Pages

KAPIPI TV

Friday, September 26, 2014

Skylight Band Divas Mary Lukos(Wa kwanza Kushoto) Aneth Kushaba(katikati) Na Digna Mpera (Wa kwanza Kulia) wakitoa burudani ya nguvu Kwa Mashabiki Wao Ndani ya Kijiji cha Maraha Thai Village Ijumaa Iliyopita.Kila Ijumaa ya mwisho wa wiki Band Ya Skylight Wanapiga show Ndani ya Thai Village.Karibu Leo Upate burrudani ya nguvu yenye kukonga Roho yako na kutakuwa na Supriseeeeeee kibaoooo ndani ya Thai Village
          Hashimu Donode Akiimba kwa raha zake ndani ya Thai Village 
Shabiki huyu hakuweza kujizuia hisia zake pale alipoguswa na muziki mzuri uliokuwa ukiimbwa na Hashimu Donode
Donode Akiendelea kuimba na shabiki wake kwa Raha zaooooo
Digna Mpera akizipiga zile voca; kali za kumtoa nyoka pangoni
Mary Lukos Akifurahi na kucheza ala nzuriiii toka kwa wapiga vyombo wa Skylight Band Hawapo Pichani
Mary Lukos Kwa Rahaaaa zakeee akifurahia Muziki mzuri
Aneth Kushaba (wa kwanza kulia)akiimba kwa Furaha kuwapa burudani mashabiki wake ndani ya Thai village
Mary Lukos Akiimba Kwa Hisia kaliii Huku akipewa sapoti na Wenzake kushoto


Sony Masamba(mutoto ya Congo)akiimba kwa Raha zakee ndani ya Thai Village
Joniko Flower(mutu Ya Congo)Akizipiga zile vokali kaliii za kilingala ndani ya Thai Village
Vijana wa Skylight Band Joniko Flower(wa Kwanza Kushoto)Sony Masamba (katikati)Na Sam Mapenzi Wa mwisho kulia wakiyarudi mauno vilivyo kutoa burudani kwa mashabiki wao
Weweee Joniko Flower Akiwaongoza Wenzake kutoa burudani
Muziki ni raha na Hisia kama Sam mapenzi(wa kwanza kulia)anavyoonekana akiyarudi   mauno kwa rahaa zake
Hebu tazama mashabiki hawa wakiwa na mshangao wa furahaaaa kupata muziki mzuriiiiiiii huku wakichezaaaa kwa raha zaoooo
Hahaha Vijana wa Skylight hwa nao hakusita kucheza muziki mzuriiii uliokuwa ukiporomoshwa
Imma Mpiga Gita wa Skylight Band akizichana nyuzi vilivyooo ili kutoa burudani ya nguvuuuuuuu
Idrisa akizipiga drumsss zake kuleta redha ya muziki mzuriiiiiiiiii
Wapiga Kinanda wa Skylight Band wakifurahia ukodak wa nguvuuuu
Mpiga kinanda wa Skylight Band akivipiga vitufee vya kinandaa kwa rahaaa kabisa 
Mpiga Tumba wa Skylight Band Daudi Tumba  kitia ladha zake za tumba
Haya Skylight Band Huwa inawapenda sana mashabiki wake kama pichani inavyoonekana mashabiki hupata mda na wasaa wa kusheherekea siku zao za kuzali kwa kuimbiwa na kukata keki,Operation Manager Wa Mo Blog Zainul Mzige akilishwa keki ya Birthday kwa rahaa kabisaaa
Burudani imenoga sasa Hebu jionee mwenyewe mashabiki hawa wakiyarudiiii vya kutoshaaa kwa rahaaa zaoooo
Hahahaha Ni furahaaa na Kucheza muziki tuuuu jionee mwenyewe hapa
Mpaka juu mpaka juuuuuu kwa rahaaa zao kabisa mashabiki hawaaaaa
Hapoooo sasa ni viunoooo viunoooo mpaka basiiii,wakifurahia muziki mzuri toka kwa bendi yao Skylight
Safi sanaaaaa Unaona kiunoooo kileeee mwisho katikati ni furaha ya muziki mzuri wa skylight Band
Mashabiki wakiendelea kufurahia muziki mzuriiiii
Tazama shabiki huyuuuu akifurahi na kushangaaa baada ya kupigwa moja ya nyimbo anazopendaaa
Hapo sasaaaaa unaambiwa mwanamke nyongaaaaaa
Mikono juuu mikono juuuuu mashabiki wakichezeshwa muziki na waimbaji wa Skylight Band
Nyomiiiiiii lakutoshaaaaa wakifurahia burudaniiii kwa raha zaooooo
Wanamanyoya haoooo wakipata Ukodak wa Nguvuuuuuuuuu
Operation Manager wa Mo Blog Zainul Mzige(wa pili toka kushoto) akipata ukodak na wanamanyoya
Cathbert Kajuna Mmiliki wa KajunaSon Blog(wa kwanza Kushoto)akiwa na Hussein mmiliki wa Ujanatz Blog Na Makubwa Haya  Blog nas mkewe kulia wakipata Ukodak wa Nguvu
Le Mutuz Baharia mmiliki wa Blog ya wanainchi akipata ukodak na Aneth Kushaba meneja wa skylight Band,Usikoseeee Leo kutakuwa na Supriseeee Kibaoooooooo Ndani ya Thai Village

