Pages

KAPIPI TV

Friday, March 20, 2015

MADIWANI WA MANISPAA YA LINDI WATEMBELEA MRADI MAPINGA SATELLITE WA UTT-PID ULIOPO BAGAMOYO

Diwani wa Kata ya Nachingwe, Lindi Mjini, Omary Chitanda (katikati) akiuliza swali kwa mtaalamu wa mradi huo
Diwani wa Kata ya Nachingwe, Lindi Mjini, Omary Chitanda (katikati) akiuliza swali kwa mtaalamu wa mradi huo.

*Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID) ilianza kazi zake Julai 1, 2013. Taasisi hii ilirithi kazi za miradi zilizokuwa zinafanywa na Taasisi mama yaani UTT.
Andrew Chale wa Mo dewji blog aliyekuwa Bagamoyo

Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Lindi Machi 17, wametembelea miradi mbali mbali ya UTT-PID iliyopo Dar es Salaam ikiwemo ule wa Bagamoyo wa New Mapinga Satellite.
Madiwani hao waliweza kujifunza mambo mbalimbali dhidi ya mradi huo ulivyoandaliwa na kufanya kazi na namna ulivyopangiliwa kwa ustadi mkubwa.

Katika ziara hiyo inayotarajia kumalizika Machi 19, mwaka huu. Madiwani hao wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaaa ya Lindi, Frank Magali alipongea juhudi za UTT-PID kwa kufanikisha ziara hiyo kwani wamejifunza mengi na pindi watakaporejea Lindi, watakuwa mfano wa kuigwa.

“Kule kwetu Lindi pia tuna mradi uliopo katika hatua mbaali mbali na UTT-PID tayari wamesha pima baadhi ya viwanja katika mfumo kama huu wa kisasa tunaojifunza hapa hivyo itatusaidia sana kwa sasa” alisema Meya Magali.
Diwani wa Kata ya Nachingwea, Manispaa ya Lindi, Omari Chitanda akielezea namna alivyojifunza kwenye mradi huo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani)
Diwani wa Kata ya Nachingwea, Manispaa ya Lindi, Omari Chitanda akielezea namna alivyojifunza kwenye mradi huo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani).

Kwa upande wake, Diwani wa Nachingwea, Omari Chitanda alieleza kuwa, wamepata kuielewa vyema UTT-PID na naamna ya ufanyaji wake wa kazi.

“tunaipongeza UTT-PID kwani imetufungulia mwangaza wa kimaendeleo. Tutakapo rejea Lindi tutaenda kufanya mambo ya kimaendeleo katika kuubadilisha mji wetu” alisema Diwani Chitanda.

Aidha kwa upande wake msimamizi wa mradi huo wa Mapinga kutoka UTT-PID, Godfrey Charles alisema kuwa hdi sasa mradi huo umefanikiwa kwa kiwango ambapo tayari vimebaki viwanja vichache kati ya zaidi ya 500 vilivyochukuliwa.
Madiwani na maofisa kutoka UTT-PID wakifuatilia kwa makini maelezo ya msimamiz wa mradi huo wa Mapinga uliochini ya UTT-PID (Hayupo pichani
Madiwani na maofisa kutoka UTT-PID wakifuatilia kwa makini maelezo ya msimamizi wa mradi huo wa Mapinga uliochini ya UTT-PID (Hayupo pichani).

Pia madiwani hao, walipata elimu pamoja na ufanyaji wa kazi wa UTT-PID na wadau wanaoshirikiana nao huku hadi sasa ikiwa inasimamia miradi mbalimbali ikiwemo mikoa ya Pwani, Morogoro, Kagera, Dar es Salaam, Lindi na mikoa mingine hapa Nchini.
Aidha, kwa upande wa Madiwani hao walipongeza UTT-PID kwa hatua hiyo ya kuwapa elimu sambamba na kutembelea baadhi ya miradi inayoendeeshwa na taaisis hiyo.
..
New Mapinga Satellite town located 30km from Mwenge along new Bagamoyo road with hundreds of serviced plots for residential, commercial and trade purpose ready for sale. The town is fully installed with electrical, water and roads facilities.
DSCN9635
DSCN9651
DSCN9663
madiwani wa Lindi wakijadili jambo
Madiwani wa Lindi wakijadili jambo.

