango huo wa matumizi ya Tehama utasaidia wanafunzi kufahamu kusoma na kuandika kabla ya kuendelea na masomo ya darasa la tatu.
“Maonesho haya yanafanyika katika wakati muafaka ukizingatia tunataka kupiga hatua kubwa katika kuboresha elimu yetu. Washiriki wa maonesho haya wamekuja kutuonesha utawaalamu wao unaoweza kutumika kufundishia.
Lengo letu ni kuwafikia wanafunzi wengi zaidi ambapo tumeazimia kuzifikia shule zaidi ya 2000 katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 na hivyo tutakuwa katika kiwango bora zaidi cha utoaji wa elimu inayojitosheleza,” alisema Habichi.
IMG_3142
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akizungumza kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katika maonesho hayo serikali imesema inatarajia kuanza kutumia rasmi Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika kufundishia wanafunzi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya elimu ambayo ni chekechea.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alisema matumizi ya Tehama katika ufundishaji wa wanafunzi wa chekechea yataimarisha kiwango cha elimu.
“Dunia imebadilika sana hasa katika sekta ya elimu na mawasiliano, hatuna budi kuendana nayo kwa kasi ileile ya ukuaji wake kwa kuimarisha mifumo yetu ya ufundishaji,” alisema Profesa Mchome.
Alisema wizara yake imeanzisha mpango maalum utakaosaidia wanafunzi kujifunza kwa njia ya kisasa ya kutumia mbinu za kielektroniki katika kujifunza na hivyo kuimarisha uelewa na kuongeza hamasa ya ufundishaji kwa wanafunzi.
Profesa Mchome alisema maonesho hayo yana lengo la kupata wadau mbalimbali waliobuni programu zinazoweza kutumika katika kufundishia kwa kutumia mifumo ya kielektroniki na hivyo watachaguliwa wachache wenye sifa na watakowezesha mafunzo hayo katika shule za Msingi na baadae katika ngazi ya sekondari.
IMG_3160
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akijianda kuzindua rasmi maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
IMG_3161
Sasa yamezinduliwa rasmi.
IMG_3214
Ofisa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika lake katika kuendeleza sekta ya elimu nchini kwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome (kushoto) mara baada ya kuzindua maonesho hayo ambapo pia UNESCO inashiriki. Katikati ni Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa.
IMG_3217
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (katikati) akimsikiliza mmoja wa wadau wa elimu aliyetembelea banda la UNESCO kwenye maonesho ya TEHAMA yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Miradi ya Elimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo.
IMG_2982
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (kulia) akiwa na wadau wengine wa elimu wakipitia makbrasha mbalimbali katika mkutano huo.
IMG_3006
Pichani juu na chini ni baadhi wadau wa elimu waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho hayo.
IMG_3004
IMG_3028
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi jijini Dar walioshiriki hafla hiyo.
IMG_3105
Mkurugenzi Mkuu wa Shule Direct, Faraja Nyalandu akipozi na wadau kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam yanakoendelea maonesho ya TEHAMA.

MAENDELEO ENDELEVU 17 YA DUNIA YAZINDULIWA TANZANIA

IMG_3349
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins-Falk (katikati) wakipata picha ya kumbukumbu sambamba na mmoja wa wadau wa maendeleo. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Mwandishi wetu
UMOJA wa Mataifa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wamezindua rasmi malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).

Malengo hayo ambayo pia yanajulikana kama malengo ya dunia yamezinduliwa jana Septemba 29 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Uzinduzi huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy, na Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame kwa niaba ya serikali, Bi. Fionnuala Gilsenan, Balozi wa Ireland na Bi. Liz Lloyd, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa niaba ya wadau wa mradi wa Project Everyone Partners.

SDGs ni wito wa dunia wa kuchukuliwa kwa hatua za kuufuta umaskini, kuihami dunia dhidi ya uharibifu wa mazingira na kuhakikisha kwamba kila mwanadamu anaishi maisha stahiki katika amani na ustawi.

