Pages

KAPIPI TV

Monday, May 18, 2015

"CCM ITASHINDA KWA KIASI KIKUBWA UCHAGUZI MKUU 2015"-NAPE AZUNGUMZIA HILO AKIWA NJE YA NCHI

Karibu kwenye sehemu ya kwanza kati ya mbili za mahojiano yetu na Katibu Uenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania.
Ameeleza mengi akianza na Hali ya chama hivi sasa.

NHC YAFANYA UKAGUZI WA MASHINE ZA KUFYATULIA MATOFALI ILIYOZITOA KWA VIJANA KATIKA WILAYA 168 NCHINI

New Picture (11)
Kiongozi wa kikundi cha vijana 40 cha Wajenzi Isoso, Wilayani Kishapu akisoma risala kwa Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya (wa pili kushoto walioketi) mara baada ya Meneja huyo kumaliza mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kishapu Bi. Jane Mutagurwa ambaye alimhakikishia ushiriki makini wa Halmashauri hiyo katika kuwasaidia vijana kazi, mtaji na maeneo endelevu ya kufanyia kazi yao ya kufytaua matofali yanayofungamana. Aliishukuru NHC kwa msaada wa mashine kwa Halmashauri hiyo ambazo zimewapa vijana ajira.
New Picture (12)
Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya na Meneja wa NHC Mkoa wa Shinyanga Bw. Ramadhani Macha (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bw. Festo Kang’ombe mara baada ya kufanya mazungumzo naye ya kuhamasisha Halmashauri hiyo kutoa ushirikiano kwa vijana waliopewa msaada wa mashine na NHC ya kuytatulia matofali yanayofungamana.
New Picture (13)
Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya akiwa katika eneo la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga maarufu kwa ajili ya vijana wa Juakali wanaotengeneza matofali ya kufinyanga na kuchoma, ambapo aliendesha zoezi la kukinyang’anya mashine iliyotolewa na NHC kama msaada kikundi cha vijana cha Amanias katika Manispaa hiyo baada ya kugundua kuwa kikundi hicho kimeacha kutumia mashine hiyo na kujiunga na kazi za juakali za kutengeneza matofali ya udongo wa kufinyanga.
New Picture (14)
Wakufunzi wa VETA Shinyanga wakiwa eneo la Kata ya Usanda wakimueleza Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya namna wanavyoshiriki kurekebisha hitilafu ndogondogo zinazojitokeza katika mashine za vijana za kufytatua matofali yanayofungamana alipokagua vikundi vya vijana katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
New Picture (15)
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Bi. Isabella Chilumba akiueleza ujumbe wa NHC na watendaji wake namna Halmashauri hiyo inavyoshiriki kikamilifu kuwawezesha vijana waliopewa msaada na NHC wa mashine ya kufyatulia. Halmashauri hiyo imewapa vijana mtaji, maeneo ya kufanyia kazi na kazi za kujenga maabara, kuta za shule mbalimbali na majengo mengine ikiwa ni sehemu ya kusaidia kikundi hicho chenye vijana 70 kuwa na ajira endelevu.
New Picture (16)
Kikundi cha vijana katika Halmashauri ya Ushetu kikijenga ukuta wa shule ya Sekondari Ukune iliyoko kilometa 70 kutoka Kahama kwa kutumia matofali yanayofungamana baada ya kupewa msaada wa mashine za kufyatulia matofali hayo na NHC mwaka 2014.
