Pages

KAPIPI TV

Friday, March 20, 2015

TANZANIA, JAPAN WATILIANA SAINI UJENZI WA KITUO CHA UFUNDI STADI ILEJE

1





2





3



4



5
6

UMOJA WA ULAYA EU WAMPA TUZO MAMA HELEN- KIJO BISIMBA

MAMA
Umoja wa Ulaya umemtunuku Mama Helen Kijo- Bisimba (pichani) kutokana na mchango wake kwa ajili ya kutetea na kulinda haki za binadamu nchiini.
Tuzo hiyo, ilitolewa juzi na EU siku ya Jumanne wiki hii jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mwaka wa Maendeleo Ulaya 2015.
Balozi wa Umoja wa Ulaya bwana Filberto Sebregondi alitoa tuzo hizo na kusema kuwa lengo lake ni kusimamia haki kwenye masuala ya kiulimwengu ikiwemo kupambana na umasikini na kuhamasisha raia kujihusisha na maendeleo.
Wengine waliotunukiwa tuzo katika hafla hiyo pamoja na Mama Bisimba ni wanamziki
Keisha Saban, Fareed Kubanda (FID Q), na Balozi Mpungwe, pamoja na Paul Ndunguru ambae ni msanii na mchoraji.
EU imekuwa mstari wa mbele kupambana na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu hususani ukatili dhidi ya Wanawake na watoto ikiwemo vitendo vya ukeketaji, ndoa za utotoni, na mauaji ya vikongwe.
Vilevile, EU imekuwa mstari wa mbele kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na kupinga adhabu ya kifo.

ZIARA YA MHESHIMIWA WILLIAM LUKUVI LONGIDO ARUSHA

20
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akipewa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC maelezo ya uendelezaji wa eneo la Usa-river lililonunuliwa na NHC kwa ajili ya kujenga Jiji la kisasa hapo jana.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Williama Vangimembe Lukuvi jana alifungua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido na kuwataka wananchi kununua nyumba hizoili NHC iweze kujenga zingine kusaidia Wilaya hiyo kupata makazi bora. Picha zote na Muungano Saguya- Longido, Arusha
19
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akiondoka eneo la Meru Residential arpatments alipomaliza kukagua nyumba za makazi zilizojengwa na NHC na kuuzia wananchi hapo jana.
18
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akimweleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi juu ya mpango wa NHC wa kujenga maduka makubwa ya kibiashara ili kuhudumia wananchi na wakazi walionunua nyumba za makazi za Meru alipomtembeza Waziri huyo hapo jana
9
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa nyumba na kuingia ndani kukagua nyumba hizo.
3
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akisalimiana na wafanyakazi wa NHC waliokuwa wamejipanga kumpokea Waziri Lukuvi kufungua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido.
2
Hizi ni nyumba za gharama nafuu zilizokamilika kujengwa na NHC Wilayani Longido na ambazo ziko tayari kuuzwa kwa wananchi. Ufunguzi wa nyumba hizi ulifanywa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
1
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akikagua maandalizi ya ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido, Arusha kabla ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi kufanya ufunguzi huo jana.
New Picture (127) New Picture (126)
Mbunge wa Longido Mhe. Lekule Laizer akilishukuru Shirika la Nyumba kwa kuiweka Wilaya ya Longido katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC katika Halmashauri mbalimbali za Wilaya hapa nchini.
New Picture (125)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akihutubia halaiki ya wananchi wa Longido (hawapo pichani)waliohudhuria ufunguzi alioufanya wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani humo.
New Picture (124)
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Ntibenda akilishukuru Shirika la Nyumba kwa kujengwa nyumba Wilayani Longido eneo ambalo ni kame na lenye changamoto kubwa ya kutekeleza ujenzi wa nyumba bora
New Picture (123)
Watendaji wa Wizara ya Ardhi Mkoani Arusha na wananchi wakifuatilia matukio ya ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido jana.
New Picture (122)
Mkuu wa Wilaya ya Longido Bw. Ernest Kahindi alitoa nasaha zake wakati wa ufunguzi rasmi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido jana.
New Picture (121)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelezo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi ya mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa Wilayani Longido.
New Picture (120)
Wananchi wa Wilaya ya Longido wakifuatilia kwa makini hotuba mbalimbali zilizotolewa wakati wa ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido
New Picture (119)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akikagua vyumba mbalimbali vya nyumba bora zilizojengwa na NHC Wilayani Longido.
New Picture (117)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akifungua rasmi nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Ntibenda, Mbunge wa Longido Mhe. Lekule Laizer na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu.
New Picture (116)
Wafanyakazi wa NHC nao hawakuwa nyuma kumpokea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi alipowasili mradi wa NHC Longido kufanya ufunguzi rasmi.
New Picture (115)
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mikoa na Utawala wa NHC Bw. Raymond Mndolwa akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi alipowasili Longido kufungua rasmi nyumba za ghrama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido.
New Picture (114)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akimpokea kwa furaha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi alipowasili katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC ili kufanya ufunguzi rasmi.
New Picture (113)
Msafara wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi ukiingia eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu zilijengwa na NHC Wilayani Longido ili kufungua rasmi nyumba hizo baada ya kukamilika ujenzi wake.
New Picture (111)
Hizi ni nyumba za gharama nafuu zilizokamilika kujengwa na NHC Wilayani Longido na ambazo ziko tayari kuuzwa kwa wananchi. Ufunguzi wa nyumba hizi ulifanywa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
New Picture (127)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akikagua nyumba za makazi zilizojengwa na NHC eneo la Levolosi Jijini Arusha.Nyumba hizi zinauzwa kwa wananchi.