Wednesday, September 24, 2014

KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII SI DHAMBI,TUITUMIE VIZURI KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA.


PIX 1
Meneja mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bwana Innocent Mungy akisisitiza jambo.

Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
Mitandao ya kijamii ni mizuri katika kuhabarisha umma endapo inatumiwa kulingana na madhumuni iliyotengenezwa, kwani ina nguvu ya kusambaza habari kwa haraka na kwa wakati hapa duniani.

Pamoja na umuhimu nwa mitandao hii ya kijamii, kuna baadhi ya watu ambao wao hujiona kuwa wameendelea katika ulimwengu wa kisayansi na teknolojia kiasi cha kuanza kuitumia mitandao hiyo kinyume na malengo kwa kutumia kuiba taarifa mbalimbali za watu na hata usalama wa maeneo muhimu ikiwemo benki, ofisini, mashuleni na sehemu kadha wa kadha.

Watu hawa kwa jina la kisayansi na teknolojia hujulikana kama ‘Hackers’ au Wezi wa mitandao kwa kisawahili, na wamekuwa wakivumbua mbinu mbalimbali kila kukicha ili kuweza kutimiza adhma yao ya kuingilia mitandao mingi iliyopo duniani na wakati mwimngine wamekuwa wakitumika katika shughuli za kigaidi ulimwenguni.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali toka mitandaoni, kuna mbinu nyingi zitumiwazo na hackers hawa katika kuiba taarifa mbalimbali kutoka kwenye takirishi (Computer) hata simu za mkononi kwa njia ya mtandao (internet) na njia hizi huwa zimekuwa zikiboreshwa kila kukicha.

Wezi wa mitandao wengi wamekuwa wakitumia visaidizi vya kompyuta (softwares) zijulikanazo kama Keyloggers ambazo ni hatari sana katika kuiba taarifa toka sehemu yoyote endapo tu mmiliki wa kompyuta ataiacha kompyuta yake kutumiwa na watu wasiofahamika ama katika ofisi mtu mharibifu ataingia na kuingiza katika mfumo wa kuongozea kompyuta kisaidizi kama hiko, kutokana na hilo software hizo hukusanya taarifa za mtu pasipo mtumiaji kujua kinachoendelea na taarifa hizo hutumwa kwa njia ya barua pepe kwenda kwa mharifu ambaye yeye anakuwa anazipata kadri atakavyo juu ya chochote akifanyacho mtu, na moja ya sifa za software hizo ni kwamba hazionekani ndani ya mfumo wa kuongozea kompyuta kirahisi.

Mbinu nyingine watumiazo watu hao ni kwa njia ijulikanayo kwa kimombo kama ‘Phising’ ambapo ukurasa unaofanana sawia na ukurasa halisi wa website hutengenezwa kwa madhumuni thabiti ya kuiba nenosiri ama taarifa zozote kuhusiana na kitu chochote, njia hii ni hatari pia ingawa haina tofauti sana na njia ile ya key logging kwani katika njia hii kazi kubwa inayofanyika ni kuweko kwa kurasa feki ambayo inayofanana na kurasa halisi ya website fulani.