New Picture (17)
Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya akiwapa zawadi ya fedha za kuwaongezea hamasa vijana wa kikundi cha vijana wapatao 70 Wilayani Ushetu kama sehemu ya kuunga mkono juhudi zao baada ya kukagua shughuli za maendeleo walizofanya kwa kutumia mashine za kufyatulia matofali yanayofungamana walizopewa na NHC ili kujiajiri.
New Picture (18)
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Bw. Patrick Kalangwa akitoa maelezo ya jinsi kikundi cha vijana waliyopewa msaada wa mashine za kufyatulia matofali na NHC kinavyosaidiwa na Halmashauri hiyo. Hata hivyo, alikiri kuwa shughuli za migodi ya madini zinafanya baadhi ya vijana hao kuacha kutengeneza matofali na kujihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini.
New Picture (19)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kahama Mji Bw. Michael Nzengula akitoa maelezo kwa viongozi wa NHC waliomtembelea Ofisini kwake kufahamu namna Halmashauri hiyo inavyoshiriki katika kusaidia vijana wanaotengeneza matofali ya kufungamana kwa kutumia msaada wa mashine walizopewa na NHC.
New Picture (20)
Meneja wa NHC Mkoa wa Tabora Bw. Erasto France Chilambo akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bw. Florence Mwale ya nia ya NHC ya kuinyang’anya Halmashauri hiyo mashine za kufyatulia matofali walizopewa na NHC baada ya Halmashauri hiyo kutosimamia kikamilifu vijana.
New Picture (21)
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Kaliua Bw. Mabula Isambula akieleza ujumbe wa NHC namna Halmashauri hiyo mpya inavyowawezesha vijana mitaji na maeneo ya kufanyia kazi za kufytaua matofali yanayofungamana kwa kutumia mashine walizopewa na NHC ili kuwezesha vijana kujiajiri.
New Picture (22)
Meneja wa NHC wa Huduma kwa Jamii, Bw. Muungano Saguya akizungumza na kikundi cha vijana Wilayani Kaliua waliopewa msaada wa mashine na NHC ili kujiajiri alipowatembelea kuwapa hamasa na kukagua shughuli zao.
New Picture (23)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Bw. Gervas Magashi aklipokutana na ujumbe wa NHC na kuueleza mkakati wa Halmashauri hiyo wa kusaidia vijana waliyopewa mashine kutengeneza matofali yanayofungamna na NHC ili kujiajiri.
New Picture (24)
Ofisa Miliki wa NHC Bw. Rockussy Sanka na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Bw. Muungano Saguya wakikagua ubora wa matofali yaliyotengenezwa na kikundi cha vijana cha Tujiajiri na Miti ni Mali Wilayani Nzega.
New Picture (25)
Meneja wa NHC Mkoa wa Singida Bw. Ladislaus Bamanyisa akimpa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Iramba Bi. Halima Mpita hundi kwa ajili ya kusaidia vijana waliyopewa msaada na NHC wa mashine za kufyatulia matofali yanayofungamana
New Picture (26)
Meneja waHuduma kwa Jamii na Meneja wa Mkoa wa Singida wakiwa katika Halmashauri ya Ikungi kuhakiki shughuli za vijana za kutengeneza matofali yanayofungamana. Vijana hao wameshajenga jingo la Ofisi yo ya kuendeshea kazi zao.

