Pages

KAPIPI TV

Sunday, October 19, 2014

RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS KABILA ARUSHA

ZOEZI LA KIJESHI USHIRIKIANO IMARA BURUNDI 2014

JWTZ USHIRIKIANO IMARA
2a
Meja Jenerali James Mwakibolwa wa nne kulia akiwa na Brigedia Jenerali Joseph Chengelela wa tano kulia na Mwambata wa JWTZ nchini Burundi kanali Venant Mutashobya wa tatu kulia mara baada ya ufunguzi wa zoezi USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI.
jes Picha ya Pamoja ya maofisa wa serikali ya Burundi na Maafisa Wakuu wa Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya ufunguzi wa zoezi USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI
unnamed
Majeshi hayo yakiwa katika mazoezi.
………………………………………………………………………..

Zoezi la Ushirikiano Imara linalojumuisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki limefunguliwa leo nchini Burundi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa chi hiyo. Gwaride maalumu linalojumuisha majeshi yote ya nchi wanachama lilikuwa limesimama mbele ya wageni mbalimbali katika uwanja wa kambi ya kijeshi ya Muzinga nje ya mji wa Bujumbura wakati Makamu huyo wa Kwanza wa Rais alipokabidhi Bendera ya jumuiya kuashiria kuanza rasmi wa mazoezi hayo.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) liliwakilishwa na Meja Jenerali James Mwakibolwa ambaye ni Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita Makao Makuu ya Jeshi.
Mazoezi haya ya medani hufanyika kila mwaka katika moja ya nchi wanachama kwa utaratibu wa kupokezana yakiwa na lengo kuu la kudumisha ushirikiano katika masuala ya ulinzi na usalama.

Pamoja na mambo mengine, mazoezi haya yatatoa fursa kwa nchi wanachama kuandaa na kuweka mikakati ya pamoja katika kukabiliana na matishio mbalimbali yanayoweza kutokea katika ukanda wetu wa afrika mashariki.
 
Maudhui makuu ya zoezi la mwaka huu yanajikita katika kukabiliana na changamoto katika ulinzi wa amani, majanga ya asili na ya kibinadamu, ugaidi, pamoja na uharamia ambavyo vimekuwa tishio katika maeneo mengi duniani.
 
Aidha, kutakuwa na mazoezi ya kuyaweka tayari majeshi yetu katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ili kupunguza na kuzuia kabisa madhara ya magonjwa hayo. kwa ujumla, mazoezi haya ni kipimo cha jinsi gani nchi yetu imejiandaa na kujiweka tayari kupambana na changamoto hizi kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na jumuiya.
 
JWTZ limejiadaa vyema katika ushiriki likishirikisha waajeshi wa fai malimali ili kutimiza malengo ya nchi yetu na jumuiya kwa ujumla katika kukabiliana na changamoto zilizotajwa.
 
Aidha, kikosi cha Tanzania kupitia kitengo cha Uhusiano na Raia (Civil Military Cooperation) kimepanga kutoa misaada mbalimbali kwa wananchi wa Burundi waishio maeneo ya karibu na kambi ikiwa ni pamoja na vifaa kwa ajili ya wanafunzi. Ikumbukwe kuwa, jeshi bora ni lile ambalo askari wake wamefunzwa vizuri na kupata mzoezi ya mara kwa mara katika kutimiza majukumu yao, mazoezi ndiyo hulifaya jeshi letu kuwa tayari wakati wote kuwatumikia wananchi.

Friday, October 17, 2014

WANAFUNZI WABAKANA KILA BAADA YA MUDA WA MASOMO,WALIMU WATUPWA LUPANGO.

Na Magreth  Magosso,Kigoma

WANAFUNZI wa shule ya Msingi ya Kikunku iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji,wameamua Kuandamana kwenda kituo cha Polisi kati katika ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Jafari Mohamed ,kwa lengo la kutaka walimu Watatu wa shule hiyo wasitupwe Mahabusu kwa hofu ya kukosa masomo.

