Pages

KAPIPI TV

Tuesday, July 21, 2015

WARSHA YA KUPUNGUZA VIFO NA MAJERUHI WA AJALI ZA BARABARANI YAFANYIKA JIJINI DAR-ES-SALAAM

????????????????????????????????????
Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano akifungua rasmi warsha ya waandishi wa habari ya kupunguza ajali na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la AMEND na kufadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya EU warsha hiyo imefanyika kwenye jengo la Umoja House jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Gianluca Azzon Mwakilishi wa EU Nchini Tanzania akiwasilisha mada katika warsha ya waandishi wa habari ya kupunguza ajali na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la AMEND na kufadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya EU warsha hiyo imefanyika kwenye jengo la Umoja House jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Tom Bishop kutoka shirika lisilo la Kiserikali la AMEND akiwasilisha mada katika warsha ya waandishi wa habari ya kupunguza ajali na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani iliyoandaliwa na shirika hilo na kufadhiliwa na Jumuiya ya umoja wa Ulaya EU warsha hiyo imefanyika kwenye jengo la Umoja House jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wataalamu na taasisi mbalimbali za serikali, Umoja wa Ulaya na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na waandishi wa habari wakifuatilia mada mbalimbali katika warsha hiyo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wataalamu na taasisi mbalimbali za serikali, Umoja wa Ulaya na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na waandishi wa habari wakifuatilia mada mbalimbali katika warsha hiyo.
????????????????????????????????????
Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano akimkabidhi cheti cha ushiriki wa warsha hiyo Mkurugenzi wa mtandao wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku.
????????????????????????????????????
Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano akimkabidhi cheti cha ushiriki wa warsha hiyo Kibuda Chalila Mwandishi mwandamizi wa Michuzi Media.
????????????????????????????????????
Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano akimkabidhi cheti cha ushiriki wa warsha hiyo Mwandishi wa habari wa magazeti ya serikali TSN Bi. Regina Kumba.
????????????????????????????????????
Washiriki wa Warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika warsha hiyo
????????????????????????????????????
Na Mwandishi Wetu
Imeelezwa kuwa suala la usalama barabarani ni ni jukumu la kikosi cha usalama barabarani hali ambayo jamii imejengeka na utamaduni huo na kusahau suala hilo ni jamii nzima katika mapambano ya kupunguza ajali za barabarani.

Hayo ameyasema leo Kamishina Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Johansen Kahatano wakati wa mafunzo kwa waandishi habari juu ya kuhabarisha jamii katika suala la usalama barabarani iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU)
Kahatano amesema kuwa kikosi cha usalama barabarani kimekuwa kikitoa elimu juu ya usalama barabarani kwa wananchi pamoja na madereva katika kuzingatia sheria zilizowekwa katika kuondokana na ajali zinazotokana na makosa ya kibinadamu.

Amesema jamii ikipata mwamko wa katika kutambua sheria za usalama barabarani kuna uwezekano wa kuondokana na ajali ambazo zinapoteza watu pamoja na kuacha watu wengine wakiwa na ulemavu wa kudumu.

“Kikosi cha usalama barabani pekee yake hakiwezi ni wakati umefika kwa jamii kuweka suala hili kwenye vichwa vyao kuwa wanamchango katika wa kusukuma gurudumu katika kupambana na ajali katika sehemu zao”amesema Kahatano.

Katika kuhamasisha masuala ya Usalama Barabarani ,Mwandishi wa Citizeni Mkinga Mkinga amesema ni wakati umefika kwa waandishi kutambua umuhimu wetu wa kutoa taarifa za kuelimisha wananchi juu ya usalama barabarani.

Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana na Tanzania katika mradi wa uboreshaji wa miundombinu katika mashule ili kuweza kuondokana na ajali za wanafunzi katika maeneo ya karibu na barabara.

"LEMBELI AITOSA CCM,AJIUNGA RASMI CHADEMA"


Aliyekuwa Mbunge wa Kahama kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), James David Lembeli (kushoto) akiingia ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Dar es Salaam leo asubuhi akiwa ameongozana na mtoto wake, Wizilya Lembeli wakati akienda kutangaza kuondoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama mkoani Shinyanga, James David Lembeli, akizungumza na waandishi wa habari Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Dar es Salaam leo asubuhi wakati akitangaza kuondoka katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Pamoja na kutangaza nia ya kugombea ubunge kupitia chama hicho.
 Lembeli akizungumza na wanahabari.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

Wanahabari wakimsikiliza Lembeli. Suleiman Msuya

Na Mwandishi Wetu

ALIYEKUWA Mbunge wa Kahama James Lembeli, amehamia rasmi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tukio hilo la kuhama lilifanyika jijini Dar es Salaam leo asubuhi katika Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza ambapo aliambatana na mwanae ambaye alijitambulisha kwa jina Wizilya James.

