Pages

KAPIPI TV

Wednesday, July 1, 2015

UN TANZANIA YAKUSANYA MAONI KUHUSU UTENDAJI WAKE NCHINI NDANI YA SABASABA KARUME HALL

IMG_5730
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimwelekeza Mkurugenzi wa kampuni ya Events World, Dimo Debwe Mitiki, jinsi ya kuwasilisha maoni yake kuhusiana na kazi za Umoja wa Mataifa na nini angependa Umoja huo ufanye zaidi kwa ajili ya watanzania kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”. (Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
IMG_5736
IMG_5779
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimwelekeza mmoja wa wananchi aliyetembelea la Umoja huo jinsi ya kuwasilisha maoni yake kuhusiana na kazi za Umoja wa Mataifa na nini angependa Umoja huo ufanye zaidi kwa ajili ya watanzania.
IMG_5793
Laurean Kiiza (kushoto) kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), akimsimia Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige kuwasilisha maoni (GeoPoll) yake moja kwa moja kwenye simu ya kiganjani, alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam.
IMG_5772
Mdau wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Lemmy Hipolite (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi na Meneja mradi wa TUBEGA ART ambaye ni mtaalamu wa sanaa za uchoraji, Amos Mtambala, jinsi alivyowezeshwa na Umoja huo kupitia Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupata elimu inayomwezesha kuwa mjasiriamali kwa kuuza michoro hiyo ndani ya banda la Umoja wa Mataifa.
IMG_5710
Mkurugenzi na Meneja mradi wa TUBEGA ART ambaye ni mtaalamu wa sanaa za uchoraji, Amos Mtambala, akionyesha baadhi ya kazi zake kwa wananchi waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.
IMG_5764
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akitoa maelezo ya maeneo mbalimbali yaliyofanikiwa katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDAP) kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa na kutaka kufahamu shughuli mbalimbali za UN Tanzania.
IMG_5744
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimkabidhi makabrasha na vipeperushi mbalimbali vya Umoja Mataifa, Mwandishi wa Michuzi blog, Chalila Kibuda aliyetembelea banda hilo kwenye maonyesha ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
IMG_5701
Sophia Mataro (wapili kushoto) kutoka Shirika la UNESCO Tanzania, akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini kwa mmoja wa wananchi alitembelea banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.
IMG_5717
Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na kituo cha Televisheni cha Channel Ten kilichotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba yanaoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam.
IMG_5802
Timu ya wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa "Delivering as One" wanaotoa huduma kwenye banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara kimataifa maarufu kama “Sabasaba” yanayoendelea kurindima jijini Dar es Salaam.
IMG_5738
Muonekano wa nje wa banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Na Modewji blog team
Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania limetoa nafasi ya kipekee kwa watanzania kutoa maoni yao wakati wa kipindi hiki cha maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam, yaliyoanza kurindima Juni 28, huku wakikusanya maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi juu ya utendaji wake kwa wanaotembelea kwenye maonyesho hayo kila siku.
Aidha, katika kupokea maoni hayo, UN imeweka utaratibu wa moja kwa moja kwa wananchi kufika kwenye banda lao na kutoa maoni yao, ambayo yanaenda moja kwa moja kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini Alvaro Rodriguez.
Njia nyingine ya kuwasilisha maoni ya moja kwa moja ni kupitia mtandao wa (Online) kwa kuingia http://gpl.cc/UN2
Kupitia linki hiyo, mtumiaji anaweza kutumia simu yake ya smartphone, laptop na vifaa vingine vya kielektroniki.
Njia nyingine ni ya kutumia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055.
Na kwa njia ya tatu ni kuwasilisha namba ya simu na majina na ujumbe unaotaka na UN wataufanyia kazi.
Aidha, maoni hayo yatakuwa yakipokelewa kwa kipindi chote cha SabaSaba, hivyo wananachi wameombwa kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao ya nini UN wakifanye nchini pamoja na mambo mengine.