Wednesday, March 18, 2015

USIKOSE KIPINDI CHA NIAMBIE LIVE ,Ep1

Omby Nyongole, Salma Moshi na Queen Mkelemi
Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE
Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii. Pia kupata Tip ya siku / wiki kusaidia kuboresha maisha yako.
Ni Niambie Live....

MADIWANI WA MANISPAA YA LINDI WATEMBELEA MIRADI YA UTT-PID

Mkurugenzi Mkuu wa UTT-PID, Dk. Gration Kamugisha (kulia) akielezea juu ya Taasisi hiyo juu ya utendaji wa kazi zake hapa Nchini, kushoto kwake ni Naibu Meya wa Manispaa ya Lindi, Amida Abdala
Mkurugenzi Mkuu wa UTT-PID, Dk. Gration Kamugisha (kulia) akielezea juu ya Taasisi hiyo juu ya utendaji wa kazi zake hapa Nchini, kushoto kwake ni Naibu Meya wa Manispaa ya Lindi, Amida Abdallah na pichani chini kulia ni Mstahiki Mstahiki Meya wa manispaa ya Lindi, Frank Magali.
UTT-PID
Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Lindi, wakiendelea na mafunzo hayo kutoka kwa maofisa wa UTT-PID (hawapo pichani)
Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Lindi, wakiendelea na mafunzo hayo kutoka kwa maofisa wa UTT-PID (hawapo pichani).
Baadhi ya Madiwani kutoka Halmashahuri ya Lindi wakifuatilia mafunzo ya elimu juu ya ufanyaji wa kazi wa UTT-PID
Baadhi ya Madiwani kutoka Halmashahuri ya Lindi wakifuatilia mafunzo ya elimu juu ya ufanyaji wa kazi wa UTT-PID.
Baadhi ya Wahandisi wa Halmashahuri ya Manispaa ya Lindi wakifuatilia mafunzo hayo ya UTT-PID
Baadhi ya Wahandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wakifuatilia mafunzo hayo ya UTT-PID.
Diwani akifuatilia mafunzo ya UTT-PID
Diwani akifuatilia mafunzo ya UTT-PID.
madiwani  wa Manispaa ya Lindi wakifuatilia mkutano huo wa UTT-PID jijini Dar es Salaamk
Madiwani wa Manispaa ya Lindi wakifuatilia mkutano huo wa UTT-PID jijini Dar es Salaam.
madiwani  wakifuatilia mkutano huo wa UTT-PID  uliokuwa unafanyika jijini Dar es Salaam
Pichani juu na chini ni madiwani wakifuatilia mkutano huo wa UTT-PID uliokuwa unafanyika jijini Dar es Salaam.
madiwani  wakifuatilia mkutano huo wa UTT-PID
madiwani wa Manispaa ya Lindi wakiendelea kufuatilia mkjutano huo wa UTT-PID
Mdiwani wakiendelea na mfunzo haayo ya UTT-PID
Madiwani wakiwa kwenye mafunzo hayo ya UTT-PID.

Na Andrew Chale wa Mo dewji blog
Madiwani wa Manispaa ya Lindi wapo jijini Dar es Salaam katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo mbinu iliyo chini Wizara ya Fedha (UTT-PID), iliyopo jijini Dar es Salaam na nje ya Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza na kuelewa utendaji wa kazi wa taasisi hiyo hapa nchini.

Katika ziara hiyo inayotarajia kumalizika Machi 19, mwaka huu. Mapema leo Machi 16, Madiwani hao wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaaa ya Lindi, Frank Magali waliweza kupatiwa elimu juu ya utendaji kazi wa taasisi hiyo ya UTT-PID na miradi inayoendesha hapa nchini.

