Pages

KAPIPI TV

Tuesday, July 21, 2015

JERRY SLAA AREJESHA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UKONGA

IMG_9354
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akionyesha fomu aliyojaza kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote, wakati aliporejesha fomu hiyo katika ofisi za CCM wilaya ya Ilala aliyoikabidhi kwa Katibu Msaidizi wa CCM wilaya ya ILALA (kushoto).
Jerry Slaa aliongozana na Mwenyekiti wa tawi la Gulukakwalala ambako ndio nyumbani kwake, Mwenyekiti wa CCM kata ya Gongo la Mboto pamoja na wazee wa jimbo la Ukonga.
IMG_9341
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kurejesha fomu yake ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 Mwaka huu nchini kote.
IMG_9348 IMG_9317
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM taifa, Jerry William Silaa akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi na wazee wa Ukonga aliombatana nao wakati wa kurejesha fomu.

Monday, July 20, 2015

MKUTANO WA MAGUFULI MJI MDOGO WA MGANZA FUNIKA BOVU

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa kata ya Kibehe wakati akiwa njiani kuelekeza Mganza kwenye mkutano wa hadhara wa kuwaaga wakazi wa mji mdogo wa Mganza sehemu ambayo safari yake ya Ubunge alioutumikia kwa miaka 20 ilianzia.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Kibehe wakati akiwa njiani kuelekeza Mganza kwenye mkutano wa hadhara wa kuwaaga wakazi wa kata ya Mganza sehemu ambayo safari yake ya Ubunge alioutumikia kwa miaka 20 ilianzia.


 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Nyisanzi wakati akiwa njiani kuelekeza Mganza kwenye mkutano wa hadhara wa kuwaaga wakazi wa kata ya Mganza sehemu ambayo safari yake ya Ubunge alioutumikia kwa miaka 20 ilianzia.
 Mgombea wa Urais wa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Nyisanzi ambapo aliwashukuru kwa muda wote aliowatumikia kama mbunge kwa miaka 20.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa kijiji cha Nyisanzi akiwa njiani kuelekea Mganza.
 Msafara wa mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye kata ya Mganza.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mji mdogo wa  Mganza
 Umati wa wakazi wa mji mdogo wa Mganza waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara ambapo mgombea wa Urais kupitia CCM aliwashukuru na kuwaaga kwa miaka 20 aliowatumikia kama Mbunge wao na kuwataka wananchi wachague Mbunge mchapakazi kama yeye.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Rajab Luhwavi akiwasalimu wakazi wa mji mdogo wa Mganza kabla ya kumkaribisha mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli kushukuru na kuwaaga wananchi hao.
 Mgombea wa Urais kwatiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dk.john Pombe Magufuli akiwasalimu wakazi wa Mganza kwenye mkutano wa kuwaaga baada ya miaka 20 ya kuwatumikia kama Mbunge wao.
 Wakazi wa mji mdogo wa Mganza wakimsikiliza mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli wakati wa kuwaaga baada ya kuwatumikia kama mbunge wao kwa miaka 20.



 Umati wa watu waliojitokeza kwenye mkutano wa Magufuli kwenye mji mdogo wa Mganza.
 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa kata ya Mganza ambapo aliwaaga rasmi baada ya kuwatumikia kwa miaka 20 kama mbunge wao.
 Wananchi wanaorudisha kadi zao za vyama vya upinzani wakiandikisha majina yao kwa mmoja wa viongozi wa CCM kata ya Mganzo.
 Mgombea wa Urais kwa kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akipokea kadi kutoka kwa wanachama wa vyama vya upinzani ambapo zaidi ya wanachama 150 walirudisha kadi za vyama vyao na kujiunga na CCM.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM akiwaaga wakazi wa mji mdogo wa Mganza mara baada ya kumaliza mkutano wa kuwaa

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, PAUL MAKONDA KUSOMESHA YATIMA 12

MKUU wa Wilaya  ya Kinondoni,  Paul Makonda (pichani), ameahidi kusomesha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu 12, ikiwa ni kuwalipia ada  za shule.

Hayo aliyabainisha Dar es Salaam jana wakati  Kampuni ya Simu za mkononi Zantel ikikabidhi kisima cha maji safi katika kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo  Mbezi Suka jijini Dar es Salaam.

Watoto hao 12, ambapo 8 kati yao wana elimu ngazi ya sekondari huku 3 wakitakiwa kwenda chuo kikuu na 1 kuahidiwa endapo atafaulu kidato cha nne sanjari na kuongea na mifuko ya hifadhi za jamii kuona jinsi gani wanaweza kusaidia kundi hilo katika huduma za afya.

Makonda alisema familia ni chanzo cha kuongeza idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu kutokana na ugumu wa maisha, kuoana katika umri mdogo na uelewa mdogo wa maana ya familia.

