Pages

KAPIPI TV

Friday, August 7, 2015

WASANII WAMUAGA DR. JAKAYA KIKWETE NA KUMKARIBISHA DR JOHN POMBE MAGUFULI MLIMANI CITY

1
Rais Dr. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kupitia CCM wakati alipowasili Mlimani City jijini Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki hafla ya chakula cha jioni kilichondaliwa na Muungano wa wasanii Kumshukuru Mh. Dr. Jakaya Kikwete kwa jinsi alivyowasaidia katika uongozi wake wa miaka 10 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kumkaribisha Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli, Hafla hiyo imehudhuriwa na wasanii mbalimbali wakiwemo waigizaji wa filamu, wachezaji na wanamuziki wakishiriki kwa pamoja kumshukuru Dr. Jakaya Kikwete, Kulia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MLIMANI CITY-DAR ES SALAAM) 3
Rais Dr. Jakaya Kikwete akifuatana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto, Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli na Mwigizaji Jacob Steven JB wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Diamond.
4
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kutoka kushoto ar es salaam Mh Meck Sadik na Muigizaji Jacob Steven JB.
5
Mwanamuziki Nasib Abdul aka Diamond Platnumz akiwasili na Meneja wake wa Shughuli za kimataifa Bw.Salam.
6
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto wakati wakiigia ukumbini.
7
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto,Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli wa pili kutoka kulia na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba.
8
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto,Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli kulia na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye wakipiga makofi wakati wimbo maalum ukiimbwa.
9
Davis Mosha kulia akiwa pamoja na Mboni Masimba wa The Mboni Show wakiperuzi kwenye simu.
10
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Davis Mosha na Mboni Masimba
11
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya viongozi wa bendi za muziki wa Taarab.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Bw. Godfrey Kusaga mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Primetime. 16
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Adam Mchomvu mtangazaji wa kipindi cha XXL cha Clouds Radio.
17
Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa mtandao wa FULLSHANGWE BLOG Bw. John Bukuku kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
19
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Davis Mosha kushoto ni msanii Mwana FA.
20
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wasanii mbalimbali kutoka kushoto ni Mwigizaji Jacob Steven, Mwanamuziki Jose Mara na Mwana FA.
21
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na wasanii mbalimbali kutoka kushoto ni Mwigizaji Jacob Steven, Mwanamuziki Jose Mara, Mwigizaji Monalisa aka Yvone Cherry na Mwana FA, kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Meck Sadik.
22
Kutoka kulia ni Mama Monalisa . Juma Kaseja, Dokii na Monalisa wakiwa katika hafla hiyo.
23
Ali Choki kushoto na anayefuatia ni msanii Kitale pamoja na wasanii wenzao wakiwa katika hafla hiyo.
24
Kutoka kushoto ni  Edward Mpogole, Daniel Chongolo na Juma Kengele wakipozi kwa picha.

Thursday, August 6, 2015

MASHIRIKA MATANO YA KITAIFA NA KIMATAIFA(FOS) YAUNGANA KWA PAMOJA KUTOA ELIMU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015