Katika malengo hayo 17 yapo makusudio 169 yanayotoa ramani ya utengenezaji wa sera za maendeleo na namna ya kutekeleza kwa miaka 15 ijayo.

Malengo hayo yakijengwa juu ya mafanikio ya malengo ya milenia (MDGs), yameingiza vitu vipya kama mapambano dhidi ya tofauti za kiuchumi, ubunifu, mabadiliko ya tabia nchi, lishe, amani na haki. SDGs ni mpango wa dunia unaojikita kwa ustawi wa wanancni na dunia.
IMG_3303
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (kushoto) na Kiongozi wa mabalozi wa nchi za nje hapa nchini Mheshimiwa Juma Mpango, ambaye ni balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiwa wameshikilia lengo namba 16 na 17 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ambayo yamezinduliwa rasmi nchini Tanzania jana 29, Septemba 2015.

Akizungumza umuhimu wa malengo hayo, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez amesema: “Kwa mara ya kwanza katika historia ya dunia , serikali zimekutana na kukubaliana kupeana malengo kwa ajili ya kila mtu. 

Malengo haya yatasaidia mataifa yote kushirikiana katika kuwezesha ustawi, kupunguza matumizi na kuilinda dunia dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.Katika hilo watashughulikia elementi zinazohusu maendeleo endelevu: ukuaji wa uchumi, ustawi wa jamii na kulinda mazingira.”

Akizungumzia malengo hayo Bw. Paul Kessy amesema kwamba serikali ya Tanzania ipo tayari kwa malengo hayo.

Alisema kwamba Rais Jakaya Kikwete alikuwa New York, Marekani kwa ajili ya kutia saini malengo hayo na hilo linaonesha ni kiasi gani serikali ya Tanzania iko tayari kushirikiana na wadau wengine kuufuta umaskini.

