Pages

KAPIPI TV

Thursday, May 14, 2015

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUEPUKA LUGHA ZA CHUKI

Meza kuu. (Picha zote na Geofrey Adroph wa Pamoja blog).
Mshehereshaji wa Semina Bi. Rose Mwalongo akiwakaribisha washiriki wote waliofika kwenye semina ya siku mbili iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of women in radio and television (AWRTT) kwa kushirikiana na Ethical Journalism Network ambapo wamewakutanisha wanahabari mbalimbali kutoka nchini Tanzania pamoja na nchi za Afrika.
Bi. Rose Haji Mwalimu kutoka IAWRT Tanzania akifungua semina kwa kwa washiriki ambao walikuwa ni wanahabari (hawapo pichani) mbalimbali kutoka nchini Tanzania pamoja na nchi za Afrika wa pili kutoka kushoto ni Rais wa IAWRT Bi. Rachael Nakitare, wa pili kutoka kulia ni Bi. Elisabeth Scwabe-Hansen pamoja na Mkurugenzi wa Ethical Journalism Network (EJN).
Rais wa IAWRT Bi. Rachael Nakitare akitoa semina kwa wanahabari namna ya kusimama katika ukweli na uwazi na pia kuepuka lugha ambazo zinaweza kuleta chuki kwa jamii, na baadae kusababisha machafuko kwenye Uchaguzi mkuu wa 2015.
Bi. Elisabeth Scwabe-Hansen kutoka ubalozi wa Norway akiwasisitiza washiriki wa semina hiyo kuwa makini kipindi chote wanapochukua au kutafuta taarifa ili kuondoa vurugu kwa nchi hasa Tanzania inayotegemea kufanya uchaguzi mwaka huu.
Mkurugenzi wa Ethical Journalism Network (EJN), Aidan White akitoa semina kwa wanahabari pamoja na wadau wa habari (hawapo pichani) kuhusu matumizi mazuri ya uandishi hasa kwenye hiki kipindi cha Uchaguzi.
Baadhi ya washiriki wa semina.
Rais wa Shirikisho la waandishi wa Habari Afrika (FAJ), Mohamed Garba.
Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Bi. Imelda Lulu Urio akielezea kuhusu vyombo vya habari vya Tanzania vilivyoanza kuonekana kama kuna aina ya lugha ambazo hazikuwepo hapo awali ambapo amesema kuwa ni wakati sasa wa kuanza kuzuia maana zinaleta chuki kwa taifa hasa suala la udini ambalo limeonekana kushika kasi hapa chini Tanzania.
Bi. Irene Burungi Mugisha kutoka IAWRT nchini Uganda akizungumza jambo.
Wadau wakifuatilia mada kwa umakini.
Mhariri mkuu wa gazeti la The New Times la nchini Rwanda, Bw. Kennedy Ndahiro akitoa mada kwa wanahabari pamoja na wadau wa habari waliohudhuria kwenye semina ya matumizi mazuri ya vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu unaotegemea kufanyika mwaka huu.
Rais wa Umoja wa waandishi nchini Uganda, Bi. Lucy Ekadu akiwaasa waandishi wa habari kuwa makini katika utoaji wa habari katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu unaotegemea kufanyika mwaka huu na pia kutoa elimu ya msingi kwa wanahabari ili kutochochea vurugu.
Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Ayoub Rioba akitoa semina kwa washiriki (hawapo pichani) akiwasilisha mada yake kwenye semina iliyofanyika kwenye hoteli ya Peacock jijini Dar.
Mshiriki Borry Mbaraka akiuliza swali kwa watoa mada.
Rais wa IAWRT, Bi. Rachael Nakitare (wa tatu kutoka kushoto) akiuliza swali kwa mtoa mada (hayupo pichani).
Mtafiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Patience Mlowe akiwasilisha mada yake kwa wanahabari(hawapo pichani).
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena akiuliza swali kwa mmoja wa watoa mada wakati wa semina iliyofanyika jana katika hoteli ya Peacock jijini Dar.
Mweka hazina kutoka IAWRT Tanzania, Razia Mwawanga akikazia jambo kwenye semina ya wanahabari.

Wadau wakifuatilia kwa umakini mada.
Washiriki wa Semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja.  

