Pages

KAPIPI TV

Monday, March 30, 2015

UN KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA KUTANZUA CHANGAMOTO ZA MAENDELEO

DSC_0065
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile (katikati) akiwasili katika ukumbi wa mikutano kwenye hoteli ya Hyatt Regency akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (kulia) pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez kwa ajili ya kuzindua rasmi ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Nyuma yao ni Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF), Dk. Tausi Kida.

Na Mwandishi wetu
UMOJA wa Mataifa umesema kwamba utaendelea kuisaidia serikali ya Tanzania katika kutanzua changamoto za maendeleo zinazoikumba nchi hii.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja huo (UNDP), Alvaro Rodgriguez wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2014 mwishoni mwa wiki.

Ripoti hiyo imeandaliwa na Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na jamii- ya ESRF kwa ufadhili wa UNDP na inagusia changamoto za Maendeleo .

Katika hotuba yake amesema kwamba Umoja wa Mataifa unaona juhudi za serikali katika kuwakwamua wananchi katika umaskini na kutokana na hali hiyo wataendelea kusaidia mipango mbalimbali ya maendeleo pamoja na utafiti wenye kulenga kutoa suluhu kwa changamoto za maendeleo ya wananchi.
DSC_0207
Mshehereshaji wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, Taji Liundi akiitambulisha meza kuu kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) waliohudhuria uzinduzi huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Ripoti hiyo ambayo inazungumza: "mabadiliko ya kiuchumi kwa maendeleo ya watu" imesheheni mipango mbalimbali ya maendeleo na shida zake na namna ya kukabiliana na shida hizo.

Katika utafiti huo imeelezwa kuwa pamoja na uchumi wa Tanzania kukua kwa kasi umaskini bado ni kero kubwa kutokana na kukosekana kwa uhusiano kati ya ukuaji wa kiuchumi na kufutwa kwa umaskini miongoni mwa wananchi wa kawaida.

Kuanzia mwaka 2001 uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa zaidi ya asilimia 6.
Mratibu huyo wa UN nchini amesema kwamba kutokana na kasi ya uchumi kutoenda sambamba na uchumi ndio maana UN inashirikiana na serikali kuona namna bora ya ukuaji uchumi kwenda sawa na uondoaji wa umaskini miongoni mwa wananchi waliowengi.
DSC_0209
Meza kuu Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo, Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.

Wakati huo huo serikali imesema imefurahishwa na uzinduzi wa ripoti hiyo ambayo inatumaini itasaidia katika kuboresha sera na kujibu masuala muhimu ya kukabiliana na umaskini nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Servacius Likwelile katika tukio hilo la uzinduzi wa ripoti.

Alisema serikali inaamini kwamba mambo yaliyomo katika ripoti hiyo yatasaidia katika harakati zake za kukabili umaskini ikiwa ni pamoja wa mipango ya maendeleo kwa kuzingatia dira ya taifa ya maendeleo ifikapo mwaka 2025.

Tanzania inajipanga kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 ikitegemea viwanda katika uchumi wake badala ya kilimo kama ilivyo sasa.
DSC_0131
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kutoa hotuba ya uzinduzi rasmi wa Ripoti ya Maendele0 ya Binadamu 2014 Tanzania uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.

Alisema kwamba serikali imefurahishwa na jinsi ripoti ilivyojikita katika kuainisha maendeleo ya watu na sehemu kubwa ya ushauri utazingatiwa kwa mipango mipya ya maendeleo.

Ripoti ya maendeleo ya watu ni mkakati wa serikali ya Tanzania ulianzishwa Machi 2013 kwa lengo la kutafiti namna bora ya kunasua wananchi katika umaskini wakati taifa likiendelea kukuza uchumi.