"Familia ni chanzo kizuri cha kuongeza au kupunguza idadi ya watoto wa mitaani, familia nyingi hazina uvumilinu ndani ya ndoa zao...msijitazame kama yatima kwasababu hamtaweza kuwa na maendeleo mazuri,"alisema Makonda.

Kwaupande wake Mkurugenzi mtendaji Kampuni ya  Zantel, Pratap Ghose alisema kampuni hiyo imekuwa ikionesha jitihada za kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenye jamii inayoizunguka.

"Kampuni yetu inalenga kugusa maisha ya wananchi  wanaotuzunguka, na ndio maana tumeamua kutoa msaada wa kisima ili kiweze kukisaidia kiyuo hiki kumaliza moja ya matatizo yaliyokuwa yanawakabili kwa muda mrefu,"alisema Ghose.

Mkuu wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Evance Tegete alisema awali kituo kilikuwa kinategemea maji kutoka Dawasco ambayo upatikanaji wake ulikuwa si wa uhakika, hivyo wanaishukuru kampuni hiyo kwa kuwachimbia kisima hicho. 

Kituo cha Watoto Wetu tanzania kilianzishwa mwaka 2001,ambapo hadi sasa kina watoto 70, kuanzia umri wa miaka 5 hadi 25 kutoka mikoa mbalimbali kikiwa na lengo la kuhakikisha watoto wasio na wazazi au walezi wanapata matunzo na elimu bora.  ((Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba-0712-727062)

DC WA KINONDONI, PAUL MAKONDA AZINDUA KISIMA CHA MAJI SAFI KATIKA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA WATOTO WETU TANZANIA KILICHOJENGWA NA KAMPUNI YA SIMU YA ZANTEL.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (katikati), akimkaribisha  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakati akiwasili kwenye hafla ya kuzindua kisima cha maji safi katika Kituo cha Watoto Yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka Dar es Salaam jana.

DC Makonda akisaini katika kitabu cha wageni katika kituo hicho.
Mmoja wa vijana wa kituo hicho akiigiza igizo kuonesha changamoto zinazowakabili watoto waishio katika mazingira hatarishi.
Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Evans Tegete (kulia), akizungumza katika hafla ya kuzindua kisima hicho. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose na  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Naibu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Theobard Bubelwa (kulia), akiteta jambo na Chief Commerial Officer wa Zantel, Sukwinder Bajwa wakati wa hafla hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Pratap Ghose (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Watoto wa kituo hicho na wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Watoto wa kituo hicho wakitoa burudani.
DC Makonda akipokea risasi ya watoto wa kituo hicho.
Vijana wa kituo hicho wakitoa burudani.

DC Makonda akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alitoa ahadi ya kuwasomesha baadhi ya wanafunzi wa kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, akifungua pazia wakati akizindua kisima cha maji katika Kituo cha Yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka Dar es Salaam jana. Kisima hicho kimejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Simu ya Zantel.
DC Makonda akifungua bomba kuashiria uzinduzi wa kisima hicho.
Hapa DC Makonda akimtwisha maji mmoja wa wanafunzi wa kituo hicho baada ya kukizindua.
DC Makonda akimkabidhi kitabu, mtoto Yusla Omari kwenye uzinduzi huo.
DC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na timu nzima ya kituo hicho.



Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Simu ya Zantel jana ilitoa msaada wa kisima cha maji kwa watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania,ikiwa na lengo la kumaliza tatizo la maji na kuhakikisha  upatikanaji wa maji safi na salama kwa takribani watoto 70 wa kituo hicho.
Tatizo la maji ni moja ya matatizo sugu katika mkoa wa Dar es salaam pamoja na Tanzania kwa ujumla hivyo msaada huu ni wa muhimu kwa watoto wa kituo hicho.
Kisima hicho kilichokabidhiwa jana kitatoa maji safi na salama na yaliyotayari kwa matumizi ambayo yatawasaidia watoto kuepukana na maradhi yanayosababishwa na maambukizi ya maji yasiyo salama na machafu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zantel, Pratap Ghose alisema kampuni ya Zantel imekuwa siyo tu ikitoa huduma bora na zenye unafuu kwa wateja wake bali pia imekuwa ikifanya jitihada za kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwenye jamii inayoizunguka

‘Kampuni yetu inalenga kugusa maisha ya wananchi wanaotuzunguka, na ndio maana tumeamua kutoa msaada huu wa kisima ili kiweze kukisaidia kituo hiki kumaliza moja ya matatizo yaliyokuwa yanawakabili kwa muda mrefu’ alisema Pratap.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika shughuli ya makabidhiano hayo, aliipongeza kampuni ya Zantel kwa msaada huo akisema ni ishara inayofaa kupongezwa.

