Pages

KAPIPI TV

Tuesday, April 21, 2015

MAHOJIANO NA LINDA BEZUIDENHOUT (LB) Pt 1

Karibu katika sehemu ya kwanza ya mahojiano na mbunifu wa kimataifa wa mitindo mwenye asili ya Tanzania, Linda Bezuidenhout Ameeleza mengi ikiwa ni pamoja na historia yake kwa ufupi, safari yake kwenda nje ya nchi, alivyorejea na kuanza harakati zake za mitindo Nani alimfanya ashawishike na fani hii? Maisha yake kimahusiano je? Familia yake sasa na inavyokabiliana na kazi zake? Angalia kupitia KAPIPI ONLINE TV

MKUTANO MKUBWA WA NENO LA MUNGU WA WASABATO WATANZANIA WAISHIO NCHINI MAREKANI WATOTO WATENGEWA SEHEMU YAO

 Watoto wakiwa sehemu yao chini ya uangalizi maalumu huku wazazi wao wakihudhuria mkutano mkubwa wa neno la Mungu unaondelea DMV kwa siku nne ikiwa leo Jumampili April 19, 2015 ndio hitimisho la mkutano huo.
 Watoto wakiangalia vipindi vya watoto kwenye luninga.
 Msimamizi wa watoto Tanya Muganda akielekeza jambo.
 Tanya Muganda akiwapatia zawadi watoto

BALOZI LIBERATA MULAMULA AHUDHURIA MKUTANO MKUU WA WASABATO WAISHIO NCHINI MAREKANI


Mchungaji Wilbert Nfubhusa akihubiri kwenye mkutano mkubwa wa neno la Mungu wa Wasababto waishio nchini Marekani uliofanyika siku ya Jumamosi April 18, 2015 Silver Spring, Maryland. Kulia ni Michael Mwasumbi akitafsiri mahubiri kwa lugha ya Kiingereza.Mkutano huu umehudhuriwa na Watanzania kutoka majimbo mbalimbali wakiwemo wengine kutoka Tanzania.
 Mhe. Liberata Mulamula. Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiushukuru uongozi wa Wasabato nchini Marekani kwa kuweza kufanikisha mkutano wao na kuweza kumleta mchungaji Wilbert Nfubhusa na kuelezea amefurahishwa kwa makaribisho mazuri na kuwatakia mkutano mwema huku akiomba Mwenye Mungu aushushie baraka zake.

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha mdogo wake  Joycelyne Rutageruka ambaye amekuja kumtembelea Mhe. Balozi toka nyumbani Tanzania nae akitoa neno kwenye mkutano mkuu wa Wasabato wa Watanzania waishio nchini Marekani uliofanyika siku ya Jumamosi April 18, 2015 Silver Spring, Maryland.  

Nchungaji Herry Mhando akifanya mamombi maalum kabla ya kumkaribisha mchungaji Wilbert Nfubhusa kutoa mahubiri,

Mshereheshaji Magoma akifafanua jambo

Mhahubiri yakiendelea
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

Sunday, April 19, 2015

KINANA ASHIRIKI KATIKA BONANZA LA VILABU VYA JOGGING MKOA WA DAR ES SALAAM, VIJANA WANATAKIWA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA

k01
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akianza mazoezi wakati akishiriki katika bonanza la Jogging lililoandaliwa na Kundi la Kaza Moyo Jogging Club la Ukonga Sitakishari ili kuhamasishwa vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura . Mazoezi hayo yameanzia katika viwanja vya Gonga Gongo la Mboto kupitia Kipawa na kuishia kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga ujumbe mkuu wa Bonanza hilo ulikuwa ni kuwataka vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kupata haki ya kupiga kura kuliko kuwa mashabiki tu, Bonanza hilo la mazoezi limeshirikisha vilabu mbalimbali vya Joging kutoka mkoa wa Dar es salaam, Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mogo George Shinga Mtambalike, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida na kulia ni Bona Kaluwa Diwani wa Kata ya Kipawa.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
k1
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu akiendelea na mazoezi wakati akishiriki Mazoezi katika bonanza la Joging lililoandaliwa na Kundi la Kaza Moyo Joging Club la Ukonga Sitakishari ili kuhamasisha vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura . Mazoezi hayo yameanzia katika viwanja vya Gonga Gongo la Mboto kupitia Kipawa na kuishia kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga, Kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mogo George Shinga Mtambalike, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida
k2
Wakiendelea na mazoezi hayo.
k3
Makundi mbalimbali ya Jogging kutoka mkoa wa Dar es salaam yakishiriki katika mazoezi hayo.
k4
k6
Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na mazoezi hayo katika maeneo ya Kipawa pamoja navijana na watoto wadogo kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida na kushoto ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mogo George Shinga Mtambalike,
k7 k9
Mazoezi yakiwa yapepamba moto eneo la uwanja wa Ndege
k10 k11
Kinana akifurahia jambo na watoto katika mazoezi hayo huku Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida kulia akimuangalia.
k12
Makundi mbalimbali ya vilabu vya Jogging mkoa wa Dar es salaam yakiwasili katika viwanja vya Social Sitaki Shari Ukonga.
k13 k14 k15 k16 k17 k18
Umati wa vijana kutoka Vilabu mbalimbali vya Jogging mkoa wa Dar es salaam wakiendelea na mazoezi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Social Ukonga Sitaki Shari.
k19
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiongoza Mazoezi hayo kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga.
k20 k21
Msanii wa musiki wa Mchiriku Maarufu kama Mkaanga Sumu akitumbuiza katika bonanza hilo.
k22
Mratibu wa bonanza hilo Bw.Msafiri akizungumza na vijana waliojitokeza kwa wingi.
Mk23 k24
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinanakulia akifurahia jambo na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
k25
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinanaakizungumza na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida.
k26
Dogo Asley wa Yamoto Band ya Mkubwa na Wanawe akifanya vitu vyake jukwaani katika bonanza hilo.
k27
Kundi zima la Yamoto Bandi likifunika kwa shoo kali katika bonanza hilo.
k28 k29
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha na pamoja na vijana wa klabu ya Kaza Moyo Jogging Club mara baada ya kushiriki katika bonanza lao, Kulia ni Bona Kaluwa Diwani wa Kata ya Kipawa na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mogo Ndugu George Mtambalike.
k30
Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotoa wito kwa tume ya uchaguzi kuhakikisha wanawahamasisha vijana ili kuiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura

BALOZI HENRY MDIMU WA IMETOSHA FOUNDATION ATOA WITO KWA VYOMBO VYA HABARI NA JAMII!


Balozi Henry Mdimu akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za gazeti la Mwananchi mjini Mwanza.


Henry Mdimu ametoa wito kwa vyombo vya habari na jamii nchini kulichukua suala la ukatili na mauaji kwa watu wenye ualbino kama lao ili kuiondoa nchi yetu katika aibu hii. Aliyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za gazeti la Mwananchi ambao ni wadhamini wa habari wa ujio wa kamati ya Imetosha katika kanda ya ziwa.
Kutoka kushoto ni Salome Gregory, Henry Mdimu Mgaya, Issaya Mwakilasa na Zaytun Biboze.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Balozi Mdimu

Imetosha
Kila sauti inasikika.
PIGA KELELE uunge mkono haki ya KUISHI

Ndugu waandishi wa habari, Mwakilishi wa Tanzania Bloggers Network, mabibi na mabwana…..

Tuko hapa kuueleza Ulimwengu kupitia vyombo mbali mbali vya habari juu ya harakati yetu ya IMETOSHA. Harakati hii hii  imeanzishwa na mimi mwenyewe, Henry Mdimu, mwanahabari mwenzenu ambaye nimeamua kwa moyo mmoja kuwa Balozi wa kujitolea wa harakati za kukomesha mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu  wa ngozi, maarufu kwa jina la Albino.

Mimi na ujumbe wangu tumekuja Mwanza kutambulisha harakati za IMETOSHA na ikiwa sehemu ya kuandaa shughuli zitakazofanyika kanda ya Ziwa ikiwa ni sehemu ya kupambana na mauaji na unyanyasaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi.

Mwezi ujao ujumbe wa IMETOSHA utakuja na kuweka kambi ya kudumu Mwanza itakayozunguka kanda ya Ziwa na kutembelea nyumba kwa nyumba zenye wahanga wa matukio ya mauaji na kutoa elimu kwa jamii kuwa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi hayasababishi utajiri.