Mradi huo unatekelezwa na taasisi ya ESRF ikishirikiana na Wakala wa taifa wa Takwimu (NBS), Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali ya Zanzibar na kitivo cha uchumi cha chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Mradi huo unafadhiliwa na UNDP na umejikita zaidi katika kuangalia vipaumbele katika maendeleo, mambo yanayojitokeza, fursa na changamoto.
Ripoti hii inapatikana kwenye anuani zifuatazo
DSC_0223
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile akitoa hotuba kwenye uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
DSC_0228
Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau waalikwa wakifuatilia htouba ya mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo.
DSC_0233
DSC_0241
DSC_0201
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akisoma risala kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
DSC_0247
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile akikata utepe kuzindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (kulia).
DSC_0259
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akizindua chapisho la Kiswahili la Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania huku mgeni rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF wakishuhudia tukio hilo.
DSC_0271
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo akizundua chapisho la kingereza la Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
DSC_0277
Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile (katikati), Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo kwa pamoja wakionyesha ripoti hiyo kwa waandishi wa habari na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
DSC_0290
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (kulia), Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile (katikati) na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez wakipitia nakala za ripoti hiyo mara baada ya kuzinduliwa rasmi jijini Dar.
DSC_0297
Mgeni rasmi kwenye picha ya pamoja na wadau waliofanikisha maandalizi ya ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania.
DSC_0451
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP nchini Tanzania, Philippe Poinsot (kushoto) wakati wa kupiga picha ya kumbukumbu. Kulia ni Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Amon Manyama.

PROF.JUMANNE MAGHEMBE: SERIKALI IMEVALIA NJUGA TATIZO LA UKOSEFU WA MAJI NCHINI

Akizungumzia tatizo la maji nchini kwa ujumla Prof. Maghembe amesema serikali iko katika utekelezaji wa miradi ya maji awamu ya pili ambapo serikali inatekeleza miradi ya maji katika miji mikuu mbalimbali hapa nchini, ambapo ifikapo mwaka 2025 upatikanaji wa maji katika miji mbalimbali kufikia asilimia 75% wakati katika jiji la Dar es salaam upatikanaji wa maji utafikia asilimia 95, hata hivyo Prof. Maghembe amongeza kwamba miradi hiyo inatekelezwa kwa gharama kubwa na serikali ina nia ya dhati ya kumaliza tatizo hilo nchini kwa kiwango kikubwa. 2Mbunge wa jimbo la Mwanga na Waziri wa Maji Mh. Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na wananchi katika kata ya Kileo ambapo alikagua ujenzi wa nyumba za walimu. 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu katika shule ya sekondari ya Kileo wilayani Mwanga. 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Waziri Prof. Jumanne Maghembe wakikagua skimu ya umwagiliaji kijiji cha Kivulini wilayani Mwanga. 5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Waziri Prof. Jumanne Maghembe wakishiriki ujenzi wa mifereji ya skimu ya umwagiliaji kijiji cha Kivulini wilayani Mwanga. 6Wananchi wa Kijiji cha Kivulini wakitafakari jinsi ya kukwamua pikipiki yao ambayo ilikwama kwenye moja ya mifereji yenye tope katika skimu hiyo ya umwagiliaji. 8Nape Nnauye akijaribu kuendesha Skaveta mtambo wa kuvunia mpunga katika kijiji cha Kivulini wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro. 9Nape Nnauye akishuka kwenye Skaveta mtambo wa kuvunia mpunga katika kijiji cha Kivulini wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro. 10Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiwasili katika kijiji cha Mangara Lembeni wilayani Mwanga. 11Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Waziri Prof. Jumanne Maghembe kushoto wakipiga makofi kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika ofisi ya CCM tawi la Mangara Lembeni wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro. 12 Waziri Prof. Jumanne Maghembe akicheza ngoma ya asili ya wapare huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia ngoma hiyo wakati alipowasili katika moja na vijiji alivyotembelea na kuzungumza na wananchi wilayani Mwanga. 13Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Waziri Prof. Jumanne Maghembe wakishiriki ujenzi wa jengo la KKKT Mwaniko wilayani Mwanga 14Waziri wa maji na Mbunge wa jimbo la Mwanga Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mwaniko Ugweno wilayani Mwanga 15Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo. 16Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo. 18Nape Nnauye akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji cha Mwaniko Ugweno wilayani Mwanga. 19Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano huo uliofanyika kijiji cha Mwaniko Ugweno wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Sunday, March 29, 2015