Miongoni mwa elimu hiyo ni pamoja na ufanyaji wa kazi wa UTT-PID na wadau wanaoshirikiana nao huku hadi sasa ikiwa inasimamia miradi mbalimbali ikiwemo mikoa ya Pwani, Morogoro, Kagera, Dar es Salaam, Lindi na mikoa mingine hapa nchini.

Awali akiwakaribisha madiwani hao wa Manispaa ya Lindi, Mkurugezi Mkuu wa UTT-PID. Dk. Gration Kamugisha alieleza kuwa, UTT-PID imekua ikifanya kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo viongozi wa Siasa, wananchi, wadau na wabia binafsi pamoja na serikali katika kutekeleza mipango yake.

“Karibu sana UTT-PID, miradi yetu tunafanya kwa kushirikiana na watu mbalimbali. Wakiwemo wanasiasa, ndio maana leo tupo nanyi Madiwani ambao munawawakilisha wananchi huko munako toka” alieleza Dk. Gration Kamugisha.

Aidha, kwa upande wa Madiwani hao walipongeza UTT-PID kwa hatua hiyo ya kuwapa elimu sambamba na kutembelea baadhi ya miradi inayoendeeshwa na taasisi hiyo.

ZIARA YA LUKUVI MKOANI ARUSHA YAANZA

Monday, March 16, 2015

TAHARIRI: JUHUDI HIZI ZA WAZIRI MKUU PINDA KUSAIDIA SHULE ALIYOSOMEA ZIUNGWE MKONO

photo 4
Pichani juu na chini ni baadhi ya majengo yaliyokamilika ya Shule ya msingi Kakuni yaliyojengwa na Waziri Mkuu Pinda kupitia michango ya wadau wa maendeleo.

Na Andrew Chale wa modewji blog
Kila mmoja wetu anatambua mchango mkubwa wa elimu hasa ile inayotolewa ikiwemo ngazi ya Awali, Msingi, Sekondari na elimu ya juu ikiwemo chuo. 

Pia katika hilo ni jamb la msingi sana na la maana hasa unapokumbuka mahala ulipopatia elimu husika.

Waziri Mkuu alipaata elimu yake katika Shule ya msingi Kakuni. Kwa kusoma hapo darasa la kwanza hadi la nne. Lakini kwa mapenzi mema na juhudi za kutaka kuona watoto wa hali ya chini hasa wa wakulima wanapata elimu bora, kwa juhudi zake binafsi, ameweza kusaidia shule hiyo ikiwemo kutafuta wafadhili mbalimbali wa kuipiga tafu, akiwa kama Mizengo Pinda. Ambapo unaweza kusoma kiunganishi hichi hapa cha mtandao ili kusoma habari hiyo zaidi ya wadau kumuunga Waziri Mkuu Pinda katika kuisaidia shule ya Kakuni: photo 1
Mtandao huu unapongeza juhudi hizo za Waziri Mkuu Mizengo Pinda hivyo pia nawe ukiwa ni miongoni mwa unayeguswa na maendeleo ya elimu hapa nchini, ni wakati wa kutembelea shule yako uliosoma awali iwe elimu ya ‘vidudu’ yaani Chekechea/Awali, Shule ya Msingi ama Sekondari basi ni wakati wa kurejea na kusaidia chochote kile ili kuendeleza Elimu hapa Nchini.

Bila shaka kama Watanzania tutaiga juhudi hizi za Waziri Mkuu Mizengo Pinda, bila shaka elimu ya Tanzania itapanda maradufu kwani tumeweza kushuhudia kwa upande wa juhudi hizo za Mizengo Pinda ikiwemo kushawishi wadau ikiwemo Serikali ya Japan, kutoa msaada wa dola za Marekani, 90,286, ambazo ni sawa na Sh. Milioni 160.

Fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule ya Awali kwenye Shule ya Msingi, Kakuni iliyopo kijiji cha Kibaoni, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi.
PM-PINDA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda.

Juhudi za Mizengo Pinda za kuanzisha wazo hilo la kusaidia kuijenga shule yake ni kama njia ya kumshukuru Mungu na kuwashukuru wananchi waliosaidia kumfikisha hapo alipo.

