Pages

KAPIPI TV

Thursday, January 29, 2015

KINANA CHAKE CHAKE PEMBA



 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Chake Chake Pemba ambapo aliwataka viongozi wa CCM kutenda haki, kujipanga na kuchagua viongozi wanaokubalika.
 :
 Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdala akisalimia wananchi wa Mchangani, ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alifika kushiriki ujenzi wa tawi la CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akishiriki ujenzi wa ofisi ya Tawi la  CCM Mchangani,kushoto aliyebeba tofali ni MNEC wa Chake Chake Daudi Ismaili akisaidia ujenzi, Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kujenga, kuhamasisha na kuimarisha Chama Cha Mapinduzi,Pemba.
 Vijana wawili kutoka vyama vya upinzani kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema Uwandani Chake Chake Pemba Kombo Ali Abdala na Kulia ni Mwenyekiti wa ADC Uwandani Mohamed Said Abdalla wakishiriki ujenzi wa darasa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Vijana wawili kutoka vyama vya upinzani kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chadema Uwandani Chake Chake Pemba Kombo Ali Abdala na Kushoto ni Mwenyekiti wa ADC Uwandani Mohamed Said Abdalla wakiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya kumaliza kushiriki ujenzi wa madarasa katika skuli ya Uwandani Pemba.
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na viongozi na wananchi kuelekea Kilindi Pemba kuona maendeleo ya kikundi cha kutunza mazingira cha Hatugombani pamoja na kushiriki kupanda miti ,Pemba.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Hadija Abood akishiriki kupanda mti wa mkungu wakati walipotembelea kikundi cha kutunza mazingira cha Hatugombani.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Chake Chake Pemba ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa na utamaduni wa kuuliza maswali kwa viongozi wao hasa wabunge na wawakilishi wanapokuja kuwahutubia kwani wamekuwa wakipoteza muda mwingi kuwahutubia wananchi hao kuhusu CCM badala ya kuzungumzia namna wanavyoshughulikia changamoto za wananchi kwenye majimbo yao.
 Wananchi wa Chake Chake pemba wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipohutubia kwenye viwanja vya Pujini Kunvini, mkoa wa Kusini Pemba.
 Kijana Said Abdalla Ibrahim akionyesha kadi yake ya CUF ambayo ameamua kuirudisha na kujiunga na CCM mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Pujini Kunvini,Chake Chake Pemba

 Kijana Said Abdalla Ibrahim akionyesha kadi yake ya CUF mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa hadhara Chake Chake Pemba.
 :
 Kijana Ghalib Bedui Khamis akionyesha kadi yake ya CUF kabla ya kumkabidhi Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pujini Kunvini,Chake Chake Pemba.
 Kijana Ghalib Bedui Khamis akitangaza kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Pujini Kunvini,Chake Chake Pemba.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai akihutubia wakazi waliohudhuria mkutano wa hadhara na kuwaambia CUF wanaanza kukiuka makubaliano ya MUAFAKA na kutaka CUF kuheshimu makubaliano hayo.
 Wananchi wakisikiliza mkutano kwa makini.
 Shadia Mohamed Mwakilishi wa Chake Chake Pemba akihutubia kwenye mkutano uliofanyika Pujini Kunvini ,Pemba.
Mbunge wa Viti Maalum Asha Omar akihutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadahara uliofanyika Pujini Kunvini na kuwaambia vijana waache kutumika na watu wasiokuwa na manufaa kwao.
 Mbunge wa Viti Maalum Faida Bakari akihutubia wakazi wa Chake Chake Pemba na kuwaambia masuala yanayohusu ardhi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Pujini Kunvini.
 Mwakilishi wa Kuteuliwa na waziri wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,Vijana na Wanawake akihutubia wananchi waliohudhuria mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana na kuwataka wananchi hao hasa wanawake kuisoma kwa makini Katiba mpya iliyopendekezwa