Wasemaji kutoka Mashirika Matano Kutoka kushoto ni Msemaji kutoka LHRC,OXFAM, Restless Development, BBC na VSO
  Mkurugenzi Mkuu Mkazi wa Oxfam Jane Foster ambao pia ndio waandaaji wa Mkutano huu na waandashi wa Habari akieleza kwa kina nia ya Mkutano huo ambao lengo kuu ni kuzungumzia maswala ya Uchaguzi kuwa kila mtu anahaki ya kupiga kura.
  Hellen Kijo Bisimba ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki  za binadamu (LHRC) (Kushoto) akiongea jinsi walivyo endesha zoezi zima la kusimamia uandikishaji wa Daftari la uandikishaji wa wapigakura la kudumu BVR na ushiriki wao kwa ujumla.
Meneja wa Programu kitengo cha Governance kutoka Oxfam Bi.  Betty Malaki  akiendelea kutoa utaratibu katika Mkutano huo.
 Mwakilishi kutoka Shirika la Restless Development Bi. Rahma Bajun ambao jukumu lao limelenga sana kwa vijana , akitoa taarifa ya Jinsi walivyo washirikisha vijana katika kuwahimiza na kuwapa elimu ya uchaguzi na kupiga kura ambapo wanafanya kazi hasa katika mikoa ambayo ipo Pembezoni ambayo ipo 11 .
 Mwakilishi kutoka Shirika la Utangazaji la BBC Bi.Neema Yobu akielezea jinsi wanavyo simamia na kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari nchini, kutoa elimu ya uandishi bora wa Habari za kipindi cha uchaguzi mkuu 2015.
 Mwakilishi kutoka Shirika la Innovation Skills Results Bw. Jean Van Wetter akieleza jinsi wanavyohusika kwa ukaribu kabisa hasa katika upande wa vijana wa umri wa kati kuwaelimisha juu ya umuhimu wa Uchaguzi ambapo alisisitiza kuwa vijana wanatakiwa kupewa mapema elimu hii ili wanapokuwa wafahamu umuhimu wa uchaguzi.
 Mmoja wa wasemaji kutoka VESO Bi. Lina Muro akisisitizia Jambo<!--[if gte mso 9]>
Baadhi ya waandishi wa Habari wakiwa katika Mkutano huo.

Umoja wa Mashirika Matano yanaounda ushirika wa Fahamu,Ongea Sikilizwa(FOS) ambayo ni Oxfam,BBC Media Auction, Legal and Human Rights Centre, Restless Development, and VSO leo wamekutana na waandishi wa Habari kwa ajili ya kuzungumzia mambo Mbalimbali yanayohusiana na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2015 na kueleza malengo ya muungano huo.
Akizungumza Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Bi. Jane Foster ambao ndio waandaaji wa Mkutano huo na waandishi wa Habari alisema kuwa Lengo kubwa la Umoja huo ni kusisitiza na kuwaelimisha wananchi wote kwa ujumlan juu ya Uchaguzi mkuu 2015 ambapo Oxfam wao jukumu lao kubwa ni kuwahimiza wanawake na wasichana wadogo  kuelekea uchaguzi Mkuu kama wapiga kura, na ili kuyafikia makundi yote haya waliandaa na wanaendesha Midaharo mbalimbali, kuunda makundi ya wanawake na zaidi wanatumia mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter kuwapa taarifa juu ya uchaguzi.
BBC kwa upande wao wanajukumu la kusimamia mashirika mbalimbali ya utangazaji Nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu na kanuni za uandishi bora wa Habari za uchaguzi Mkuu 2015 

Nao kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ambao walikuwa na jukumu la Kusimamia zoezi zima la uasdikishaji wa wapiga Kura ambapo walikuwa na watu 165 nchi nzima wakiangalia na kuangalia makosa yaliyojiokeza na kupeleka Maoni yao sehemu husika, na pia katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 wameandaa kitengo maalumu cha Teknolojia ambacho kitasimamia uchaguzi wote.

Wakati huo huo restless Development wamewafundisha vijana 22 ambao wamesambazwa katika mikoa 18 Nchi nzima kwa lengo kuwakusanya vijana katika makundi mbalimbali kwa nia ya kuwapa elimu kwa ajili ya uchaguzi mkuu 2015, sambamba na hapo wamelenga kuwapa elimu viongozi wa ngazi za chini yaani Wilaya, Pia vyombo vya habari pamoja na Polisi, ambapo kwa sasa Shirika hili linaandaa ajenda mbalimbali kuelekea uchaguzi Mkuu 2015.

Pia Shirika la Voluntary service Overseas nao wameendesha mafunzo kwa viongozi wa chini, viongozi wa Dini katika mikoa Nane(8) Tanzania ambao wanashirikishwa moja kwa moja katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Mikoa hiyo ni Pamoja na Lindi, Mtwara, Kagera na Mikoa mitano Zanzibar ambayo ni Wete,Chakechake, Unguja, Makokotoni na Unguja Kaskazini. wakieleza juu ya uchaguzi Mkuu 2015.

