Pages

KAPIPI TV

Thursday, August 28, 2014

ZAIDI YA WANAWAKE 600 KUNUFAISHWA NA ELIMU YA UJASILIAMALI MKOANI MWANZAZAIDI YA WANAWAKE 600 KUNUFAISHWA NA ELIMU YA UJASILIAMALI MKOANI MWANZA

Afisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile pamoja
na Meneja wa Kanda ya ziwa wa PPF Bwana Meshach Bandawe wakifuatilia mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika ukumbi wa Gold Crest kuwahabarisha kuhusu kampeni ya Mwanamke ya Uchumi itakayofanyika jijini Mwanza tarehe
4-5 Septemba, 2014 katika viwanja vya Mwaloni Kirumba Jijini Mwanza.
(Na Mpiga Picha Wetu)
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Naima Malima akizungumza
na na waandishi wa habari kuhusu Kampeni ya Mwanamke na Akiba inayotarajiwa
kufanyika Mkoani Mwanza kuanzia Septemba 4-5, ambapo zaidi ya wanawake wajasiriamali 600 wanatarajiwa kufaidika na mafunzo hayo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Angels Moment, Naima Malima akizungumzana na waandishi wa habari kuhusu Kampeni ya Mwanamke na Akiba inayotarajiwakufanyika Mkoani Mwanza kuanzia Septemba 4-5, ambapo zaidi ya wanawake wajasiriamali600 wanatarajiwa kufaidika na mafunzo hayo. 
Afisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile akielezea jukumu la TBS katika kuwaelimisha wanawake wajasiriamali wa Kitanzania watakaoshiriki katika kampeni ya Mwanamke na Uchumi juu ya ubora na viwango katika bidhaa wanazoandaa.
Afisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile akielezea jukumu la TBS katika kuwaelimisha wanawake wajasiriamali wa Kitanzania watakaoshiriki katika kampeni ya Mwanamke na Uchumi juu ya ubora na viwango katika bidhaa wanazoandaa.

RAIS KIKWETE AZINDUA PROGRAMU YA UIMARISHAJI WA MIPAKA YA KIMATAIFA MKOANI KAGERA

n6 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipata maelezo na kuangalia vifaa vya upimaji  eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka 
n1Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakiangalia moja ya alama katika eneo la mpaka kati ya Tanzania na Burundi la Mugikomero wilayani Ngara mkoani Kagera kwa upande wa Tanzania na eneo la Nteritare  kwa upande wa Burundi wakati wa sherehe za  uzinduzi wa programu ya uimarishaji wa mipaka ya kimataifa Jumatano Agosti 27, 2014. Kushoto kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka n3

JUKWAA LA KATIBA TANZANIA LATOA TATHIMINI YA WIKI MBILI YA MWENENDO WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA KUANZIA TAREHE 11-23 AGOSTI2014

 Jengo la Makao Makuu ya Ofisi za Jukwaa la Katiba.
 Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Hebron Mwakagenda.
  Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Hebron Mwakagenda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akitoa tathimini hiyo. Kulia ni Mratibu wa Jukata, Diana Kidara na Mwakilishi wa Taasisi ya TANLAP, George Mollel.
   Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Hebron Mwakagenda (kulia), akionesha Katiba ya Tanzania wakati akizungumza na wanahabari. Kushoto ni Mwakilishi kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Rodirick Maro na Mwakilishi wa Taasisi ya TANLAP, George Mollel
 Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata),
Hebron Mwakagenda (kulia), akisisitiza jambo wakati
akizungumza na wanahabari. Kushoto ni Mwakilishi kutoka Kituo cha  Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Rodirick Maro na
Mwakilishi wa Taasisi ya TANLAP, George Mollel
 Mwakilishi kutoka Taasisi ya NKM, Hezron Kaaya (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com. simu namba 0712-727062)
  Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata),
Hebron Mwakagenda (wa tatu kushoto), akiwa na viongozi wenzake. Kulia ni Mwakilishi kutoka UVIATA, 
Martha Mwanyeza.
 Mratibu wa Jukata Diana Kidara (wa tatu kulia), akiwa na viongozi wenzake. Kulia ni Mwakilishi kutoka Shirika la Shinyawata, Maria Chale.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 
Dotto Mwaibale
JUKWAA la Katiba Tanzania (Jukata), limemtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Samuel Sitta kufuata sheria na kaanuni za bunge hilo. 
 
