Pages

KAPIPI TV

Wednesday, October 7, 2015

DK. JOHN POMBE MAGUFULI AIPASUAPASUA CHADEMA ARUSHA, ASEMA "NITAMUENZI SOKOINE VITA YA UFISADI"

????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeis jijini Arusha wakati akiwaomba wananchi wa jiji hilo kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika nchini kote na kushirikisha vyama mbalimbali vya kisiasa.
Amesema Mara atakapochaguliwa na kuongoza taifa la Tanzania serikali yake itamuenzi Wazriri Mkuu wa zamani kutoka jimbo la Monduli Mzee Edward Moringe Sokoine katika kupambana na Rushwa ambapo mzee huyo hakupenda kabisa watu ambao ni wala rushwa na wabadhirifu wa mali ya umma serikalini alipambana kufa na kupona ili kuwasaidia wananchi waliowanyonge.
Katika mkutano huo pia wanachama kadhaa waliokuwa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo CHADEMA wamejiunga na chama cha Mapinduzi CCM na kutangaza rasmi katika mkutano huo, wanachama hao ni Japhet Sironga aliyekuwa Mwenyekiti Chadema wilaya ya Monduli na Jeremiah Mepukori Mwenyekiti BAVICHA wilaya ya Monduli ambapo wamekabidhi kadi zao kwa Dk. John Pombe Magufuli na kadi hizo kukabidhiwa kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-ARUSHA)
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika jijini Arusha leo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi waliofurika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Kattibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Arusha katika mkutano wa kampeni wa mgombea wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Kattibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Arusha katika mkutano wa kampeni wa mgombea wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
????????????????????????????????????
Mjumbe wa kamati ya ushindi ya CCM Ndugu Christopher Ole Sendeka akimnadi Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Ni Full Nyomi tu Aursha.
????????????????????????????????????
Msanii Ali Kiba akitumbuiza katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakiwa wamekaa meza kuu wakati mkutano huo ukiendelea jijini Arusha kutoka kulia ni Ndugu Christopher Ole Sendeka na Michael Lekule Laizer
????????????????????????????????????
Kindi la TOT likitumbuiza katika mkutano huo uliofanyika jijini Srusha.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakicheza muziki mara baada ya kuwasili kwenye mkutano katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakimsikiliza mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya kampeni CCM Ndugu Christopher Ole Sendeka.
????????????????????????????????????
Baadhi ya akina mama wa kimasai wakiwa katika mkutano wa kampeni mjini Monduli.
????????????????????????????????????
Magufuli hapa kazi tu.
????????????????????????????????????
Dk. John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakiteta jambo walipkutana Longido.
????????????????????????????????????
Jeremiah Mepukori aliyekuwa Mwenyekiti BAVICHA wilaya ya Monduli akikabidhi kadi yake kwa Dk. John Pombe Magufuli huku Japhet Sironga aliyekuwa Mwenyekiti Chadema wilaya ya Monduli mwenye kofia akifurahia baada ya wote kujiunga na CCM jijini Arusha leo.
????????????????????????????????????
Arusha ni Magufuli tu leo.
????????????????????????????????????
Wasanii mbalimbali wakiimba wimbo maalum kwa ajili ya kampeni za Dk. John Pombe Magufuli uliozinduliwa leo jijini Arusha.
????????????????????????????????????
Wasanii wakiimba wimbo huo.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwana viongozi mbalimbali wakiwa katika jukwaa kuu kwenye mkutano huo jijini Arusha.
????????????????????????????????????
Yamoto Band wakafanya mambo makubwa sana Sheikh Amri Abeid.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Wabunge wanaogombea ubunge viti maalum mkoa wa Arusha CCM Viola Mfuko na Catherine Magige wakiwatunza vijana wa Yamoto Band wakati walipokuwa wakitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni wa CCM jijini Arusha.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa jiji la Arusha mara baada ya kuwahutubia kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
????????????????????????????????????

WATUMISHI HOUSING COMPANY, BENKI YA CRDB WATIA SAINI MKATABA WA MIKOPO YA NYUMBA KWA WATUMISHI WA UMMA


Mkurugenzi wa Benki ya CCRD, Dk.Charles Kimei (kulia) na Mkurugenzi wa Watumishi Housing Company, Dk. Fred Msemwa wakisaini mkataba wa mikopo ya nyumba kwa watumishi wa Umma Dar es Salaam leo asubuhi.

Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambo (kulia), akitia saini mkataba huo. Kutoka kushoto ni Chief Operation Officer wa WHCTZ, Weja Ng'olo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Oscar Mgaya, Mkurugenzi wa Watumishi Housing Company, Dk.Fred Msemwa na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Charles Kimei.
Mkurugenzi wa Benki ya CCRD, Dk.Charles Kimei (kulia) na Mkurugenzi wa Watumishi Housing Company, Dk. Fred Msemwa wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wa mikopo ya nyumba kwa watumishi wa Umma.
Hapa hati zikioneshwa kwa wanahabari baada ya kusainiwa.
Mkurugenzi wa Watumishi Housing Company, Dk. Fred Msemwa akizungumza katika mkutano huo.
wadau kutoka benki ya CRDB na Watumishi Housing Company wakiwa kwenye mkutano huo.

Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
wadau kutoka benki ya CRDB na Watumishi Housing Company wakiwa kwenye mkutano huo.

Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

TAASISI ya Watumishi Housing Campany (WHC ),imeingia mkataba na Benki ya CRDB ikiwa ni katika kuwawezesha watu wa  hali ya chini kupata mikopo ya nyumba bora kwa bei nafuu.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi Mkurungezi wa wa taasisi hiyo, Dk.Frank Msemwa alisema wameamua kuanzisha mikopo ya nyumba za bei nafuu ikiwa ni mkuinua watu wenye vipato vidogo.

Dk Msemwa alisema   tayari wameshalenga soko la nyumba nchini watajenga nyumba zenye gharama nafuu ambazo kila mtu ataweza kukopa.

"Zitakuwa ni nyumba bora na kwa gharama nafuu kabisa kila mtu ambaye anakipato ataweza kukopa nyumba hizo," alisema Dk Msemwa.

Alisema mahitaji ya nyumba nchini ni zaidi ya bilioni 1.9 ambapo kwa jiji la dar es salaam pekee hitaji la nyumba ni laki nne kwa kila mwaka.

Naye Mkurugenzi wa CRDB Charles Kimei alisema  Dira ya taifa inaangalia nymba ikiwani kama azina ya kudumu na isiyo haribika huivyo ni vyema watu wakawekeza kwenye nyumba.

Alisema nyumba nzuri ni matokeo ya watoto wenye uelewa mzuri shuleni kwani hupata sehemu safi kwa kujisomea .

"CRDB ilikuwa ikikopesha nyumba ila si kwa njia rahisi kama hii inayoanza leo hivyo watu waje kwa wingi kukopa nyumba ambazo ni bora,"alisema Kimei.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

HATIMAYE VIJIJI VINNE WILAYANI HANANG’ VIMEPOKEA HAKIMILIKI ZA KIMILA

  Mzee wa heshima akielezea historia ya umiliki wa ardhi miaka ya nyuma ukilinganisha na sasa.
 Wanakijiji wakifuatilia tukio la makabidhiano ya hati za hakimiliki za kimila za vijiji vya Mureru, Ming'enyi, Dirma na Gehando vilivyopo wilayani Hanang’.
 Makko Sinandei Mratibu wa Miradi wa shirika la UCRT alisema wamekutana na changamoto za migogoro ya mipaka katika vijiji ambayo inazuia kushindwa kupima mipaka katika vijiji husika
 
 Baadhi ya akina mama wa Kijiji hicho wakifuatilia tukio
 Eveline Mirai, afisa ardhi wa wilaya ya Hanang' alitoa wito kwa wananchi kuheshimu mipaka inayowekwa kisheria kwa sababu mipaka hiyo inawekwa kwa gharama na wananchi wenyewe wanakuwa wameikubali.
 Laurent Wambura Meneja wa program ya ufugaji kutoka Oxfam aliwapongeza wakazi wa vijiji hivyo vinne pamoja na wananchi mmoja mmoja ambao nao walipokea hati zao siku hiyo.
 Mkutano ukiwa unaendelea huku wanakijiji wakifuatilia
 Mmoja wa wanakijiji akiongea wakati wa Shughuli hiyo ya kukabidhi hati
 Mgeni rasmi wa hafla hizo katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John Gabriel akizungumza kabla ya kukabidhi rasmi vyeti.
 Mwenyekiti wa kijiji cha Mreru James Gejaru akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi ya kimila ya kijiji chake.
 Kaimu Mwenyekiti wa kijiji cha Dirma Agustino Majawa akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi ya kimila ya kijiji chake
 hati ya hatimiliki ya kimila
  Mwanakijiji akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi yake
 Mwanakijiji akipokea hati ya hakimiliki ya ardhi yake
 Wananchi na viongozi wa Serikali ya kijiji  wakipitia kwa makini hati za hakimiliki za kimila za ardhi.
Sherehe zilipambwa na ngoma ya wa-Barbaig

Na mwandishi wetu
Wenyekiti wa vijiji vinne vya wilaya ya Hanang’ wamepokea hati za hakimiliki za kimila za ardhi ya vijiji vyao baada ya kuwa vimepimwa na wao kupewa mafunzo ya matumizi bora ya ardhi kwa ufadhili uliotolewa na shirika la Oxfam kupitia shirika la Ujamaa Community Resource Team - UCRT.