Pamoja na shughuli tutakazofanya tukiwa Kanda ya Ziwa mwezi wa tano ni pamoja na maetmbezi ya hisani, kutakua na mpira kati ya Simba na Yanga ambapo IMETOSH itavalisha wachezaji Thisrts zake ikiwa ni sehemu ya kutangaza harakati zetu.

Pia tutakua na tamasha litakaloshirikisha wasanii mbalimbali watakaotumbuiza nyimbo mbamimbali zitakazokua na ujumbe wa kukemea na kupinga mauaji na manyanyaso dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Nimeamua kufanya hivi baada ya kushuhudia ndugu zangu wakiteseka kwa muda mrefu. Awali nilishindwa kuanzisha harakati hizi nikiamini kuna vyombo vinavyohusika na utetezi wa watu wenye ulemavu wa ngozi.

Harakati hizi zimeanza baada ya kuona kadri muda unavyokwenda matukio yamezidi kuongezeka na hali kuwa mbaya. Nashuhudia ndugu zangu wakinyanyaswa, wakibezwa mtaanai na hata kudhihakiwa huku baadhi ya wanaoshuhudia haya wakicheka tu.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na vyombo vya habari vilimkariri Rasi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania muheshimwa Jakaya Kikwete akisema kesi mbili za mauaji ya watu wenye ulemavuwa ngozi zililipotiwa kwa mwaka 2012 na 2013.

Taarifa hizo ziliongeza kuwa kti ya mwaka 2006 na 2015, watuhumiwa 139 wameshikiliwa na kesi 35 zimeandikishwa. Watuhumiwa 73 waliachiwa huru na wengine 15 wamekutwa na makosa.

Hivyo nimeamua niweke jitihada zangu binafsi niisaidie Serikali yangu katika kuondoa doa hili linaloichafua Nchi  yetu yenye sifa ya Amani duninia nzima. Hivyo nawaomba Watanzania wenzangu mniunge mkono tukishirikiana na Serikali ili mauaji haya yakome.

Kutokana na ushawishi nilionao kama Mwandishi, Mtangazaji wa redio na Blogger naamini nitaleta mabadiliko makubwa katika kuhakikisha haki ya kusihi kwa ndugu zangu inaheshimiwa na kubaki historia. Salamu zangu ziwafikie wanyanyasaji, wauaji na wenye kufanya dhihaka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi kuwa IMETOSHA.

Uchunguzi wangu wa awali umebaini ukosefu wa elimu juu ya watu wenye ulemavu wa ngozi hupelekea tatizo hili kukua na hatimaye kuuana kw aimani za kishirikina. Hivyo basi, silaha ya Elimu ni sehemu kubwa ya haraki hizi.

Mimi pamoja na mafariki zangu wanaoniunga mkono tutakwenda Kanda ya Ziwa kutoa Elimu kabla tatizo hili halijaenea Nchi nzima. Swali moja tujiulize kwa nini Kanda ya Ziwa? Tutatoa Elimu kwa njia ya ushauri nasaha, pia wanamuziki  sanaa
Nina mpango wa kwenda kanda ya Ziwa kuhangaika na hili mpaka nione mwisho wake. Na ni rahisi kumaliza hili tatizo kabla halijaenea nchi nzima. Maana Walemavu wa ngozi wako nchi nzima lakini jiulize kwa nini Kanda ya Ziwa tu?

Mimi pamoja na rafiki zangu hawa, tunatoka kuelekea huko kutoa elimu kwa njia ya sanaa, na washauri nasaha. Pia tutakua na team ya wanamuziki wanaoandaa nyimbo mbali mbali za kutoa mafunzo ya kutokomeza ukatili huu.

Wasanii hao ni paoma na Jhikoman, Kassim Mganga, Profesa J, Ray C, Fid Q, Roma Mkatoliki na Dami Msimamo.  Tutaishi na jamii hii kwa muda tukiongea nao kwa lugha yao kwa kutumia wakalimani kwa wsifahamu Kiswahili kuwashawishi waamini hakuna ukweli katika Imani hizo.

Naamini nguvu ya vyombo vya Habari hivyo naomba ushirikaiano wenu katika kuhakikisha tunatokomeza mauaji ya wenzetu ili mwisho wa siku wanunuzi wa viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi wafukuzwe watakaanza kuuliza jinsi ya kufanya mauaji haya.