Ili tuweze kujikinga na matukio haya ya wizi wa taarifa kwa njia ya mtandao kuna mambo muhimu ya kuzingatia ambayo tunapaswa kuwanayo makini wakati wote tunapozitumia kompyuta zetu.

Kwanza kabisa, ili tuweze kujiepusha na njia itumiwayo na hackers ijulikanayo kama Key-logging ni vema kuepuka kuazimisha kompyuta zetu kwa watu tusiowajua ama kutumia mbinu ya kubofya kitufe cha Ctrl + shift + Alt + K vyote kwa pamoja ili kuweza kujua uwepo wa kisaidizi kama hiko katika kompyuta na kama ikitokea kimekuja kisanduku kinachokudai kuweka nenosiri basi ujue hapo kuna mtu anachunguza taarifa zako katika kompyuta yako pasipo wewe kujua, hivyo chukua tahadhari kwa kumtafuta mtaalam aweze kuondoa kisaidizi hiko.

Pia yatupasa kuhakikisha kuwa Windows Firewalls zilizopo ndani ya mifumo ya kuongozea kompyuta zetu ziko wazi wakati wote kwani firewall inasaidia kulinda takirishi yako dhidi ya wezi wa mitandao (hackers) ambao wanaweza kujaribu kuiharibu kwa lengo la kutaka kupata taarifa zilizomo ndani, kufuta taarifa, na hata kuiba baadhi ya neno siri za baadhi ya taarifa zako.

Ili kujikinga na wizi wa taarifa zetu katika kompoyuta zetu, tunapaswa kuzingataia kuingiza ama ku-update Vizuizi virusi (Antivirus) mara kwa mara kwani vizuizi hivyo vimetengenezwa kwa ajili ya kuzuia virusi ama visaidizi kompyuta chokozi ili zisiweze kuiingia ndani ya mfumo wa kompyuta na endapo ikitokea imegundua kirusi cha namna yoyote ile, basi inafanya kazi ya kukiondoa ama kukifanya kisiweze kudhuru kompyuta wakati wote.

Bila shaka lolote, Virusi vinaweza kuharibu mfumo wa kuongozea kompyuta pasipo mtumiaji mwenyewe kujua licha ya baadhi ya vizuizi virusi kuwa na tabia ya kuji-update vyenyewe.

Kuweka ama ku-update Antispyware Technology ni jambo linghne la usalam dhidi ya hackers kwani Baadhi ya spyware huwa na tabia ya kukusanya taarifa za mtu pasipo ridhaa yake kama ilivyo kwenye key-logging na Phising au huwa na tabia yakuweka matangazo yasiyo na ulazima katika kurasa Fulani iliyopo katika mtandao wa kompyuta, sasa hii ni hatari kwa usalama wa taarifa za mtu kwani hutumika pia kukwapua, hivyo hatunabudi kuwa makini na baadhi ya matangazo yenye kututaka kupakua visaidizi fulani pasipo malipo kwani mara nyingi huwa ni feki na wakati mwingine huwa na virusi vyenye kuweza kutumika kuiba taarifa ndani ya takirishi yako.

Katika hali yoyote ile ni vema kwa watumaiji wa mitandao ya kijamii kuepuka kutunza nenosiri katika kompyuta zao kwa lengo la kuondoa usumbufu wakati wanapotaka kuingia tena katika kurasa zao kwani njia hiyo nayo ni hatari kwasababu mtu anapoacha nenosiri lake liko (logged in) au unaposema (remember me next time) unatengeneza njia rahisi kwa hacker kujua nenosiri lako kwa kufanya kitendo kijulikanacho kama (Inspect elements Q) yaani zile doti zinazowakilisha neno siri lako (******).