Pia alisema:“Wakati huu, masuala ya uimarishaji wa muundo wa utekelezaji na kuamsha upya ushirikiano wa kidunia katika maendeleo ni msingi mzuri”
Naye Kamishina wa mipango wa Zanzibar, Bw Ahmed Makame : “Nikiangalia malengo haya 17 ya SDGs, ninafuraha kuona kwamba Zanzibar imekuwa sehemu ya mchakato huu...”.
IMG_3392
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd akipozi kwa picha na lengo na tisa kabla ya uzinduzi rasmi wa Malengo ya Dunia kwa Maendeleo Endelevu.
Aidha alisema kwamba Tanzania imeanza vyema katika utekelezaji wa malengo hayo.
Alisema kwa kuangalia uzoefu uliopatikana katika malengo ya milenia, inaonekana namna bora ya kuuoanisha malengo ya kitaifa na ya dunia.
Ninafurahi kusema kwamba Zanzibar tuko katika mchakato wa kutengeneza mkakati wa maendeleo wa kitaifa na tumepanga kufikia malengo ya SDGs.
Akisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha maendeleo, Bi.Fionnuala Gilsenan, amesema taifa lake Ireland lipo tayari kusaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.
“Malengo ya dunia yaliyojengwa katika Malengo ya Milenia yamelenga kukabiliana na matatizo ya zamani kwa mbinu mpya. Zimelenga kukabiliana na tatizo la umaskini na ukosefu wa usawa katika masuala ya uchumi. SDGs haiwezi kufanikiwa bila kuyaangalia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usawa wa jinsia, haki za biandamu na kukabiliana na mfumo inayobagua.”
Akizungumza kwa niaba ya wadau wa Project Everyone, Bi. Liz Lloyd alielezea umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na Umoja wa Mataifa na serikali ya Tanzania katika kusambaza ujumbe wa malengo ya dunia.
IMG_3397
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), nchini Tanzania, Dk.Rufaro Chatora akipozi la lengo namba 3.
“Kama benki huwa tunazungumza na umuhimu wa kuendelea kuwapo. Huu si tu msemo bali ahadi tunayoishi nayo kila siku. Malengo ya Dunia yanatoa nafasi adhimu ya ushirikiano na taasisi kubwa duniani, kutekeleza malengo 17 kwa nia ya kufufua ushirikiano wa dunia kwa maendeleo endelevu.
Standard Chartered inajisikia furaha ya kuwa nchini Tanzania kwa miaka mingi na inatumaini kwamba kwa ushirikiano huu kila mtu anayeishi nchini hapa atafaidika na maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.”
Malengo ya Maendeleo Endelevu yalizinduliwa Septemba 25 wakati viongozi wa dunia walipokutana pamoja mjini New York. Malengo haya yataanza kutumika Januari 1,2016.
IMG_3226
Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akipozi na lengo na 17.
IMG_3280
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa kabla ya uzinduzi rasmi wa malengo hayo nchini Tanzania.
IMG_3390
Mtaalam wa mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza (kushoto) sambamba na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama katika picha ya ukumbusho.
IMG_3789
Meza kuu katika halfa ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) nchini Tanzania, kutoka kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya uchumi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan, Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd.
IMG_3781
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3554
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd akielezea ushiriki wa benki yake katika utekelezaji wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3580
Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy akizungumza kwa niaba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3640
Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame akiwakilisha serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
IMG_3772
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha maendeleo.
IMG_3754
Baadhi ya wadau wa maendeleo kutoka mashirika na balozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
IMG_3796
Baadhi ya wageni waalikwa na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakifuatilia maoni na maswali yaliyokuwa yakiwasilishwa kwenye hafla hiyo.
IMG_3829
Mmoja wa wawakilishi wa vijana akiuliza swali meza kuu.
IMG_3868
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole akijibu moja ya swali lililoulizwa na kijana (hayupo pichani).
IMG_3857
Sehemu ya wadau wa Maendeleo, taasisi mbalimbali, asasi za kiraia, waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
IMG_3851
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem akifafanua jambo katika kipindi cha maswali na majibu.
IMG_3900
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kulia), Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame ( wa pili kulia), Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan (kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahaya (wa pili kushoto) kwa pamoja wakifunua pazia maaluma kuashiria uzinduzi rasmi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3912
Sasa yamezinduliwa rasmi.
IMG_3921
Shamra shamra za uzinduzi zikiendelea.
IMG_3950
Fataki zikisherehesha uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3975
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchangayiko na wadau mbalimbali wa maendeleo, waandishi wa habari wakiwa kwenye picha ya pamoja na vibao vya malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3997
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchangayiko walioshiriki kutengeneza tangazo maalum la kuelimisha jamii kuhusiana na malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_4021
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
IMG_4029
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Mwanahabari mkongwe Mama Eda Sanga walioshiriki kwenye uzinduzi huo.
IMG_4097
Bendera ya Umoja wa Mataifa, SDG's na bendera za nchi mbalimbali zikipepea kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
IMG_4078