Kwani alipata kusoma darasa la kwanza hadi la nne katika shule ya msingi Kakuni mwaka 1957 hadi 1960.

Hivyo, tunatambua wapo wasomi wengi, wapo wabunge, wapo Mawaziri, wapo Wakurugenzi na wengine wenye vyeo vikubwa Serikali, sekta binafsi na waliopo ndani nje ya nchi, shime tujitokeze kwa wingi kwa kila mmoja kwenda kwenye shule aliyosoma na kuchangia chochote.

Tunatambua sisi tumepata elimu wakati gani na kiwango cha elimu wakati huo kilikuwaje, hivyo tutakapojitokeza kama alivyofanya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, hii itasaidia kukuza elimu yetu hapa Nchini.
photo 3
Muonekano wa majengo yaliyokamili ya shule ya msingi Kakuni alipopata elimu ya msingi Waziri Mkuu Pinda na kuamua kuijenga upya kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.3/- kutokana na michango ya wadau mbalimbali wa maendeleo.
photo 5

NCAA, UNESCO WAANGALIA UTALII ENDELEVU NGORONGORO

DSC_0015
Mkufunzi ambaye pia ni mtaalamu mshauri wa Unesco, katika masuala ya utalii endelevu, James Banks akiendesha mafunzo kwenye warsha ya siku nne ya kutengeneza mkakati wa utalii endelevu hifadhi ya Ngorongoro iliyomalizika mwishoni mwa wiki mji mdogo wa Karatu, mkoani Arusha na kuandaliwa na Shirika la UNESCO kwa kushirikiana na Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA). Pichani chini kulia ni Mmoja wa wakufunzi wa warsha hiyo, Tamim Amijee.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na modewjiblog, Karatu
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) likishirikiana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wameandaa kongamano la siku nne lililofanyika mjini hapa kuangalia mkakati mpya wa kuendeleza utalii kama kitovu cha mapato katika hifadhi ya Ngorongoro.

Kongamano hilo ni moja ya makongamano kadhaa ambayo yameandaliwa kwa pamoja kwa lengo la kutoa mwelekeo mpya katika hifadhi hiyo ambayo binadamu na wanyama huishi pamoja.

Akizungumza na mtandao huu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues, alisema kwamba kongamano hilo limeandaliwa kwa lengo la kujenga uwezo kwa wadau mbalimbali wa sekta ya utalii kutambua haja ya utalii endelevu ambao pia utazingatia maslahi ya wananchi wanaoishi katika eneo hilo.

Alisema wakati NCAA inaangalia upya mkakati wake wa maendeleo katika hifadhi hiyo ambayo pia ni urithi wa dunia, UNESCO kama washirika wa karibu wamekubaliana kuendesha kongamano ambapo wadau wote kuanzia wananchi wanaoishi katika hifadhi hiyo na waendesha utalii zikiwemo hoteli na watawala kuangalia namna bora ya kuendesha hifadhi na kuneemesha wananchi.
DSC_0207
Zulmira alisema kwamba hifadhi hiyo inaingiza fedha nyingi ambazo zingeweza pia kuwafikia wananchi moja kwa moja kwa kuanzisha mikakati ambayo inahusisha wananchi wenyewe na wadua mbalimbali wa sekta hiyo.

Alisema kwamba idadi ya watalii wanaoingia hapo wanaingiza fedha nyingi serikali kuu lakini kiasi hicho hakionekani wazi wazi kwa wananchi na hivyo ipo haja ya kuangalia mwelekeo mpya ambao utaendelea kuhifadhi urithi huo huku wananchi wake wakifaidika na uwapo wa urithi huo.

Wakati wa kongamano hilo washiriki walifanya ziara katika maeneo mbalimbali ya kitalii kabla ya kufanya majadiliano na kuweka mwelekeo wa namna bora ya kutengeneza mkakati utakaoshirikisha wadau wote wa utalii katika eneo hilo.