TAHARIRI: TCRA IZIMULIKE BLOGS ‘UCHWARA’ NA KUZICHUKULIA HATUA KALI

11039142_10200327749914253_7953568182828634952_n
"Screen shot" ikionyesha moja ya habari zilizorushwa kwenye moja ya blog uchwara kuhusiana na taarifa za uzushi wa kifo cha mchungaji Gwajima.
…Ni zile zinazoandika habari za uongo, matusi

Na Andrew Chale wa Modewji blog
Miongoni mwa mambo ambayo Tanzania tunapitia kwa sasa ni pamoja na teknolojia mbalimbali ikiwemo mawasiliano ya simu, intaneti vyombo vya habari na mengine mengi, Lakini mawasiliano hayo kwa sasa ikiwemo Intaneti wapo wanayoyatumia vibaya.

Kupitia BLOG, mtandao ambao mtu anaweza kutengeneza chombo chake cha kutolea taarifa ama kufanyaia jambo lolote lile liwafikie wengi kwa mema, lakini kwa sasa hilo halipo kwani licha ya kuwa kila mtu anaweza kuanzisha blog imetoa mwanya kwa wengine kuzitumia blog hizo kinyume na matarajio.

Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na BLOG nyingi ambazo asilimia kubwa mtu yoyote anaweza kuanzisha tena bure kama ilivyo akaunti yako ya Email, watu wanaoziendesha BLOG hizo wamekuwa wakiongoza kwa kuweka habari za uongo, upotoshaji, habari zinazoenda kinyume na maadili, pamoja na habari ambazosi za kweli.

Tunaamini wapo watu wanaofanya shughuli hizi za BLOG, ambao ni Ma-blogger wazuri tu licha ya kuwa si wanahabari, lakini kwenye blog zao wana weka ‘POST’ habari nzuri na zinazoendana na maadili pia wamekuwa wakitoa habari za kuelimisha jamii, kuifunza jamii na wanapata wasomaji wanaotembelea wengi sana kiasi cha hata kupewa matangazo na baadhi ya Makampuni binafsi ya kibiashara, Serikali na watu wengine, lakini shida ni kwenye hizi ‘Blog uchwara’ ambazo kila kukicha wao kazi yao kukopi na ku-paste habari za kwenye magazeti na kuzipa ‘kiki’ kwenye blog zao wengine habari hizo hizo za kwenye magazeti wao kazi yao kubadilisha kichwa cha ‘habari tu ilimradi apate wasomaji wengi? Jamani kweli hii ni haki?, tena kichwa hicho cha habari hakiendani na maadili ya Mtanzania ama kinakiuka maadili hii si sawa, TCRA, muamke na kuchukua hatua kali.
1
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Profesa John Nkoma.
Tunaamini Mamlaka yaa Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), ( https://www.tcra.go.tz/) mpo na mnafuatilia lakini sijui kama mnaliona hili ni tatizo ama si tatizo.

Tukumbuke huko nyuma kulikuwa na mitandao kama hii tena ya watanzania ambao waliifungua ambapo walianza kuweka picha za kawaida na baadae ikawa inabadilika kuwa wanaweka picha za utupu… wakaachiwa hivi hivi baadae wakawa wanaweka picha za viongozi wakiwemo viongozi wakuu wa Nchi mwisho wa siku Mamlaka husika wakaja kukumbuka shuka wakati mambo yamekua si mambo.