JAPAN YACHANGIA SH. MILIONI 160 SHULE YA MSINGI KAKUNI

DSC_0144






DSC_0168


DSC_0148




PG4A5435 (1)



DSC_0186
DSC_0134
DSC_0215
DSC_0244

MADIWANI WA MANISPAA YA LINDI WATEMBELEA MRADI MAPINGA SATELLITE WA UTT-PID ULIOPO BAGAMOYO

Diwani wa Kata ya Nachingwe, Lindi Mjini, Omary Chitanda (katikati) akiuliza swali kwa mtaalamu wa mradi huo
Diwani wa Kata ya Nachingwe, Lindi Mjini, Omary Chitanda (katikati) akiuliza swali kwa mtaalamu wa mradi huo.

*Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID) ilianza kazi zake Julai 1, 2013. Taasisi hii ilirithi kazi za miradi zilizokuwa zinafanywa na Taasisi mama yaani UTT.
Andrew Chale wa Mo dewji blog aliyekuwa Bagamoyo

Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Lindi Machi 17, wametembelea miradi mbali mbali ya UTT-PID iliyopo Dar es Salaam ikiwemo ule wa Bagamoyo wa New Mapinga Satellite.
Madiwani hao waliweza kujifunza mambo mbalimbali dhidi ya mradi huo ulivyoandaliwa na kufanya kazi na namna ulivyopangiliwa kwa ustadi mkubwa.

Katika ziara hiyo inayotarajia kumalizika Machi 19, mwaka huu. Madiwani hao wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaaa ya Lindi, Frank Magali alipongea juhudi za UTT-PID kwa kufanikisha ziara hiyo kwani wamejifunza mengi na pindi watakaporejea Lindi, watakuwa mfano wa kuigwa.

“Kule kwetu Lindi pia tuna mradi uliopo katika hatua mbaali mbali na UTT-PID tayari wamesha pima baadhi ya viwanja katika mfumo kama huu wa kisasa tunaojifunza hapa hivyo itatusaidia sana kwa sasa” alisema Meya Magali.
Diwani wa Kata ya Nachingwea, Manispaa ya Lindi, Omari Chitanda akielezea namna alivyojifunza kwenye mradi huo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani)
Diwani wa Kata ya Nachingwea, Manispaa ya Lindi, Omari Chitanda akielezea namna alivyojifunza kwenye mradi huo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani).

Kwa upande wake, Diwani wa Nachingwea, Omari Chitanda alieleza kuwa, wamepata kuielewa vyema UTT-PID na naamna ya ufanyaji wake wa kazi.

“tunaipongeza UTT-PID kwani imetufungulia mwangaza wa kimaendeleo. Tutakapo rejea Lindi tutaenda kufanya mambo ya kimaendeleo katika kuubadilisha mji wetu” alisema Diwani Chitanda.

Aidha kwa upande wake msimamizi wa mradi huo wa Mapinga kutoka UTT-PID, Godfrey Charles alisema kuwa hdi sasa mradi huo umefanikiwa kwa kiwango ambapo tayari vimebaki viwanja vichache kati ya zaidi ya 500 vilivyochukuliwa.
Madiwani na maofisa kutoka UTT-PID wakifuatilia kwa makini maelezo ya msimamiz wa mradi huo wa Mapinga uliochini ya UTT-PID (Hayupo pichani
Madiwani na maofisa kutoka UTT-PID wakifuatilia kwa makini maelezo ya msimamizi wa mradi huo wa Mapinga uliochini ya UTT-PID (Hayupo pichani).

Pia madiwani hao, walipata elimu pamoja na ufanyaji wa kazi wa UTT-PID na wadau wanaoshirikiana nao huku hadi sasa ikiwa inasimamia miradi mbalimbali ikiwemo mikoa ya Pwani, Morogoro, Kagera, Dar es Salaam, Lindi na mikoa mingine hapa Nchini.
Aidha, kwa upande wa Madiwani hao walipongeza UTT-PID kwa hatua hiyo ya kuwapa elimu sambamba na kutembelea baadhi ya miradi inayoendeeshwa na taaisis hiyo.
..
New Mapinga Satellite town located 30km from Mwenge along new Bagamoyo road with hundreds of serviced plots for residential, commercial and trade purpose ready for sale. The town is fully installed with electrical, water and roads facilities.
DSCN9635
DSCN9651
DSCN9663
madiwani wa Lindi wakijadili jambo
Madiwani wa Lindi wakijadili jambo.