Friday, September 25, 2015

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO NA REACH FOR CHANGE WAZINDUA SHINDANO LA WAJASIRIAMALI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa shindano la Wajasiriamali ambapo ametoa wito kwa watu kushiriki ili wajiweke katika nafasi ya kushinda fedha taslimu dola za kimarekani 20,000 ambazo kila mshindi atapewa azitumie katika utekelezaji wa mawazo yao ya kibunifu.
  Meneja wa nchi wa Reach for Change, Peter Nyanda, akizungumza katika mkutano huo.
 Muhasisi wa Mfuko wa APPS and Girls, Carolyne Ekyasisiima, akizungumza jinsi mfuko huo unavyofanyakazi ya kusaidia watoto katika masomo.
 Mwanzilishi wa Shule Direct, Iku Lazaro akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Ni furaha tupu kwenye uzinduzi huo.
 Meneja wa Mawasiliano wa Tigo, John Wanyanja akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Wadau wakiwa kwenye uzinduzi.
 Mkutano wa uzinduzi huo ukiendelea.
 Madada hawa wenye fulana za uzinduzi huo wakifuatilia matukio yote kwa karibu 'Wamependeza'
Hawa ni baadhi ya wanafunzi walionufaika na mradi huo.
Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Simu ya Tigo kwa kushirikiana na taasisi ya Reach for Change zimezindua shindano la wajasiriamali jamii liitwalo “Tigo Digital Change-makers”lenye lengo la kuibua mawazo ya kibunifu ambayo yatasaidia kutatua matatizo yanayo wakabili watotona vijana nchini.

Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez leo ametangaza uzinduzi wa shindano hilo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam ambapo ametoa wito kwa watu kushiriki ili wajiweke katika nafasi ya kushinda fedha taslimu dola za kimarekani 20,000 ambazo kila mshindi atapewa azitumie katika utekelezaji wa mawazo yao ya kibunifu.

“Tigo ikishrikianana Reach for change itatoa tuzo ya dola za kimarekani20,000 kwa kila mmoja kwa washindi wawili ambao wataku wa na mawazo ya bunifu zaidi kiteknolojia na kidijitali yaliyo na uwezo wa kuchangia kuleta maisha bora kwa watoto katika jamii ya kitanzania,” alisema Gutierrez.

Aliongezeakwamba, “Lengo letu ni kupata mawazo ya kibunifu ya kidijitali ambayo yataleta na kutatua matatizo ya nayo wakabili watoto kwa kiwango kikubwa huku tukiendelea kuwekeza katika kukuza na kuimarisha huduma zetu za mawasiliano katika maeneo yote nchini.”

Mawazo yatakayo wasilishwa kupitia shindano hili yanatakiwa kuonyesha uwezo wa kutumia simu kidijititekinolojia ya habari na mawasiliano kuleta ufanisi wa utekelezaji wa mradi husika.
Watakaopenda kushiriki shindano hili wanaweza kutuma maombi kupitia mtandao wa www.tigo.co.tz/digitalchangemakers, kwa  mujibu wa Gutierrez.

Kwa upande wake, Meneja wa nchi wa Reach for Change, Peter Nyanda, alisema licha ya kupatakitita cha dola 20,000 washindipia watapewa vifaa vya kuendeleza utekelezaji wa mawazo yao ikiwa ni pamoja na kupata ushauri kutoka kwa wafanyakazi waandamizi kutoka Tigo na Reach for Change.

Aidha wata unganishwa na wajasiriamali wengine ambao tayari wamenufaika kutokana na mpangohuo.

Mchakato huu wa kuwapata wajasiriamali jamii wakidigitali unaendana na mkakati waTigo wa kuendeleza maisha ya kidijitalinchini.

Huu ni mwaka wa nne mfululizo ambapo taasisizaTigo na Reach for Change zimekuwazikishirikiana kuwasaidia wajasiriamali nchini. Jumla ya wajasiriamali watano wa menufaika na mpango katika kipindi hiki ambao kwapamoja na kupitia utekelezaji wa miradi yao wamewasaidia jumla ya watoto zaidi ya 10,000 nchini.



VUGU VUGU LA AJENDA YA WATOTO NA UCHAGUZI MKUU LAENDELEA KIBAHA MKOANI PWANI.