‘Ustawi wa watoto na vijana ni jambo muhimu katika jamii, hivyo nakipongeza kituo hiki kwa kazi kubwa wanayofanya, na pia kampuni ya Zantel kwa kulikumbuka kundi hili muhimu katika jamii, na ninatoa wito kwa makampuni mengine kushiriki na kusaidia kituo hiki’ alisema Makonda.

Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Suka jijini Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 2001, kwa lengo la kuhakikisha watoto wasio na wazazi au walezi wanapata matunzo na elimu bora.

Akitoa neno la shukurani Mkuu wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania,Evance Tegete alisema awali kituo kilikuwa na tatizo kubwa la maji, lakini sasa shukrani kwa Zantel tatizo hilo limemalizika.


‘Awali tulikuwa tunategemea maji kutoka DAWASCO ambayo upatikanaji wake si wa uhakika,tunawashukuru Zantel wameweza kutusaidia kutatua tatizo hili’ alisema Tegete. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

KALUNDE BAND KATIKA UBORA WAO, WAFANYA KWELI KLABU YA GMB MBEZI

????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi akiimba wakati bendi hiyo ilipotumbuiza katika klabu ya GMB Mbezi jijini Dar es salaam Maarufu kwa Mbaga katika siku ya pili ya sikukuu ya Idd , kulia ni mwanamuziki Bijuu wa bendi hiyo.
????????????????????????????????????
Wanamuziki wa bendi hiyo wakiimba katika onesho hilo lililofanyika kwenye klabu ya GMB Mbezi jijini Dar es salaam.
???????????????????????????????????? ????????????????????????????????????
Mwanamuziki Debora Nyangi wa pili kutoka kulia mwimbaji na Meneja wa bendi hiyo akioongoza waimbaji wenzake wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitumbuiza jana kwenye klabu ya GMB Mbezi.
????????????????????????????????????
Mwanamuziki wa bendi hiyo Bijuu akiimba huku wanenguaji wakifanya vitu vyao.
????????????????????????????????????
Mwanamuziki wa bendi ya Kalunde Gringo Junior kushoto akishoo Love na wadau wa bendi hiyo Teddy Mwanambilimbi katikati na Fina Mwanambilimbi kulia.
????????????????????????????????????
Gringo Junior akifanya vitu vyake jukwaani.
????????????????????????????????????
Wangenguaji wa bendi hiyo wakifanya vitu vyao jukwaani.

Saturday, July 18, 2015

STARTIMES YAKABIDHI MSAADA WA CHAKULA SHULE YA MSINGI MAALUMU YA AIRWING JIJINI DAR ES SALAAM

Kutoka kulia ni wafanyakazi wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Elena Liu na Paulina Kaka wakifurahia jambo pamoja na Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili, Bw. Issa Mkasa wakati wa kukabidhi msaada wa vyakula na mahitaji mengineyo shuleni hapo. Akishuhudia tukio hilo kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Bi. Fabiola Malisa.
Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (mwenye hijab) akikabidhi moja ya msaada wa chakula na mahitaji mengineyo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Airwing, kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili kwa niaba ya wafanyakazi wa kampuni hiyo. Wakishuhudia tukio hilo kutoka wa pili kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Bi. Fabiola Malisa na Mwalimu wa Kitengo hiko, Bw. Issa Mkasa.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Bi. Fabiola Malisa (kushoto) akifurahia jambo pamoja na Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kulia) wakati wa kukabidhi msaada wa vyakula na mahitaji mengineyo kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kitengo maalum cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili shuleni hapo. Akishuhudia tukio hilo katikati ni  Mwalimu wa Kitengo hiko, Bw. Issa Mkasa.
Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (mwenye hijab) akikabidhi moja ya msaada wa chakula na mahitaji mengineyo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Airwing, kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili kwa niaba ya wafanyakazi wa kampuni hiyo. Wakijumuika pamoja naye katika tukio hilo wa pili kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Bi. Fabiola Malisa na wa pili kushoto ni Mwalimu wa Kitengo hiko, Bw. Issa Mkasa.


Na Mwandishi Wetu 

Serikali yaombwa kutilia mkazo kuhakikisha kila shule ya msingi inakuwa na kitengo maalumu cha wanafunzi wenye ulemavu wa viungo mbalimbali ili kuwapatia na wao fursa ya kupata elimu.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Shule ya Msingi ya Airwing, Bi. Fabiola Malisa wakati wa kupokea msaada wa chakula na mahitaji mengineyo kutoka kwa wafanyakazi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa ajili ya kitengo maalumu cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili.

Bi. Malisa alisema kuwa shuleni kwake wanacho kitengo cha kuwafundisha wanafunzi wenye ulemavu wa akili ambao kwa sasa wapo jumla ya 65, wanafunzi 20 ni wasichana na wanafunzi 45 ni wavulana.

