Pages

KAPIPI TV

Thursday, August 27, 2015

SERIKALI KUZINGATIA USHAURI WA RIPOTI YA ESRF YA MAENDELEO YA BINADAM

IMG_4859
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (katikati) akimlaki Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia (kushoto) mara baada ya kuwasili katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha kufungua warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
IMG_4862
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia (kushoto) akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dk. Tausi Kida (katikati) pamoja Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kuelekea sehemu maalum ya mapumziko kabla ya kuingia katika ukumbi wa mikutano.
IMG_4869
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akifafanua jambo kuhusu warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na ESRF kwa mgeni rasmi (aliyeipa mgongo kamera) na meza kuu kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mikutano.
IMG_4966
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Hawa Ghasia akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya uwasilishaji wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya iliyofanyika jijini Arusha katika hoteli ya Ngurdoto.
IMG_4954
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Dk. Tausi Kida (katikati) pamoja Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakifuatilia kwa ukaribu hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani).
IMG_4927
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
IMG_4990
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 na Wakuu wa mikoa, wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa mikoa iliyofanyika katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
IMG_5217
Naibu Mkurugenzi Mkazi, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Amon Manyama akiwasilisha mada ya Mageuzi ya kiuchumi yanayoendelea: kuangalia zaidi ukaji wa uchumi wakati wa warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa kwa Wakuu wa mikoa, wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa mikoa katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
IMG_5012
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone (kushoto) wakifuatilia kwa umakini na viongozi wenzake wakati mada mbalimbali zizokuwa zikiwasilishwa kwenye warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa jijini Arusha.
IMG_4900
Pichani juu na chini ni Wakuu wa Mikoa, Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa waliohudhuria warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
IMG_5009
IMG_5019
IMG_4807
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto) katika picha ukumbusho na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa (katikati) na Mkuu wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Queen Mlozi (kulia).
IMG_5123
Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa (kushoto) katika picha ya ukumbusho na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema nje ya ukumbi wa mikutano Ngurdoto Mountain Lodge.
IMG_5088
Pichani juu na chini Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia na meza kuu katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makatibu Tawala wa Mikoa waliodhuria warsha ya uwasilishwaji wa ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya Mwaka 2014 iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
IMG_5095
IMG_5110
Mgeni rasmi na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).
IMG_5077
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akiteta jambo na mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Hawa Ghasia mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.
Na Mwandishi wetu, Arusha
SERIKALI imesema itazingatia ushauri uliotolewa katika Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania ya Mwaka 2014 iliyowasilishwa kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya katika warsha yao iliyofanyika Ngurdoto, Arusha.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh. Hawa Ghasia wakati akifungua warsha yenye lengo la kujadili na kuielewa.
Ripoti hiyo ambayo imejadiliwa kama “Mageuzi ya Kiuchumi kwa Maendeleo ya Binadamu” ilizinduliwa rasmi mwezi machi mwaka huu wa 2015 inawasilishwa kutokana na haja ya viongozi hao kutambua yaliyomo na namna ya kusonga mbele katika mipango ya baadae.
Ripoti hiyo ambayo ni matokeo ya utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imelenga kusaidia kufahamu yaliyomo katika ripoti hiyo ili kuwawezesha viongozi hao kupata uelewa mpana juu ya dhana hii ya masuala ya Maendeleo ya Binadamu.
Warsha hiyo imewezesha na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Ghasia alisema utafiti huo umelenga kuzijengea uwezo mamlaka za mikoa na serikali za mitaa ili kuziwezesha kutoa huduma bora kwa wananchi.
Ripoti hiyo ambayo imezungumzia masuala ya mageuzi ya kiuchumi kwa Maendeleo ya Binadamu imetafakari kwa undani namna ya kufanya mageuzi ya kiuchumi katika taifa ili kuleta maendeleo ya Binadamu.
Akizungumzia maendeleo alisema mwanzoni mwa karne ya 21, mataifa mengi ya kiafrika yalitengeneza Dira za Maendeleo kuwa mwongozo wa ujenzi wa uchumi na maendeleo.
“Kwa upande wa taifa letu, Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 inalenga katika kulifanya taifa letu kuwa nchi ya uchumi wa kati wenye kutegemea zaidi sekta ya viwanda na huduma.
“ Kwa maneno mengine, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 inalenga siyo tu katika ukuzaji wa uchumi bali kubadilisha muundo wa uchumi; kwa miaka mingi uchumi wa Taifa letu umekuwa unategemea zaidi kilimo ambacho kina tija ndogo.” alisema Ghasia.
Alisema kwamba Sera za Maendeleo ya taifa letu tangu uhuru zimekuwa zikiweka kipaumbele katika dhana ya Maendeleo ya Binadamu.
“Kwa mfano, Azimio la Arusha la mwaka 1967, ambalo liliamua taifa lifuate mfumo wa ujamaa na kujitegemea lilielekeza kwamba sera, mipango na mikakati yote lazima zizingatie uboreshwaji wa maisha ya watu kwani lengo la maendeleo ni watu.” Alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akizungumzia warsha hiyo alisema kwamba utafiti huyo uliofanywa na taasisi yake uliwezekana kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Idara ya uchumi), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali ya Zanzibar.
Alisema Toleo hilo la Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania ya 2014 ni toleo la kwanza nchini.
Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo hapa nchini na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, alizungumzia umuhimu wa mabadiliko ya kiuchumi ili taifa liwe la kipato cha kati.
Alisema ipo haja kwa taifa hili kuhakikisha kwamba linatumia vyanzo vyake vya kifedha kubadilika kutokana na hali halisi ilivyo kwa sasa.
Aidha alisema ipo haja ya kuzingatia mipango madhubuti ya kuondoa umaskini na kulinda mazingira, mambo ambayo yapo katika mpango mkakati wa Umoja wa Mataifa wa UNDAP wa maendeleo kuanzia mwaka kesho hadi 2021.