Hivyo ni wakati sasa kwa TCRA, kuchukua hatua blog zote zinazoendana kinyume na maadili ikiwemo kupotosha, kuweka pichaa za ngono na kugombanisha watu basi zichukuliwe hatua.

Mtandao huu unaamini kuwa na unaungana na wadau wote wanaendelea kutoa maoni yao juu ya kuzitaka blog hizi zichukuliwe hatua. Kwani mpaka tunaandika habari hii ni pamoja na baada ya Mdau Yusuph Mhoja kuchukizwa na moja ya habari kwenye miongoni mwa blog hapa nchini. (Tazama picha), ambapo Mdau huyo aliuliza: “Hivi huyu mwandishi anajua kiswahili kweli? Yuko mochwari kwani amefariki huyo?” wakati anajiuliza hayo, hii ni kuwa inawatokea watu wengi sana wanaapokutana na habari kwenye hizo blog uchwara.

Wadau waliochangia mada ya Mhoja: Pendi Mahundi yeye alieleza hivi: “hahaha.... hili ndiyo tatizo kubwa la kila mtu mwenye kisimu cha TECNO bongo kujifanya blogger and a self-appointed journalist... UJINGA mtupu, huwa naziona habari kwenye viblogu mpaka kichefu chefu... full of attention-seeking sensationalism... utakuta heading: HATARI, Vilio na majonzi, Breaking news, Unbelievable..kisa tu kutaka watu wazisome blog zao.” Alieleza Mahundi.

Hata hivyo wachangiaji wengine waliomba serikali kupitisha mswada wa habari na sheria ya ICT ili kukomesha wandishi wa viblog uchwara.
IMG-20150310-WA0045
Modewji blog tunaamini pia Mtandao wa wanabloga Tanzania (Tanzania Blogger Network-TBN) wapo kwani kuna misemo mingi ya zamani inayosemwa, ikiwemo ule wa SAMAKI MMOJA AKIOZA…? Jibu watatupatiaa TBN ama kama si lao basi bomu likilipuka tusimtafute mchawi huko mbeleni.
Hata hivyo, mtandao huu wa Mo dewji blog tunaungana na TCRA na kusema kuwa: “ #Ukipata ujumbe wa chuki, matusi au uongo, FUTA DELETE KABISA!.
Tuandikie maoni yako kupitia kwenye mtandao huu hapo chini ama kupitia simu 0719076376 au 0714940992.

TCRA KUZIMA MITAMBO YA ANALOJIA KIGOMA 31,MACH,2015

Na Magreth Magosso,Kigoma

MAMLAKA ya mawasiliano (TCRA) imetoa agizo kwa watoa huduma ya vi`ngamuzi waliopo katika  Manispaa  ya kigoma Ujiji Mkoa wa Kigoma wahakikishe kuwepo na vingamuzi vya kutosha kwa kuwa ifikapo Machi,31,2015 watazima mitambo ya televisheni aina ya analojia.

Pia  aonya  wachane na tabia ya kukatisha  huduma ya upashaji habari kupitia chaneli zaTbc,Startv,Chanel10,Itv,ambazo kimsingi zinatolewa bure hata kama mteja hajalipa  ada yake ya mwezi kw2a mujibu wa sheria ya mamlaka husika.

Akitoa kauli hiyo mbele ya wandishi wa habari kigoma Ujiji( juzi) Mhandisi wa kanda ya kati Tcra  Charles Ambele alisema ,utaratibu wa uzimaji wa mitambo ya analojia yatagusa maeneo yenye matangazo ya digitalitu.kwa maeneo yasiyo na miumdombinu hiyo hawaguswi na uzimaji huo keshokutwa.
 
Ambele alisisitiza kuwa, wananchi watoe ushirikiano wa karibu kutoka kwa wadau wa sekta ya utangazaji katika kipindi hiki cha uzimaji wa mitambo hiyo,ili Serikali itemize  malengo ya kuwafikia watu zaidi ya 20% kati ya 24% ya waliokuwa wakipata huduma hiyo ya analojia.