“Hapa kitengo maalumu cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili ukiachana na wanafunzi wengine wa kawaida. Kwa sasa tunalo darasa moja ambalo tunawafundishia kwa kupeana amu na wanafunzi wa darasa la pili. Yaani wao wanaingia asubuhi na kutoka saa tano baada ya hapo wanafunzi wengine hulitumia hilo darasa. Tumeamua kufanya hivi kutokana na uhaba wa madarasa wenyewe.” Alisema Bi. Malisa

“Kuanzishwa kwa kitengo hiki lengo ni kuwafundisha watoto hawa wenye ulemavu wa akili nao waweze kupata stadi mbalimbali za kujumuika pamoja na jamii inayowazunguka. 

Jamii hudhani kuwa motto akizaliwa na ulemavu wa aina yeyote ile anakuwa ni mtu tegemezi. Sisi tunakanusha suala hilo kwani tunao hapa ambao tunawafundisha na wengi wameonyesha maendeleo mazuri. Kwa mfano kuna ambao baada ya kumaliza vipindi darasani hurudi wenyewe majumbani na hata kuja wenyewe shuleni kila siku.” Alisema na kuongezea Bi. Malisa

“Sisi kama uongozi wa shule tunajitahidi kadiri ya uwezo wetu kuwasaidia watoto hawa ili wajitambue na kuweza kuishi na jamii. Na tumefanikiwa kwa hilo, kwa mfano tunao wanafunzi wawili ambao baada ya kufundishwa kwenye kitengo hiki na kuonyesha maendeleo mazuri wamejiunga na wanafunzi wa kawaida, mmoja yuko darasa la saba na mwengine la nne,” alisema na kuongezea Mwalimu Mkuu, “Na tena wanasoma bila shida yoyote na wanafunzi wengine wamewazoea wanasoma pamoja nao.”

“Changamoto kubwa tunayokumbana nayo nib ado tuna uhaba wa madarasa kama nilivyoelezea awali tunatumia darasa kwa awamu. Kwani wao wanahitaji muda zaidi tofauti na wanafunzi wa kawaida. Japokuwa tunapokea msaada kutoka serikalini, kwa makampuni na taasisi zingine bado hautoshi. Tunaomba serikali itilie mkazo zaidi kwa kila shule kuwepo na kitengo cha namna hii kwani hali hiyo itapelekea wazazi kutowaficha watoto majumbani. Pia vituo hivi huwapunguzia wazazi mzigo mkubwa wa kuwalea kwani huwa salama mahali hapa na kuwafanya wao kufanya shughuli zingine za kujenga taifa.” Alihitimisha Bi. Malisa

Naye kwa upande wake akiongea kwa niaba ya wafanyakazi, Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amesema kuwa wao kama kama kampuni na watanzania wameguswa sana na ustawai watoto hawa ambao jamii huwachukilia tofauti.

“Bado watanzania tunayosafari ndefu ya kubadili mtazamo juu ya watoto wenye ulemavu. Tunatakiwa kuondoa dhana ya bado kufikiria ukiwa na motto mlevu basi atakuwa tegemezi kwa maisha yake yote duniani. Ulemavu unatofautiana na ule ambao unaweza kutibika watoto hawa wasaidiwe. Lakini jambo hili halitowezekana kama serikali haitojenga vituo hivi kwenye kila shule ya msingi na pia wadau nao kujitokeza kuziunga mkono.” Alisema Bi. Hanif

“Na kusema ukweli mahitaji ambayo yanahitajika katika shule hizi yamo ndani ya uwezo wetu watanzania. Bado tunahitaji mwamko wa kutosha kwani si wazazi wote wanao uwezo wa kumudu gharama za kuwahudumia watoto wenye ulemavu. 

Tumekuja hapa tumezungumza na walimu wametupa hali halisi kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi hawa uwezo wao ni mdogo hivyo wanahitaji misaada yetu,” alisema na kumalizia Bi. Hanif, “Hivyo basi kwa msaada wetu huu ambao sisi wafanyakazi wa StarTimes tumejikusanya na kuutoa, tunatarajia pia makampuni na taasisi nyingine wataiga na kufanya hivyo. Ni jukumu letu sote kuwasaidia na kuwalea watoto hawa kwani Mungu ana makusudio yake kuwaumba hivi.”


Msaada wa wafanyakazi wa StarTimes Tanzania uliotolea kwa kitengo hiko cha wanafunzi wenye ulemavu wa akili shuleni Airwing ni pamoja na sukari, mikate, majani ya chai, blueband, chumvi, sabuni za unga na mche, vibiriti, na mengineyo. Msaada huo umelenga kuwahudumia wanafunzi hao kwa muda ambao wapo shuleni na kwa wazazi na walezi wa wanafunzi hao. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)