KATIBU MKUU TAMISEMI, SAGINI ASISITIZA UIMARISHAJI WA ELIMU

DSC_0069

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya kukutana na wadau wa elimu walioshiriki mkutano wa kutathmini sekta ya Eimu nchini kwa mwaka 2014 uliofanyika katika kumbi za mikutano Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Modewjiblog team
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini amesema elimu ya sasa inaelekezwa zaidi katika kumwezesha mtu kujitegemea.
Kauli hiyo ameitoa katika mahojiano maalum na mtandao wa habari wa modewjiblog kuhusu maendeleo na changamoto kwenye sekta ya elimu nchini katika wiki ya maadhimisho ya elimu inayofikia tamati leo mjini Dodoma.
Alisema katika mahojiano hayo kwamba mfumo sasa unawaondoa watu kwenye ajira ya serikali na kutokana na hilo uimarishaji wa elimu ndio kitu cha msingi kabisa.
Alisema katika maadhimisho ya elimu watu wanajifunza usimamizi kama msingi mkubwa wa maendeleo ya elimu nchini.
Alisema kuna mambo mengi ambayo yanastahili kuangaliwa kwa sasa kutokana na vigezo vya ufanisi wa elimu kuonesha changamoto zinazokabili sekta hiyo pamoja na kuimarika kwake.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kupungua kwa uandikishaji wa watoto na mdondoko.
Alisema viongozi, wazazi pamoja na walezi wamesahau wajibu wao na kumwachia mwalimu pekee katika kumlea mwanafunzi kimasomo na hii ndio chanzo kikubwa cha mdondoko na ufaulu mbaya.
Alisema ni vyema watu wakajiuliza hawa wanaondoka wanakwenda wapi na wanafanya nini.
“kuna sheria ambapo viongozi wa kata wanaruhusiwa kuwachukulia hatua na kuwafikisha mahakamani wazazi wanaokwamisha elimu, lakini watu hawachukia sheria hiyo” alisema.
Aidha alisema ubora wa elimu una vigezo vingi ikiwa ni pamoja na kujituma kwa walimu katika ufundishaji na kuwa na dhamira ya kuwapa watoto vitu vyenye maana.
Alisema kuna mambo mengi yanatakiwa kufanywa kuinua elimu na usimamizi unapokuwa mkali na wahusika kuadhibiwa ndio ufanisi unafanyika na mdondoko kuangaliwa.
Alisema ipo haja kubwa ya kuwekeza kwenye elimu kwa viongozi na wadau kutimiza wajibu wao.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Makuru Petro akitoa tathmini ya sekta ya elimu kwa wadau wa sekta ya elimu alisema pamoja na ongezeko la ufaulu ndani ya miaka miwili ipo haja ya kutathimini uimara wa mfumo katika kutoa huduma ya elimu.
Alisema pamoja na ufanisi kuwapo kwa idadi kubwa ya watu wanaokacha shule kunaonesha mfumo kuwa na kasoro na lazima uangaliwe.
Aidha alisema sekta ya elimu wamepokea asilimia 97 ya bajeti yake na kwamba asilimia 70 imeenda kwenye halmashauri ambako ni watekelezaji wa miradi ya elimu.
Tathmini hiyo inayowakilisha wizara zote zinazoshughulikia elimu kama TAMISEMI, Elimu na Maendeleo ya jamii na wadau wengine wa elimu ni sehemu ya shughuli inafanywa kila mwaka kwa lengo la kutambua kilichofanyika, changamoto na namna ya kukabiliana na tatizo hilo.
Hata hivyo walisema kwamba ndani ya miaka miwili kumekuwepo na maendeleo makubwa katika sekta ya elimu hasa ufaulu na ubora wa elimu.
DSC_0078
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) mjini Dodoma.
DSC_0252
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (kulia) akimweleza yaliyomo kwenye taarifa ya ripoti ya hali ya Elimu ilivyo dunia (EFA Global Monitoring Report 2015) “Education For All 2000-2015” ambayo inaonyesha mafanikio na changamoto kidunia iliyoandaliwa na Shirika la UNESCO alipomtembelea ofisini kwake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja mjini Dodoma ambapo pia alikutana na wadau wa sekta ya elimu walioshiriki mkutano wa kutathmini sekta ya Elimu nchini kwa mwaka 2014 uliofanyika katika kumbi za mikutano Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
DSC_0254
DSC_0258
DSC_02611
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akimwonyesha takwimu za Tanzania zilizomo kwenye ripoti hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini.
DSC_0276
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) akiuliza swali kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues wakati wa mazungumzo ofisini kwake mjini Dodoma.
DSC_0273
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (kulia) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la UNESCO, Zulmira Rodrigues (katikati) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini (kushoto) katika ofisi za TAMISEMI mjini Dodoma.

Sunday, May 17, 2015

MAPATO YA NDANI YAIMARISHWE KUFANIKISHA MALENGO YA MILLENIA

IMG_7697
Mkurugenzi wa kupunguza umaskini kutoka Wizara ya Fedha, Ana Mwasha (kulia) akifungua kongamano, linalojadili yaliyojiri katika Malengo ya Millenia na nini kinastahili kufanywa katika SDG's ili kuhakikisha mafanikio katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dk.Oswald Mashindano na Katikati ni Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)- Programme, Amon Manyama.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI wa Kupunguza Umasikini kutoka Wizara ya Fedha, Anna Mwasha amesema changamoto za uwezo wa kifedha kutekeleza miradi mbalimbali iliyokuwa katika Malengo ya Milennia, zinatoa ishara tosha ya kubadili mikakati ili kuwa na mafanikio katika Mipango ijayo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)

Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na washiriki wa kongamano, linalojadili yaliyojiri katika Malengo ya Millenia na nini kinastahili kufanywa katika SDGs ili kuhakikisha mafanikio.