Alisema kwa muda mrefu tangu hifadhi hiyo iwe urithi UNESCO na NCAA walikuwa wakiangalia zaidi suala la hifadhi kiasi cha wananchi kuona kama wameachwa nyuma hivyo mkakati wa sasa ni kuwawezesha wananchi kufaidi matunda ya urithi huo kwa kila kada kupewa wajibu wake na kuona namna ya kuutekeleza ili ndoto iwe kweli.
DSC_0030
Mkufunzi ambaye pia ni mtaalamu mshauri wa Unesco, katika masuala ya utalii endelevu, James Banks akiwaelekeza jambo washiriki wa warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa wiki mji mdogo wa Karatu, mkoani Arusha.

“Tumedhamiria kujenga uwezo… kusaidia wananchi kuongeza kipato chao kutoka kwa watalii … ukiangalia katika kreta unaweza kuona magari mengi yakiwa na watalii… tunataka watu wanaoishi katika eneo hili pia wafaidike …” alisema.

Hifadhi hii inatambulika duniani kwa kreta yake kubwa, mbuga yenye wanyama wengi na eneo ambalo inasadikiwa binadamu wa kwanza aliishi kabla ya kutawanyika duniani
Ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 8,300 Hifadhi ya Ngorongoro ndio hifadhi pekee duniani ambapo wanadamu wanaishi pamoja na wanyama kwa usalama.

NCA ilianzishwa mwaka 1971na kutangazwa kuwa urithi wa dunia na UNESCO mwaka 1979 lakini kwa muda sasa kumekuwepo na mawazo kwamba dhima kubwa imekuwa kulinda wanyama na mazingira na kusahaua kwamba pale pana binadamu ambao wanamahitaji na wanataka kufaidika pia na mazingira ambayo wanayalinda.
DSC_0164
Pichani juu na chini ni washiriki na wadau wa sekta ya utalii kwenye warsha ya siku nne ya kutengeneza mkakati wa utalii endelevu hifadhi ya Ngorongoro iliyomalizika mwishoni mwa wiki mji mdogo wa Karatu, mkoani Arusha na kuandaliwa na Shirika la UNESCO kwa kushirikiana na Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA).

Kwa mwaka zaidi ya watalii 450,000 huzuru Ngorongoro ikiwa ni asilimia 60 ya watalii wanaofika nchini.

Mtaalamu mshauri wa Unesco, James Banks, ameelezea kufurahishwa kwake na kongamano hilo na kusema kwamba linatoa mwanya wa wadau mbali mbali muhimu Ngorongoro kuona mwelekeo mpya unaostahili kuchukuliwa ili kuwa na utalii endelevu.

Alisema matokeo ya mkakati huo sio tu utaongeza mapato serikalini bali pia utaimarisha utalii kutokana na ushiriki wa moja kwa moja wa jamii zinazoishi ndani ya hifadhi hiyo.

Mshiriki mwingine wa kongamano hilo Flora Assey, Afisa Utalii kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha alielezea kufurahishwa na kongamano hilo hasa kwa kuchukua mlengo wa masomo kwa vitendo hali ambayo anaamini itabadili kabisa utekelezaji wa mkakati unaobuniwa kwa sasa.
DSC_0035
Naye Meneja mkuu wa Ngorongoro Serena Safari Lodge, Dismas Simba alielezea kuridhishwa kwake na kongamano hilo na kusema litawezesha wadau wote kufanyakazi kwa pamoja kuhakikisha kwamba utalii unakuwa endelevu katika eneo hilo hasa kwa kuzingatia kwamba eneo hilo ndilo pekee duniani ambako wanyama na wanadamu wanaishi pamoja.

Naye Ofisa Mwandamizi wa Miradi na Mratibu wa UNESCO katika masuala ya urithi wa dunia na utalii endelevu, Peter DeBrine amepongeza hatua iliyofikiwa na wadau katika kongamano hilo na kusema raundi ya pili Juni mwaka huu itatoa mwangaza zaidi kwani utarejesha majibu ya maswali ambayo kila mtu amepewa kuyafanyia kazi.