Akizungumzia uamuzi wake huo Lembeli alisema amekuwa ndani ya CCM kwa miaka yake yote lakini kutokana na vitendo vinavyofanyika ndani ya chama hicho ameaona akae pembeni.

Lembeli alisema, ndani ya CCM ili ufanikiwe kupita michakato yote sahihi ni lazima utoe rushwa au kuiba kura jambo ambalo yeye analipiga vita hivyo kutofautiana na viongozi wa chama ngazi ya Wilaya.

"Ndani ya CCM rushwa imekuwa ibada inasumu kali kuliko ukimwi hivyo nimeshindwa kuvumilia naona Chadema wana viashiria vinavyofanana na mimi ngoja tukafanye kazi," alisema Lembeli.

Alisema katika harakati za kupata wagombea katika jimbo la Kahama kila mwaka ni lazima rushwa itumike lakini chama kimekuwa kimya na kuwabeba wale watoa rushwa.

Mbunge huyo alisema ushahidi wa watu kutoa rushwa hasa katika kipindi hiki umeonekana lakini wahusika wameendelea na hatua zingine bila kukemewa.

"Mimi mwaka 2010 nilikuwa nimekatwa lakini huruma ya Rais Jakaya Kikwete nilirejeshwa sasa nimeona hakuna sababu ya kuendelea kulazimisha kama viongozi hawakutaki," alisema.

Alisema iwapo angechukua fomu CCM mkakati ambao ulikuwepo ni kumkata kwa kile ambacho wanaamini kuwa amekuwa akisimamia misimamo ambayo ina madhara kwa Serikali.

Lembele alisema kutokana na dhana hiyo ni vema aende katika chama ambacho kinaonekana kuwa wabunge wake wanauchungu na nchi yao na sio kubebana kusiko na sababu.

"Kufanya kosa sio kosa lakini kurudia kosa ni kosa kubwa sana hivyo siwezi kurudia kosa la 2010 hivyo huku Chadema ndiko sahihi," alisema.

Alisema ukiona mwenzako ananyolewa ni vema kujiandaa kwa kutia maji nywele jambo ambalo ameliona na ameamua kufanya hivyo.

"Siwezi kutoa rushwa kwa sababu sijafunzwa hivyo na hata wananchi wa Kahama wanajua kuwa mimi sio mtoa rushwa hivyo ukiwa hutoi rushwa CCM ni ngumu kukubalika jambo ambalo linafanya kuwa rushwa iwe mbaya kuliko ukimwi," aliongezea.

Akizungumzia kugombea ubunge kupitia Chadema, alisema atafanya hivyo kwani ukweli ni kuwa anakubalika kwa wananchi wote kutokana na misingi yake ya utumishi.

Alisema mpaka anafanya uamuzi huo ameshafanya utafiti ambapo anaamini kuwa atashinda tena kwa kishindo kwani wananchi wa jimbo hilo wanamkubali.

Lembeli alisema kimsingi jimbo la Kahama wapinzani wapo tangu yeye akiwa Mbunge, hivyo anaamini kuwa iwapo atafanikiwa kushinda hatapata wakati mgumu kufanya kazi.

"CCM imefanya mambo mengi ambayo kimsingi hayana afya ndani ya chama ukiwa wa kwanza kwa kura ndani ya CCM unakuwa wa mwisho hali ambayo inakatisha tamaa na hilo lilitokea 2010 na Chadema wakapata ushindi," alisema

Pia alisema amepokea simu na meseji nyingi ambazo kutoka kwa wananchi zinamtaka agombee kupitia chama Chadema hivyo pamoja na ukweli kuwa ni uamuzi mgumu ila hawezi kula matapishi.

Alisema ilimchukua masaa 10 kumuelezea mama yake juu ya uamuzi huo lakini baadae alielewa hivyo kwa sasa ana baraka zote za mama na familia kwa ujumla.

Kuhusu uhusiano na 4U Movement

Akizungumzia kuhusu uamuzi huo kuhusishwa na kundi la 4u Movement, alisema kimsingi kundi hilo analiona kupitia mitandoa ya kijamii ila hana uhusiano nalo na hahitaji kuwa katika hao.

Lembeli alisema wananchi wa Kahama ni watu makini wanajua nini cha kufanya hivyo uamuzi ambao watafanya utakuwa ni kwa uelewa wao na sio kwa msukumo wa kundi hilo linalotajwa kuwa ni wafuasi wa Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa.

