Pages

KAPIPI TV

Tuesday, February 3, 2015

RAIS WA UJERUMANI JOACHIM GAUCK AKARIBISHWA IKULU NA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE

1
Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha mgeni wake Ikulu Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck ambaye ameongozana na mke wake Bibi schadt leo tarehe.03.02.2015.
2
Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akimtambusha Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa waliojitokeza kumpekea leo tarehe.03.02.2015 katika viwanja vya Ikulu.
3
Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mgeni wake Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck wakipata mapokezi kwa kuimbwa kwa nyimbo za taifa za mataifa hayo mawili.
4
Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na kikosi cha jeshi la wananchi wa Tanzania kwa ajili yake leo katika viwanja vya Ikulu
5
Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na ujembe kutoka ujerumani uliondamana na Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck wakati Rais huyo alipowasili Ikulu.
6 8 10
Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck akipokelewa na wanafanyakazi wa Ikulu,wananchi mbalimbali pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za mkoawa wa Dar es salaam waliojitokeza viwanja vya Ikulu leo tarehe.03.02.2015 kumpokea.
11
Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck Ikulu na kufanyanaye mazungumzo.
12
Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Rais wa Ujerumani Mhe. Joachim Gauck pamoja na ujumbe wake .
(PICHA ZOTE NA FREDDY MARO)

CCM TABORA YAWATUNUKU VYETI MAKADA WAKE WALIOKISAIDIA CHAMA HICHO KUPATA USHINDI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bi.Jannat Kayanda akimkabidhi cheti mmoja kati ya makada wa chama hicho Bw.Emmanuel Mwakasaka waliokisaidia kupata ushindi wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji wilaya ya Tabora mjini ambapo CCM ilipata ushundi mkubwa dhidi ya vyama vya upinzani.
Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bi.Jannat Kayanda akizungumza katika maadhimisho ya 38 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kijiji cha Mwisole wilayani Uyui ambapo aliwataka wananchi kuendelea kukiamini chama hicho kwakuwa kimewaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na utulivu wa Taifa.
Hawa ni makada mahili wa CCM mkoa wa Tabora("MAJEMBE YA CCM TABORA")ambao wametambulika michango yao katika kukisaidia chama kwa hali na mali na kuhakikisha chama kinaendelea kujenga heshima yake katika kuwaongoza wananchi.
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini ambaye ni kada wa chama hicho  Bw.Emmanuel  Mwakasaka akionesha heshima ya utii mbele ya viongozi baada ya kupokea cheti cha kumpongeza na kutambua mchango wake katika kukisaidia chama kupata ushindi uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji wa mwaka 2014 ambapo CCM iliibuka mshindi dhidi ya vyama vya upinzani.




DKT. NCHIMBI ASEMA CCM HAINA TATIZO LA KIMUUNDO WALA MFUMO

nchimbi 3



nchimbi 4




nchimbi 2



nchimbi 1

MBUNGE FILIKUNJOMBE ALAZAMIKA KULALA KATIKA “PAGALE” AKITEKELEZA AHADI YA UMEME KIJIJI CHA KILONDO

Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa Deo Filikunjombe akiwahutubia  wananchi wa  kijiji  cha Kilondo Ludewa
Mbunge  Filikunjombe  akisisitiza jambo  wakati akizungumza na  wananchi wa kijiji cha Kilondo
Mwenyekiti wa kata ya  Kilondo wa Chadema Bw  Edgar Kyula  akimpongeza  mbunge wa  wa Ludewa  Deo Filikunjombe kushoto  wakati wa mkutano wake  kijijini Kilondo
Baadhi ya  viongozi wa kata ya  Kilondo  wakimpongeza Filikunjombe  kulia
Mbunge  Filikunjombe akikabidhi nyavu za  kuvulia  samaki kwa ajili ya vikundi  vya vijana  wote  Kijiji cha  Kilondo na Lusisi Ludewa
Filikunjombe kushoto akikabidhi vifaa  vya  michezo kwa  vijana  kijiji cha Kilondo ili baada ya kazi kufanya  michezo
 