Alisema ipo haja ya kuimarisha makusanyo ya fedha za ndani na kuacha kutegemea wahisani, kwa kuwa moja ya sababu za kushindwa kutekelezwa kwa Malengo ya Millenia ni ahadi za wahisani kutotekelezwa.

Alisema kipengele cha nane katika Malengo ya Millennia, kiligusia ushirikiano wa kimataifa, ahadi ambazo amesema ukiachia nchi za Luxemburg, Denmark, Sweden na Norway, mataifa mengi hayakutoa asilimia 0.7 ya pato lao la ndani, ambalo lilikubalika kimataifa kusaidia Malengo ya Millennia kwa nchi masikini.

Alisema ili kuwepo na mafanikio katika miradi mipya na ile inayoendelezwa kutoka MDGs, iko haja ya kuangalia jamii iliyopo vijijini, ambako ndiko kwenye umasikini wa kutisha, ingawa Tanzania imefanya vyema kuondokana na umasikini wa chakula.

Umasikini wa chakula umepungua hadi asilimia 9 wakati Malengo ya Millenia yalikuwa ni asilimia 11.

Alisema ipo haja ya kufungua mawasiliano ya vijijini, kuinua kilimo, kuwapatia nafasi ya masoko na kuinua huduma za jamii.

Pamoja na kuzungumzia uwezo wa kifedha, alisisitiza haja ya wadau kuangalia namna ya kushirikisha sekta binafsi katika kutafuta vyanzo vya fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ili kukabili umasikini.
IMG_7692
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)- Programme, Amon Manyama akizungumza kwenye kongamano la siku moja linalojadili yaliyojiri katika Malengo ya Millenia na nini kinastahili kufanywa katika SDG's ili kuhakikisha mafanikio lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF).

Alisema mahitaji ya msingi katika kupunguza umasikini, hayajafikiwa kwani tumefikia asilimia 28.2 wakati tulitakiwa kuwa asilimia 19.

Alisema ipo haja kubwa ya kuangalia utekelezaji wa malengo endelevu kwa kuoanisha na mikakati mingine ya kidunia na ya kikanda, huku kazi kubwa ikiwa kuhakikisha malengo yote 17 yanatekelezwa katika muda uliopangwa.

Katika kongamano hilo, washiriki walipata nafasi ya kumsikia Balozi Celestine Mushy kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akichambua jinsi mataifa yalivyofikia SDGs, michakato inayoendelea na namna ambavyo anafikiri Tanzania inaweza kunufaika na mkakati mzima wa maendeleo.

Pia katika majadiliano, washiriki waliozungumzia haja ya kuangalia takwimu kwa kuoanisha kwani zimekuwa zikitafutwa na kila mtu mpaka hazijulikani nani yuko sahihi.
Aidha, walitaka mkakati wa kiviwanda ndio uzingatiwe kwani ndio unaoonesha dira ya kufanikisha maendeleo ya kitaifa, kikanda na kibara.

Kongamano hilo liliendeshwa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Uchumi (ESRF) kwa ufadhili wa UNDP.
IMG_7742
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF) Dk.Oswald Mashindano akizungumza kwenye kongamano hilo.
IMG_7724
Pichani juu na chini ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano Wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy akiwasilisha mada jinsi mataifa yalivyofikia SDGs, michakato inayoendelea na namna ambavyo Tanzania inaweza kunufaika na mkakati mzima wa maendeleo.
IMG_7721 IMG_7771
Dk. Kenneth Mdadila kutoka kitengo cha uchumi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo.
IMG_7701
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye kongamano hilo.
IMG_7707 IMG_7792
Pichani juu na chini baadhi ya wadau walioshiriki kwenye kongamano hilo wakichangia mada kwenye kongamano hilo.
IMG_7800

Thursday, May 14, 2015

BALOZI MPYA WA MALAWI NCHINI MAREKANI ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON DC

 Mhe balozi mpya wa Malawi Nector Mhura akipokelewa na Afisa ubalozi Swahiba Mndeme alipotembelea ubalozi.
 Mhe, balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na mgeni wake balozi wa Malawi Nector Mhura.
 Mhe, balozi wa Malawi nchini Marekani akiweka saini kwenye kitabu maalum cha wageni.
 Mhe, balozi wa Malawi nchini Marekani Nector Mhura akimsikiliza kwa makini mwenyeji wake balozi Liberata Mulamula alipokua akijitambulisha.
  Mhe, balozi wa Malawi nchini Marekani Nector Mhura akiwa ameambata na mkuu wa utawala wa ubalozi wa Malawi bi, Jane Nankwenya.
 Mhe, balozi wa Malawi nchini Marekani Nector Mhura akiwa ameambata na mkuu wa utawala wa ubalozi wa Malawi bi, Jane Nankwenya, kulia ni balozi wa Tanzania nchini Marekani Liberata Mulamula na Afisa wa ubalozi Swahiba Mndeme.

                   PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI.

MWENYEKITI WA VUGUVUGU NCHINI BURUNDI AONGEA NA WANAHABARI HOTEL YA SERENA JIJINI DAR

Kikao Kikiwa kinaendelea Jana usiku
Mwenyekiti wa Vuguvugu kutoka nchini Burundi Bw. Mugwengezo Chauvineau akiongea na waandishi wa Habari  Serena Hotel Dar jana usiku .
Dkt. Christine Mbunyingingo Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa Nchini Burundi, Akiongea na waandishi wa Habari jana usiku . 
*****
Mwenyekiti wa vuguvugu za Maandamano Burundi kwa Mara ya kwanza amefika Nchini Tanzania ili kuweza kushuhudia Mkutano wa Dharula kati ya viongozi watano wa Jumuia ya Afrika Mashariki  kuhusu nchi ya Burundi ambayo sasa imeingia katika machafuko baada ya Rais aliyepo Madarakani kutaka kuongeza muda wake.

Akiongea na Waandishi wa Habari usiku huu Mkuu huyo wa vuguvugu wa Burundi amesema kuwa wananchi hawaridhiki na Rais wao kuendelea kuwa madarakani ambapo hata sheria na katiba hairuhusu na pia sasa ni wiki ya tatu ambapo wananchi wanaendelea kupinga Rais kuendelea kuwania kwa Muhura wa Tatu.

Amezungumzia juu ya waandamanaji  baada ya wiki tatu bado wapo barabarani ambapo wameweza kuwa ni kiungo, wameweza kuwa ni njia kwa sababu wanadai kumekuwa na mabadiriko kuhusu Rais wao, na kuwashukuru waandamanaji hao kwa kuonesha moyo wa uzalendo na kuwa wameweza kudhihilisha na kuwa walikuwa ni watulivu na kutulia kungoja utekelezaji wa mambo ambayo yamezungumziwa.

Amesema kwamba anaomba vurugu hizi zipate kwisha ambapo watu zaidi ya laki mbili wamekimbia nchi na anaomba vurugu ziishe ili wapate kurejea nchini kwao.

Pia ameiomba Jumuia ya kimatafa iweze kufuatilia kwa karibu hali inayoendelea kwa sasa  Nchini Burundi ambapo jumuia iyo tangia zamani imeweza kusimamia mambo ya usalama nchini Burundi na amani ili Burundi iweze kufikia malengo ya Mkataba wa amani wa Arusha na kufikia malengo ya katiba ambayo ndio uti wa mgongo wa taifa hilo.

Kuhusu jaribio la Mapinduzi kiongozi huyo amesema hayupo Miongoni mwa wale ambao wameandaa tukio hilo 

Kuhusu jambo baya alilofanya Rais wa Burundi Kiongozi huyo amaesema kwamba ni kuongezea Muhula wakati tayari alisha tawala kwa Miaka 10, na katika miaka hiyo alishindwa kuweka usawa baina ya warundi, hajatekereza swala la haki za Binadamu , aliongeza kuwa Muhura wake ni Muhura baki na Haramu hauko sambamba na Katiba wala Sheria ya Burundi pamoja na Mkataba wa Arusha na angetekeleza yote hayo hizi vurugu zisinge kuwepo. Pia hata makubaliano ya Arusha yanasema hakuna Rais ataenda Mihula mitatu. Pia warundi wanafanya hivyo kwa sababu hawataki shuhudia tena Damu inamwagika.

Mwisho amewaomba Marais watano wamalize salama Mkutano na kuhakikisha maamuzi yote yanafanyiwa kazi.