Na Mwandishi wetu 
 Ikiwa Tanzania inajiandaa kwa ajili ya zoezi la uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, waandishi wa habari nchini wameaswa kujiepusha na lugha za chuki pamoja na uchochezi kipindi chote cha uchaguzi jambo ambalo linaweza kusababisha machafuko kama inavyoonekana katika nchi mbalimbali barani Africa na duniani.  

Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam katika semina ya siku mbili iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of Women in Radio and Television (IAWRT) kwa kushirikiana na Ethical Journalism Network (EJN) ambapo wamewakutanisha wanahabari mbalimbali kutoka nchini Tanzania pamoja na nchi za Afrika mashariki kwa lengo la kujadili masuala yanayohusiana na lugha za chuki kwa vyombo vya habari vya Afrika pamoja na madhara yake kwa wananchi.  

Akifungua warsha hiyo mgeni rasmi ambaye ni Raisi wa shirikisho la wanahabari Africa (FAJ) Bw. Mohamed Gabra amesema kuwa moja ya mambo ambayo yamekuwa yakisababisha machafuko makubwa katika nchi nyingi za Afrika na duniani kwa ujumla ni lugha zinazotumika na wanahabari wakati wakiripori baadhi ya habari lugha ambazo amesema kuwa zimekuwa zikileta chuki baina ya watu na mwisho wake kusababisha madhara makubwa ambayo yangeweza kuepukika kama hatua zingechukuliwa mapema.  

Ametolea mifano kwa nchi kama Rwanda, Kenya, na nchi nyingine za ulaya ambazo zimewahi kuingia katika machafuko ya kisiasa katika kipindi cha uchaguzi kutokana na vyombo vya habari pamoja na wanahabari wenyewe kutumia kalamu zao kuwajengea chuki wananchi na mwisho kusababisha kuibuka kwa machafuko makubwa.  

Amesema kuwa ili kuhakikisha kuwa Tanzania inafanya uchaguzi mkuu kwa mafanikio na amani ni lazima wanahabari wahakikishe kuwa wanasimama kwenye ukweli na kuhakikisha kuwa wanawaambia wananchi kile ambacho kinatokea na sio kujenga na kutengezeza maneno ambayo mwisho yatasababisha chuki kwa watanzania.  

Awali akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo Rais wa (IAWRT) Bi. Rachael Nakitare amesema kuwa ni lazima kipindi hiki cha Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu ni kipindi cha wanahabari kusimama katika ukweli,uwazi na kuepuka lugha ambazo zinaweza kuleta chuki kwa jamii,na baadae kusababisha machafuko.  

Baadhi ya watu waliotoa mada katika warsha hiyo ni pamoja na wakili na Mkurugenzi wa uwezeshaji na uwajibikaji kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Bi. Imelda Lulu Urio ambapo pamoja na mambo mengine ameelezea jinsi vyombo vya habari vya Tanzania vimeanza kuonekana kama kuna aina ya lugha ambazo hazikuwepo hapo awali ambapo amesema kuwa ni wakati sasa wa kuanza kuzuia mambo hayo ili kuepuka mambo makubwa ambayo yanaweza kujitokeza hapo baadae.  

Wengine waliopata nafasi ya kuchangia katika warsha hiyo ni mwandishi mkongwe nchini ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Dk. Ayoub Rioba ambapo amesema kuwa katika chaguzi mbalimbali katika nchi za Afrika kwa sasa wanasiasa wamekuwa wakiwatumia wanahabari kutaka kujinufaisha wao kisiasa bila kujali madhara ambayo yanaweze kutokea endapo wanahabari watakiuka maadili ya taaluma zao. 

 Baadhi ya wanahabari kutoka mataifa ya nje ya Tanzania kama Kenya, Uganda,wamesema kuwa hakuna tofauti kubwa sana kati ya ufanyaji wa kazi za wanahabari zinazofanywa nchini Tanzania na mataifa yao bali tofauti iliyopo ni sheria zinazowaongoza wanahari katika mataifa hayo.

Tuesday, May 12, 2015

RATIBA YA USAJILI WA TMT SEASON 2 KWA MIKOA YA MBEYA, MTWARA NA DAR

CHAWATIATA TABORA YATOA ONYO KALI KWA WAGANGA WA TIBA ZA ASILI

Na  Allan Ntana,Tabora

WAGANGA wanaojishughulisha na utoaji tiba asilia mkoani Tabora wameonywa kutojihusisha na vitendo vyovyote vinavyochochea uvunjifu wa amani kwa kuhamasisha mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi(albino).