Katika hilo, mharifu anachokifanya hapo ni kuhailaiti hizo doti (nyota) kisha anabofya katika kipanya upande wa kulia (right clicking) kisha anaenda mwisho katika sehemu iloandikwa (inspect elements Q) kisha anafanya uhariri (editing) katika kipengele kilichokuwa hailaitedi kwa rangi ya bluu kilichoandikwa neno ‘passoword’, hapo anafuta na kuandika neno ‘TEXT’ kisha anabofya kitufe cha ‘Enter’ na akishamaliza kufanya hivyo nenosiri lenyewe linajibadilisha kwenda mfumo wa maneno badala ya doti kama ilivyokuwa hapo mwanzo, hivyo humuwezesha kujua tarakimu za nenosiri la akaunti yako ya mtandao wa kijamii uliocha wazi.

Njia nyingine ya jinsi ya kujikinga na wizi wa kimtandao, tunahitaji kuwa makini na vitu tunavyopakuwa toka mitandaoni hasa vibebaji (attachments) toka kwa watu tusiowafahamu au wakati mwingine kwa watu tunaowajua kwani hata hao hutumika katika kusaidia kuibwa kwa taarifa zetu kwa malengo yao binafsi.

Pia ni vema kuepuka kukubali marafiki tusiowajua katika mitandao mingi ya kijamii ikiwemo facebook, twitter, Whatsapp, na mingineyo kwani baadhi ya hackers wanatumia majina yasiyosahihi (fake names) kuomba urafiki kisha hutumia mwanya huo pia katika kuiba taarifa zetu kiurahisi.

Kwa upande wa mabenki, ni vema kuachana na mifumo ya kizamani ya kuongozea kompyuta iliyounganishwa na Mashine za kutolea fedha maarufu kama (ATM) au Automatic Teller Machine kwa kimombo, kwani hiyo ni hatarishi kwasababu mifumo ya kizamani, mfano Microsoft Windows XP ni mifumo ilikwishapitwa na wakati na hata Kampuni yenyewe ya Microsoft imewataka watumiaji kuwa makini nayo kwani haina-updates tena hali inayopelekea kuwa katika hatari ya kuvamiwa na wezi wa mitandao kwa kutumia software za kisasa zenye uwezo wa hali ya juu katika kuiba taarifa.

Katika matumizi ya kadi zetu za kutolea fedha benki (ATM Cards) tunapaswa kuwa makini kuepuka kushea namba za siri kwa marafiki au wapenzi na tujitahidi kuacha tabia ya kutumia nenosiri la kadi hizo kama nenosiri katika akaunti za mitandao ya kijamii kwani hackers nao wamekuwa watu wazuri wa kubashiri taarifa pindi wanapomlenga mtu.

Ili kujiweka salama dhidi ya wezi wa mitandao, basi tujitahidi kutoa taarifa zozote za kiusalama kwa vyombo vya usalama yaani Polisi au kupeleka malalamiko kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pindi tunapoona taarifa za uvunjwaji wa sheria za matumizi ya mitandao, mfano mtu akiona kuna hitilafu katika taarifa za muamala wa fedha zake katika akaunti yake ya benki fulani basi atoe taarifa kwa benki husika ili wao waweze kutafuta tatizo na kutoa ufumbuzi.

Pamoja na haya yote Watanzania wamehimizwa kuacha matumizi mabaya ya mitandao ya jamii ikiwemo kuweka picha za utupu, kusababisha ugomvi, kuwahimiza wengine kwa mambo yasiyo ya kweli, kupotosha jamii na kuvuruga maendeleo.

Akitoa rai hiyo Meneja mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bwana Innocent Mungy alisema kuwa kuna ongezeko la matumizi ya intanenti kwa watanzania hasa mitandao ya kijamii ambayo ni facebook, twiter, Instagram, BBM, LinkedIn na Blogs mbalimbali kwa mambo yasiyofaa na kuleta athari kwa jamii.

Alisema matukio yanayofanyika katika mitandao hiyo na kuleta athari ni utapeli, kulipiza kisasi na ugomvi unaoanzia mitandaoni na kuendelea hadi kwenye uhalisia.

“Kuna utapeli wa kutumia huduma za mawasiliano na ugomvi wa makundi yakugombana kupitia mitandao kwa majina kama timu fulani na timu fulani inayosababisha kuvunjika kwa amani na kusababisha matusi pande zote,” alisema Mungy.

Mungy aliongeza kuwa ni kosa la jinai kutumia mawasiliano vibaya kama ilivyoainishwa katika sheria ya mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 na kutaka mawasiliano yatumike vizuri kudumisha amani ya Tanzania.