Nae Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa amewashukuru kwa uvumilivu wao na kuendelea kupinga Rais wao kuendelea kuwa madarakani kwa awamu ya Tatu.

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUEPUKA LUGHA ZA CHUKI

Meza kuu. (Picha zote na Geofrey Adroph wa Pamoja blog).
Mshehereshaji wa Semina Bi. Rose Mwalongo akiwakaribisha washiriki wote waliofika kwenye semina ya siku mbili iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of women in radio and television (AWRTT) kwa kushirikiana na Ethical Journalism Network ambapo wamewakutanisha wanahabari mbalimbali kutoka nchini Tanzania pamoja na nchi za Afrika.
Bi. Rose Haji Mwalimu kutoka IAWRT Tanzania akifungua semina kwa kwa washiriki ambao walikuwa ni wanahabari (hawapo pichani) mbalimbali kutoka nchini Tanzania pamoja na nchi za Afrika wa pili kutoka kushoto ni Rais wa IAWRT Bi. Rachael Nakitare, wa pili kutoka kulia ni Bi. Elisabeth Scwabe-Hansen pamoja na Mkurugenzi wa Ethical Journalism Network (EJN).
Rais wa IAWRT Bi. Rachael Nakitare akitoa semina kwa wanahabari namna ya kusimama katika ukweli na uwazi na pia kuepuka lugha ambazo zinaweza kuleta chuki kwa jamii, na baadae kusababisha machafuko kwenye Uchaguzi mkuu wa 2015.
Bi. Elisabeth Scwabe-Hansen kutoka ubalozi wa Norway akiwasisitiza washiriki wa semina hiyo kuwa makini kipindi chote wanapochukua au kutafuta taarifa ili kuondoa vurugu kwa nchi hasa Tanzania inayotegemea kufanya uchaguzi mwaka huu.
Mkurugenzi wa Ethical Journalism Network (EJN), Aidan White akitoa semina kwa wanahabari pamoja na wadau wa habari (hawapo pichani) kuhusu matumizi mazuri ya uandishi hasa kwenye hiki kipindi cha Uchaguzi.
Baadhi ya washiriki wa semina.
Rais wa Shirikisho la waandishi wa Habari Afrika (FAJ), Mohamed Garba.
Mkurugenzi wa Uwezeshashi na Uwajibikaji wa LHRC, Bi. Imelda Lulu Urio akielezea kuhusu vyombo vya habari vya Tanzania vilivyoanza kuonekana kama kuna aina ya lugha ambazo hazikuwepo hapo awali ambapo amesema kuwa ni wakati sasa wa kuanza kuzuia maana zinaleta chuki kwa taifa hasa suala la udini ambalo limeonekana kushika kasi hapa chini Tanzania.
Bi. Irene Burungi Mugisha kutoka IAWRT nchini Uganda akizungumza jambo.
Wadau wakifuatilia mada kwa umakini.
Mhariri mkuu wa gazeti la The New Times la nchini Rwanda, Bw. Kennedy Ndahiro akitoa mada kwa wanahabari pamoja na wadau wa habari waliohudhuria kwenye semina ya matumizi mazuri ya vyombo vya habari kuelekea uchaguzi mkuu unaotegemea kufanyika mwaka huu.
Rais wa Umoja wa waandishi nchini Uganda, Bi. Lucy Ekadu akiwaasa waandishi wa habari kuwa makini katika utoaji wa habari katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu unaotegemea kufanyika mwaka huu na pia kutoa elimu ya msingi kwa wanahabari ili kutochochea vurugu.
Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Ayoub Rioba akitoa semina kwa washiriki (hawapo pichani) akiwasilisha mada yake kwenye semina iliyofanyika kwenye hoteli ya Peacock jijini Dar.
Mshiriki Borry Mbaraka akiuliza swali kwa watoa mada.
Rais wa IAWRT, Bi. Rachael Nakitare (wa tatu kutoka kushoto) akiuliza swali kwa mtoa mada (hayupo pichani).
Mtafiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Patience Mlowe akiwasilisha mada yake kwa wanahabari(hawapo pichani).
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena akiuliza swali kwa mmoja wa watoa mada wakati wa semina iliyofanyika jana katika hoteli ya Peacock jijini Dar.
Mweka hazina kutoka IAWRT Tanzania, Razia Mwawanga akikazia jambo kwenye semina ya wanahabari.