Kauli  hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Waganga na tiba asilia (CHAWATIATA) katika Manispaa ya Tabora  Bw.Ramadhani Rajabu alipokuwa akizungumza na  Mwandishi wa gazeti hili kuhusu tuhuma zinazowakabili baadhi ya wananchama wake kujihusisha na vitendo hivyo viovu.

Alisema anaunga mkono kauli ya Serikali ya kuwakamata waganga wote wanaojihusisha na vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na wale wanao tumia ramli chonganishi kwani wanaweza kuondoa amani ya nchi yetu ikiwa ni pamoja na kuwapa hofu ya kuishi wazee na albinism.

Alisema kila halmashauri ya wilaya mkoani humo inatakiwa kuwatambua waganga wa kienyeji waliopo na wenye  vibali vya kufanya kazi hiyo kutoka kwenye chama na endapo mamlaka husika na kubainisha kuwa yule atakayebainika kwenda kinyume na masharti ya katiba ya chama hicho atachukuliwa hatua kali za kisheria na ikiwemo kufikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma hiyo.

“Haiwezekani mganga anayetibu ama kutoa tiba ya kweli amshawishi mteja wake kuleta viuongo vya maalbino, huyo siyo mganga na hakuna tiba yoyote ya asili inayo tumia kiungo cha binadamu isipokuwa viungo vya baadhi ya wanyama ila sio binadamu,''alisema Rajabu.

Alisema inasikitisha  sana  kuona waganga wa tiba asili wakituhumiwa kuhusika na mauaji ya albino  pamoja vikongwe jambo linawachafua hata waganga wengine ambao wanafuata maadili ya utoaji tiba hizo, na kuongeza kuwa hao ni matapeli na ni wenye tamaa ya fedha.

Hili haliwezi kuvumilika nilazima hatua kali zichukuliwe dhidi yao, aliongeza.

Aliitaka Jamii kutambua kuwa hakuna Mganga ambaye anaweza kumwagiza mteja wake kumletea kiungo cha albno ili kuweza kutibiwa kwani hata waganga wana watoto ambao ni albinism, ndugu na wengine ni baba zao, mama zao,shangazi au wajomba hivyo suala hilo linatakiwa kupigwa vita kwa nguvu zote ili kuwaokoa hawa wenzetu wanao wamaoangamia bila sababu.

Aidha alisema  Serikali inatakiwa kulitambua hili kama janga la kitaifa na siyo kwamba mauaji haya yanawahusu waganga wa kienyeji wote kama inavyoonekana bali inatakiwa kukaaa chini na kulitafutia ufumbuzi kwani mauaji hayo ni sawa na vita ambayo inaaza kwa kuwabagua walemavu hao na vigongwe.

Hata hivyo aliomba wanachi kuungana kwa pamoja kuhakikisha ulinzi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi unakuwepo na kutoa taarifa sehemu husika pale inapotokea albino au kikongwe kufanyiwa unyama wa aina yoyote ile ili kumaliza janga hili linalowakabili. 

Aidha ameyataka medhehebu yote ya dini kuungana kwa pamoja kuliombea taifa juu ya janga hili la mauaji ya albino na vikongwe linalo zidi kushika kasi hapa nchini ikiwa ni pamoja taifa kupata sifa mbaya kwenye anga za kimataifa.  