Tuesday, June 30, 2015

WAZIRI NYALANDU AZINDUA KAMPENI YA UHAMASISHAJI WATANZANIA KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA

????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko na Utalii wa TANAPA Bw. Ibrahim Musa wakati alipowasili kwenye klabu ya Yacht ya Mwanza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji watanzania kutembelea Mbuga za Taifa iliyozinduliwa leo jijini Mwanza ikiwashirikisha Bodi ya Utalii Tanzania TTB, Katika Picha kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA Dr. Allan Kijazi.
Kampeni hiyo ambayo inaanza kesho Julai 1 itakuwa ni ya miezi 6 mpaka Desema 31 na kauli mbiu yake inasema "Tembelea Hifadhi Uzawadiwe".(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MWANZA)
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA Dr. Allan Kijazi akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bi. Devotha Mdachi wakati wa uzinduzi huo.
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA Dr. Allan Kijazi akifuatana na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu wakati alipowasili kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji Watanzania kutembelea Mbuga za taifa kulia ni Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA Bw. Ibrahim Mussa.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akiongozana na Mkurugenzi wa Masoko na Utalii TANAPA Bw. Ibrahim Mussa na Johnson Manase Meneja wa Utalii TANAPA.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wahariri wakiwa katika uzinduzi huo
????????????????????????????????????
Baadhi ya wahariri wakiwa katika uzinduzi huo
????????????????????????????????????
Baadhi ya maofisa wa TANAPA wakiwa katika uzinduzi huo
????????????????????????????????????
Wahariri wakifuatilia matukio mbalimbali katika uzinduzi huo
????????????????????????????????????
Mwandishi Jimmy Mengere na Kasilda Mrimira wakiperuzi simu zao wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii akiwa katika meza kuu wakati hotuba za viongozi mbalimbali zikiendelea kulia ni Mkurugenzi wa TANAPA Dr. Allan Kijazi na kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TTB Bi. Devotha Mdachi, Mkurugenzi wa Masoko na Utalii TANAPA Bw. Ibrahim Mussa na Katibu Tawala wa mkoa wa Mwaza Bw. Faiza Issa.
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Masoko na Utalii TANAPA Bw. Ibrahim Mussa akizungumzia kampeni hiyo.
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa TANAPA Dr. Allan Kijazi akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Mwanza leo.
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Masoko na Utalii TANAPA Bw. Ibrahim Mussa kulia na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bi. Devotha Mdachi wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
????????????????????????????????????
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Bw. Faiza Issa akimkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu ili kuzungumza katika uzinduzi huo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya magari ya kubeba watalii yaliyozinduliwa leo katika kampeni hiyo iliyozinduliwa jijini Mwanza.
????????????????????????????????????
Waziri Nyalandu akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo
????????????????????????????????????
Waziri Nyalandu akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo na kuwaasa wanafunzi wa vyuo vikuu kushiriki kikamilifu katika Kampeni hiyo
????????????????????????????????????
Waziri Nyalandu akikata utepe kuzinduz boti maalum za kubeba watalii kutoka jijini Mwanza kuelekea kisiwa cha Saanane kwa ajili ya kujionea utalii ulioko katika kisiwa hicho.
????????????????????????????????????
Waziri Nyalandu akiwaaga baadhi ya watalii wa ndani waliokuwa wakiondoka na boti kuelekea kiswa cha Sanane kilichopo mkoani Mwanza.
????????????????????????????????????
Boti iliyobeba watalii hao wa ndani ikiondoka jijini Mwanza kuelekea kisiwa cha Sanane
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa magari ya kubeba watalii jijini Mwanza katika mpango wa kampeni ya kuhamasisha watanzania kutembelea mbuga za taifa.
????????????????????????????????????
Waziri Nyalandu akipiga picha ya pamoja na wahariri wa vyombo vya habari mara baada ya kuzindua magari ya kubebea watalii jijini Mwanza.
????????????????????????????????????
Waziri Nyalandu akiwaaga watalii hao wakati walipokuwa wakiondoka.
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA Dr. Allan Kijazi na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu wakipiga picha ya pamoja na kupongezana mara baada ya uzinduzi huo.
???????????????????????????????????? Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA Dr. Allan Kijazi akiwaaga watalii hao wakati walipokuwa waiondoka.

USAFIRI UNAOTUMIKA KUSAFIRISHA ABIRIA MKOANI GEITA ENEO LA BUSERESERE NI HATARISHI

Gari Aina ya Pro Box Ikiwa tayari kusafirisha abiria
 Wakazi wa Mkoa wa Geita maeneo ya buseresere na katoro wapo katika hatari kubwa ya maisha yao kutokana na usafiri wanaoutumia kutoka eneo moja kwenda jingine.Mwakilishi wa kikundi cha usalama barabarani Fungo Agustus ametutumia Tukio hili ambalo ni hatari kwa abiria mkoani Geita.Gari ndogo aina ya Pro Box zimeingia kwa wingi mkoani Geita na kutumika kubebea abiria katika mazingira ambayo si salama na ni hatarishi kwa abiria hao.Abiria wamekuwa wakipakiwa kwenye mabuti ya kuwekea mizigo tena kwa msongamano mkubwa.Zifutazo chini ni picha za kinachoendelea kwenye usafirishaji eneo la Buseresere.                         