Mbunge  Filikunjombe wa tatu  kulia akiwa na viongozi wa kijiji  cha Kilondo na Lusisi ambao aliwapa nyavu na vifaa vya  michezo
Mbunge  Filikunjombe akiwa amembeba mmoja kati ya  watoto  kijiji cha Kilondo  wakati wa mkutano wake kijijini hapo
Kikongwe  mkazi wa kijiji cha Kilondo  akisalimiana na mbunge wa  Ludewa Deo  Filikunjombe baada ya  kumalizika kwa mkutano  wake kijijini hapo
 
Mtaalam  wa  umeme akimuelekea  mbunge Filikunjombe mambo ya kitaalam baada ya  kutembelea  maporomoko ya mto Makete ambao utatumika kuzalisha  umeme  kushoto ni katibu wa mbunge Filikunjombe Bw Stany Gowele
Mtaalam akimwonyesha maporomoko hayo ya maji mbunge Deo  Filikunjombe
Huu  ndio mto  utakao  zalisha umeme kijiji cha Kilondo Ludewa
Mbunge Filikunjombe akitazama mto huo
Huu ni mto  Makete  unaomwaga maji yake ziwa nyasa
Mbunge  Filikunjombe akitazama mto Makete
Wataalam  wakimwaga maji  yenye  chumvi mto  Makete  ili kupima  nguvu ya maji katika mto huo kwa ajili ya kuanza uzalishaji  wa umeme katika kijiji cha Kilondo Ludewa
Kipimo kwa ajili ya  kujua kasi ya maji katika mto Makete
Wakazi wa kijiji  cha Kilondo Ludewa
Mbunge  Filikunjombe akiongoza  msafara  wake kwenda  kupanda  bodi baada ya  kuamka alfajiri katika kijiji  cha Kilondo Ludewa
Mbunge wa  jimbo la  Ludewa Deo Filikunjombe (kulia) akiwa katika  boxhuku ameshika tama  eneo la kando ya  ziwa  nyasa juzi alfajiriakisubiri  usafiri wa bodi kuelekea  Matema wilayani Kyela baada ya kufanya  ziara ya  siku  mloja  kijijini Kilondo  wengine  pichani nimkurugenzi wa kampuni ya Kilondo Investment  Bw Erick Mwambeleko  wapili  kushoto ,katibu mwenezi mkoa wa Njombe Honolatus Mgaya na katibu
mwenezi wilaya ya Ludewa Bw  Felix
Msafara  wa mbunge  Filikunjombe ukijiandaa kupanda katika  bodi  Ziwa nyasa
Mwanahabari  Emmanuel Msigwa wa Chanel  Ten akipanda katika bodi
Baadhi ya  wasafiri  wa ziwa nyasa  wakisafiri kutoka Matema Kyela  kwenda Manda Ludewa
Na matukiodaimaBlog
WANANCHI
wa  kijiji  cha KIlondo kata ya  Kilondo  wilayani Ludewa
mkoani Njombe
wamempongeza  mbunge wa  jimbo la  Ludewa Deo Filikunjombe  kwa  kuwa
mbunge  pekee  katika  jimbo  hilo kufika kulala chini ardhini kwenye
nyumba isiyo na mlango wala dirisha (Pagale) katika
kijijini hicho
toka  nchi ipate uhuru wake mwaka 1961.Mbunge
Filikunjombe na  msafara  wake  wa watu  zaidi ya 15  walifika katika
kijiji  hicho  cha Kilondo kilichopo mwambao mwa ziwa nyasa  kwa lengo
la mbunge  huyo kuwaanzishia  mchakato  wa kupatiwa umeme  kupitia
shirika  lisilo la  kiserikali la Kilondo Investment linalofadhiliwa na
mradi  wa usambazaji  vijijini (REA)
Akizungumza
kwa niaba ya  wananchi  wa kijiji   hicho mwenyekiti wa  serikali ya
kijiji   hicho Bw Laurian Kyula alisema  kuwa  jimbo  hilo  limepata
kuwa na  wabunge zaidi ya  5 ila   hakuna  mbunge  ambae  alifika na
kukubalia  kulala  katika  kijiji  hicho  kutokana na  kuwa na miundo
mbinu mibovu na  kutokuwa na nyumba  ya  kisasa  ya
kulala  wageni zaidi
ya  nyumba  za  wananchi ambazo  nyingi  zipo kienyeji  zaidi hazina hadhi .
“Kweli tumeshindwa  kuamini  kuona  mbunge anaamua  kulala  kijiji  hapa
hata  bila kuwepo kwa maandalizi mazuri ya  kulala tumekuwa na wabunge  wengi  sana ila  wapo  baadhi yao hata kukejeli  kuwa  kijiji  hakina  hadhi ya  kulaza  waheshimiwa  hadi  watakapoboresha mazingira kati ya  viti ambavyo hatukupata  kufikiria  ni pamoja na
kuja  kupokea  mgeni  wa  kiwilaya kuja  kulala  hapa  kijijini ila wewe  mheshimiwa wetu Filikunjombe umekuwa ni kiongozi wa aina yake”
alisema  mwenyekiti   huyo 
Akimpongeza mbunge  huyo kwa jitihada  zake za  kuwasogezea  huduma  ya  umeme
kijijini hapo  mwenyekiti  huyo    alisema kijiji  hicho   ni moja kati vijiji ambavyo  vipo mwambao  mwa  ziwa nyasa na  uwezekano  wa kuunganishwa na  umeme  wa gridi ya  Taifa   kutoka  Ludewa mjini ama
Kyela mkoani Mbeya ni  vigumu  kutokana na kuzungukwa na milima  na maji
hivyo  kwa  upande  wao  waliamini kabisa kamwe hawatakuja  fikiwa na
huduma  za umeme.
“Tunashindwa kujua ni  kiasi gani mbunge  wetu  unavyotuhangaikia  kwa
mambo ambayo  wengine  waliotangulia  walituhakikishia  kuwa ni  vigumu
kufikiwa na huduma ya  umeme kwa  kuwa ni porini labda  haditutakaposogea karibu na vijiji  vya nje ya  Mwambao kauli ambazo vilitufanya  kukata tamaa kabisa kwa  umeme kwetu ni huduma  isiyo wezekana ila  tunashangazwa leo kupitia mbunge wetu Jembe
Filikunjombe unatuletea wataalam wa kuanza kujenga mradi wa umeme hapa
kijijini”
 