Chanzo cha mandamano hayo ni   haki na ukweli wa kesi  dhidi ya walimu hao ambao ni Baraka Kilatunga (28),Jeje Msiba(34) naMichael Mugumwe(34) ambao  wanakabiliwa na tuhuma za  kumwadhibu fimbo nne za makalio mwanafunzi  wa darasa la tatu aliyetajwa kwa jina la Abrahaman  Ramadhan (9) kwa kitendo cha kushawishi na hatimaye kubaka mwanafunzi wa darasa la pili .

Kwa nyakati tofauti wakifafanua hilo Hajira  Ndola  na Jafari  Ramadhani walisema baada ya kuona mwalimu amebebwa kwenye gari la afisa elimu na askari polisi walijua ni ile kesi ya kutoa adhabu kwa mwenzao, kiuhalisia ana haki ya kupewa adhabu kwa kuwa  wanafanya mapenzi shuleni na mwanafunzi mwenzake wakati kila baada ya masomo.

Akifafanua hilo mwalimu  wa nidhamu Nicolausi Ulimwengu alisema Alhamis ya wiki iliyopita mzazi wa Tatu  Masoud (8)  alienda shuleni hapo kuhoji uchafu unaofanywa na watoto hao ilihali walimu wanashindwa kukemea huku kijana huchelewa kufika nyumbani mapema pia ni utovu wa nidhamu.

“ameona ni busara kulileta shule ili uongozi ujue uchafu huo,angekwenda kwa mzazi wa kiume wangeishia kutoleana lugha chafu,walipoulizwa hilo mbele ya walimu wanne ,walikiri kufanya hivyo si chini ya mara tano ,tuliwapa adhabu ya fimbo nne kila mmoja” alisema Ulimwengu.

Cha kushangaza ijumaa ya wiki iliyopita tukapewa taarifa kuwa Abrahaman ameumizwa vibaya hadi kutundukiwa dripu la maji hospitali ya Rufaa Maweni wakati si kweli yupo darasani, wazazi ni chanzo cha maovu na wakiwajibika kikamilifu wanasimangwa na jamii husika. 

Kwa upande wa diwani wa kata ya Katubuka Moses Bilantanye alisema kuna upotoshaji wa taarifa zilizopo kituo cha polisi ,ambapo mzazi anadai kijana amezidiwa na ukiuliza wanafunzi wenzao na baadhi ya walimu wanasema wana tabia ya kufanya mapenzi kila wakati na kuwataka wazazi wafuatilie tabia za vijana wao na si kukomoa walimu.

Akithibitisha hilo Kamanda  wa Polisi wa hapa Jafari Mohamed alisema Octoba ,10,2014 saa 6.00 mchana ,katika shule hiyo Abrahaman Ramadhan(9) darasa la tatu alipigwa na walimu  watatu kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi Tatu Masoud(8) darasa la tatu na watafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.

Awali gazeti hili litonywa kuwa,vijana hao ni kawaida yao kufanya mapenzi kila watokapo shule,ambapo Abrahaman humpa visenti Tatu vya kununua barafu na mihogo kwa makubaliano ya kufanya tendo la ndoa kinyume cha sheria ilihali Tamwa wanataka jamii na wasimamia sheria wawajibike ili kupunguza matukio ya ubakwaji.

SHIRIKA LA NYUMBA NCHINI NHC LAELEZEA LINAVYOSAIDIA VIJANA KWA MRADI WA MASHINE ZA MATOFALI NA UJENZI WA NYUMBA KWA GHARAMA NAFUU

Thursday, October 16, 2014

SERIKALI YAFUTA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr.Shukuru Kawambwa akizungumza wakati alipotembelea Shule ya Sekondari ya Tabora Wavulana

Na Allan Ntana, Tabora

SERIKALI imefuta kozi zote za mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti kuanzia mwaka huu kwa lengo la kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini.

Tamko hilo limetolewa jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr Shukuru Kawambwa alipokuwa akizungumza na wanachuo wa Chuo Cha Ualimu Tabora kilichoko katika Manispaa ya Tabora.

Alisema kuanzia mwaka huu serikali imeamua kuondoa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti ikiwa ni mkakati maalumu wa kuanza kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini ambapo waalimu watakaoajiriwa kufundisha shule za msingi na sekondari watatakiwa kuwa na elimu ya kiwango cha diploma na kuendelea.