Akizungumza na waandishi wetu mmoja wa wakurugenzi  wa mashirika hayo, Hellen Kijo Bisimba ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki  za binadamu (LHRC), alisema kuwa moja kati ya mapungufu yaliyoonekana katika uchaguzi huo ni kuwepo kwa imani potofu hasa katika kipindi cha kujiandikisha kwa kutumia mashine za BVR ambapo wananchi wengi hasa wa vijijini walikuwa na dhana kuwa mashine hizo huweza kuwapima watu Ukimwi na wengine kushikana uchawi hasa wale ambao alama zao za vidole hazikuonekana au zilipatikana kwa shida.
Katika mikoa mingine mkurugenzi huyo alisema kuwa watu walifikia mbali zaidi na kuaminishana kuwa mashine hizo ni za Freemason na makundi ya wanyonya damu mambo ambayo yalichangia wengi wao wasishiriki zoezi zima la uandishaji na kuongeza kuwa changamoto zote hizo walizibaini na kuzifikisha kwa tume.
“Kuna maeneo walihamasishana kabisa kutojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura hasa kwa njia BVR wakidai kuwa ni ya Freemason au wanyonya damu huku wengine wakishikana uchawi kwa kuwa alama zao za vidole hazisomi kwenye mashine hizo. Hizo zote ni changamoto na tumezifiksha kwenye tume,” alisema Bi Hellen na kuongeza kuwa hata hivyo muamko wa vijana mwaka huu ni mkubwa sana jambo linalotoa tafsiri kuwa uchaguzi huu utakuwa shirikishi kuliko hapo awali.


KUJIUZURU KWA LIPUMBA NYADHIFA ZAKE ZOTE CUF NA UKAWA KUMEWATIA SHAKA WANANCHI

???????????????????????????????????? Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Peacock leo jijini Dar es salaam wakati akitangaza kujuuzulu nyazifa zake zote katika chama hicho na kubaki mwanachama wa kawaida kutokana kile alichokiita dhamira inamsuta.(NA KIKOSKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) ???????????????????????????????????? Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba akionyesha rasimu ya katiba iliyoandaliwa na tume ya katiba mpya iliyokuwa ikipendekezwa iliyoandaliwa na Jaji Joseph Warioba ambayo anadai imefinyangwa.

 Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amejiuzulu kama mwenyekiti wa chama hicho akisema dhamira inamsuta.

Profesa Ibrahim Lipumba Amezungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo, Profesa Lipumba amesema amejitahidi kujenga chama hicho hasa Tanzania bara, amejenga umoja wa Wazanzibari hivyo anajiuzulu kulinda heshima yake.

Amesema ameikabidhi Ofisi ya Katibu Mkuu, barua yake ya kung’atuka nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, lakini ataendelea kuwa mwanachama wa CUF na kadi yake imelipiwa mpaka mwaka 2020.

Ameeleza sababu za kujiuzulu ni Umoja wa huo wa UKAWA kushindwa kuenzi Tunu za Taifa katika umoja wao kwa kuwakaribisha watu waliopitisha rasimu iliyochakachuliwa kwenye Bunge Maalumu la katiba.

Profesa Lipumba amekiri kushiriki katika vikao mbalimbali vya Ukawa mpaka hapa walipofikia . lakini akasema . Nafsi yangu inanisuta kuwa katika maamuzi yetu tumeshindwa kuenzi na kuzingatia Tunu za Taifa za utu, uadilifu, uzalendo, uwajibikaji,, umoja,na uwazi .

Aidha muda mfupi mara baada ya kuripotiwa kwa hatua hiyo ya Prof.Lipumba imezua maswali mengi kwa wananchi ambayo yanaashiria kuwa huenda kuna jambo lingine nyuma ya pazia kuliko kile kilichozungumzwa na kiongozi huyo ambaye ameanza kutajwa kuwa anataka kukihama chama hicho kwa madai kwamba kuna mpasuko wa ndani kwa ndani. 

MSD YAWAVUTA WANANCHI KATIKA BANDA LAO MAONYESHO YA NANENANE YANAYOENDELEA MKOANI DODOMA


Wananchi wakisubiri kupata huduma katika banda la MSD kwenye Maonyesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Dodoma.

Ofisa Mdhibiti Ubora wa MSD, Betia Kaema, akitoa dawa kwa mgonjwa aliyefika katika banda la MSD kwenye maonyesho hayo.

Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dodoma, Sara Wangilisasi akitoa dawa kwa mgonjwa aliyefika kwenye banda la MSD kwenye maonyesho hayo.

Ofisa Mauzo, Juliana Mbogo na Ofisa Udhibiti Ubora, Betia Kaema wakiandaa dawa za kumpatia mgonjwa aliyefika katika banda la MSD.Na Mwandishi Wetu

Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wametakiwa kufika banda la Bohari ya Dawa (MSD), katika maonyesho ya Nanenane ili kujua kazi mbalimbali zinazofanywa na MSD hapa nchini.

Mwito huo umetolewa na Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Dodoma, John Kisembi wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma kwenye maonyesho hayo ambayo kilele chake ni Agosti 8, mwaka huu.

Kisembi alisema kila mwaka MSD imekuwa ikishiriki  katika maonesho
hayo na kutoa elimu kwa wananchi juu ya mambo mbalimbali yanayoihusu MSD.

Alisema mwaka huu MSD imeshiriki katika maonesho hayo ambayo yapo kikanda mkoani Dodoma ambapo wananchi na wadau mbalimbali wanaelimishwa kuhusu mambo mbalimbali ya kimafanikio yaliyofikiwa na MSD na yale yanayoweza kuongezea uwanda wao wa kibiashara hivyo kuongea mauzo yao.

Alitaja mambo yaliyozingatiwa katika maonesho hayo kuwa ni upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vyenye ubora kote nchini, upanuzi wa maghala hivyo kuongeza uwezo wa kuhifadhi dawa kwa wingi pamoja na usambazaji dawa na vifaa tiba kwa kutumia mfumo wa Direct Delivery (DD)

Mambo mengine ni matumizi ya mfumo mpya wa TEHAMA (Epicor 9),  Uwekaji wa nembo ya GOT katika vidonge, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara ilikutofautisha dawa za serikali na za binafsi, uanzishaji wa  maduka ya dawa ya jumla karibu na wananchi (MSD 24hours Community Outlets) , pamoja kutoa elimu, sehemu maalumu ya kutolea dawa ambapo wagonjwa wanaopatiwa vipimo katika banda la Hospitali ya Mkoa wanakuja kupatiwa dawa katika banda la MSD. 







MUDA WA KUJISAJILI KWENDA HIJJA WASOGEZWA MBELE TOKA JUNI 15 HADI AGOSTI 25, 2015


 Naibu Mwenyekiti Ofisi Kuu ya Hijja Tanzania (BIITHA), Yusuf Musun (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kusogezwa mbele muda wa kujisajili kwenda Hijja kutoka Juni 15 hadi Agosti 25 mwaka huu. Kulia ni Ofisa Habari wa Biitha, Hamisi Tembo na Mratibu wa Biitha, Abdallah Khalid.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.


Mkutano na wanahabari ukiendelea.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)




BALOZI LIBERATA MULAMULA AONDOKA RASMI MAREKANI KURUDI TANZANIA.

 Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja  na baadhi ya Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC walipokwenda kumuaga nyumbani kwake Bethesda Maryland.


                               Safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Dulles ikianza.
 Mhe Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Agnes Mutta Mke wa Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC.
Mhe Balozi Liberata Mulamula pamoja na Mkuu wa Utawala Lily Munanka wakibadilishana mawazo pamoja na familia ya Mwambata wa Jeshi.
 Mhe Balozi Liberata Mulamula akiwa pamoja na Mwambata wa Jeshi Col. Adolph Mutta pamoja na Mkewe Agnes Mutta.
               Mhe Balozi Liberata Mulamula akitoa  pasi yake ya kusafiria kwaajili ya kujisajili tayari kwa kuondoka.
                        Mhe Balozi Liberata Mulamula  akiwa katika hatua za mwisho za usajili.
                           Mhe Balozi Liberata Mulamula tayari usajili ulipokamilika
Mhe. Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi pamoja na familia zao.
Mhe. Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula akiwa tayari anajiandaa kwa ukaguzi wa mwisho na kuelekea kwenye ndege.
 Kwa pamoja tunasema Safari Njema na Ubarikiwe Sana Balozi Mulamula daima tutakukumbuka.
                   