Bw Kyula  alisema kati ya  mambo ambayo  wao  hawata kuja  kusahau maishani mwao ni utendaji kazi wa mbunge  huyo na  maendeleo makubwa
aliyoyafanya katika  jimbo  hilo la  Ludewa kwa kipindi  cha miaka minne ya  ubunge  wake huku  wapo waliokaa miaka  mitano  bila  kufanyajambo linaloonekana kwa   wananchi  wao.
Hivyo alisema  iwapo  chama  cha mapinduzi (CCM)  kitataka  kulipoteza  jimbo
hilo la Ludewa ni pamoja na  kujaribu  kufanya maamuzi yasiyo hitajika
kwa  wananchi yakiwemo ya  kukata  jina la mbunge  wao katika mchakato
wa kuomba  kugombea ubunge    jimbo  hilo la Ludewa na kumpa nafasi  mtu
wa kwao watashangazwa na maamuzi magumu ya  wananchi kwa  kulitoa
jimbo hilo upinzani kama  fundisho kwa CCM kupenda wanachopenda  wao na
sio wananchi.
Awali mkurugenzi mtendaji wa  mradi wa Kilondo Investment Bw  Erick
Mwambeleko akielezea  mradi huo alisema  kuwa  mpango  wa kuwaunganisha
wanakijiji  hao na umeme  ulikuwepo toka  wakati mbunge Profesa Raphael
Mwalyosi akiwa madarakani  ila cha kushangaza kila alipomfuata  kutaka
kusaidia kufanikisha kuanzishwa  kwa mradi huo  aliishia  kutoa kauli
za kukatisha tamaa  kuwa haweza  kusaidia  kupeleka  umeme kijijini hapo
kwa kuwa ni gizani sana hakuna faida yoyote .
“Ni  kweli kijiji  hiki cha Kilondo  kipo porini  zaidi  ila  kuna
watu  wanaishi hata  mimi Mwambeleko ni mzaliwa wa hapa  hivyo
nimesoma  sayansi na kutumia elimu yangu nikaona  ngoja  nishirikiane na
mbunge Filikunjombe  kuleta ukombozi  wa  umeme  huku kwa kupitia
kampuni yangu ya Kilondo Investment kampuni ambayo mchango wa mbunge  ni
mkubwa zaidi hadi leo tunaanza mchakato wa kuleta  umeme hapa”Alisema
kuwa tayari  fedha kiasi cha  zaidi ya Tsh milioni 300  zimepatikana
kwa ajili ya kuanza  utekelezaji wa mradi huo ambapo  fedha  hizo kiasi
zimetoka REA na nyingine ni fedha  ambazo ni mchango wa mbunge
Filikunjombe .
Pia alisema  umeme   huo  utazalisha  kijijini hapo  kupitia maporomoko ya
maji ya mto Makete  ambayo yanaingia katika  ziwa nysa  na kuwa
maporomoko hayo yana nguvu  ya  kuzalisha  umeme KV 50 na  kasi ya maji
katika maporomoko hayo ni lita  za ujazo 9312 kwa  sekunde maji ambayo
yanatosha kabisa kwa  uzalishaji wa umeme  wa kutosha kaya  zote
kijijini hapo na kijiji cha jirani.
 