Kwa upande wa ofisa habari wizara ya habari vijana,utamaduni na michezo Lydia Churi alisisitiza kuwa,mchakato huo ni awamu ya pili na walengwa ni wakazi wa mji wa kigoma Ujijina mitambo itazimwa saa sita usiku wa mwezi huu kwa kuwa vigezo vimetimia kwa kufanya hivyo.

Alitaja kigezo hicho ni pamoja na uwepo wa utangazi wa mfumo wa analojia na digitali kwenye eneo husika,upatikanaji wav in`gamuzi na uwepo wa chaneli tano mtambukwa za kitaifa kwenye mfumo wa digitali.

Baadhi ya wananchi waliohojiwa na gazeti hili juu ya kuzimwa mitambo hiyo kwa nayakti tofauti  Antony Kayanda na Diana Lubanguka  walisema changamoto iliyopo kwa watoa huduma kukatisha huduma za matangazo kwa chaneli za taifa tatu ikiwa ujalipia ada ya mwezi.

Akijibia hilo Mtoa huduma kupitia king`amuzi cha Agape alisema kufanya hivyo ni moja ya kuhamasisha walengwa watambue wajibu wa kulipa ada na wasipofanya hivyo hawalipi ni hasara katika uendeshaji wa mfumo wa digitali .

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMPOKEA MAKAMU WA RAIS DR. GHARIB BILAL MKOANI ARUSHA

1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA tayari kwa kumpokea Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe ambaye atafungua mkutano wa Vijana Viongozi wa Afrika na China unaofanyika kwenye hoteli ya Ngurudoto mkoani Arusha ukijumuisha vijana kutoka China na nchi za kiafrika. Dr. Gharib Bilal alipokelewa na katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurlahman Kinana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Arusha.2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA 3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Kulia ni Ndugu Andulrahman Kinana Katibu Mkuu wa CCM.4Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA mkoani Arusha kwa ajili ya mkutano wa Vijana viongozi wa Afrika na China, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Felix Ntibenda na kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Steven Masele Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo na Sadifa Hamis Juma 
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa.
 9 
8

RAIS ROBERT MUGABE WA ZIMBABWE AWASILI ARUSHA TAYARI KWA KUFUNGUA MKUTANO WA VIJANA VIONGOZI WA CHINA NA AFRIKA NGURUDOTO

13 14Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akishuka kwenye Ndege wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro International Airport (KIA) tayari kwa kuufungua mkutano wa Vijana Viongozi wa Afrika na China (African- China Young Leaders Forum) unaofanyika kwenye hoteli ya Ngurudoto Mkoani Arusha kwa siku 4 ukijumuisha vijana kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na China, Mzee Robert Mugabe amepokelewa na Makamu wa Rais Mh. Dr. Gharib Bilal kulia na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi mbalimbali wa CCM na serikali mkoani Arusha. MUGABE NA KINANARais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa KIA mkoani Arusha. 17Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akiongozana na mwenyeji wake Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA. 18Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akiongozana na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Gharib Bilal. 20Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe na Mwenyeji wake Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal wakiangalia vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa mapokezi, kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. 21Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati walipokuwa wakiangalia vikundi vya ngoma vikitoa burudani. 22Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe, Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto wakiangalia vikundi vya ngoma. 24Rais Mugabe na mwenyeji wake Mamaku wa Rais Dr. Gharib Bilal pamoja na viongozi wengine wakielekea kwenye chumba cha mapumziko kwenye uwanja wa Ndege wa KIA. 25Mwenyekiti wa Kamati ya Maandaliazi Mh. Steven Masele akizungumza na vyombo vyahabari kwenye uwanja wa KIA mara baada ya kuwasili kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.