Vijiji hivyo vya Mureru, Ming'enyi, Dirma na Gehando vimekabidhiwa hati hizo na katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John Gabriel aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo katika hafla fupi iliyofanyika katika kijiji cha Mureru na kuhudhuriwa na wakazi zaidi ya 100 kutoka katika vijiji hivyo vinne.

Akiongea kwa niaba ya wenyeviti wa vijiji hivyo vinne, Mbisha Gicharoda ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha Ming’enyi aliyashukuru mashirika ya Oxfam na UCRT kwa kuwapatia elimu ya matumizi bora ya ardhi na kuwasaidia kupata hati za hakimiliki za ardhi ya vijiji. "Sisi kama wafugaji tulikua hatujui thamani ya ardhi yetu, sasa tumeamka na kujua haki zetu na manufaa ya kuwa na cheti cha umiliki wa ardhi", aliongezea.

Aidha mwenyekiti huyo alisema vijiji vyao kupata hati za hakimiliki za ardhi itawasaidia kuwa na eneo la pamoja la malisho na itawasaidia kuwa na nguvu zaidi ya kuilinda ardhi yao na kuisimamia vyema hali ambayo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi.

Katika hatua nyingine, afisa ardhi wa wilaya ya Hanang' Bi Eveline Mirai aliyashukuru mashirika ya Oxfam na UCRT kwa kuwasaidia wakina mama wajane nao kupata hati za hakimiliki za maeneo yao iliyoenda sambamba na kusaidia vijiji hivyo vinne kupata hati za vijiji.

Eveline alitoa wito kwa wananchi kuheshimu mipaka inayowekwa kisheria kwa sababu mipaka hiyo inawekwa kwa gharama na wananchi wenyewe wanakuwa wameikubali. “Mtakapoheshimu mipaka, hatutakua na migogoro ya ardhi” na akawataka wananchi wenye maeneo yao kuhakikisha wanapata hati za hakimiliki za maeneo yao ili wayamiliki kisheria.

Naye meneja wa program ya ufugaji kutoka Oxfam Laurent Wambura aliwapongeza wakazi wa vijiji hivyo vinne pamoja na wananchi mmoja mmoja ambao nao walipokea hati zao siku hiyo. "Ukilinda maeneo ya wafugaji maana yake ni kwamba umewahakikishia maisha yao, tunapenda kuona haki za wafugaji zinapatikana" aliongezea.

Wambura aliishukuru serikali hususani Halmashauri ya wilaya ya Hanang’ kwa ushirikiano mkubwa ambao wameutoa kufanikisha zoezi hili na akatumia fursa hiyo kutoa wito kwa serikali kushirikisha mashirika na wadau mbalimbali wa maendeleo wakati wa ugawaji wa maeneo ya ardhi za vijiji kwani wanapogawa vijiji wakati mchakato wa upimaji unaendelea ni hasara kwa mashirika hayo kwani aidha yanalazimika kuanza kazi upya au kushindwa kwa sababu tayari fedha zinakuwa zimetumika na tatizo kwa wananchi linakuwa halijatatuliwa.

Naye Makko Sinandei Mratibu wa Miradi wa shirika la UCRT alisema wamekutana na changamoto za migogoro ya mipaka katika vijiji ambayo inazuia kushindwa kupima mipaka katika vijiji husika.

Changamoto nyingine ni pamoja na udhaifu katika uongozi wa serikali ya vijiji ambazo huchelewesha mipango lakini pia kuchelewa kupata ripoti ya matumizi ya ardhi kutoka wizarani nayo ni changamoto.

Naye Mgeni rasmi wa hafla hizo katibu tawala wa Wilaya ya Hanang’ John Gabriel aliyemuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo, alipozungumza kabla ya kukabidhi rasmi vyeti hivyo alizitaja faida za kumiliki ardhi kisheria kuwa ni pamoja na ardhi ile huwezi kupokonywa na mtu kirahisi, utajua mipaka ya eneo lako ambayo huwezi kuingiliwa na mtu na vilevile inaweza kuwa rasilimali baadaye ukapata fedha kukuwezesha kufanya vitu vingine zaidi.

Akitolea mfano, John alisema "Mara nyingi wakina mama huwa wanakosa haki yao pale mume anapofariki, huwa ananyanganywa mali yote ikiwa ni pamoja na ardhi wakati anaachiwa watoto awatunze, lakini wanapokuwa na hati za hakimiliki hakuna mtu anayeweza kuwapokonya kirahisi."