Alisema amefurahishwa na kiwango cha kujituma cha wajumbe waliofika katika kongamano hilo na kusema kwa jinsi ilivyo mabadiliko yanayofikiriwa na NCAA yatafanikiwa ili wananchi nao wawe wanafaidika moja kwa moja na uwapo wa urithi huo wa dunia katika maisha yao.
DSC_0042
DSC_0233
Flora Assey, Afisa Utalii kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha akinakili mambo muhimu wakati wa kuhitimisha warsha hiyo ya siku nne iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Kudu Lodge and Campsite iliyopo mji mdogo wa Karatu mkoani Arusha.
DSC_0106
Mwenyekiti wa Baraza la wakina Mama kata ya Oloirobi, Kijiji cha Mokilal mkoani Arusha, SEKETO OLDUMU akishiriki kwenye kikundi kazi wakati wa warsha ya siku nne ya kutengeneza mkakati wa utalii endelevu hifadhi ya Ngorongoro iliyomalizika mwishoni mwa wiki mji mdogo wa Karatu, mkoani Arusha na kuandaliwa na Shirika la UNESCO kwa kushirikiana na Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA).
DSC_0057
Meneja Mkuu wa Ngorongoro Crater Lodge | &BEYOND, Markus Schroeder (kulia) akishiriki kuchangia maoni wakati wa warsha ya siku nne ya kutengeneza mkakati wa utalii endelevu hifadhi ya Ngorongoro iliyomalizika mwishoni mwa wiki mji mdogo wa Karatu, mkoani Arusha. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni (UNESCO) Zulmira Rodrigues.
Kwa matukio zaidi bofya hapa

IDD AZZAN ATOA MSAADA WA KITI CHA MAGURUDUMU KWA MLEMAVU JIMBONI KWAKE

0D6A5197
Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mh. Iddi Azzan akikabidhi kiti maalum cha kujisaidia pamoja na kiti cha magurudumu kwa mama huyo mlemavu.

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mh. Iddi Azzan (CCM) ametoa msaada wa kiti cha magurudumu kwa Rehema Nditi mkazi wa Magomeni Mwembe Chai kama msaada kutokana na taabu aliyokuwa akiipata.

Idd Azzan ametoa msaada … ambapo baada ya kuona Rehema Nditi kupataa tabu ya kukosa kiti hicho.

Mbunge huyo amekua akisaidia maendeleo mbalimbali ikiwemo shughuli za kijamii ndani ya jimbo lake hilo.

Aidha, Mh. Iddi Azzan ametoa rai kwa Watanzania kuungana nae katika kuchangia pesa kwa ajili ya kununua Bajaji ambayo itafanya biashara ili waweze kuendesha maisha ya kila siku.

“Watanzania tuungane kumchangia mama huyu kiasi chochote ilikununua bajaji kwa ajili ya kufanya biashara ili waweze kuendesha maisha yao ya kila siku kupitia kipato cha biashara hiyo ya Bajaji” alieleza Idd Azzan.

Kwa upande wake, Mtangazaji wa kipindi cha "Mimi na Tanzania, Kinachoerushwa na kituo cha Channel Ten, Hoyce Temu amefungua michango hiyo kwa kutoa kiasi cha Tsh. 500,000/- ili kuhamasisha na wengine kuchangia.

Michango hiyo inaweza kuwasilishwa kwenye ofisi za Mbunge wa jimbo la Kinondoni ama unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Rehema Nditi kupitia namba TIGO PESA +255 719-543075 AU M-PESA +255 754 097 527
0D6A5129

Saturday, March 14, 2015

WAJAWAZITO WAASWA KUHUDHURIA KLINIKI YA UZAZI MAPEMA

Baadhi ya akinamama wanaoishi na virus vya Ukimwi katika Tarafa ya Ilolangulu wilayani Uyui mkoani Tabora wakiwa na Afisa habari na Mawasiliano ya Umma wa Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kupambana na Maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi EGPAF,Bi.Mercy Nyanda



ILI kuepuka madhara mbalimbali yatokanayo na uzazi, akina mama wajawazito mkoani Tabora wameaswa kuanza huduma za kliniki mapema sana ili kutunza ujauzito wao vizuri kupitia huduma za afya ya uzazi kwa mama na mtoto zinazotolewa katika vituo mbalimbali vya afya.
 