Alieleza kuwa kuanzia sasa wizara yake inataka ubora wa elimu upatikane kutokana na ubora wa waalimu huku akibainisha kuwa waalimu wote watakaoajiriwa katika shule za msingi na sekondari kuanzia mwaka huu lazima wawe na elimu ya kiwango cha kuanzia diploma na kuendelea huku akifafanua kuwa wale wasiokuwa na diploma watapewa fursa ya kujiendeleza bila tatizo lolote.

Aidha alisema waalimu wa shule za msingi na sekondari na wahitimu wa kidato cha sita waliopata daraja la 1-3 waliochaguliwa kujiunga na kozi maalumu ya mafunzo ya ualimu tarajali ngazi ya cheti wote watapelekwa vyuoni kupata masomo ya ngazi ya diploma katika vyuo maalumu vilivyoandaliwa.

Aidha katika kuhakikisha mpango huu mpya unatekelezwa, Dr Kawambwa alisema wizara inaandaa waraka maalumu wa maelekezo utakaotumwa kwa wakurugenzi wote wa halmashauri zote hapa nchini.


Akijibu swali la wanafunzi wa chuo hicho waliotaka kujua ni kwa nini mda wa  kwenda kufanya mazoezi (BTP) umepunguzwa na kuwa wiki 3 badala ya siku 60, waziri alisema utaratibu huo ni wa dharura tu kutokana na uhaba wa fedha ila akaahidi kuwa watajitahidi kurekebisha hali hiyo kadri hali ya kifedha itakavyoruhusu.

Aidha kuhusiana na ombi la kuongezwa posho ya mazoezi kutoka sh 4500 wanazolipwa sasa wanafunzi hao wa mafunzo ya ualimu hadi sh 7500 wanazolipwa wanafunzi wa ngazi ya shahada, waziri aliahidi kulifanyia kazi kutokana na bajeti ya wizara yake itakavyokuwa.

Aidha waziri aliwataka wanafunzi wote wa vyuo vya ualimu kuhakikisha wanafaulu masomo yao yote wanayofundishwa chuoni ili waweze kuajiriwa na serikali vinginevyo watalazimika kukaa benchi.

‘Wakati naingia wizarani  nilisema sitaajiri waalimu waliofeli na nitaendelea na msimamo huo huo kwa nia njema kabisa, jitahidini kufaulu masomo yenu yote ya kufundishia na yale ya ziada vinginevyo hatuwapi kazi, alisema Dr Kawambwa.


RAIS KIKWETE ALIPOTEMBELEA BANDA LA BIMA YA AFYA WAKATI WA WIKI YA VIJANA TABORA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete akisisitiza jambo kwa maafisa wa NHIF wakati alipotembelea banda la maonesho la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  NHIF wakati wa wiki ya Vijana iliyofanyika kitaifa mkoani Tabora.
Rais Kikwete akisalimiana na baadhi ya maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya

Rais Kikwete alishuhudia baadhi ya wananchi wakipata huduma za upimaji wa magonjwa mbalimbali shughuli iliyokuwa inafanywa na Mfuko huo wa Bima ya Afya ambapo idadi kubwa ya watu ilijitokeza kupata huduma hiyo.
Baadhi ya maafisa wa Mfuko wa Bima ya Afya wakiwa na Meneja mwandamizi wa Mfuko wa Bima ya Afya kanda ya Magharibi Bw.Emmanuel Adina






UJUMBE WA TANZANIA WAKUTANA NA MWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA TANZANIA, UGANDA, RWANDA NA BURUNDI