Kwa upande  wake  mbunge  Filikunjombe akielezea  sababu ya  kulala kijijini hapo alisema  kuwa moja kati ya ahadi yake kwa  wananchi wa
Ludewa ni  kufikisha maendeleo kila  kona ya  jimbo  hilo na kuwa akiwa katika  ziara  pale ambapo  jua litazamia ndipo atakapolala  bila kujali uwepo wa maandalizi ama lah.
 
“Wananchi wote wa Ludewa ni  wapiga kura  wangu hivyo imekuwa ni kawaida  yangu
kuwa nao  wakati  wote na  kulala popote na  kula  chochote ambao  wao
wanakula  siku  zote hivyo  jua linapozamia nikiwa
ziarani
nitalala hapo bila  kujali maandalizi lengo  kuona  nashirikiana na wananchi wangu kwa mazingira  yoyote yale nimefurahi  sana  leo kulala katika  nyumba  hii inayojengwa ambayo haina sakavu ,milango wala
madirisha (Pagale) mimi ni siufanyi ubunge kama ufalme kuwa nikija mimi ziarani  wananchi wangu  wasumbuke kufanya maandalizi yasiyo ya
kawaida”
Kuhusua mradi  huo wa umeme Filikunjombe alisema  kuwa lengo lake kuona
wananchi hao  wanapatiwa umeme mapema  zaidi  ikiwezekana ndani ya mwaka
huu wananchi hao  waweze na  umeme  katika makazi yao  hivyo  kuwaomba
wananchi kutoa  ushirikiano kwa mafundi  waliofika kijijini  hapo
kuanza  utekelezaji wa mradi huo pamoja na kuwasaidia  kufanya tathimini
ya mahitaji ya taa na ufungaji  umeme katika  nyumba  zao.

Monday, February 2, 2015

JK AONGOZA KILELE CHA MIAKA 38 YA CCM MJINI SONGEA

 Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete  akiwapungia mkono wananchi katika uwanja wa Majimaji.
 Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete akikagua gwaride la chipukizi


TFDA YATEKETEZA BIDHAA FEKI ZENYE THAMANI YA SH MIL.5 SIKONGE

Baadhi ya bidhaa zilizoteketezwa na Maofisa wakaguzi wa TFDA wilayani Sikonge (Picha na Allan Ntana)
Maofisa wakaguzi wa TFDA kanda ya kati wakijiandaa kuteketeza bidhaa zilizoisha mda wake ikiwemo vinywaji wilayani Sikonge (picha na Allan Ntana)

Na Allan Ntana, Sikonge

MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kati imefanikiwa kukamata na kuteketeza bidhaa mbalimbali za chakula, vinywaji, dawa za binadamu na mifugo, vipodozi na vifaa tiba vilivyoisha muda wake na vingine feki vyenye thamani ya zaidi ya sh mil.5 katika halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

Akisoma taarifa ya ukaguzi mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo hapo juzi Afisa Mkaguzi wa Chakula Kanda ya Kati Sifa Chamgenzi alisema ukaguzi huo ulilenga kuangalia ubora na usalama wa dawa za binadamu na mifugo, uwepo wa vipodozi vilivyopigwa marufuku na bidhaa zingine zilizoisha muda wake wa matumizi.