SANAA FASHION SHOW KUFANYIKA KESHO NDANI YA UKUMBI WA MBEZI GARDEN HOTEL

 
image4
Na Andrew Chale, modewjiblog
(Dar es Salaam)-Ile shoo kubwa yamaonyesho ya mavazi ubunifu ya Tanzania katika kuibua vipaji vya wanamitindo chipukizi na models lililoandaliwa na kampuni ya Crown River Fame likijulikana kama Sanaa Fashion Show, linatarajia kufanyika Ijumaa hii ya Agosti 28, ndani ya ukumbi wa Mbezi Garden Hotel, ambapo pia kutakuwa na shoo kabambe kutoka kwa msanii wa THT, Msami.
Akizungumza na mtandao huu Meneja Mradi wa Crown River Fame, Mr. Rahul anasema tayari taratibu zote zimeshakamilika na models pamoja na wabunifu wa mitindo wameshakamilisha kazi zao na kinachosubiriwa na shoo hiyo kabambe na ya aina yake kwa upande wa fashion show.
"Tunataraji kuwa na Models zaidi ya 20, watakaonyesha mavazi ya ubunifu katika shoo hii ya Sanaa Fashion, na pia tunatarajia kuwa na wabunifu zaidi ya 15 wakiwemo wakongwe na wanaochipukia kwa maana 'Upcoming Desgners'.
Ili kuleta mageuzi katika tasnia hii ya urembo na ubunifu, jukwaa hili la Sanaa Fashion Show, lina lengo kuu la kuinua models wanaochipukia 'Upcoming models' na pia kuendeleza tamaduni zetu kwa maana hiyo tumeipa jina la Sanaa.".
Aidha, anabainisha kuwa, baadhi ya wabunifu wa mavazi watakaoshiriki kwenye kuvisha Models, katika show hiyo ni pamoja na Mama wa Mitindo nchini, Asia Idarous, Mohammed Abdul, Joyce na wengine wengi.
Kwa upande wa kiingilio ni V.I.M ni Sh 20,000 huku V.I.P yenyewe ikiwa ni sh 40,000.
Kwa upande wa wadhamini ni pamoja na MODEWJIBLOG, 8020Fashions, Shear Illusions, Mbezi Beach Garden, BR Production, MC na wengine wengi.
Abdul AmadHusna Tandika akimfanyia make up, Model, Abdul-Amad katika duka la Shear Illusions Millenium Tower, jijini Dar es Salaam. Ikiwa tayari kwa maandalizi ya shoo hiyo ya kesho!
Jonetha Peter
Jonetha-Peter. akipakwa make up na mfanyakzi wa Shear Illusions, Agnes Rafael..
Barnabas Lukindo
Barnabas Lukindo akifanyiwa make up..
Calisah Abdulhameed
Calisah Abdulhameed akifanyiwa make up
Husna Tandika wa Shearshen na Natasha Mohammed
Husna Tandika akimpaka Natasha Mohammed model make up
Calorine Benard
Calorine-Benard. akifanyiwa make up
Calorine Benard.jpge3
Jazyline Gerad
DSC_0024
DSC_0025