DR.SLAA: "NIKO SALAMA, NITAZUNGUMZA MUDA UKIFIKA"

By Florence Majani na Daniel Mjema

Dar/Moshi. Siku tatu baada ya Baraza Kuu la Chadema kuridhia kumpumzisha kwa muda Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa baada ya kutofautiana na Kamati Kuu kwa kumkaribisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kiongozi huyo amesema yupo salama na wakati mwafaka ukifika atazungumza ya moyoni.

Akizungumza kwa mara ya kwanza na gazeti hili tangu Chadema imkaribishe Lowassa na hatimaye kumpitisha kuwania urais kupitia muungano wa Ukawa, Dk Slaa alisema amekuwa akisikia mengi yakisemwa juu yake lakini yote yamekuwa yakimchekesha tu.

Hakuhudhuria vikao muhimu vya chama hicho na vile vya Ukawa, vikiwamo; wakati Lowassa akitambulishwa rasmi, akichukua fomu, kikao cha Baraza Kuu na juzi Mkutano Mkuu na hakuwa akipatikana kwa simu yake ya mkononi.

Wakati kimya kikitawala juu ya hatima yake, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika kuwa amejivua uanachama Chadema.

Lakini jana alisema: “Naangalia mambo mengi yanayoendelea kwenye mitandao halafu ninacheka tu, usifikiri sifuatilii, nafuatilia kinachoendelea na ninabaki nikicheka.”

Kuhusu hatima yake kisiasa na madai ya kujiuzulu uanachama ndani ya Chadema, alisema hawezi kuzungumza lolote kwa sasa na atafanya hivyo wakati mwafaka ukifika. “Usijali wakati wangu wa kuzungumza ukifika nitasema tu, sasa hivi nawaachia mzungumze, lakini nitazungumza,” alisema.

Kadhalika, alipoulizwa kuhusu taarifa zilizozagaa kuwa maisha yake yapo hatarini kwa kuwa anatishwa, Dk Slaa alisema hata hilo pia atalizungumzia wakati mwafaka ukifika.

“Ndiyo hayohayo ninayosema, wala msijali nitazungumza wakati ukifika,” alisema na kusisitiza: “Nipo salama.”

Dk Slaa alisema kwa sasa yupo mapumzikoni nje ya jiji la Dar es Salaam ingawa hakutaka kueleza ni eneo gani.

Juzi, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alifafanua tofauti iliyojitokeza kati ya Kamati Kuu ya Chadema na Dk Slaa wakati wa mchakato wa kumpokea Lowassa.
Katika mkutano huo wa Baraza Kuu la Chadema, Mbowe alisema wamekubaliana katibu mkuu huyo apumzike kwa muda... “Nina hakika kwa tabia na hulka za Dk Slaa… kwa sababu anajua tunampenda na yeye anakipenda chama hiki, tunamwombea kwa Mungu ampe nguvu na ujasiri wa kuona kwamba kauli ya wengi ni kauli ya Mungu.”

Ndesamburo na siri nzito
Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo na makada wengine wa Chadema, jana walikwenda kuonana na Dk Slaa nyumbani kwake na kufanya naye kikao cha faragha.

Picha zilizomuonyesha Ndesamburo akiwa na Dk Slaa na makada wengine akiwamo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Jaffar Michael, zilisambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii jana na kuibua mijadala.

Baadhi ya waliochangia mijadala hiyo walidokeza kuwa huenda Ndesamburo anayeheshimika ndani ya chama hicho alikwenda kujaribu kusawazisha hali ya mambo.

Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene alikiri kuwa picha hizo ni halisi, baadhi zilipigwa juzi na nyingine jana mchana, lakini hakutaka kuingia undani wa mkutano wa wanasiasa hao.

Ndesamburo alithibitisha kukutana na Dk Slaa: “Ni kweli tulikwenda, kwani kuna tatizo gani? Si mzee mwenzangu? Halafu bado ni mwanachama wetu, hajatoka Chadema, hivyo tuna kila haki ya kwenda kumsalimia.”