Mama mjawazito akienda kliniki hufanyiwa uchunguzi wa afya yake ili kubaini kama ana upungufu wa aina yoyote ile mwilini au maambukizi ya virusi vya ukimwi na inapobainika huanzishiwa matibabu mara moja ili kuimarisha afya yake na kumlinda mtoto atakayezaliwa asije akadhurika.


 Hayo yamebainishwa jana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Gunini Kamba alipokuwa akielezea hali ya afya za akinamama wajawazito mkoani humo kwa Mratibu wa Mawasiliano wa Shirika lisilo la kiserikali la EGPAF Bi.Mercy Nyanda aliyeambatana na Mratibu wa huduma za afya ya uzazi Dr. Samson Kishumbu na waandishi wa habari.

Kamba alisema ni muhimu sana akina mama wajawazito wakaanza huduma za kliniki mapema kwani hii itawasaidia kutunza afya zao vizuri na hata mtoto atakayezaliwa atakuwa na afya bora lakini wakichelewa wakaanza kliniki dakika za mwisho hawawezi kutimiza uchunguzi unaostahili.


‘Ni hatari sana kwa mama mjamzito kutohudhuria kliniki mapema au kuhudhuria mara chache tu na hasa dakika za mwishoni hii inaweza kuathiri afya yake au ya mtoto na hatimaye kushindwa kujifungua salama ikiwemo kupoteza maisha yake na mtoto, au kumwambukiza mtoto ugonjwa wa ukimwi’, aliongeza.


Alibainisha kuwa ni hatari sana kwa mama mjamzito kujifungulia majumbani ama kwa wakunga wa mitaani kwani athari zake kwa afya ya mama na mtoto ni kubwa sana huku akibainisha mkakati wa serikali wa 0-0-0 yaani kuhakikisha maambukizi mapya ya ukimwi yanabaki 0, unyanyapaa 0 na vifo vitokanavyo na maambukizi 0.


Alieleza kuwa ili mkakati huu wa serikali ufanikiwe hatuna budi kuhamasisha akinamama wajawazito wote wajifungulie kwenye vituo vya afya sambamba na kuwahamasisha wapitie hatua zote 4 za mahudhurio ya kliniki ili kuwa na afya zilizo bora zaidi kwa mama na mtoto.

Akizungumzia changamoto zinazowakabili, Kamba alisema akina mama wengi wanaobainika kuwa na maambukizi ya VVU wanaanzishiwa matibabu lakini baada ya mda wanakimbia, hawafiki tena kliniki, huku akibainisha kuwa wale wanaohudhuria kliniki kwa uaminifu afya zao ni nzuri sana, na hata watoto wadogo walio na maambukizi wana afya njema.

Awali Mratibu wa Mawasiliano wa shirika hilo Mercy Nyanda alieleza kuwa EGPAF imeazimia kuzuia maambukizi mapya toka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto na vifo vyote vitokanavyo na uzazi, ili kufanikisha haya jamii ni lazima ihabarishwe ili ijue nini inatakiwa kufanya.


Baadhi ya akinamama wanaoishi na VVU katika kata ya Ilolangulu wilaya ya Uyui mkoani hapa walitoa ushuhuda wao wazi wazi pasipo kificho jinsi walivyogundua kuwa na maambukizi baada ya kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito na kuanzishiwa matibabu sambamba na kupewa ushauri nasaha uliowawezesha kujifungua watoto wenye afya nzuri na wasio na VVU.


Akinamama hao Martha Steo (29), Tamasha Mussa (32) na Jenifa Japheti (25) mbali na kutoa wito kwa watu wote kujitokeza kupima afya zao ili wapate huduma mapema walitoa shukrani zao kwa watoa huduma za afya ya uzazi na kwa shirika la EGPAF kwa jinsi wanavyowahudumia vizuri mpaka sasa kiasi kwamba wana afya njema na watoto wao.