TANZANIA MEDIA IN THE FRONTLINE: JOURNALISTS TARGET POLITICAL HATE IN UPCOMING ELECTION

hate specch banner
Journalists and African media leaders from the region are meeting this week to highlight the role of media and journalism in combating hate-speech and intolerance in the upcoming election campaign.
The meeting, organised by the International Association of Women in Radio and Television (IAWRT) and the Ethical Journalism Network (EJN), opens in Dar Es Salaam today (Tuesday) and comes after fresh regional conflict with recent terrorist attacks in Kenya and fears of genocidal violence in Burundi.
The meeting will involve a workshop at the Peacock Hotel on how journalists and media can help stop the spread of hateful political propaganda and will reinforce the Africa-wide campaign,Turning the Page of Hate, which was launched last year in Kigali to mark the 20th anniversary of the Rwandan genocide.
Among the speakers will be Mohammed Garba, President of the Federation of African Journalists and Imelda Lulu Urio, from the Tanzanian Legal and Human Rights Centre.
“This conference could not come at a more important time for Tanzanian journalists,” said Rose Haji Mwalimu, head of IAWRT for Tanzania. “Media here are in the frontline of a struggle for democracy and pluralism. We have to ensure that we keep a lid on the voices of hate and, at the same time, give people the right to free speech.”
This challenging task will involve helping journalists to identify hate-speech and to lower the temperature of confrontation that often comes at election time, she said. The journalists and media will be encouraged to use a special 5-point test for hate-speech that has been developed in co-operation between media and the United Nations human rights commission.
“The violence in recent months inspired by terrorists in Kenya and the continuing shadows over Burundi suggest that it’s a matter of urgency for journalists to eliminate the voices of intense hatred and incitement,” said Aidan White, Director of the EJN. “This meeting comes only a few months before the hotly-contest general election in Tanzania when the political temperature will rise and media have to guard against being used by hate-mongers.”
In recent years, Tanzania has seen much foul play by candidates from all parties with hate speech and threats on all sides. There have been reports of acid attacks, kidnappings and killings. This meeting will focus on practical actions for journalists to help reduce the level of confrontation.
The meeting will:
1. Call upon government and all political leaders to respect the freedom of the press and ensure that journalists operate in a safe environment;
2. Call on media and journalists to boycott hate speech or any language that can stir violence;
3. Promote ethical standards at all levels of the press, broadcasting and online communications;
4. Call on politicians to ban hate speech in their own ranks;
5. Call upon citizens to boycott meetings or activities where candidates or political activists use hateful, violent and discriminatory language to promote their brand of politics.
6. Reiterate the need for all media to be aware of legal restrictions, including the Newspaper Act of 1976 that could see media banned for hate speech;
7. Call upon the Tanzanian Parliament to review provisions in the Statistics Act as well as the Cyber Crime Act which may violate the freedom of the press as well as the right to information.
“None of this will be easy,” said Rose Haji Mwalimu, “But this is an important opportunity for journalists and media to strengthen their role in ensuring the coming elections are a beacon for democracy and not an excuse for settling political score by acts of hatred and violence.”
More information:
Rose Haji Mwalimu:rohamu2004@yahoo.co.uk or 0754270856/0655434444
Aidan White: aidanpatrickwhite@gmail.com or 00447946291511

WAKAZI WILAYA YA KAKONKO WATAKIWA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF-KIGOMA

Katibu tawala wilaya ya Kakonko Bi.Zainab Mbunda akifungua Mkutano wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Afya ya Jamii CHF uliofanyika katika Ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko huo wa hiari ambao unawawezesha kupata huduma za matibabu kwa muda wa mwaka mzima baada ya kujiunga na kuchangia kiasi cha shilingi elfu kumi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko Bi.Jaina Msangi akizungumza namna ambavyo Halmashauri inavyosimamia Mfuko huo wa CHF na kueleza kuwa wamekuwa wakihamasisha Jamii kujiunga na Mfuko huo ili waweze kunufaika na huduma za Afya.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF Bw.Rehan Athuman akitoa maelezo mafupi kuhusu Mfuko wa Afya ya Jamii CHF na namna ambavyo ulivyoweza kuwafikia watanzania na kunufaika na huduma za Mfuko huo unaolenga kuboresha afya za wananchi hususani wenye kipato cha chini na cha kati.
Baadhi ya Wadau wa Mfuko wa Bima ya Afya waliohudhuria katika Mkutano huo wakiwemo Madiwani,Watendaji wa vijiji,Kata na Vitongoji,Viongozi wa Dini,Vyama vya Siasa,Mashirika,Asasi mbalimbali na Wazee Maarufu wa wilaya ya Kakonko(Picha zote na  KAPIPIJhabari.COM) 