Alipoulizwa kama alikwenda kumsihi Dk Slaa arejee kuendesha mapambano ya kuing’oa CCM, Ndesamburo alisisitiza kuwa walikwenda kumsalimia.
Michael alipoulizwa nia ya safari hiyo alijibu kwa kuuliza; “Dk Slaa ni katibu mkuu wetu kwani tunazuiwa kwenda kumsalimia?”

Dk Slaa aligombea urais mwaka 2010 na kushika nafasi ya pili baada ya Rais Jakaya Kikwete na ndiye aliyekuwa akitajwa kuwania tena nafasi hiyo kupitia Chadema na Ukawa kabla ya “kubadili gia angani” na kumteua Lowassa.
Chanzo:-Gazeti la Mwananchi.

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO, HUAWEI WAZINDUA SIMU YA WATU WA HALI YA CHINI JIJINI DAR ES SALAAM

 Meneja wa Vifaa vya Huawei,  Peter Zhang Nchini (kulia), akionesha aina ya simu ya Huawei Y 360 na Y 625 ambazo zina uwezo wa hali ya juu katika matumizi ya nyanja mbalimbali wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi katika uzinduzi wa simu hizo. Kushoto ni Meneja wa Vifaa na Intaneti kutoka Tigo, Mkumbo Myonga.
 Meneja wa Vifaa na Intaneti kutoka Tigo, Mkumbo Myonga, akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabri kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa ya uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Tigo na ile ya kutengeneza simu za mkononi ya Huawei, wameshirikiana kuzindua simu mpya mbili za kisasa kwa ajili ya watumiaji wa simu za hali ya chini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja wa Vifaa vya Huawei,  Peter Zhang alizijata simu hizo ni Huawei Y 360 na Y 625 ambazo zina uwezo wa hali ya juu katika matumizi ya nyanja mbalimbali.

Alisema simu hizo zinapatikana kwa bei nafuu ambayo mwananchi yeyote atakuwa na uwezo wa kununua kwa ajili ya kwenda na kasi ya teknolojia ya digitali.

Kwa upande wa Meneja wa Vifaa na Intaneti kutoka Tigo, Mkumbo Myonga alisema wanaendelea kubadilisha maisha ya Watanzania ili wote waweze kuwa kwenye digitali na kwa kuzindua simu hizo itasaidia jamii kuingia kwenye ulimwengu huo.

Alisema wateja wanaotumia mtandao wao watakaponunua simu hizo watapata ofa mbalimbali zitakazowasaidia kuendelea kupata huduma zikiwemo vifurushi na kusikiliza muziki bure kwa miezi sita. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

WASHIRIKI WA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2015 WAWASILISHA MIRADI YAO YA KILIMO NA MAZINGIRA KWA WANAKIJIJI CHA KISANGA WILAYANI KISARAWE PWANI


 Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwa katika Bwawa la Lamboni wakipata maelezo kutoka kwa wanakijiji hii ikiwa ni moja ya sehemu ya ziara yao jana .
 Wenyeji pamoja na  Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula wakielekea Mabondeni..Ilikuwa ni nafasi yao ya kufahamu maeneo mbalimbali Kijijini hapo...
 Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula wakioneshwa Madhari ya shule ya Msingi ya Kisanga na mmoja wa wanakijiji aliyesimama Mbele Kulia.
 Hapa washiriki wa Shindano la Mama Shijaa wa chakula 2o15 linalo andaliwa na Oxfam kupitia kampeni yao ya Grow , kipindi kinachoruka kila siku ITV kuanzia Saa Kumi na mbili  Jioni na Kurudiwa saa Tano na nusu asubuhi  wakiwa katika ofisi ya Kusindika zao la Mihogo
 Hapa washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 msimu wa nne wakiwa katika moja ya kisima ambacho maji yake yananukia Mafuta, maji haya yanatumika zaidi katika shughuli za Kufulia Nguo.
 Mwakilishi kutoka Oxfam Eluka Kibona aliyesimama (Kulia) akizungumza na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Pamoja na wanakijiji katika Kijiji Cha Kisanga jana.
 Kundi la kwanza la Washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Mazingira..
 Wanakijiji na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasikiliza jinsi Miradi inavyo wasilishwa.
 Kundi la pili la washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Kilimo Bora.