 Abiria wakiwa wamekusanywa kwenye buti eneo la kubebea mizigo huku wakiwa sambaba na watoto wadogo.
 Aina nyingine ya Gari ndogo inayotumika kubebea abiria
 Mizigo na Watoto wakiwa wamekusanywa pamoja na mizigo nyuma ya Gari hiyo

MKUU WA MAJESHI MSTAAFU JENERARI SARAKIKYA APEWA TUZO YA HESHIMA NA TANAPA KWA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO MARA 38

????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu aki mkabidhi tuzo maalum ya heshima Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerari Sarakikya akiwa na mkewe kwa kupanda mlima Kilimanjaro mara 38, Jenerari Sarakikya pia amepewa Kadi maalum ya kuingia mbuga zozote za TANAPA Bure yeye pamoja na familia yake lakini ambapo katika hatua nyingine atalipiwa gharama zote za kushiriki mkutano wa masuala ya utalii kuhusu milima mirefu zaidi duniani yeye pamoja na mke wake huko nchini Marekani, Katika mkutano huo Jenerari Sarakikya anatarajiwa kutoa mada kuhusu mlima Kilimanjaro.
Jenerari Mrisho Sarakikya amekabidhiwa tuzo hiyo katika hafla ya utoaji wa tuzo za TANAPA za waandishi wa habari za utalii iliyofanyika kwenye hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo ambapo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wamepewa tuzo hizo.
Katika picha kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MWANZA)
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo za TANAPA za waandishi wa habari kwenye hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu katikati, Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi wa TANAPA na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Mwanza kwenye hoteli ya Gold Crest.
????????????????????????????????????
Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi wa TANAPA akizungumza katika hafla hiyo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu wa pili kutoka kulia akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru wa tatu kutoka kulia, Kutoka kushoto ni Devotha Mdachi Kaimu Mkurugenzi wa (TTB), Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Ndugu Baraka Konisaga na Kushoto ni Mkurugenzi wa TANAPA Dr. Allan Kijazi.
????????????????????????????????????
Theophil Makunga Mhariri Tendaji wa Jambo Leo akisoma jina la mmoja wa washindi katika hafla hiyo, Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga na Mkurugenzi wa TTB Bi. Devotha Mdachi.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Humphrey Mganga mwandishi bora wa habari za utalii katika magazeti katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Fredy Sikagonamo mwandishi bora wa habari za utalii vipindi vya redio katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Magessa Maggesa mwandishi bora wa habari za utalii kwa vipindi vya Televisheni kutoka Stars TV katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Jimmy Mengere kutoka Chanel Ten Morogoro mwandishi bora wa habari za utalii kwa habari za Utalii aliyeandika kuhusu wanyama wanavyouwawa kwa ajali katika mbuga ya Mikumi.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Kasilda Mrimila Mwandishi bora wa habari za utalii za Televisheni kutoka Star TV Morogoro kwa kuandika kukauka kwa mto Ruaha Mkuu , kulia ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Jackson Kalindimya Mwandishi bora wa habari za Utalii Magazeti katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Frank Leonard
????????????????????????????????????
Baadhi ya wakuu wa vitengo wa mamlaka ya hifadhi za taifa TANAPA wakiwa katika hafla hiyo kulia ni Mkuu wa Mawasiliano Pascal Shelutete na na wa pili ni Ibrahim Mussa Mkurugenzi wa Masoko na Utalii TANAPA.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu katikati akiwa na viongozi wengine katika hafla hiyo kulia ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA , kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga na katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru.
????????????????????????????????????
Meneja wa Mawasiliano TANAPA Bw. Pascal Shelutete akitoa utaratibu wa utoaji wa tuzo hizo.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akitambulishwa katika hafla hiyo.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerari Mrisho Sarakikya na mkewe wakitambulishwa katika hafla hiyo.
????????????????????????????????????
Mwimbaji Mariam akitumbuiza katika hafla hiyo
????????????????????????????????????
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga akizungumza katika hafla hiyo
????????????????????????????????????
Jaji mkuu wa tuzo hizo Dkt. Ayoub Rioba akitambulisha majaji wenzake waliofanya kazi ya kutafuta washindi wa tuzo hizo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Wanenguaji wa bendi ya Utalii wakitumbuiza katika hafla hiyo
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akipiga picha ya pmaoja na washindi.