MAGUFULI ALIVYOITIKISA WILAYA YA MOMBA,TUNDUMA NA ILEJE

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tunduma waliofurika kwa wingi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma,mkoa wa Mbeya mapema leo mchana,kwenye mkutano wa kampeni wa kuwaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano,ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Oktoba 25  mwaka huu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akizungumza jambo na mlemavu wa miguu ndugu Joseph,mkazi wa kijiji cha Lwasho wilaya ya Momba,ambapo alimuahidi kumletea baiskeli ya kutembelea.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akiombewa na Watawa wa kijiji cha Lwasho,mara baada ya kumaliza mkutano wa kampeni katika kijiji cha Lwasho,wilaya ya Momba.
 Maelfu ya Wananchi wa Tunduma waliojitokeza  kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika uwanja wa shule ya msingin Tunduma mkoani Mbeya.


   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya,Mh.Abbas Kandolo alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Nzoka Wilaya ya Momba mkoani humo,pichani kati ni Mgombea Ubunge wa jimbo la Mbozi Mh Godfrey Zambi.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mgombea Ubunge wa jimbo la Ileje Mh.Janet Mbene,mara baada ya kuwasili wilayani humo kuhutubia mkutano wa kampeni.
Wananchi wakiwa wamefurika katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchama kumsikiliza mgombea urais wa CCM akimwaga sera zake kuwaomba Watanzania wamchague na kumpa ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano.
Wananchi wa wilaya ya Ileje wakiwa wamekusanyika katika uwanja wa Ileje mjini wakimshangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni wilayani humo.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa kwa shangwe na wananchi alipokuwa akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana kwa ajili ya mkutano wa kampeni.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tunduma waliofurika kwa wingi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma,mkoa wa Mbeya mapema leo mchana,kwenye mkutano wa kampeni wa kuwaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano,ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Oktoba 25  mwaka huu.
  Maelfu ya Wananchi wa Tunduma waliojitokeza  kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mkoani Mbeya.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli ,akiwapigia debe madiwani wa CCM kwa wananchi (hawapo pichani),katika kijiji cha Nzoka wilayani Momba,mkoani Mbeya kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Wananchi na wafuasi wa chama cha CCM katika kijiji cha Nzoka wilaya ya Momba mara baada ya kuwahutubia kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wa kijiji cha Lwasho wilayani Momba wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano huo wa kampeni uliofanyika leo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea udiwani wa CCM kwa wananchi wa kijiji cha Lwasho,wilaya ya Momba katika mkutano wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mbunge wa viti maalum wa CCM,Dkt Marry Mwanjelwa
Wananchi wa kijiji cha Ndalambo wakimshangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  alipopita kijijini hapo kuwasalimia wakati akielekea wilaya ya Ileje kuhutubia mkutano wa kampeni.
Palikuwa hapatoshi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana wakati mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipowasili katika viwanja hivyo na kuwahutubia wananchi.
Palikuwa hapatoshi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana wakati mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipowasili katika viwanja hivyo na kuwahutubia wananchi.
Bango la wagombea
Baadhi ya Wananchi wa Ileje wakiwa na mabango yao.
 Nyomi la Watu katika mkutano wa kampeni.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akimnadi mmoja wa wagombea Ubunge katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma,kwenye mkutano wa kampeni.