Kuhusu Katiba iliyopendekezwa Lembeli alisema yeye ni muumini wa Serikali tatu na alionesha hilo katika vikoa vyote vya bunge lile ambapo alikuwa katika kamati namba moja.

Alisema kutokana na ukweli huo ni dhahiri kuwa ameenda chama ambacho wanafanana kifra kwani bila Serikali tatu hatma ya Tanzania itakuwa mashakani.

"Kwa hili siwezi kubadilika mimi msimamo wangu hadi leo ni Serikali tatu ambapo pia ni msimamo wa Chadema hivyo wengi ndio walishinda lakini mimi sio mmojawapo," alisema.

Aidha Lembeli alitumia muda huo kufafanua ni kwanini alitoa hoja ya kutaka Lowassa na wengine ambao wamekutana na majanga ndani ya bunge wasafishwe ambapo alisema haki haikutendeka kusafisha watu baadhi na wengine kuachwa.

Lembeli alisema katika taarifa ya Operasheni Tokomeza haikusema mawaziri fulani wanamakosa ila iliweka bayana kuwa kulinga na nafasi zao wanapaswa kuwajibika kisiasa.

Alisema mfumo wa kusafisha watu fulani na wengine kuwaacha sio mzuri kwani hauendani na misingi ya haki za binadamu ni ubaguzi.


Kwa upande wa mtoto wake wa pili Wizilya James Lembeli alisema wanamuunga mkono baba yao kwa uamuzi huo na kuwa wako nyuma yake.

Alisema uamuzi ambao amechukua baba yake ni mgumu hasa ukilinganisha na kipindi husika lakini hakuwa na njia nyingine kwani ni mtu wa siasa.

Akizungumzia ujio huo Ofisa Habari wa Chadema ambaye ndiye alimpokea Lembeli alisema kimsingi mwanachama huyo mpya alikiwa ni mpinzani kiroho hivyo hawana shaka naye.

Makene alisema wanaamini kuwa wamepata mtu ambaye anapenda mabadiliko kwani alionekana ndani ya bunge na nje kwa kusimamia rasilimali za nchi bila uoga.

Alisema Chadema itaendelea kupokea wanachama wapya kutoa CCM na vyama vingine hadi Julai 25 kwani lengo lao ni kuhakikisha kuwa nchi inafikia kwenye mabadiliko chanya.

Lembeli amekuwa Mbunge wa jimbo la Kahama, tangu mwaka 2005 hadi 2015 ambapo awali alikuwa  mwandishi na mtumishi katika shirika la Hifashi ya Taifa (Tanapa).

NEW MUSIC VIDEO : EMANUEL AUSTIN FEAT. BEN POL -RUKA JUU


MFAHAMU EMANUEL AUSTIN MTANZANIA MWANAMUZIKI AISHIYE UJERUMANI.

Emanuel  Austin alizaliwa 27.10.1990 Jijini Dar es salaam Tanzania, na ilipofika mwaka 1996  alihamia Ujerumani Kuishi na wazazi wake, Kipaji chake cha kucheza na kuimba kilianza kuonekana mapema.
Akiwa na Miaka mitano Emanuel Austin alianza kuigiza kama anacheza movie pamoja na rafiki zake wa Kiafrika akiwemo Gregory Msuya na Michael Jackson.  Alipofika umri wa Miaka 15 alianza kupenda na kuimba muziki wa Kugani yani ‘Hip hop’
Baadaye alitafuta baadhi ya wenzake ambao aliona wanaweza kuingia studio na kufanya muziki wa Kughani yaani Rap baadhi ya marafiki zake walikuwa ni pamoja na Miguel Amil Matos, Bernado Ernest na Patrick Kitchens ambapo kwa Mara ya kwanza walifanya vizuri.
Mnamo mwaka 2002 wazazi wake na Emanuel walianzisha Mradi mkubwa wa shule kwa ajili ya kufundisha Salsa huko Großkrotzenburg  jirani na  Frankfurt , ambapo yeye binafsi alijifunza Salsa na sasa amekuwa ni mwalimu mzuri wa Mtindo huo. Na kuanzia mwaka 2005 Emanuel  na baba yake wamekuwa wakiendesha programu ya kuwafundisha watoto salsa.
Kipaji cha nyota Mwanamuziki Emanuel Austin kilianza kuonekana wakati ameanza kuimba Lebo ya MarciRecords moja ya sehemu ambayo inawaunganisha wanamuziki mbalimbali na vijana ambao wanavipaji katika sanaa ya Muziki, akiwa huko Emanuel alishinda tuzo ya Msanii anayechipukia ndani ya Mji wa Hanau, Ujerumani  mwaka 2006.
Mwaka 2007 Emanuel alifanya video yake ya kwanza kupitia wimbo wake wa Put your hands up wimbo uliotoka katika album yake ya Put your Hands up, Album hiyo ilitengenezwa na Muandaaji wa Muziki Dj Verde.
Mwaka 2008 Emanuel alifanya ngoma nyengine ambapo alitoa audio pamoja na video , ngoma hiyo ilikwenda kwa jina la Master of the Game, chini ya usimamizi wa mwandaaji wa Muziki Axel Breitung hii ilikuwa ni nyimbo ambayo ilimuongezea umaarufu zaidi na kusikika katika chanel maarufu za Televisheni kama VIVA na MTV.
Kutokana na mafanikio hayo makubwa Emanuel alianza kuandaa matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na matamasha ya muziki , Mwaka 2008 Emanuel aliamua kufungua darasa la mafunzo ambapo ilikuwa ni Shule ya Muziki inayoitwa Tanzschule Weiss iliyopo Offenbach, ambapo wanafundisha Hip hop, Kuwafundisha watoto kucheza na Salsa Cubana na anampango wa kuanzisha shule ya Muziki Nchini Tanzania.
Kwa sasa Emanuel Austin anafanya kazi katika moja ya shule kubwa ya Muziki wa Dance nchini  Ujerumani  ambapo wachezaji maarufu wa Dance kama Don Omar wapo humo , hata hivyo Emanuel huja nyumbani Tanzania kila mwaka  na sasa Amekuja na ngoma mpya ambayo amemshirikisha Ben Pol inaitwa ruka juu.