Alisema lengo la TFDA ni kufuatilia utekelezaji wa sheria na.1 ya mwaka 2003 ya chakula, dawa na vipodozi kwa wauzaji na wasindikaji wa vyakula na dawa   lililolenga kutekeleza mpango kazi wa Mamlaka hiyo wa kufuatilia ubora na usalama wa bidhaa hizo kwa mtumiaji.

Ukaguzi huo uliofanyika tarehe 20-29 Januari 2015 uliongozwa na Maafisa wakaguzi wawili kutoka TFDA Kanda ya Kati Fredrick Luyangi na Sifa Chamgenzi ambao waliungana na wakaguzi wenyeji wawili toka Ofisi ya Mkurugenzi Idara ya Afya na askari polisi wanne wilayani Sikonge na jumla ya majengo 118 yanayojihusisha na biashara ya chakula, vinywaji, dawa, vipodozi na vifaatiba yalikaguliwa.

Katika ukaguzi huo baadhi ya maduka yalikamatwa na vipodozi vilivyopigwa marufuku vikiwa na uzito wa kilo 164.4 na thamani ya sh 1,856,000/- na katika maduka ya vyakula walikamata vyakula vilivyoisha muda wake vyenye uzito wa kilo 825.5 vikiwa na thamani ya sh 2,720,000/-

Na katika maduka ya dawa za binadamu na mifugo walikamata jumla ya kilo 37 za dawa zilizoisha mda wake na feki zenye thamani ya sh 1,200,000/-.

Aidha katika ukaguzi huo kiasi cha sh 1,580,000 kilipatikana kutokana na ada za usajili wa maduka ya biashara ya chakula ambapo 40%  ya kiasi hicho sawa na sh 632,000 inabakia katika halmashauri kwa ajili ya kufanya kazi za TFDA.

Akizungumzia mambo waliyoyabaini wakati wa ukaguzi huo, Chamgenzi alisema ukaidi na uelewa mdogo wa sheria na.1 ya mwaka 2003 wa kulipa ada na tozo husika kwa baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya chakula, dawa na vipodozi bado ni tatizo sambamba na kutotoa ushirikiano kwa Afisa wakaguzi.

Aidha uwepo wa dawa bandia (feki) zilizoondolewa sokoni, dawa na vyakula vilivyoisha muda wake, kukosekana feni za kutunzia dawa katika stoo ya kituo cha afya Kitunda, maduka ya dawa za kilimo kuuza dawa za mifugo kinyume cha sheria, utunzaji mbovu na mlundikano wa dawa zilizoisha muda wake, viwanda na mashine za unga kuwa katika makazi ya watu ni miongoni mwa yaliyobainika.

Wakaguzi hao pia hawakuridhishwa na hali ya machinjio ya halmashauri hiyo kukosa uzio, kutokuwa na chanzo cha maji cha kuaminika na sakafu kuwa na mashimomashimo hali iliyosababisha kutuama kwa maji na damu na hivyo kuhatarisha afya za walaji, hivyo wakamwagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo Shadrack Mhagama kufanyia kazi mapungufu hayo kwani yanarekebika, jambo ambalo aliliafiki na kuahidi kutekeleza mara moja.

DIAMOND PLUTNAMZ ATUA NA MPENZI WAKE ZARI MJINI SONGEA

1Mwanamuziki Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Songea tayari kwa kufanya onesho kubwa kwenye sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM zinazofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea leo ambapo viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Dr. Jakaya Kikwete.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SONGEA. 2Diamonda Plutnamz akiongozana na mpenzi wake Zari wakiondoka kwenye uwanja wa ndege wa Songea kuelekea hotelini. 3Mkuu wa wilaya ya Songea Bw.Joseph Mkirikiti akisalimiana na Zari Mpenzi wa Diamond Plutnamz. 4 5 6Diamond Plutnamz akifanya vitu vyake kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati wa sherehe za miaka 38 ya CCM. 7 8 9Diamond Plutnamz akiima pamoja na mwanamuziki Abdul Misambano wa kundi la TOT katika sherehe za miaka 38 ya CCM mjini Songea mchana huu. 10Umati wa wananchi waliohudhuria katika uwanja huo 11