 Kundi la Tatu la washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakiwasilisha Mradi wao wa Kilimo Bora cha Mboga Mboga na Hihogo.
********
Ni siku nyingine tena katika kijiji cha Kisanga, jua la saa nne asubuhi ni kali huku  mti huu mkubwa wa mkorosho uliopo eneo la makutano unatusitiri. Washiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula Shindano lililiondaliwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow, walikuwa wamesimama vikundi vikundi, bila shaka walikuwa wanahadithiana chakula walichowapikia wenyeji wao jana. 

Siku ya ilikuwa  inaanza kwa waandaaji wa shindano kutengeneza makundi matatu ya kina Mama Shujaa wa Chakula watano watano. 

Kwa muda watakaokaa hapa kijijini Kisanga, kila kundi linatakiwa kutengeneza mradi wa maendeleo endelevu kwa manufaa ya kijiji cha Kisanga. Ili kufahamu fursa na changamoto zilizopo, uongozi wa kijiji unawatembeza sehemu nne. 

Upatikanaji wa maji ya uhakika kijijini hapa ni changamoto. Kina Mama Shujaa wa Chakula wanaletwa sehemu hii yenye bwawa, wenyeji wanaiita lamboni. Inasadikika kuwa zamani kulikuwa na kisima, ila kwa sasa kimefunikwa na wingi wa maji. Pia kuna viumbe wakali kama vile chatu. 

Elimu ya msingi katika kijijini Napo inatolewa katika shule ya msingi Kisanga. Wakina Mama Shujaa wa Chakula wanaoneshwa mandhari ya shule na mwenyeji. 

Wakazi wa kijiji cha Kisanga wanapata maji ya kunywa na kupikia katika visima vilivyopo eneo hili linaloitwa Mfuru. Kufuatia msimu wa mvua ulioisha, visima vyote vinne vina maji ya kutosha, japo kisima kimoja maji yake hayatumiwi kwa kunywa kwani yana harufu inayosadikika kuwa ni ya mafuta. Hata hivyo, wakati wa kiangazi kina mama (wenyeji) wanalazimika kuamka saa tisa alfajiri kutokana na uhaba wa maji, na kibaya zaidi usalama wao wakiwa njiani ni wa mashaka kwani hawapewi msaada na waume zao (kwa walioolewa). 

Ziara ya kutembelea kijiji inafika kwenye hospitali/kituo cha afya cha Kisanga. Kina Mama shujaa wa chakula wanashangaa kuambiwa bei kubwa ya matibabu katika kituo hicho, ambacho kwa siku ya leo kimefungwa. 

Zao kuu la Kisanga ni mihogo. Ziara ya kina Mama Shujaa wa Chakula inaishia katika kituo cha kusindika mihogo. Hapa kunasagwa unga wa mihogo, pia tambi na keki za unga wa mihogo zinatengenezwa hapa. 

Naam, muda wa makundi kuwasilisha mapendekezo ya mradi wa maendeleo endelevu waliopanga mbele ya wanakijiji wa Kisanga unawadia.

KUNDI LA KWANZA 

Kutoa elimu juu ya mazingira, Kuchimba mashimo ya taka. Wafanyabiashara wanawake walio barabarani wafunike chakula ili vumbi lisiingie.Wana Kisanga wote watahitajika kufanya usafi jumamosi.  Kuanzisha shamba darasa na kutoa elimu.

KUNDI LA PILI
Biashara cha mboga na matunda kwenye bonde (karibu na bwawa) kwa kutumia mbolea asili na maji yaliyopo. Kutoa elimu kwa kupitia shamba darasa jinsi ya kutumia rasilimali za kijiji kwa ajili ya maendeleo ya kijiji

KUNDI LA TATU
Mradi wa kilimo bora. Kilimo cha mbogamboga na kilimo cha mihogo na mahindi kwenye muinuko wa bonde. Wananchi kupewa elimu ya kilimo bora, kutumia wataalamu waliopo

Siku inaisha kwa waandaaji kupanga makundi matatu mapya ambayo watapewa kazi ambayo lazima iishe kesho hiyohiyo.

ILI KUMPIGIA KURA MSHIRIKI  BOFYA HAPA>>>