Kufahamu zaidi juu ya Emanuel Austin   Mfuate hapa
.
www.instagram.com/emanuelaustinofficial 
www.facebook.com/emanuelaustin 
YouTube : Emanuel Austin 
Twitter: emanuelaustin27 

www.twitter.com/emanuelaustin27

"DOGO" AJITOSA UDIWANI KUPITIA CHADEMA KATA YA KORONGONI MJINI MOSHI.

Mpambanaji aliyejitambulisha kwa mwandishi wa blog hii kwa jina la Liberatus Oba Mawalla "Dogo" (pichani juu) amechukua na kurudisha fomu za kugombea udiwani kata ya Korongoni wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Amesema endapo atapata ridhaa hatapenda wamuite mheshimiwa na badala yake anataka wapiga kura wake wamuite ndugu. Angalia picha zaidi hapa chini

Dogo akiwa na wanachama hicho

Msafara kuelekea kurudisha fomu ukijipanga.

Hapa ni furaha tupu.

Dogo akiwa na vijana wa chama hicho.

Akisaini wakati akichukua fomu.

Hapa ni ushindi tu.


Msafara huo kurudisha fomu.

Ni alama ya vidole viwili chadema .



Ni furaha tu kwa kwenda mbele.




Dogo ndani ya mchuma akienda kurudisha fomu.

Ni kama wanasema ushindi ni lazima.

Msafara huo wa kwenda kurudisha fomu.

Dogo akipongezwa na vijana wenzake.

JERRY SLAA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UKONGA

IMG_9354
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akionyesha fomu aliyojaza kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote, wakati aliporejesha fomu hiyo katika ofisi za CCM wilaya ya Ilala aliyoikabidhi kwa Katibu Msaidizi wa CCM wilaya ya ILALA (kushoto).
Jerry Slaa aliongozana na Mwenyekiti wa tawi la Gulukakwalala ambako ndio nyumbani kwake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Gongo la Mboto pamoja na wazee wa jimbo la Ukonga.
IMG_9341
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kurejesha fomu yake ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote.
IMG_9348 IMG_9317
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi na wazee wa Ukonga aliombatana nao wakati wa kurejesha fomu.

Monday, July 20, 2015

MKUTANO WA MAGUFULI MJI MDOGO WA MGANZA FUNIKA BOVU

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa kata ya Kibehe wakati akiwa njiani kuelekeza Mganza kwenye mkutano wa hadhara wa kuwaaga wakazi wa mji mdogo wa Mganza sehemu ambayo safari yake ya Ubunge alioutumikia kwa miaka 20 ilianzia.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Kibehe wakati akiwa njiani kuelekeza Mganza kwenye mkutano wa hadhara wa kuwaaga wakazi wa kata ya Mganza sehemu ambayo safari yake ya Ubunge alioutumikia kwa miaka 20 ilianzia.