THE GOVERNMENT OF TANZANIA EXPANDS ITS NEW BIRTH REGISTRATION SYSTEM TO MWANZA

Baby Veronica being registered
Baby Veronica being registered.
The new system is set to drastically increase the number of children under 5 with birth certificates
The Deputy Minister of the Ministry of Constitutional and Legal Affairs of the United Republic of Tanzania, Honorable Ummy Ali Mwalimu, launched today in Mwanza the new simplified birth registration initiative for children under-five in Tanzania. The event took place in Mwanza, the second largest city in mainland Tanzania. Mwanza will be the second region, after Mbeya, to benefit from the new, easily accessible and free birth registration system which is set to register over 400,000 children under-five by December 2015.
This new birth registration system, which is being supported by a generous contribution from the Government of Canada through the Department of Foreign Affairs, Trade, and Development, was first field tested in 2012 in Temeke, the largest district of the city of Dar es salaam and in 2014 was officially launched in Mbeya. According to the Acting Chief Executive Officer of RITA, Ms. Emmy Hudson, this simplified system marks a significant shift in accelerating birth registration in Tanzania after years of stagnation.
“RITA has embarked on several initiatives to improve birth registration in Mainland Tanzania, especially to newborn babies to ensure that each baby is captured and registered shortly after birth and closest to home. Through this initiative we see this dream realized and thank our development partners for unwavering support. Temeke and Mbeya have set good examples and we hope to register even better results in Mwanza.”
The 2010 Tanzania Demographic and Health Survey showed that only 16 per cent of children in Tanzania under the age of five were registered with civil authorities, and only about 8 per cent have a birth certificate.[1] Registration in Zanzibar is much more widespread than on the mainland with 78.7 per cent of under-fives registered (63 per cent with a certificate) versus 14.6 per cent registered (6.2 per cent with a certificate) on the mainland.[2]
Prior to the roll-out of the Birth Registration Initiative in Mbeya it was estimated that only 8.7 per cent of the under-five population had a birth certificate. In less than two years after the roll-out, Mbeya saw approximately a 48 per cent increase and now it is estimated that nearly 56 per cent of under-fives in Mbeya have a certificate.
[1] See Tanzania Demographic and Health Survey (2010), pg. 27.
[2] Ibid. and See p.28, Table 2.11 Birth Registration for Children Under Five
Baby Veronica and her Birth Certificate
Baby Veronica and her Birth Certificate.
The new decentralized birth registration and certification system capitalizes on the existing health infrastructure and personnel to register newborn babies soon after birth or within 12 months when visiting health facilities for vaccinations. Registration information is uploaded using mobile phone technology to a centralized data-base resulting in real-time data availability, and a certificate is issued the same day.
This new birth registration and certification system will be operational in Mwanza soon after today’s launch. With financial support from the Canadian Government, this new system will also be rolled out over the next five years to ten additional regions, namely, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Iringa, Njombe, Tabora, Kagera, Kigoma and Dodoma.
Paul Speech
UNICEF Tanzania Deputy Representative, Paul Edwards.
UNICEF Tanzania Deputy Representative, Paul Edwards, commended the Government of Tanzania for its commitment to prioritizing child rights and reaffirmed UNICEF’s commitment and support towards making birth registration and certification a reality for all children.
“With this initiative RITA has taken an important step towards facilitating birth registration. Registration Assistants are now able to upload information instantly over mobile phones, making data available in ‘real time.’ This type of information is crucial in planning for Tanzania’s future. And it goes without saying that the certificate itself provides protection for children - proof of age informs the State as to who is a child, and provides protection against the exploitation of children and child marriage.”
Tigo Lake Zone Director, Ally Maswanya said: “The support provided by Tigo towards this initiative is in line with the company’s corporate social responsibility strategy which aims at empowering community with information and communication technology tools such as mobile phones. The under-five birth registration initiative demonstrates our commitment as telecommunication experts and attests the potential of mobile technology in development programs.”
The VSO Country Director Jean Van Wetter praised the strong partnership between Government, UN, private sector and civil society: “Birth registration is fundamental to guarantee child rights and further improve the social services delivery system in the country.”

TAASISI YA IMETOSHA YATOA MSAADA KWA KITUO CHA BUHANGIJA SHINYANGA


Toka kushoto ni Kathrin Hoff, kijana Paulo, Masoud Kipanya na Balozi Henry Mdimu.
Taasisis ya Imetosha ya jijini Dar es Salaam leo hii imepeleka misaada mbali mbali katika kijiji cha watoto wasioona cha Buhangija, Shinyanga ambacho kwa sasa kinahifadhi pia watoto na vijana wenye ualbino takriban 300. Misaada hiyo ikiwemo mabelo ya mitumba 2 moja la masweta na jingine la suruali za jeans, unga, mchele, maharage, sukari, chumvi, ndoo 3 za mafuta ya kupikia, sabuni za kufulia box 8, vile vile box 3 za vifaa vya hedhi vitakavyodumu miezi miwili pamoja na nguo za ndani dazeni 12 vyote hivo  imegharimu Tsh milioni mbili na elfu sitini(2,060,000) ambazo zimetolewa na wanachama wa taasisi hiyo iliyojikita kupambana na mauaji ya watu wenye ualbino kwa njia ya elimu.