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Wednesday, January 28, 2015

ZIARA YA MKURUGENZI MTENDAJI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA NHC MIKOANI

New Picture (4)Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu wakikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya NHC kujenga nyumba za gharama nafuukatika Halmashauri ya Wilaya Serengeti-Mugumu. Eneo hili lina ekari 134 na miundombinu ya maji na umeme.
New Picture (5)Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mugumu Serengeti akimuonyesha Mkurugenzi Mkuu wa NHC ramani ya mpango Miji inayoonyesha eneo la NHC la kujenga nyumba za gharama nafuu.
New Picture (6)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiongea na kikundi cha vijana Wilayani Serengeti waliyosaidiwa mashine na NHC kwa ajili ya kujiajiri kupitia utengenezaji wa matofali yanayofungamana
New Picture (7)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakikagua jingo la biashara lililojengwa na NHC eneo la Mukendo Musoma.
New Picture (8)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelekezo ya matumizi bora ya dari la jengo la biashara la Mukendo lililojengwa na NHC katika Manispaa ya Musoma ili kuongeza mapato ya Shirika.
New Picture (9)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akikagua ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Buhare Musoma. Jumla ya nyumba 50 zinatarajiwa kukamilika Julai 2015.
New Picture (10)Vijana wakishiriki kujenga misingi ya nyumba za gharama nafuu eneo la Buhare Manispaa ya Musoma
New Picture (11)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akijadili namna ya kuongeza ubora wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Amesisitiza kupunguza gharama ya ujenzi ili nyumba zinazojengwa ziwe nafuu.
New Picture (12)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake walipotembelea Wilayani Tarime kujionea nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC mwaka 1968 na ambazo hadi hivi sasa zinasaidia familia mbalimbali. Nyumba hizi ni za vyumba viwili na zilipewa Halmashauri hiyo mwaka 1991.
New Picture (13)Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Isibania nchini Kenya kujionea namna nchi hiyo ilivyopanga eneo lao la mpakani.
New Picture (14)Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Sirari kuona eneo la kujenga nyumba ili kuboresha taswira ya mpaka wa nchi yetu. Ujumbuliongozwa na Maafisa Ardhi wa Wilaya ya Tarime.
New Picture (15)Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake pamoja naongozi wa Wilaya ya Butiama wakikagua eneo lililotengwa na Wilaya hiyo ili NHC ijenge nyumba za gharama nafuu. Bw. Mchechu amesisitiza kuwa NHC itajenga nyumba katika Wilaya hiyo ili kuenzi mchango wa Mwalimu Nyerere wa kulianzisha Shirika la Nyumba la kwanza nchini Tanzania mwaka mmoja tu baada ya uhuru.
New Picture (17)Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiangalia mnara wa kumbukumbu ya mahali ambapo ilikuwepo nyumba aliyozaliwa Baba wa Taifa.
New Picture (18)

UNESCO YATAKA UBIA NA MWEDO

DSC_0005




DSC_0031



DSC_0019




DSC_0051



DSC_0057
DSC_0079
DSC_0094

Tuesday, January 27, 2015

UN TANZANIA WAADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA MAADHIMISHO YA WAHANGA WA MAANGAMIZI MAKUU YA MOTO DHIDI WAYAHUDI JIJINI DAR LEO

Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mh Egon Kochanke akitoa historia fupi ya wahanga wa maangamizi Makuu ya Moto Dhidi ya Wayahudi katika maadhimisho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Utamaduni wa Russia na kuandaliwa na Umoja wa Mataifa Tanzania.
 Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi Usia Nkhoma akiwakaribisha wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dar pamoja na wanafunzi wa Vyuo Vikuu vilivyopo Jijini Dar ambavyo Kuna Klabu za Umoja wa Mataifa katika ukumbi wa utamaduni wa Russia wakati wa Siku ya Kimataifa ya Kuadhimisha na kuwakumbuka wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto Dhidi ya Wayahudi.
 Stella Vuzo, Afisa habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC) akimwelezea Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Mh Egon Kochanke wakati alipotembelea katika ukumbi wa Utamaduni wa Russia ambapo baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vikuu waliweza ushiriki katika Kuadhimisha na Kuwakumbuka Wahanga Wa Maangamizi Makuu ya Moto dhidi ya Wayahudi
 Balozi wa Ujerumani, Mh Egon Kochanke akisoma moja ya bango lililobandikwa katika Ukumbi wa Utamaduni wa Kirusi wakati wa Maadhimisho ya Wahanga wa Mahangamizi Makuu ya moto yanayofanyika kila tarehe 27 January kwaajili ya kumbukumbu
  Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani, Kibasila, Azania na Kisutu wakisoma moja ya bango lenye historia fupi ya Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto.
 Stella Vuzo, Afisa habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC) akimwelezea Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Mh Egon Kochanke wakati alipotembelea katika ukumbi wa Utamaduni wa Russia ambapo wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo waliweza kupata historia fupi ya Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto
 Wanafunzi wakifuatilia historia fupi ya Wahanga iliyokuwa ikitolewa na Afisa Habari wa UN, Bi Usia Nkhoma
 Stella Vuzo, Afisa habari wa Kituo cha Taarifa cha Umoja wa Mataifa Tanzania (UNIC) akitoa neno mbele ya Mgeni rasmi ambae ni Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Mh Egon Kochanke wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya maadhimisho na kumbukumbu ya Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto dhidi ya Wayahudi ambapo maadhimisho hayo ufanyika kila tarehe 27 Januari.Picha Zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog