Pages

KAPIPI TV

Tuesday, September 23, 2014

ABAS MTEMVU AFANYA ZIARA KATIKA MATAWI TEMEKE, AGAWA VIFAA VYA MICHEZO

  Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu akiwa anaingia  Ofisi ya katibu kata,ya chama cha Mapinduzi CCM Buza Dar es Salaam (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) wa Blog ya ( UJIJIRAHAA). yenye herufi kubwa www.ujijirahaa.blogspot.com
 Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu akitia saini katika kitabu cha wageni Ofisi ya katibu kata ya chama cha Mapinduzi  CCM Buza Dar es Salaam.
 Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu,(wapili kulia) wakipiga makofi wakiimba wimbo wa chama hicho mara alipo wasili Ofisini hapo,kuanzia kushoto ni Mwenyekiti UVCCM kata ya Buza,Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Jimbo la Temeke na msaidizi wa Mbunge wa jimbo hilo upande wa Vijana.Peter Sillo,aliye vaa shati la kijani ni  Mwenyekiti wa CCM kata ya Buza, Shabani Bambo  na wakwanza ni Katibu kata ya Buza Shabani Abdallah.
 Katibu kata ya Buza Shabani Abdallah, akimkaribisha Mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu, na akitambulisha  katika hafla fupi ya kukabidhi jezi na pesa taslim kwa  matumizi mbalimbali ya kiofisi, katika moja ya ahadi aliyoitowa kwa majimbo matano kwa wanachama wa chama cha Mapinduzi(CCM) Buza.
 Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Temeke (CCM),Ally Mehalla ,akisalimia wanachama wa chama hicho
 msaidizi wa Mbunge wa jimbo la Temeke upande wa Vijana.Peter Sillo kushoto akisalimia wanachama wa chama cha Mapinduzi (kushoto) Mwenyekiti wa( CCM)  kata ya Buza, Shabani Bambo anaye fatia ni Mbunge wa jimbo la Temeke Abbas Mtemvu na kulia ni Katibu kata ya Buza Shabani Abdallah.
 Viongozi wa Matawi kata ya Buza
 Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu(kulia), akikabidhi Pesa Taslim kwa katibu wa Uchumi wa chama hicho Hawa Zuberi, kwa matumizi mbalimbali ya kata ya Chungu Buza Dar es Salaam.
Mbunge wa jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Wabunge Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Mtemvu(kulia) akimkabidhi Jezi na pesa taslim katibu wa Tawi la Mashine ya Maji5 Baraka Mohamedi
 Mbunge wa Jimbo la Temeke na Mwenyekiti wa Wabunge  Mkoa wa  Dar es salaam,Abbas Mtemvu (kulia),akimkabidhi Mwenyekiti wa CCM kata ya Buza seti ya Jezi pamoja na Pesa taslim Sh.milioni moja na laki moja.  Johari Mkonde (kushoto), kati ya ahadi aliyoitowa kwa majimbo matano kwa wanachama wa chama cha Mapinduzi . anaye shuhudia ni Mwenyekiti wa chama hicho kata ya buza, Shabani Bambo.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke akitoka na viongozi kwanda eneo lililo haribiwa na Mvua na kusababisha njia hiyo kutopitika na Magari yakawa hayapiti katika njia hiyo, kati ya Vituka Machimbo na Buza Shule na jinsikani wataweza kuweka Daraja katika Mto wa Buza ili wanafunzi na wananchi waweze pita kwa urahisi kutokana na ukaribu wa eneo hilo.
 Wakiwa katika kituo kidogo cha Polisi cha Buza ,kujionea maendeleya ya kituo hicho baada ya kutoa Pesa awamu ya kwanza na kuahidi kukimalizia na kuwawekea Fenicha mbalimbali kituoni hapo.
 Njia iliyo haribiwa na Mvua na Gari kuto pita tena
 Mto Buza ulivyo ulivyo haribiwa na Mvua

Monday, September 22, 2014

UMOJA WA MATAIFA WATAKA CHANZO CHA SIASA KALI ZINAZOLETEA MIGOGORO ZICHUNGUZWE

DSC_0007

Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuhudhuria maadhimisho hayo na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Joseph Masasi (wa pili kulia), Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Bw. Dunford Makala (katikati) na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania , Bw. Ali Rajab (kulia) pamoja na viongozi wengine taasisi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinizim). (Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog)

Na Mwandishi wetu
WAKATI Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon anahimiza serikali duniani kutafuta chanzo cha kukosekana kwa amani na kuongezeka kwa watu wenye misimamo mikali, wasemaji katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa amani Duniani wameitaka serikali ya Tanzania kutupia macho makali mauaji ya albino nchini.

Akimwakilisha Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika adhimisho lililofanyika viwanja vya Mnazi mmoja leo Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Alvaro Rodriguez, alisema ili kudumisha amani kuna mambo mengi yanatakiwa kufanyiwa kazi hasa kutambua chanzo cha migogoro inayosababisha msuguano mkubwa katika jamii na kukosekana kwa amani.

Alisema amani ina maana kubwa kwa jamii na ndio maana Umoja wa mataifa miaka 13 iliyopita iliamua kuadhimisha siku hiyo kwa lengo la kushawsihi makundi yanayosigana kupata nafasi ya kuzungumzia na kuona maana ya amani.

Alisema pamoja na kuwepo kwa hatua kubwa tangu kupitishwa kwa azimio la Umoja wa Mataifa la kuadhimisha amani, safari ya kufikia amani ni ndefu na ili kufanikiwa pande zote ni lazima kwenda hatua kwa hatua kwa kushirikiana.

Alisema mafanikio ambayo yamepatikana ni pamoja na UN kufanikiwa kufundisha kada ya habari juu ya uandishi katika mazingira tete na kusaidia majadiliano ya kitamaduni yanagusa masuala ya amani.
DSC_0031Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (katikati) akimtambulisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili kwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania (THBUB), Bi. Mary Massay.

Aidha alisema kwamba wanafanyakazi na Wizara ya mambo ya ndani kuhakikisha kwamba wanastawisha mipango yote inayolenga kuzuia ghasia na kuboresha mipango inayoimarisha amani.

Akihutubia bada ya mashuhuda kuzungumzia hali ya tishio la amani nchini Tanzania hasa la kukosekana kwa amani miongoni mwa watu wenye ulemavu wa ngozi albino, Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa aliipongeza serikali ya Tanzania kw ajuhudi zake za kuimarisha amani katika kanda ya maziwa makuu na kushiriki katika operesheni mbalimbali za Umoja wa Mataifa ziliziolenga kuleta hali bora zaidi ya maisha kwa watu wanaoishi katika hekaheka za kivita.

Akiwa na mwezi mmoja tangu awalisili nchini mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa nchini amesema kwamba anatarajia kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali na wananchi wa Tanzania kuhakikisha taifa la Tanzania linaendelea kuwa na amani

Wakati Mwakilishi huyo amesema kwamba watu wengi duniani wanawaonea gere wananchi wa Tanzania kwa amani wlaiyonayo, mwakilishi wa Under the Same Sun, Vicky Ntetema ametaka kupitiwa upya kwa sheria ya uchawi ya mwaka 1928 iliyofanyiwa mabadiliko mwaka 2002 ili kukabiliana na mauaji ya albino nchini ambayo kwa kiasi kikubwa yanachochewa na waganga wa kienyeji.
DSC_0039Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid meza kuu.
Alisema sheria hiyo ina mwanya mkubwa wa wauaji kucheza nayo na kusababisha sehemu kubwa ya kesi zilizopo kushindwa kuwatia hatiani wahusika.
Alisema wakati tukielekea katika uchaguzi mkuu mauaji ya albino na ukataji wa viungo umeongezeka.

Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi 25 za afrika zinazofanya ukatili dhidi ya walemavu wa ngozi, toka mwaka 2006 watu 74 wameuawa, 56 wamenusurika na 11 wameongezewa ulemavu huku makaburi 18 ya albino yakinajisiwa kwa kufukuliwa.

Watu wa kituo cha haki za binadamu wamesema pamoja na kuwepo na matukio 120 ya ukatili dhidi ya albino kesi 11 tu ndio zilizofikishwa mahakamani huku tano zikiwa zimekatiwa hukumu ambazo hazijaridhisha.

Vicky alisema katika matukio yote hayo chanzo ni ushirikina lakini kutokana na kukosekana zimeshindikana kuzimaliza zinavyotakiwa.
DSC_0082Brass band ya jeshi la Magereza ikiongoza maandamano ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya amani wakiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho hayo jana.

Vicky aliitaka jamii kuwalinda albino kwani serikali pekee haiwezi kufanya kitu chochote huku akisema kwamba hesabu ya albino mmoja katika kila wananchi 1,400 haiwezi kulindwa kwa dhati na serikali kutokana na idadi ya polisi kutokua sawa na wananchi.

Aidha alishauri serikali kutoa msaada wa kisheria kwa waathirika kabla ya kuingia mahakamani ili waweze kusimulia vyema kadhia zao na pia wasiangushwe na wanasheria ambao wanatumia udhaifu wa kisheria kuwatoa watuhumiwa hatiani.

Pamoja na Vicky Ntetema kushawishi wananchi kulinda albino na kuwafichua wauaji Kaimu Mufti Sheikh Ismail Habibu Makusanya ameitaka serikali kuhakikisha kwamba kila mwananchi anapata utulivu wa kutosha kuendelea na shughuli zaka na kuhimiza mahakama kutenda haki.

Aliwakumbusha wananchi kama alivyosema Sydina Omar kwamba kila mmoja ataulizwa amefanya nini kukomesha madhila katika jamii wakati wa kiama na kusema serikali isipowajibika itasema nini na wananchi nao pia watajibu nini.
DSC_0100Pichani ni baadhi wadau kutoka taasisi mbalimbali pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) wakiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja huku wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kuhamasisha amani nchini na kupinga mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinism) nchini wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika jana jijini Dar.

Alisema amani hailetwi kama mvua , inatafutwa na kusema watu wasipotafuta amani na kuhakikisha amani inakuwapo itakuwa shida kubwa kwa taifa hili ambalo miaka yote limeogelea katika bahari ya amani.

Aliwasihi waumini wa Kiislamu na wananchi wengine kuhakukisha kwamba amani inakuwa ajenda ya kudumu kila wanapokutana pamoja.

Katika maadhimisha hayo ambapo wananchi walianza maandamano shule ya Uhuru Mchanganyiko hadi viwanja vya Mnazi mmoja, mgeni rasmi Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk Seif Rashid alisema serikali imejipanga kuhakikisha inakomesha mauaji ya albino na kuwataka wananchi kuisaidia kwa kutokuwa waoga kutoa ushahidi na pia kuwaripoti watuhumiwa.

Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ya haki ya amani kwa watu wote, komesha mauaji ya albino inahamasiaha umma wa Tanzania kulaani,kukemea na kukomesha mauaji kwani yanakwenda kinyume na katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 14 ambayo inaeleza kwamba kila mtu ana haki ya kupata hifadhi katika jamii.

Aidha waziri alitaka kutekelezwa kwa agizo lake kuhusu tiba mbadala na za asili na kusema serikali itaendelea kulinda amani na kutoa ulinzi kwa wathirika.
DSC_0108Meza kuu ikipoeka maandamano ya siku ya kimataifa ya amani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
DSC_0248Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Joseph Masasi akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi Mh. Seif Rashid (wa pili kulia). Kutoka kushoto ni Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Bw. Dunford Makala, Balozi wa Uturuki nchini, Mh. Ali Davutoglu.
DSC_0593Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Seif Rashid, akisoma hotuba kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
DSC_0415Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani.
DSC_0418Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipongezwa na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu baada ya kusoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
DSC_0279Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akisoma risala yake kwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
DSC_0284Kaimu Mufti Sheikh Ismail Habibu Makusanya, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ambapo alilaani vikali mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinizim) na kusema kuwa watu wote wanaoshiriki katika mauaji hayo kamwe hawatoiona Pepo ya Mwenyezi Mungu.
DSC_0384Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Ali Davutoglu akisoma ujumbe kwa niaba wa umoja wa mabalozi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani.
DSC_0300Baadhi ya wadau kutoka taasisi na asasi mbalimbali nchini walioshiriki kwenye maadhimisho hayo.
DSC_0420Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania (THBUB), Bi. Mary Massay akitoa nasaha kutoka kwa Tume hiyo, ambapo alitoa rai kwa mtu yeyote yule ambaye ana malalamiko au matatizo katika Haki za Binadamu anakaribishwa kwenye tume hiyo kwa ajili kupata msaada wa kisheria.
DSC_0519Shuhuda aliyenusurika kwenye mauaji ya Albino ambaye amekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford akitoa ushuhuda wake na killio chake mbele ya meza na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mnazi mmoja.
DSC_0534Mke wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, akilia kwa uchungu baada ya kusikia shuhuda kutoka kwa mhanga wa mauaji ya Albino aliyekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford (hayupo pichani) ambaye hadi sasa anapewa matunzo na Shirika la Under The Same Sun.
DSC_0540Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akimfariji mke wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar.
Kwa matukio zaidi ingia humu

SHEREHE YA MWAKA YA MFUKO WA PENSHENI WA PPF YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

 Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey Mlimuka akizungumza na wafanyakazi wa mfuko wa pensheni wa PPF wakati wa sherehe ya Mwaka iliyofanyika katika Ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Jijini Dar Es Salaam Mwishoni mwa wiki
 Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey Mlimuka akiwapongeza Vijana wanaounda kundi la The Voice ambao ni wasanii wa fani ya Akapela mara baada ya Kutoa burudani katika sherehe ya Mwaka ya Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam.
Kundi la The Voice likitoa burudani katika sherehe ya Mwaka ya Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Blue Pearl
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika Sherehe ya Mwaka ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Ukumbi wa Blue Pearl.
Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Janeth Ezekiel akipokea cheti na zawadi kutoka Kwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey Mlimuka mara baada ya kutangazwa kuwa mfanyakazi bora wa mwaka 2013 kutoka Idara ya Mahusiano na Masoko ya Mfuko wa Pensheni wa PPF katika sherehe ya mwaka ya PPF iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Blue Pearl, Jijini Dar Es Salaam
 Pichani Juu Ni baadhi ya wafanyakazi kutoka Idara Mbalimbali za Mfuko wa Pensheni wa PPF waliojipatia zawadi kwa kuwa wafanyakazi bora wa Mwaka 2013.
Wafanyakazi wa PPF wakifuatilia Burudani iliyokuwa ikitolewa na Kundi la The Voice katika Sherehe ya Mwaka ya PPF iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Hotel ya Blue Pearl.
Mmoja wa wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF akimtunza Mmoja ya waimbaji wa kundi la the voice lililokuwa likitoa burudani wakati wa sherehe ya Mwaka ya Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika Mwisho mwa Wiki katika hoteli ya Blue Pearl, Jijini Dar 
Wadau wakiserebuka Muziki mara baada ya wafanyakazi bora kupewa motisha na zawadi zao katika sherehe ya Mwaka ya PPF iliyofanyika Mwishoni mwa Wiki katika Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Jijini Dar Es Salaam.Pichote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Sunday, September 21, 2014

KINANA ATINGA KIHABA, AKAGUA NA KUFUNGUA MIRADI YA MAENDELEO

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kuvyeka miti wakati wa uzinduzi wa kambi ya Umoja wa Vijana wa CCM, ya mafunzo ya kilimo katika eneo la Boko Timiza, Kibaha mjini mkoa wa Pwani. Katika kambi hiyo vijana wanatarajiwa kufanya mafunzo ya kilimo kwenye shamba la ekari 25.

 Kijana akihamasisha vijana wenzake, walioko kwenye kambi hiyo ya mafunzo ya kilimo, eneo la Boko Timiza wilaya ya Kibaha mjini.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua jiwe la msingi ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani leo, Septemba 19, 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanda mti kwenye kiwanja unakofanyika ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani, baada ya kuzindua ujenzi huo leo, Septemba 19, 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Kushoto ni Mbunge wa Kibaha Mjini, Silvestry Koka.

 Kinana akipata burudani ya Ngonjera kutoka kwa vijana Chipukizi baada ya kuzindua ujenzi Ofisi ya CCM wilaya ya Kibaha mjini leo. Wapili kulia ni Nape.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimfurahia Chipukizi wa CCM,  Suma Iddi, aliyekuwepo wakati akizindua ujenzi Ofisi ya CCM, wilaya ya Kibaha mjini

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua tangi la maji alipokagua ujenzi wa mradi wa maji katika kitongoji cha  Muheza, wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani.

 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Tumbi wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani akimpatia maelezo Katibu Mkuu wa CCM, Kinana kuhusu wodi ya wagonjwa mahututi iliyopo kwa sasa kwenye hospitali hiyo, ambapo alisema bado inahitajika kuwepo dawa za kutosha kuliko ilivyo sasa.
Mganga Mkuu wa  Huduma za Afya Hospitali ya Tumbi Dk. Peter Dattani akieleza changamoto mbali mbali walizonazo hospitali ya Tumbi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alieleza bado hospitali hiyo inahitaji vifaa na madawa kwani inapokea majeruhi kwa asilimia mia moja

ELIMU YA AWALI BADO NI TATIZO TUNDURU,YAENDESHWA BILA VITABU


Wanafunzi wa darasa la awali Shule ya Msingi Nakayaya wakiwa darasani. Hata hivyo shule hii haina chumba cha darasa la awali chumba hiki kimejengwa kwa matumizi mengine na kwa sasa kinatumika kwa muda kwa kuwa kipo katika ujenzi.
Wanafunzi wa darasa la awali Shule ya Msingi Nakayaya wakiwa darasani. Hata hivyo shule hii haina chumba cha darasa la awali chumba hiki kimejengwa kwa matumizi mengine na kwa sasa kinatumika kwa muda kwa kuwa kipo katika ujenzi.
Mwalimu Christina Komba (kulia) wa darasa la awali Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko akiwa darasani.
Mwalimu Christina Komba (kulia) wa darasa la awali Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko akiwa darasani.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Majengo, Madina Mkali.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Majengo, Madina Mkali akizungumza na mwandishi wa habari hizi (hayupo pichani) ofisini kwake.
Mwalimu wa muda wa darasa la awali, Shule ya Msingi Nakayaya, Teckla Milanzi akionesha baadhi ya nakala za vitabu walivyonavyo.
Mwalimu wa muda wa darasa la awali, Shule ya Msingi Nakayaya, Teckla Milanzi akionesha baadhi ya nakala za vitabu walivyonavyo.

