Pages

KAPIPI TV

Friday, August 29, 2014

KIKWETE AAGIZA HALMASHAURI ZINUNUE NYUMBA NHC


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. (Picha zote kwa hisani ya Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa)
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Abdulkarim Shah.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene  katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia jiwe la msingi mara baada ya kufungua  mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma wanaoshuhudia ni pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na Mbunge wa Afrika Mashariki Adam Kimbisa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza katika hafla hiyo jana
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akizungumza katika hafla hiyo jana
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu wakati akitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. Mradi huo una jumla ya nyumba 44..
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. Mradi huo una jumla ya nyumba 44.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene akizungumza wakati akitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. Mradi huo una jumla ya nyumba 44.
 Wageni waliokuwapo katika hafla hiyo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoka ndani ya nyumba ya mfano baada ya kufungua nyumba za  gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na Mbunge wa Afrika Mashariki Adam Kimbisa.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na Mbunge wa Afrika Mashariki Adam Kimbisa.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria ufunguzi mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma wanaoshuhudia ni pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meneja wa NHC mkoa wa Dodoma Itandula Gambalagi wakati wa ufunguzi wa nyumba hizo za gharama nafuu.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene akizungumza na Meneja wa NHC Dodoma Itandula Gambalagi wakati akitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. Mradi huo una jumla ya nyumba 44.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma, wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika jjana.
Msafara wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ukiwasilia katika eneo la tukio 
  • Imeandikwa tarehe 29 Agosti 2014
Na Sifa Lubasi, Kongwa
 
HALMASHAURI nchini zimetakiwa kununua nyumba za bei nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba (NHC) ili kuwapangisha watumishi wake.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akifungua mradi wa nyumba nafuu katika eneo la Mnyakongo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya maeneo watumishi wa halmashauri kukaa mbali na sehemu zao za kazi kwa visingizio vya kukosa makazi.

Alisema sababu hiyo sasa haina msingi katika maeneo ambayo NHC imejenga nyumba zao kwani halmashauri inaweza kununua nyumba hizo na kuwapangisha watumishi wake.

‘’ Hawa NHC wana utaratibu kwa kupitia mabenki wanayoshirikana nayo hivyo kwa kutumia utaratibu huo halmashuri mnaweza kwenda katika hizo benki na kuingia mkataba na kukopa nyumba hizo na kisa kuwapangisha watumishi…’’ alisema.

Aidha Rais Kikwete alisema shirika hilo linafanya kazi nzuri katika ujenzi wa nyumba hizo za bei nafuu huku akilitaka kuongeza zaidi idadi ya nyumba. Alisema ni vyema sasa halmashuri zikaongeza maeneo ya kujenga nyumba hizo ili wananchi wengi zaidi waweze kuishi katika nyumba bora.

Akizungumza katika ufunguzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa NHC Nehemia Mchechu alisema mradi huo ni utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu. Alisema mradi huo wenye nyumba 44 hadi kukamilika utakuwa umegharimu Shilingi bilioni 1.2.

Alisema nyumba hizo zinauzwa kwa gharama kati ya Sh milioni 35 hadi 40 kulingana na ukubwa wa nyumba husika.

Hata hivyo alisema bado kuna tatizo la kodi katika uuzaji wa nyumba hizo na ndio kinachofanya kuuzwa kwa bei kubwa.

Alimuomba Rais kusaidia katika kusukuma nia ya kushusha kodi ili nyumba hizo ziuzwe kwa bei nafuu na kila mwananchi aweze kununua.