BENKI YA DUNIA TANZANIABaadhi ya viongozi wa Wizara ya fedha wakifuatilia kwa makini mkutano uliokuwa ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile, ambapo ujumbe kutoka Tanzania ulikutana na Mwakili Mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Phippe Dongier hawapo kwenye picha kwa madhumuni ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uchumi wa Tanzania. Kutoka kushoto ni Bw. John Cheyo ambaye ni Kamishna wa Bajeti, anayefuata ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar Bi Amina na wa kushoto kwake ni Bw. Said Magonya ambaye ni Kamishna wa Fedha za nje Wizara ya Fedha.(Picha zote na Ingiahedi Mduma – Washington DC).
2aKatibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius Likwelile alipokuwa akitoa msimamo wake kuhusu sera zinazopendekewa na Benki ya Dunia kwa mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Phippe Dongier.
3aDr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali akiwa pamoja na ujumbe kutoka Tanzania. Kutoka kulia ni Gavana wa Benki kuu ya Tanzania na kutoka kushoto ni Bi. Natu Mwamba Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania wakimsikiliza kwa makini Bw. Phippe Dongier ambaye ni mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi hayupo kwenye picha, alipokuwa akijibu hoja zilizowekwa mezani.
4aBw. Phippe Dongier ambaye ni mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi alipokuwa akijibu hoja zilizotolewa na Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali na kuahidi kuzifanyia kazi.

JK AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU CCM MJINI DODOMA

 Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu  ya Halmashauri Kuu ya Taifa CCM kwenye ukumbi wa NEC,CCM Makao Makuu Dodoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma taarifa fupi ya ufunguzi wa kikao kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
 Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Bi.Zakia Meghji akizungumza na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Mohamed Seif Khatib wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa mjini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Mwigulu Nchemba akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye katika ukumbi wa NEC kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.

Tuesday, October 14, 2014

RAIS KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA MKOANI TABORA


KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU TABORAKiongozi wa mbio za mwenge 2014 Rachel Kassandra akikabidhi mwenge wa Uhuru kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge ulius  na kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora leo.Kulia ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na michezo Dkt.Fenela Mkangara. 4 (2)Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenge wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge ziizofanyika mkoani Tabora leo. 5 (3)Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mbio za mwenge mwaka huu wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio hizo zilizofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora lei(picha na Freddy Maro)

Monday, October 13, 2014

WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI TABORA WAUSHAURI MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA KUHAMASISHA MASHULENI

PROF.TIBAIJUKA AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA USIKU CHUO CHA ARDHI TABORA

Waziri wa ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Prof.Anna Tibaijuka akikagua moja ya mabweni ya wanafunzi wa Chuo cha Ardhi Tabora ambapo ziara hiyo ameifanya kwa kushitukiza majira ya saa moja usiku.

Prof.Tibaijuka akimpongeza mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora Bw.Biseko Musiba kwa kukisimamia vizuri chuo hicho licha ya ukosefu wa masuala mbalimbali ya msingi ikiwa ni pamoja na upungufu wa watumishi,vifaa vya kufundishia kama kompyuta na vinginevyo.
Prof.Tibaijuka alitembelea pia maktaba ya chuo hicho ambacho haina kompyuta kama nyenzo muhimu za kujifunzia wanachuo.
Prof.Tibaijuka alipata fursa ya kuzungumza na wanafunzi na walimu na watumishi wa chuo hicho.
Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora Bw.Biseko Musiba akisoma taarifa fupi ya chuo hicho na namna chuo kinavyokabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhakikisha kinatoa wataalamu wenye fani inayojitosheleza kwenye masuala ya ardhi nchini.





MAMA KANUMBA NA LULU NDANI YA FILAMU MPYA IITWAYO "MAPENZI YA MUNGU"

Hivi karibu Msanii Mahiri na Nguli katika tasnia ya filamu nchini Elizabeth Michael almaarufu kama LULU ataibuka na filamu yake Mpya na yenye kusisimua iitwayo "MAPENZI YA MUNGU" ambapo moja kati ya washiriki katika filamu hiyo ni Bi Flora Mtegoha ambae ni Mama Mzazi wa aliyekuwa Msanii Nguli wa Kiume Hapa Bongo Marehemu Steven Kanumba.
Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" ni moja ya filamu ambayo Lulu ameonyesha uwezo wa hali ya na kuthibitisha kuwa ni mmoja kati ya wasanii wa kike hapa Tanzania ambae ana kipaji cha hali ya juu katika kuuvaa uhusika ambapo ana uwezo wa kubadilika badilika kutokana na muongozo anaopewa.
Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" itakuwa Sokoni hivi Karibu Kwa Wauzaji wa Filamu kote Nchini.
Filamu hii itasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Ltd.