Wadau wakifuatilia kwa umakini mada.
Washiriki wa Semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja.  

Na Mwandishi wetu 
 Ikiwa Tanzania inajiandaa kwa ajili ya zoezi la uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, waandishi wa habari nchini wameaswa kujiepusha na lugha za chuki pamoja na uchochezi kipindi chote cha uchaguzi jambo ambalo linaweza kusababisha machafuko kama inavyoonekana katika nchi mbalimbali barani Africa na duniani.  

Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam katika semina ya siku mbili iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of Women in Radio and Television (IAWRT) kwa kushirikiana na Ethical Journalism Network (EJN) ambapo wamewakutanisha wanahabari mbalimbali kutoka nchini Tanzania pamoja na nchi za Afrika mashariki kwa lengo la kujadili masuala yanayohusiana na lugha za chuki kwa vyombo vya habari vya Afrika pamoja na madhara yake kwa wananchi.  

Akifungua warsha hiyo mgeni rasmi ambaye ni Raisi wa shirikisho la wanahabari Africa (FAJ) Bw. Mohamed Gabra amesema kuwa moja ya mambo ambayo yamekuwa yakisababisha machafuko makubwa katika nchi nyingi za Afrika na duniani kwa ujumla ni lugha zinazotumika na wanahabari wakati wakiripori baadhi ya habari lugha ambazo amesema kuwa zimekuwa zikileta chuki baina ya watu na mwisho wake kusababisha madhara makubwa ambayo yangeweza kuepukika kama hatua zingechukuliwa mapema.  

Ametolea mifano kwa nchi kama Rwanda, Kenya, na nchi nyingine za ulaya ambazo zimewahi kuingia katika machafuko ya kisiasa katika kipindi cha uchaguzi kutokana na vyombo vya habari pamoja na wanahabari wenyewe kutumia kalamu zao kuwajengea chuki wananchi na mwisho kusababisha kuibuka kwa machafuko makubwa.  

Amesema kuwa ili kuhakikisha kuwa Tanzania inafanya uchaguzi mkuu kwa mafanikio na amani ni lazima wanahabari wahakikishe kuwa wanasimama kwenye ukweli na kuhakikisha kuwa wanawaambia wananchi kile ambacho kinatokea na sio kujenga na kutengezeza maneno ambayo mwisho yatasababisha chuki kwa watanzania.  

Awali akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo Rais wa (IAWRT) Bi. Rachael Nakitare amesema kuwa ni lazima kipindi hiki cha Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu ni kipindi cha wanahabari kusimama katika ukweli,uwazi na kuepuka lugha ambazo zinaweza kuleta chuki kwa jamii,na baadae kusababisha machafuko.  

Baadhi ya watu waliotoa mada katika warsha hiyo ni pamoja na wakili na Mkurugenzi wa uwezeshaji na uwajibikaji kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Bi. Imelda Lulu Urio ambapo pamoja na mambo mengine ameelezea jinsi vyombo vya habari vya Tanzania vimeanza kuonekana kama kuna aina ya lugha ambazo hazikuwepo hapo awali ambapo amesema kuwa ni wakati sasa wa kuanza kuzuia mambo hayo ili kuepuka mambo makubwa ambayo yanaweza kujitokeza hapo baadae.  

Wengine waliopata nafasi ya kuchangia katika warsha hiyo ni mwandishi mkongwe nchini ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Dk. Ayoub Rioba ambapo amesema kuwa katika chaguzi mbalimbali katika nchi za Afrika kwa sasa wanasiasa wamekuwa wakiwatumia wanahabari kutaka kujinufaisha wao kisiasa bila kujali madhara ambayo yanaweze kutokea endapo wanahabari watakiuka maadili ya taaluma zao. 

 Baadhi ya wanahabari kutoka mataifa ya nje ya Tanzania kama Kenya, Uganda,wamesema kuwa hakuna tofauti kubwa sana kati ya ufanyaji wa kazi za wanahabari zinazofanywa nchini Tanzania na mataifa yao bali tofauti iliyopo ni sheria zinazowaongoza wanahari katika mataifa hayo.