SKYLIGHT BAND WAZIDI KULITIKISA JIJI LA DAR NA VIUNGA VYAKE KWA BURUDANI KALIII ILIYOKWENDA SHULE

Diva wa Skylight Band Mary Lukos Akiimba kwa uzuri kabisa Ndani ya kiota cha burudani Thai Village.Bendi yako machachari na inayopendwa zaidi ndani ya Jiji la Dar es salaam na viunga vyake vyote Skylight Band inakukaribisha wewe mdau,mpenzi na shabiki wa kweli Leo hii kuanzia mida ya Tatu kamili ndani ya ukumbi wa Thai Village masaki,ambapo burudani ya nguvu itaporomoshwa na wanamuziki mahiri wa bendi hiyo kama Aneth Kushaba,Mary Lukos,Digna Mpera,Sam Machozi,Donode,Joniko Flower na Sony Masamba.Njoo upate muziki mzuriiiii na ladha zote za kiafrika na ulaya pamoja na suprizeee kibaooooo.
Digna Mpera akiimba na kucheza kwa umahiri kabisa ili kuwapa burudani wapenzi na mashabiki wake
Anaitwa Aneth Kushaba A.K.A AK47 au Le Meneja Her Self akiimba kwa mikogooo safi ndani ya Thai Village ili kuwapa burudani ya nguvu Mashabiki wake
Le Meneja Her Self  Akiimba kwa Hisia Kaliiiiii Kabisaaaaa
Aneth Kushaba(katikati)akiongoza madiva wenzake wa Skylight Band Digna Mpera(kulia) na Mary Lukos(kushoto) kushambulia jukwaaa sawa sawa na kwa vocal kali
Hashimu Donode A.K.A Dogo Dogo akilishambulia jukwaaa kwa nguvu ili kuwapa burudsni mashabiki wake
Bana ba Kongo Joniko Flower(kushoto) na Sony Masamba(kulia) wakiimba kwa uzuriiiii kabisa zile ladha za kilingala na bolingo na kutoa burudani kaliiii kwa mashabiki wa Skylight Bnd
Hapo sasaaaa Bana ba Kongooo wakianza kuyarudi mauno taratibuuuuuuu
Joniko Flower(kushoto)akiongoza Majembe ya Skylight Band Sony Masamba(katikati) na Sam Mapenzi(kulia)kucheza masebene yaliyokuwa yakiporomoshwa ndani ya Thai Village
Sony Masamba(kushoto) na Sam Mapenzi(kulia)wakiyarudi kwa rahaaa zaooo
 Hapo sasaaa Mpaka chini taratibuuu Joniko Flower(kushoto)akiongoza Majembe ya Skylight Band Sony Masamba(katikati) na Sam Mapenzi(kulia)kucheza masebene yaliyokuwa yakiporomoshwa ndani ya Thai Village
Hapana chezea kabisa vijana hawaaaaa,si unaona mwenyewe mastepu hayooo njooo leo na wewe ufurahiiii
Hapo sasa Aneth Kushaba Le Meneja Her Self(kulia) Akiwapa tafu ya mauno lainiiiiii na nyoroti Sony Masamba(katikati) na Joniko Flower(kushoto)
Daudi Tumba Akiziadhibu vilivyo tumba zake ili kuleta ladha nzuriiiiiii ya muziki
Tophy bass Akilikung'uta vilivyo Gitaa Lake kuleta ladha tamuuuuuuu kwenye muziki
Mozee Vinanda akifurahia kuzipapasa tufe za kinanda chake na kuleta ladha tamuuuu kwenye muziki unaopigwa
Viunooooo Viunoooooooo hapo ni mashabiki wakicheza kwa raha zaooooo muziki mzuri uliokuwa ukipigwa na vijana wa Skylight Band
Hapo ni viunoooo hatari kwa mashabikii kwa mduara mzitooo uliokuwa ukipigwa
Mwanamanyoya akipata Ukodak na Mdau wa Skylight Band
Wadau wa Skylight Band Wakipata Ukodak kwa Furahaaa teleeeeee
Furaha ya muziki mzuri,ndio maana wadau hawa wa Skylight Band wana Rahaaaaaa
Weweeee na Yuleeeee usikoseeee leo ndani ya Thai village upate burudani nzuriiiiiiii!!!

Thursday, August 28, 2014

BIOLANDS YAKABIDHI MSAADA WA AMBULANCE NISSAN PATROL KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA KYELA.

Gari la Kubebea wagonjwa likiwa linaingia kwa ajili ya Makabidhiano
Meza kuu
 Meneja Mkuu msaidizi wa Biolands(Kulia) akimkabidhi na kupongezana  na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga ufunguo wa Gari la Wagonjwa katika Sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Halmashauri ya Wilaya Kyela.
 Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Malenga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Gari la Wagonjwa walilokabidhiwa na kampuni ya Biolands , akisaidiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Seif Mhina 
Wananchi na Wageni mbalimbali waliohudhuria Sherehe za makabidhiano ya Gari la wagonjwa wakifuatilia kwa makini tukio hilo
 
*****************
 
KAMPUNI ya Biolands
International Ltd imetoa msaada wa gari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) aina ya
Nissan Patrol kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela lenye thamani ya shilingi zaidi ya Milion 76.
 
Hafla ya makabidhiano ya gari hilo imefanyika  katika viwanja vya
Halmashauri hiyo baina ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela Magreth Esther Malenga,
Meneja wa Bioland Felix Mtawa na Mwenyekiti wa uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya Afya, Dk.Charles Mbwaji wakishuhudiwa na mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina.
Katika Risala ya Bioland iliyosomwa na Meneja wa Tawi, Erasto Kilongo, alisema lengo la msaada huo ni kutambua mchango wa wananchi katika maeneo wanayofanya kazi.
 
Alisema Bioland ni Kampuni Binafsi inayojishughulisha na ununuzi wa Kakao katika Wilaya za Kyela na Rungwe ambapo   inafanya kazi na na wakulima zaidi ya 20,000 katika vituo 137 vilivyopo katika wilaya hizo mbili.
 
Alisema Kampuni hiyo inafanya kazi moja kwa moja na wakulima katika kufanikisha shughuli za vyeti mbalimbali ambavyo vinasaidia kuwepo kwa uhakika wa soko la kakao, vyeti kama vile kilimo hai
(organic farming), Kilimo endelevu (Rain forest Allience),na  Usawa wa kibiashara katika jamii (social and
Fare Trade).
 
Alisema katika sekta ya Afya na usalama wa wazalishaji, Kampuni  imenuia kuhakikisha afya za wakulima na familia zao zinaendelea kuimarika wakati wote na kupata huduma za afya kwa gharama nafuu kupitia mradi wa Bima ya afya ya jamii.
 
Alisema  katika kufanikisha mradi huo, Kampuni  ilikubali kutenga kiasi cha dolla 60,000 za kimarekani kwa kipindi cha miaka 5 toka 2010 hadi 2014 kwa ajili ya kutoa ruzuku kwa wakulima wanaojiunga na bima ya afya ya jamii.
 
Aliongeza kuwa  Kutokana na umuhimu huu wa kuhakikasha afya za
wakulima na familia zao zinaimarika pia Biolands imefadhili ununuzi wa gari la wagonjwa (Ambulance)  lenye thamani  Shilingi Milioni 76,140,000/=, ambalo  limekabidhiwa kwa Halmashauri kwa niaba ya CHIF, HIMSO, CIDR na wananchi wa Kyela.
 
Awali akitoa salamu kwa niaba ya HIMSO, Dk. Charles Mwanji, alisema kazi ya HIMSO ambalo ni shirika lisilokuwa la kiserikali ni kuhakikisha wananchi wanajiunga na mfuko wa jamii
na kupata huduma ipasavyo.
 
Alisema moja ya majukumu yao ilikuwa ni kuwahamasisha Bioland kununua gari la wagonjwa kutokana na umuhimu kwa Wananchi wa Kyela ili waweze kupata huduma za mfuko wa bima kiufasaha.
 
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina, alisema Kazi ya Bioland na HIMSO ilikuwa ni kutoa gari hivyo Halmashauri ihakikishe gari linatumika katika shughuli iliyokusudiwa.
 
Alisema ili hayo yakamilike ni bora gari hilo likawa linashindwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kyela ili kuepuka matumizi tofauti ya gari kama ilivyowahi kutokea kwa magari mengine.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kyela ikishukuru kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Kyela, alisema Kampuni hiyo imemaliza kilio cha Wananchi wa Kyela cha kutaka gari la wagonjwa kilichokuwepo muda mrefu.
 
Alisema kupitia hamasa walioonesha Bioland Wilaya yake itaanza kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ili kuhakikisha kila mwananchi anatumia kadi kwenye matibabu.
 
Aidha alitoa wito kwa watumishi wa vituo vya Afya na Mahospitali kutoa kipaumbele kwa wagonjwa wenye kadi
kuliko wenye fedha mkononi ili wapate tiba kama serikali ilivyoagiza.

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA SHULE YA SEKONDARI NGONGO HUKO LINDI

1aMke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete akiangalia kinu cha kusindika unga wa mhogo kinachomilikiwa na Tawi la Mkumbara katika Kata ya Jamhuri tarehe 27.8.2014.
a3Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ngongo iliyoko Lindi Mjini tarehe 27.8.2014.
a4Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha  na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ngongo iliyoko Lindi Mjini tarehe 27.8.2014.
a5Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia watoto baada ya kulitembelea Tawi la Mtanda lililoko katika Kata ya Jamhuri huko Lindi Mjini mara baada ya kufanya kikao cha ndani katika Tawi hilo tarehe 27.8.2014.
a7Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia akina mama na watoto wao baada ya kulitembelea Tawi la Mtanda lililoko katika Kata ya Jamhuri huko Lindi Mjini mara baada ya kufanya kikao cha ndani katika Tawi hilo tarehe 27.8.2014.