WANAFUNZI WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA(TPSC) TAWI LATANGA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO PSPTB

1
Wageni wakiwasili kwenye ofisi za Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (3)
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa PSPTB, Dr Tesha akitoa hutuba ya ufunguzi kuwakaribisha wanachuo wa mwaka wa pili wa stashahada ya Ununuzi na Ugavi kutoka chuo cha TPSC Utumishi wa Umma tawi la Tanga.
New Picture (4)
Wanachuo wakimsiliza Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Bodi Dr. Tesha.
New Picture (5)
Mkurugenzi ya Mafunzo, Bw. Godfred Mbanyi akielezea juu ya madaraja ya mitihani ya Bodi na taratibu za kufanya mitihani.
New Picture (7)
Bw. Ally Songoro kutoka Kurugenzi ya Taaluma akifafanua jambo, juu ya taratibu za usajili, miiko ya wanataaluma kwa wanachuo waliotembelea Bodi.
New Picture (9)
Bw. Paul Bilabaye kutoka Kurugenzi ya Fedha na Utawala akielezea taratibu za malipo ya huduma mbalimbili zitolewazo na Bodi.
New Picture (10)
Mwanachuo mmoja akiuluza maswali juu ya kazi mbalimbali za Bodi Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (11)
Mmoja wa wanachuo akiuliza maswali juu ya kazi mbalimbali za Bodi Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (1)
Wanachuo wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye ofisi za Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi.
New Picture (2)
Baadhi ya wanafunzi kwenye picha ya pomoja pamoja na mkurugenzi Mkurugenzi mtendaji wa Bodi Dr. Clemence Tesha na viongozi waandamizi wa Bodi.
.....................................................................

Na Mwandishi wetu
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imepokea ugeni wa wanachuo sabini wa mwaka wa pili wanaosoma stashahada ya ununuzi na ugavi waliokuja kwenye ziara ya mafunzo kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tanga. Ziara hiyo ya mafunzo ililenga kujua kazi mbalimbali za Bodi ya wataalam wa ununuzi na Ugavi (PSPTB). 

  Mkurugenzi mkuu Mtendaji wa PSPTB Dr Clemence Tesha, aliupokea ugeni huo, na kuwashukuru kwa kuona nia ya kufanya ziara ya mafunzo. 

Aidha aliwaelezea umuhimu wa kuzingatia maadili , kujifunza kwa bidii ili kupata maarifa na ujuzi unaoweza kuhimili soko la ushindani la ajira . Wanachuo pia walielezewa juu ya taratibu za mitihani ya Bodi yenye ngazi ya cheti cha awaliAwali, msingi Msingi na Taaluma. 

Aidha aliwaelezea taratibu za kusajii kwa ajili ya kufanya mitihani ya kitaaluma mara baada ya kumaliza masomo yao na kwamba mhitimu wa stashahada ya ununuzi na ugavi kwa chuo kinachotambuliwa na Bodi anaanzia ngazi ya kwanza ya mitihani ya taaluma.

 Mitihani ya taaluma ina ngazi tano, ambazo huhitimishwa kwa wanafunzi kufanya mitihaniutafiti. 

Ziara hiyo pia ilitoa fursa kwa wanachuo hao kujua taratibu za kujisajili kama wataalum wataalam wa Ununuzi na Ugavi kwani ni hitaji la sheria iliyounda Bodi. 

Aidha walifahamishawa kwamba kuna ngazi mbalimbali za usajili ambazo zinatambua kiwango cha ujuzi na uzoefu wa mtaalam. “ fanyeni usajili mara mmalizapo chuo ili kutumia fursa za ajira katika fani yenu “ ” alisisitiza. 

 Tambueni kwamba taaluma ya ununuzi na ugavi inaongozwa na misingi ya maadili ambayo inawataka kutambua kuwa mnawajibika kwa umma wa watanzania, taaluama yenu, mwajili wako. Misingi hii ya wajibu ndio inayoifanya taaluma hii iwe ya kipekee. “maadili huanzia