“Mamlaka inapenda kuukumbusha umma kuwa ni kosa la jinai kuuza laini ya simu iwapo siyo wakala au mtoa huduma, kutumia simu isiyosajiliwa, kutumia njia yeyote ya mawasiliano kuvuruga amani na kumsaidia mtu mwingine atende kosa,” alisema.

Kwa mujibu wa Mungy ni kosa la jinai kuweka picha za marehemu, mtoto na zinazoonesha utupu katika mitandao ya kijamii huku akibainisha kwamba faini ya kosa hilo ni shilingi za Kitanzania 750,000 na kifungo cha miezi mitatu gerezani.

Kutokana na haya, lazima tutambue kuwa mitandao ya kijamii si dhambi wala si vibaya kuitumia, kwani haijatengenezwa kwa madhumuni ya kumkomoa fulani ama kwa lengo la kuelimisha watu juu ya namna ya kuiba taarifa za watu wengine, bali inetengenezwa ka madhumuni ya kuwakutanisha watu wa sehemu mbalimbali duniani kuweza kuhabarishana juu ya mambo mbalimbali japokuwa baadhi ya watu hao wamekuwa wakiitumia vibaya kinyume na maelngo ya uwepo wake.

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHATOA TAARIFA KUHUSU AWAMU YA PILI YA KAMPENI YA KUSAMBAZA UELEWA WA RASIMU YA PILI-KAMPENI GOGOTA


Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dk.Helen Kijo-Bisimba (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa taarifa kuhusu awamu ya pili ya kampeni ya kusambaza uelewa wa rasimu ya pili (Kampeni Gogota). Kulia ni Mratibu wa Dawati la Katiba wa kituo hicho, Anna Henga na Mwanasheria wa Kituo hicho, Harold Sungusia. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu 0712-727062)
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale
 
KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu kimedai kuwa Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea linaendeshwa kimabavu kwa na kutumia fedha za wananchi bure wakati wakijua fika hakuna katiba itakayopatikana.
 
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadam (LHRC) Dk. Helen Kijo-Bisimba, wakati akitoa taarifa kuhusu awamu ya pili ya kampeni ya kusambaza uelewa wa rasimu ya pili (Kampeni gogota) kwa wananchi.
 
“Cha kusikitisha ni kwamba tumepoteza mabilioni ya fedha ambazo zingeweza kusaidia kwenye sekta mbali mbali zikiwemo za afya na elimu kwa kuwalipa wajumbe wa bunge la katiba,” alisema.
 
Alisema wakati wa kampeni hiyo ambayo imefanyika kwenye mikoa 20 nchini kituo hicho kimebaini kuwa wapo asilimia kubwa ya wananchi wanakerwa na mwenendo wa mchakato wa bunge hilo kwa kuchakachua maoni yao yaliyokusanywa na Tume ya mabadiliko ya katiba.
 
Alisema wakati wa kampeni hiyo ya gogota kituo hicho kimefanikiwa kufika kwenye wilaya zote, na kata tatu kwa kila mkoa ambapo kilifanikiwa kurudisha ajenda ya katiba na uelewa wa rasimu ya pili ya katiba kwa wananchi.
 
Alisema hiyo ni moja ya mafanikio waliyoyapata kuyajua kwa wananchi kwenye kampeni hiyo ambayo ililenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika mchakato hususani kufuatilia bunge la katiba na upigaji wa kura ya maoni muda utakapo fika.
 
Pamoja na mafanikio hayo pia kitu hicho kimekutana na changamoto mbali mbali ikiwemo ya uelewa mdogo kuhusu katiba hususani walio pembezoni mwa miji.
 
Alitaja mikoa hiyo ni Arusha, Tanga, Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, Mbeya, Rukwa, Kilimanjaro, Manyara, Katavi, Iringa, Mara, Njombe, Ruvuma, Pemba Kaskazini, Kusini, Pemba mjini Magharibi, Unguja Kusini na Kasazini.
 
Alitaja changamoto nyingine ni kutokujua kusoma na kuandika kwa baadhi ya wananchi, umangi meza kwa badhi ya viongozi wa mikoa, hofu ya kutopata katiba na mfumo dume kwenye jamii.