Wednesday, March 18, 2015

USIKOSE KIPINDI CHA NIAMBIE LIVE ,Ep1

Omby Nyongole, Salma Moshi na Queen Mkelemi
Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE
Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii. Pia kupata Tip ya siku / wiki kusaidia kuboresha maisha yako.
Ni Niambie Live....

MADIWANI WA MANISPAA YA LINDI WATEMBELEA MIRADI YA UTT-PID

Mkurugenzi Mkuu wa UTT-PID, Dk. Gration Kamugisha (kulia) akielezea juu ya Taasisi hiyo juu ya utendaji wa kazi zake hapa Nchini, kushoto kwake ni Naibu Meya wa Manispaa ya Lindi, Amida Abdala
Mkurugenzi Mkuu wa UTT-PID, Dk. Gration Kamugisha (kulia) akielezea juu ya Taasisi hiyo juu ya utendaji wa kazi zake hapa Nchini, kushoto kwake ni Naibu Meya wa Manispaa ya Lindi, Amida Abdallah na pichani chini kulia ni Mstahiki Mstahiki Meya wa manispaa ya Lindi, Frank Magali.
UTT-PID
Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Lindi, wakiendelea na mafunzo hayo kutoka kwa maofisa wa UTT-PID (hawapo pichani)
Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Lindi, wakiendelea na mafunzo hayo kutoka kwa maofisa wa UTT-PID (hawapo pichani).
Baadhi ya Madiwani kutoka Halmashahuri ya Lindi wakifuatilia mafunzo ya elimu juu ya ufanyaji wa kazi wa UTT-PID
Baadhi ya Madiwani kutoka Halmashahuri ya Lindi wakifuatilia mafunzo ya elimu juu ya ufanyaji wa kazi wa UTT-PID.
Baadhi ya Wahandisi wa Halmashahuri ya Manispaa ya Lindi wakifuatilia mafunzo hayo ya UTT-PID
Baadhi ya Wahandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wakifuatilia mafunzo hayo ya UTT-PID.
Diwani akifuatilia mafunzo ya UTT-PID
Diwani akifuatilia mafunzo ya UTT-PID.
madiwani  wa Manispaa ya Lindi wakifuatilia mkutano huo wa UTT-PID jijini Dar es Salaamk
Madiwani wa Manispaa ya Lindi wakifuatilia mkutano huo wa UTT-PID jijini Dar es Salaam.
madiwani  wakifuatilia mkutano huo wa UTT-PID  uliokuwa unafanyika jijini Dar es Salaam
Pichani juu na chini ni madiwani wakifuatilia mkutano huo wa UTT-PID uliokuwa unafanyika jijini Dar es Salaam.
madiwani  wakifuatilia mkutano huo wa UTT-PID
madiwani wa Manispaa ya Lindi wakiendelea kufuatilia mkjutano huo wa UTT-PID
Mdiwani wakiendelea na mfunzo haayo ya UTT-PID
Madiwani wakiwa kwenye mafunzo hayo ya UTT-PID.

Na Andrew Chale wa Mo dewji blog
Madiwani wa Manispaa ya Lindi wapo jijini Dar es Salaam katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo mbinu iliyo chini Wizara ya Fedha (UTT-PID), iliyopo jijini Dar es Salaam na nje ya Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza na kuelewa utendaji wa kazi wa taasisi hiyo hapa nchini.

Katika ziara hiyo inayotarajia kumalizika Machi 19, mwaka huu. Mapema leo Machi 16, Madiwani hao wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaaa ya Lindi, Frank Magali waliweza kupatiwa elimu juu ya utendaji kazi wa taasisi hiyo ya UTT-PID na miradi inayoendesha hapa nchini.

Miongoni mwa elimu hiyo ni pamoja na ufanyaji wa kazi wa UTT-PID na wadau wanaoshirikiana nao huku hadi sasa ikiwa inasimamia miradi mbalimbali ikiwemo mikoa ya Pwani, Morogoro, Kagera, Dar es Salaam, Lindi na mikoa mingine hapa nchini.

Awali akiwakaribisha madiwani hao wa Manispaa ya Lindi, Mkurugezi Mkuu wa UTT-PID. Dk. Gration Kamugisha alieleza kuwa, UTT-PID imekua ikifanya kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo viongozi wa Siasa, wananchi, wadau na wabia binafsi pamoja na serikali katika kutekeleza mipango yake.

“Karibu sana UTT-PID, miradi yetu tunafanya kwa kushirikiana na watu mbalimbali. Wakiwemo wanasiasa, ndio maana leo tupo nanyi Madiwani ambao munawawakilisha wananchi huko munako toka” alieleza Dk. Gration Kamugisha.

Aidha, kwa upande wa Madiwani hao walipongeza UTT-PID kwa hatua hiyo ya kuwapa elimu sambamba na kutembelea baadhi ya miradi inayoendeeshwa na taasisi hiyo.