Akiongea na watoto na vijana hao Mwenyekiti Masoud Kipanya alisema taasisi hiyo inaangalia jinsi ya kutengeneza mazingira kwa kituo hicho kujijengea uwezo wa kujipatia chakula badala ya kutegemea wasamaria wema huja pale watakapojisikia wakati watoto katika kituo hicho wanahitaji kula kila siku.

Mkuu wa kituo hicho alisema anashukuru taasisi ya Imetosha kwa kuonesha mapenzi ya dhati na watoto wa kituo hicho na kuguswa na changamoto zinazowakuta, kwani si mara nyingi sana watu au taasisi kurudia kupeleka misaada kituoni hapo kitu ambacho Imetosha wamekifanya. Wiki 3 zilizopita taasisi hiyo ilipeleka msaada wa chakula kituoni hapo.

Awali mtafiti wa masuala yahusuyo watu wenye ualbino mJerumani Bi Kathrin Hoff alielezwa kufurahishwa na jitihada zinazooneshwa na Imetosha kwa uhamasishaji inayoufanya kwa jamii ya Ki Tanzania, pia amepongeza sana hatua ya Imetosha kutaka kukifanya kituo cha Buhangija kujitegemea badala ya kubaki tegemezi kama ilivyo sasa. Kathrin Hoff ni mhitimu toka chuo kikuu cha Mainz nchini Ujerumani.
Baadhi ya missada iliyotolewa na Imetosha pembeni kulia ni mabelo mawili ya mguo.
Mkuu wa kituo hicho Bw Peter Ajali akiongea na watoto wa kituo hicho akieleza dhamira ya ya asasi ya Imetosha kwao.


Hapa wakimsikiliza Masoud Kipanya
Baadhi ya wasichana wa kituoni hapo wakifurahia msaada wa nguo za ndani na vifaa vya hedhi walivyokabidhiwa na mjumbe wa Imetosha aishiye Shinyanga Bibi Herriet

Picha na habari kwa hisani ya TBN kanda ya kati.

TIMU TANZANIA YASHIRIKI MATEMBEZI YA SUSAN G. KOMEN WASHINGTON, DC


Timu Tanzania ikipata picha ya pamoja kabla ya kuanza matembezi ya saratani ya matiti ya Susan G. Komen yaliyofanyika Washington, DC siku ya Jumamosi May 9, 2015.

Wanusurika wa saratani ya matiti wakipata picha ya pamoja.

Matembezi yakianza.

Kushoto ni msaniii toka uingereza Matt Goss aliyeimba wimbo maalum wa Strong kwa ajili ya matembezi haya ya Susan G. Komen ambaye mwaka jana mama yake mzazi alifariki kutokana na maradhi ya saratani ya matiti akipeana mkono na watembeaji wa saratatani ya titi. Kati ni Nancy G. Brinker mdogo wake Susan G. Komen akipeana mkono na watembeaji siku ya maadhimisho ya matembezi ya saratani ya matiti kwa kumuenzi dada yake kwa kuanzisha oganaizesheni ya kupigana na gonjwa hili hatari mwaka 1982 kama ahadi aliyomwekea dada yake.

Mmoja ya watembeaji na mnusurika wa saratani ya titi akipatiwa huduma ya kwanza na watembeaji wenzake baada ya kuanguka na kupata majeraha kwenye paji la uso huku wakisubili gari la wagonjwa.

Timu Tanzania ikichanja mbuga kwenye matembezi hayo.

Mwanahabari wa Kwanza Production na Vijimambo Media Mubelwa Bandio(kulia) akiwa sambamba na mwimbaji Matt Goss na Nancy G. Brinker CEO wa Susan G. Komen

Timu Tanzania ikiwa imemaliza matembezi yao ya maili 3 takribani na kilomita 5

Watoto wa wazazi Watanzania wakipata picha ya pamoja baada ya kumaliza matembezi hayo na wazazi wao.

Picha ya pamoja ya kumaliza matembezi hayo pamoja na mmoja wa kikosi cha zima moto wa TDF aliyejumuika kupiga picha na timu Tanzania.

Picha zote na Kwanza Production na Vijimambo Media & Entertainment.
Kwa picha zaidi bofya HAPA