KINANA ASHIRIKI UJENZI WA MAABARA SHULE YA SEKONDARI KWALUGURU,HANDENI

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kwaluguru wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara katika shule ya sekondari Kwaluguru wilayani Handeni.
Wananchi wa kata ya Kwaluguru wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana  wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi katika shule ya sekondari Kwaluguru ambapo vyumba 83 vya maabara vinajengwa wilayani Handeni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka zege kwenye moja ya vumba vya maabara za shule ya sekondari Kwaluguru.
Mbunge wa Jimbo la Handeni Dk. Abdallah Kigoda ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara akishiriki kuweka zege kwenye moja ya vyumba vya maabara vya sekondari ya Kwaluguru.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiujenzi wa ofisi ya CCM Tawi la Kweinjugo kata ya Kwaluguru wilaya ya Handeni
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa Handeni kwenye uwanja wa mkutano Soko la Zamani Chanika.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akicheza ngoma ya asili ya wazigua  .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Handeni kwenye uwanja wa mkutano Soko la Zamani Chanika ambapo aliwaambia wajifunze kupima mambo ya viongozi wa siasa wasije wakaingizwa kwenye matatizo bila kutarajia kwani wapo zaidi kwa ajili ya maslahi yao binafsi na si ya wananchi ndio maana wanadiriki kutangaza maandamano wakati wao wenyewe hawapo wameenda nje ya nchi kupumzika.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Henry Shekifu akisalimia wakazi wa Handeni kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Handeni ambapo aliwaambia watu wanatakiwa kupewa fursa na kurahisishiwa maisha yao hivyo kodi ndogo zinatakiwa ziangaliwe upya kwani zimekuwa kero kwa wafanyabiashara ndogo ndogo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na madereva wa boda boda wa Chanika Handeni

UN WAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI KUJADILI USHIRIKIANO‏ BAINA YAO

Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan (katikati) pamoja na Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani (WHO) Dk Rufaro Chatora (kulia) kabla ya kuanza kwa mkutano wa kuboresha ushirikiano kati ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Shirika la Umoja wa Mataifa nchini UN lakutana na wanahabari kujadiliana na kudumisha ushirikiano wao katika habari ambapo wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wamekuna na viongozi mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ili kujadili kwa pamoja.

UN wameeleza kazi zinazofanywa na shirika hilo ili waweze kushirikiana kwenye mambo mbalimbali katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi, elimu na kuzifahamu kazi za mashirika hayo hapa nchini.

Hivyo waandishi na wahariri wa habari wameombwa kudumisha ushirikiano katika kazi zote zinazofanywa na mashirika yanayosaidia nchini kwa kiasi kikubwa.

Pia wameweza kuzungumzia ugonjwa wa Ebola ambao umeibuka kwa kasi sana hivyo kuwataka kuweza kuandika habari zinazowajuza jamii ili kuweza kuuepuka.

Nia na madhumuni ya mkutano huo na wahariri wa vyombo vya habari ni kuweza kujenga ushirikiano madhubuti baina yao na kuweza kushirikiana kwa karibu katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na wahiriri wa vyombo vya habari nchini ambapo alielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini ikiwemo utekelezaji wa agenda mbalimbali za malengo ya milenia.
Bwana Clioni akiendesha mjadala baina ya viongozi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini.
Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan akitoa salamu kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati wa mkutano wa kuendeleza ushirkiano baina ya Umoja wa Mataifa na vyombo vya habari nchini.
 
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole akitoa shukrani kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakati walipokutana na wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuboresha ushirikiano na mahusiano baina yao.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akisherehesha mkutano huo baina ya Umoja wa Mataifa na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo wa kuboresha mahusiano baina yao na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Untitled
Mkutano ukiendelea huku wengine wakipitia makabrasha mbalimbali yenye taarifa za Umoja wa Mataifa.
Mmoja wa wahariri akihoji swali kwa viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa wakati wa mkutano huo.
Picha ya pamoja mara baada ya mkutano wa kuboresha mahusiano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mashirika ya umoja wa mataifa nchini.