 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Nyisanzi wakati akiwa njiani kuelekeza Mganza kwenye mkutano wa hadhara wa kuwaaga wakazi wa kata ya Mganza sehemu ambayo safari yake ya Ubunge alioutumikia kwa miaka 20 ilianzia.
 Mgombea wa Urais wa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Nyisanzi ambapo aliwashukuru kwa muda wote aliowatumikia kama mbunge kwa miaka 20.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa kijiji cha Nyisanzi akiwa njiani kuelekea Mganza.
 Msafara wa mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye kata ya Mganza.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mji mdogo wa  Mganza
 Umati wa wakazi wa mji mdogo wa Mganza waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara ambapo mgombea wa Urais kupitia CCM aliwashukuru na kuwaaga kwa miaka 20 aliowatumikia kama Mbunge wao na kuwataka wananchi wachague Mbunge mchapakazi kama yeye.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Rajab Luhwavi akiwasalimu wakazi wa mji mdogo wa Mganza kabla ya kumkaribisha mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli kushukuru na kuwaaga wananchi hao.
 Mgombea wa Urais kwatiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dk.john Pombe Magufuli akiwasalimu wakazi wa Mganza kwenye mkutano wa kuwaaga baada ya miaka 20 ya kuwatumikia kama Mbunge wao.
 Wakazi wa mji mdogo wa Mganza wakimsikiliza mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli wakati wa kuwaaga baada ya kuwatumikia kama mbunge wao kwa miaka 20.



 Umati wa watu waliojitokeza kwenye mkutano wa Magufuli kwenye mji mdogo wa Mganza.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa kata ya Mganza ambapo aliwaaga rasmi baada ya kuwatumikia kwa miaka 20 kama mbunge wao.
 Wananchi wanaorudisha kadi zao za vyama vya upinzani wakiandikisha majina yao kwa mmoja wa viongozi wa CCM kata ya Mganzo.
 Mgombea wa Urais kwa kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akipokea kadi kutoka kwa wanachama wa vyama vya upinzani ambapo zaidi ya wanachama 150 walirudisha kadi za vyama vyao na kujiunga na CCM.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM akiwaaga wakazi wa mji mdogo wa Mganza mara baada ya kumaliza mkutano wa kuwaa

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, PAUL MAKONDA KUSOMESHA YATIMA 12

MKUU wa Wilaya  ya Kinondoni,  Paul Makonda (pichani), ameahidi kusomesha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu 12, ikiwa ni kuwalipia ada  za shule.

Hayo aliyabainisha Dar es Salaam jana wakati  Kampuni ya Simu za mkononi Zantel ikikabidhi kisima cha maji safi katika kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo  Mbezi Suka jijini Dar es Salaam.

Watoto hao 12, ambapo 8 kati yao wana elimu ngazi ya sekondari huku 3 wakitakiwa kwenda chuo kikuu na 1 kuahidiwa endapo atafaulu kidato cha nne sanjari na kuongea na mifuko ya hifadhi za jamii kuona jinsi gani wanaweza kusaidia kundi hilo katika huduma za afya.

Makonda alisema familia ni chanzo cha kuongeza idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu kutokana na ugumu wa maisha, kuoana katika umri mdogo na uelewa mdogo wa maana ya familia.

"Familia ni chanzo kizuri cha kuongeza au kupunguza idadi ya watoto wa mitaani, familia nyingi hazina uvumilinu ndani ya ndoa zao...msijitazame kama yatima kwasababu hamtaweza kuwa na maendeleo mazuri,"alisema Makonda.

Kwaupande wake Mkurugenzi mtendaji Kampuni ya  Zantel, Pratap Ghose alisema kampuni hiyo imekuwa ikionesha jitihada za kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenye jamii inayoizunguka.

"Kampuni yetu inalenga kugusa maisha ya wananchi  wanaotuzunguka, na ndio maana tumeamua kutoa msaada wa kisima ili kiweze kukisaidia kiyuo hiki kumaliza moja ya matatizo yaliyokuwa yanawakabili kwa muda mrefu,"alisema Ghose.

Mkuu wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Evance Tegete alisema awali kituo kilikuwa kinategemea maji kutoka Dawasco ambayo upatikanaji wake ulikuwa si wa uhakika, hivyo wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuwachimbia kisima hicho. 

Kituo cha Watoto Wetu tanzania kilianzishwa mwaka 2001,ambapo hadi sasa kina watoto 70, kuanzia umri wa miaka 5 hadi 25 kutoka mikoa mbalimbali kikiwa na lengo la kuhakikisha watoto wasio na wazazi au walezi wanapata matunzo na elimu bora.  ((Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba-0712-727062)