Harakati za IMETOSHA rasmi zimezinduliwa rasmi tarehe 3/3/2015.
Mungu atubariki.
Ahsanteni
HENRY MDIMU-0715000881 na 0787000880
Balozi wa kujitolea
Harakati za IMETOSHA

SALOME GREGORY 0717367309

Mratibu wa Habari- Harakati za IMETOSHA

KAMPENI YA IMETOSHA KWA MAUAJI YA ALBINO SHINYANGA


Ilikua mishale ya saa kumi kamili jioni ujumbe wa harakati za Imetosha ulipowasili katika kituo cha Buhangija cha kulea watoto wenye mahitaji maalumu mjini Shinyanga. Sauti za furaha za watoto zilisikika zikiimba nyimbo za kukaribisha ujumbe wa wana harakati hao ambao wako Mwanza kutambulisha harakati za Imetosha ambazo ni kupambana na kupinga unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi.

Balozi wa Imetosha Henry Mdimu akinunua mahitaji ya watoto waliopo kituoni hapo kabla ya kufika kituoni hapo.
Huyu ni Irene wa NHIF Shinyanga

Wajumbe wa Imetosha
 Akiongea na watoto kituoni hapo Mwenyekiti wa harakati za Imetosha Masoud Ali (Kipanya) alisema Imetosha inatambua umuhimu wa haki ya kuishi kwa kila binadamu ndio maana Imetosha imeanzisha harakati za kutokomeza mauaji na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.  “Tunatambua hapa kati yenu kuna vipaji vya aina mbalimbali hivyo pamoja na kupambana na harakati za kupinga na kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi tupo hapa kuwatia moyo kuwa mna uwezo mkubwa ndani yenu hivyo msijidharau” alisema Masoud.

Kipanya akimuimbisha mtoto wa kituoni hapo
Mwl Peter Alali Francis akisisitiza jambo wakati akiongea na ujumbe wa Imetosha

 Alisema“Pamoja na uhaba wa mabweni kituo kinakabiliwa na uhaba wa chakula. Muda mwingine watoto hawa hushindia mlo mmoja. Chakula mlichofikisha leo hapa kitatusogeza maana tulikua tumeishiwa chakula kabisa” alisema Francis. Ujumbe huo wa Imetosha uliwasilisha kambini hapo unga kilo 50, mchele kilo 50, chumvi kilo 5 na mafuta ya kupikia lita 10. 

Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho Peter Ajali Francis alishukuru ujio wa wanaharakati wa Imetosha kituoni hapo na kusema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1960 kikiwa chini ya Kanisa katoliki.
Kituo hicho kilikua maalumu kwa ajli ya watoto wasiiona na viziwi lakini kutokana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi kuongezeka mwaka 2006 kituo hicho kilianza kupokea watoto wenye ulemavu wa ngozi kutoka sehemu mbalimbali toka kanda ya Ziwa. Kituo kina jumla ya watoto 388 kati ta hao 284 wana ulemavu wa ngozi. Kituo hicho kinakabiliwa na uhaba wa mabweni ambapo chumba chenye uwezo wa kuchukua watoto 50 kinachukua watoto zaidi ya 100 na chenye uwezo wa kuchukua watoto 40 kinachukua watoto zaidi ya 80.


 Zaytun Biboze akiwa amebeba mmoja wa watototo wanaoishi katika ktuo hicho



Masoud Kipanya na Jhikoman wakiwaimbisha watototo wimbo waupenda wa Clap your hands!
Isaya Mwakilasa aka Wakuvwanga akiwachekesha watoto kiuoni Buhangija, Shinyanga


Magunia haya ya unga, mafuta na mchele ndio msaada wa chakula ambao Imetosha ilitoa kwa kituo hicho


Katibu wa Imetosha amabaye ki taaluma ni mwandishi wa habari akimhoji mwalimu Francis Ajali
Wanaharakati wa Imetosha wamepanga kurudi tena mjini Shinyanga mwezi Mei na kukifanya kituo hicho kuwa ngome ya kuanzishia mapambano dhidi ya unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa albino.
Picha na Mkala Fundikira habari na Salome Gregoy/ Mkala Fundikira