Pages

KAPIPI TV

Monday, March 23, 2015

WAZIRI LUKUVI AFUNGUA NYUMBA ZA NHC MRARA BABATI

1

Sunday, March 22, 2015

TANZANIA CHILDREN'S PROJECT YAFANYA HARAMBEE KUSAIDIA WATOTO TANZANIA COLUMBIA,MARYLAND

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akihudhuria harambee ya Tanzania Children's Project inayoshughulisha na miradi ya afya na elimu Tanzania iliyofanyika siku ya Jumamosi March 21, 2015 Columbia, Maryland. Kulia ni Timothy Lynch ambaye ni Rais wa NGO hiyo, Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliongozana na Afisa wa Ubalozi Switebert Mkama(pichani kushoto)
Rais wa Tanzania Children's Project Bwn. Timothy Lynch katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.
Wadau mbalimbali waliohudhuria harambee ya Tanzania Children's Project iliyofanyika siku ya Jumamosi March 21, 2015 Columbia, Maryland nchini Marekani.
 
picha ya pamoja
Picha ya pamoja
 
Kikundi cha muziki kikitoa burudani.

Saturday, March 21, 2015

ZIARA YA WAZIRI WA ARDHI MH. WILLIAM LUKUVI BABATI MKOANI MANYARA

1aMkuu wa mkoa wa Manyara ,Mhe.Joel Nkaya Bendera akizungumza katika kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa huo kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati,kushoto ni Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Babati,Crispin Meela.Mhe.Bendera amesisitiza nidhamu ya kazi katika kuhudumia wananchi na ameapa kuwaondoa watendaji wabovu mkoani humo.
2aWaziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akizungumza katika kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa wa Manyara kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati.Ameuagiza uongozi wa mkoa huo kumaliza migogoro ya ardhi ifikapo mwezi Mei mwaka huu.
3aMratibu wa Tume ya Waziri Mkuu ya kuhakiki na kuweka mipaka kwenye maeneo yenye migogoro ya ardhi mkoani Manyara,ambaye pia ni Mrasimu Ramani Mwandamizi,Bw.Benedict Mugambi akitoa maelezo ya hatua waliyofikia katika kuweka mipaka mkoani Manyara na kusema kuwa migogoro mingi ya mipaka inasababishwa na wanasiasa. 4aBaadhi ya watendaji wa sekta ya Ardhi Kanda ya Kaskazini na baadhi ya waheshimiwa wabunge akiwemo Mbunge wa Kiteto,Benedct Ole Nangoro na Mbunge wa Viti Maalum,Pauline Gekul wakifatilia maelekezo ya Mhe Lukuvi alipozungumza na watendaji wa mkoa wa Manyara jana.
5aWananchi wa mkoa wa Manyara wakimsikiliza Waziri wa Ardhi(hayupo pichani)alipokutana nao kusikiliza kero za migogoro ya ardhi inayosababishwa na watendaji wa sekta hiyo kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Babati.
6aWananchi wa mkoa wa Manyara wakipeana maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Ardhi ya namna ya kuwasilisha malalamiko yao kwa maandishi alipokutana nao kusikiliza kero za migogoro ya ardhi inayosababishwa na watendaji wa sekta hiyo kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Babati.
7aWaziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akizungumza na wananchi wa mji wa Babati waliojitokeza kuwasilisha kero zao zinahusu migogoro ya ardhi.Kikao hicho kilihudhuriwa pia na wabunge wa mkoa wa Manyara.
8aBaadhi ya watendaji wa wizara ya ardhi wakiratibu malalamiko ya wananchi katika kikao kilichofanyika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Babati,mkoa wa Manyara. 9aKatibu Tawala wa mkoa wa Manyara,Mhandisi Omar Chambo akisoma taarifa ya migogoro ya ardhi mkoani humo kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Vangimembe Lukuvi kwenye ziara yake ya kusikiliza kero za ardhi.

Friday, March 20, 2015

KINANA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI ARUSHA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya kikazi ya mkoa wa Arusha akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali ya CCM na kuhimiza uhai wa Chama Cha Mapinduzi CCM akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-ARUSHA)2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kuchimba mfereji wa kupitisha mabomba ya maji katika mradi wa maji kata ya Olmot Olkaryan jijini Arusha. 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kufungua maji ya bomba katika mradi wa maji kata ya Olmot Olkaryan jijini Arusha. 4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kuchimba mfereji wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Sombetini kwa Mromboo jijini Arusha. 5Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Sombetini kwa Mrombo mara baada ya kukagua barabara hiyo jijini Arusha. 7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi mbalimbali jijini Arusha. 8Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua shina la wakereketwa la Sakina kwa Shamsi Arusha Raha jijini Arusha. 9Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa pili kutoka kushoto akiongozana na Nape Nnauye na viongozi wa mkoa na wilaya ya Arusha wakati akielekea kutembelea soko la Kirombero jijini Arusha. 10Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana wakati alipowasili katika soko la Kilombero jijini Arusha. 11Kada wa CCM Viola naye akimwaga maneno ya sumu wakati wa mkutano wa katibu Mkuu wa Ndugu Abdulrahman Kinana na wafanya biashara wa soko la Kilombero jijini Arusha. 13Nape Nnauye akizungumza na umati wa wafanyabiashara na baadhi ya wananchi mbele ya jengo la Soko la Kilombero jijini Arusha. 14Baadhi ya wafanyabiashara na wananchi wakiwa katika mkutano huo. 15Kiongozi wa wafanyabiashara wa soko la Kilombero jijini Arusha akisoma risala kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana huku Nape Nnauye akiwa amemshikia kipaza sauti. 10Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili katika soko la Kilombero jijini Arusha. 17Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika kata ya Remala Arusha kulia ni Diwani wa kata hiyo Bw.Karim Mushi. 18Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi pikipiki Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana Maendeleo Group Peter Samwel iliyotolewa na diwani wa kata ya Remala Bw. karim Mushi kulia. 19 Mwenyekiti wa kikundi cha Vijana Maendeleo Group Peter Samwel akijaribu kuendesha pikipiki mara baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pikipiki hiyo imetolewa kwa kikundi hicho na diwani wa kata ya Remala Bw. Karimu Mushi

MAMA WA MITINDO ASIA IDAROUS KUPAMBA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI ZANZIBAR MARCH 22

11072283_933753296658934_392071823375109477_n



IMG_9704