Tunduru
SHULE nyingi za msingi zenye madarasa ya awali Wilayani Tunduru zimekuwa zikiendeshwa kwa changamoto mbalimbali ikiwemo ya kutokuwa na vitabu vya baadhi ya masomo kabisa huku zikiwa na upungufu mkubwa wa vitabu kwa masomo mengine.Hali hiyo imebainika hivi karibuni katika uchunguzi uliofanywa kwa baadhi ya Shule za Msingi za Wilaya ya Tunduru, Mkoani Ruvuma huku walimu wa madarasa hayo wakielezea jitihada binafsi wanazozifanya kukabiliana na changamoto hiyo.

Mwalimu Christina Komba wa darasa la awali Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko akizungumzia hali hiyo alisema darasa lake halina vitabu vya masomo kama ya sanaa, Haiba na Michezo na wala miongozo ya namna ya ufundishaji hivyo kila mwalimu anayefundisha darasa hilo hubuni nini afundishe katika masomo hayo.

“Madarasa ya elimu ya awali hayana vitabu, hayana miongozo…huwa tunaazima au ukipata hela yako wewe binafsi unaenda kununua kitabu kimoja au viwili ili uweze kuwasaidia watoto. Na baadhi ya masomo hayana vitabu kabisa hata ukienda madukani katika Wilaya yetu vitabu kama Haiba na Michezo, pamoja na Sanaa hazipo kabisa madukani,” alisema Bi. Komba.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nanjoka, Batadhari Mkwela akizungumzia shule yake alisema licha ya usajili wa wanafunzi wa awali kuongezeka kila mwaka upatikanaji wa bajeti ya kuendesha elimu hiyo ni changamoto kubwa huku uchangiaji kwa wazazi ikiwa wa kusuasua.“…

Darasa la awali linahitaji vitendea kazi lakini havipo, hatuna vifaa kama vitabu vya kutosha, nyenzo za kufundishia, hakuna bajeti hata ya vifaa hivi toka Serikalini, hatuna hata madawati maalum kwa ajili ya wanafunzi wa darasa hili,” alisema Mkwela.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Majengo, Madina Mkali alisema uendeshaji wa darasa la awali shuleni hapo ni wa kusuasua kutokana na kutokuwa na bajeti inayoletwa kusaidia elimu hiyo, isipokuwa kwa baadhi ya mwaka kuletwa madawati kumi kwa ajili ya wanafunzi wa awali.

“…Uendeshaji elimu ya awali hapa ni wa wastani kwa kweli kutokana na changamoto zinazotukabili, kwanza vifaa vya kuwafundishia watoto hawa ni tatizo na wazazi kwa eneo hili wamekuwa hawana mwamko wa elimu hii kabisa. 

Kwanza hawachangii michango ya chakula kama inavyotakiwa ili mtoto apate chochote awapo shuleni,” anasema mwalimu Mkali.

Kwa upande wake mwalimu wa darasa la awali, Shule ya Msingi Nakayaya, Teckla Milanzi akitolea mfano shuleni hapo alisema vitabu vya Kiswahili, Kiingereza, Sayansi na Hisabati kuna nakala moja moja tu kwa kila somo, ambazo huzitumia yeye mwenyewe.Aidha mwalimu Milanzi aliongeza kuwa darasa hilo licha ya kuwa na changamoto kedekede hata kwenye mgao wa fedha zinazoletwa shuleni kila mara halimo jambo ambalo husababisha hali kuendelea kuwa mbaya zaidi.Hata hivyo mwalimu wa darasa la awali Shule ya Msingi Majengo, Hadija Makamla alisema anavyo baadhi tu ya vitabu vinavyoitajika katika darasa hilo, nakala ambazo pia ni chache ukilinganisha na ukubwa wa darasa lake.

 “…Ninazo nakala chache kwa ajili ya mwalimu tu ila wanafunzi hawana hata kimoja…lakini kuna masomo mengine sina vitabu kabisa kama vile Sanaa na Haiba ya Michezo sina kabisa hata mimi,” anasema mwalimu Makamla. *Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa ushirikiano na HakiElimu