Mtoto Loida Goodluck Kutoka shule ya Sekondari ya  Simbani akichangia mada katika Mdahalo huo
Mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mtoto Joyce Michael akizungumza jambo wakati wa Mdahalo  huo
Jastin Moses Mratibu wa mradi wa kuzuia ukatili dhidi ya mtoto kutoka Plan International akichangia mchango wake wakati wa mdahalo huo
 Ombeni Ally Mkuu wa Shule ya Sekondari Simbani akifafanua Jambo katika mdahalo  huo
Ramadhan Lutambi mgombea udiwani kata ya Kibaha maili Moja kupitia Chadema akisisitiza Jambo
 
Rosemary Mkonyi mgombea Ubunge kupitia tiketi ya ACT akizungumza Jambo wakati wa mdahalo huo
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wanasikiliza mdahalo huo
Wananchi wakiwa wanafuatilia kwa makini mdahalo huo

Na Mwandishi wetu 
Jamii imetakiwa kuwa karibu zaidi na watoto ili kuhakikisha wanalindwa dhidi ya ukatili na kuhakikisha wanapata haki zao stahiki. Rai hiyo imetolewa na wakazi wa Kibaha Mkoani Pwani katika Mdahalo wa Walinde Watoto uliowaleta pamoja wapiga kura, watoto na wagombea wa nafasi za Ubunge na Udiwani.
Kwa upande wake mgombea Ubunge wa Kibaha vijijini kupitia ACT Wazalendo Dk. Rose Mkonyi alisema kuwa chama chake kinaangalia ni kwa namna gani watazingatia katika Lishe bora ya mtoto pamoja na namna gani mtoto atainuliwa Kielimu. Aidha Mgombea Udiwani wa kata ya maili moja kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ Ramadhani Lutambi alisema chama chake kitaangalia zaidi afya ya mtoto na kuhakikisha Bohari ya dawa inakuwa na dawa za kutosha.
Hata hivyo, Watoto waliohudhuria mdahalo huo waliwataka wagombea kutimiza ahadi wanazotoa wakati wa Kampeni ili na wao waweze kufikia malengo yao. Watoto walipendekeza serikali ijayo iangalie namna ya kuwalinda hasa wanapoelekea mashuleni kwani wamekuwa wakitembea mwendo mrefu kwenda na kurudi shule ambako wamekuwa wakipata madhara na vishawishi vingi wanapokuwa njiani. 
Aidha watoto pia waligusia suala la rushwa na kwa namna gani linavyorudisha nyuma maendeleo yao na kuwaomba wagombea wa ngazi zote katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuwa waadilifu ili watoto wapate haki zao.
Mdahalo huo ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto wakishirikiana na UNICEF uligusa maeneo kumi muhimu ya uwekezaji kwa watoto ikiwemo kuwekeza kuokoa maisha ya watoto na wanawake, kuwekeza kwenye lishe bora, kuwekeza kwenye usafi, udhibiti wa miundombinu ya maji taka na ugavi wa maji katika shule na kwenye huduma za afya pamoja na kuwekeza katika kumwendeleza mtoto akiwa bado mdogo.
Mengine ni pamoja na kuwekeza kwenye elimu bora kwa watoto wote, kuwekeza katika kuzifanya shule kuwa mahali pa usalama, kuwekeza katika kuwalinda watoto wachanga na wasichana dhidi ya VVU, kuwekeza katika kupunguza mimba za utotoni, kuwekeza katika kuwanusuru watoto na vurugu, udhalilishaji na unyonyaji pamoja na kuwekeza kwa watoto wenye ulemavu. 
Vuguvugu hili la kusambaza ajenda ya watoto kupitia midahalo na wagombea wa nafasi mbalimbali linaendelea kupita mikoa mbalimbali nchini Tanzania kwani tunaamini kuwekeza katika maeneo haya ya kipaumbele kunaweza kupunguza umasikini na kuwezesha kuwepo kwa taifa linalostawi na la usawa.
Unaweza kusikiliza kipindi cha redio cha Walinde Watoto mahali popote kupitia redio shiriki 19 ikiwemo TBC inayorusha matangazo hayo siku ya Jumamosi kuanzia saa nane mchana na pia kupitia tovuti ya www.walindewatoto.org na
 www.facebook.com/WalindeWatoto