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Kaimu Mwenyekiti wa Jukata,  Hebron Mwakagenda alisema kuwa kwa sasa Sitta hana mamlaka ya kukusanya maoni kwani ni kinyume na sheria ya tume ya mabadiliko katiba.
“Tumeshuhudia bunge maalumu la katiba likiongozwa na mheshimiwa Sitta likiendelea kupokea maoni ya makundi mbalimbali wakiwemo wafugaji, waandishi wa habari na wasanii ambapo ni kinyume na sheria,” alisema.

Mwakagenda alifafanua kuwa hatua hiyo imekwenda kinyume cha sheria namba 9 (1) ambacho kinaeleza kazi za tume ya mabadiliko ya katiba ambayo ilikuwa na kazi ya kukusanya, kuchambua, kuandika taarifa na kuwasilisha kwenye bunge ambapo kazi yake ni kuipitisha kama ilivyo kwenye kifungu cha sheria namba 25.

Katika suala la uondoaji wa vifungu kwenye rasimu hiyo alisema rasimu imezingatia kero na malalamiko ya wananchi hivyo kuyaondoa ukilinganisha na mantiki inayoendelea bungeni ni sawa na kurekebisha katiba ya mwaka 1977 na kubaki na malalamiko kwa wananchi kuwa viongozi hawawajibiki.

Pia aliyataka makundi yanayopingana kwenda kwenyekikao kinachotarajiwa kufanyika Ikulu wiki hii kwa moyo mkunjufu na kwa kuzingatia maslahi ya taifa na si vyama vyao.

Hata hivyo alisema kuwa pamoja na juhudi za kuendeleza mchakato wa katiba mpya lakini mchakato huo hautokamilika na kutumika katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Alifafanua kuwa hali hiyo imesababishwa na mwingiliano wa shughuli mbalimbali za kiserikali zikiwemo za uandikishaji mpya wa vitambulisho vya kupigakura katika mfumo mpya wa BVR.

Pia alisema kuwa kupanda kwa joto la uchaguzi kwa sasa pia inaweza kusababisha katiba kutopatikana kwani takribani wanasiasa wote wamegeukia kwenye uchaguzi na si kupatikana kwa katiba.

“Sisi kama Jukata tunashauri mchakato huu kuhairishwa hadi baada ya uchaguzi mkuu na kuanza tena januari 2016 ili kuokoa gharama za uchaguzi kwa kuunganisha na kufanyika chaguzi zote kwa mara moja,” alisema Mwakagenda.

Wednesday, August 27, 2014

BURUNDI YAZURU TANZANIA KUJIFUNZA KUHUSU MADINI,NISHATI


burundi 2Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi Mhe. Côme Manirakiza (aliyeinua mkono), akiomba kupewa ufafanuzi kuhusu sekta ya madini hapa nchini, baada ya uwasilishwaji mada zilizohusu sekta za nishati na madini za Tanzania. Waziri Manirakiza na Ujumbe wake walitembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini – Dar es Salaam, Agosti 26, 2014 kwa lengo la kujifunza namna sekta husika zinavyofanya kazi. Wengine pichani ni Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini – Tanzania (kushoto) na Ujumbe ulioongozana na Waziri (Kulia).
burundi 4Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje akiwasilisha mada kuhusu Sekta ya Madini – Tanzania kwa Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza (wa kwanza kulia) na Ujumbe wake (Kulia kwake) waliofika Makao Makuu ya Wizara – Dar es Salaam, Agosti 26, 2014 kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi. Upande wa kushoto ni Wataalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.

Na Veronica Simba
Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Mhe. Côme Manirakiza na Ujumbe wake wako katika ziara ya siku tano (24 – 28 Agosti, 2014) hapa nchini kwa lengo la kujifunza namna Sekta za Nishati na Madini zinavyofanya kazi.

Katika ziara yake, Waziri Manirakiza ametembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini – Dar es Salaam na kukutana na Wataalamu mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake wakiongozwa na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.

Wakiwa Wizarani, Waziri na Ujumbe wake walipata fursa ya kusikiliza mada zinazohusu Sekta za Nishati na Madini zilizowasilishwa na Wataalamu wa Wizara.

Ujumbe huo pia umepata nafasi kutembelea Taasisi na Mashirika mbalimbali yaliyo chini ya Wizara na yale yenye uhusiano na Wizara ikiwemo Mpango wa Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Tanzania (Tanzania Extractive Industry Transparency Initiative – TEITI), Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasimali Madini (SMMRP) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).

MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA TABORA AJIUZULU RASMI,ADAI KATIBA INAKIUKWA NA VIONGOZI WA JUU.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoa wa Tabora Bw.Kansa Mbaruku na Mwenyekiti wa kamati ya Sheria na haki za binadamu kanda ya magharibi ambaye pia ni Mwanasheria mkongwe Bw.Mussa Kwikima wametangaza kujiuzulu rasmi leo hii mbele ya waandishi wa habari kufuatia madai ya kuendelea kukiukwa kwa maadili ya viongozi kuanzia ngazi ya juu ambao wamekuwa wakivunja katiba kwa maslahi yao binafsi.Kujivua madaraka kwa viongozi hao wawili huenda ikawa pigo kubwa kwa Chadema kanda ya Magharibi baada ya mmoja kati ya makada mahili wa chama hicho wilaya ya Igunga Bw.Anuar Kashaga kuondoka Chadema na kujiunga na Chama cha Mapinduzi katika siku za hivi karibuni.Hatua ya  kuachia ngazi kwa viongozi hao imedaiwa kuwa kuna siri nzito ya wimbi la ubaguzi wa kikabila,kikanda na hata kidini ambayo bado viongozi hao wamekuwa na kigugumizi kuweka hadharani.

SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI YA VYETI HALISI WAKATI WA UOMBAJI WA KAZI SEKRETARIETI YA AJIRA


Naibu Katibu Kitengo cha Udhibiti na Ubora toka Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.Humphrey Mniachi akiongea na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani)Jinsi wanavyoshirikiana na Vyombo vingine serikalini katika Mchakato wa Ajira,wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi Hiyo Bi. Riziki Abraham.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano toka Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mambo ya kuzingatia kabla ya kuomba kazi nchini kwa  waombaji waliopotelea na vyeti, kuibiwa vyeti au kubadilisha majina,wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Katibu Kitengo cha Udhibiti na Ubora toka Ofisi hiyo Bw.Humphrey Mniachi.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwasikiliza wawasilishaji toka  Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Hassan Silayo)
Na Georgina Misama
Serikali imewataka waombaji kazi waliobadilisha majina, waliosoma nje ya Nchi, kupoteza, kuibiwa, kuharibikiwa au kuunguliwa na vyeti kufuata taratibu pindi wanapoomba kazi secretariati ya ajira.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ofisi ya Rais, Sekretariat ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Riziki alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya malalamiko toka kwa waombaji wa kazi kuwa secretariati ya Ajira imekuwa na upedeleo kwa kutowaita au kuwazuia kufanya  usaili waombaji wasiokuwa na nyaraka halisi.
Riziki alifafanua kuwa pindi waombaji wanapokabiliwa na hali hiyo hawana budi kutoa tarifaa katika mamlaka husika ili taratibu za kupata vyeti vingine zifanyike na taarifa zao kutumwa Secretariati ya Ajira kwa wakati.
Akizitaja Mamlaka hizo Riziki alisema ni Polisi, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Tume ya Vikuu (TCU), na Baraza la Usimamizi wa Elimu ya Vyuo vya Ufundi (NACTE).
Aidha, Riziki aliongeza kuwa kwa waombaji wenye majina tofauti kwenye vyeti wanapaswa kwenda mahakamani na kula kiapo kwa kamishna wa viapo au kwa wakili ili waweze kupata (Deedpal) au (Affidavity) kwa mujibu wa sheria na kwakufanya hivyo itasaidia kuthibitisha uhalali wa tofauti ya majina na kutambulika kisheria.
Sekretarieti ya Ajira inapenda kuwafahamisha wadau wake, hususani waombaji kazi Serikalini kwamba haipokei barua ya utambulisho kutoka polisi inayohusu kupoteza, kuungua, kuibiwa, utofauti wa majina kati ya cheti kimoja na kingine kutokana na baadhi yao kuzitumia vibaya.
Posted By Blogger to THE GOVERNMENT OFFICIAL BLOG

CHINA YAIMWAGIA MISAADA JESHI LA POLISI, NAIBU WAZIRI SILIMA ATOA PONGEZI

PIX 1Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kushoto) akizungumza katika hafla fupi ya kupokea misaada ya Pikipiki, Kompyuta na Samani za ofisini ambazo zimetolewa na Serikali ya China. Naibu Waziri Silima aliishukuru China kwa misaada hiyo iliyotolewa kwa ajili ya kulisaidia Jeshi la Polisi. Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 2Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing akizungumza kabla ya kumkabidhi misaada ya Pikipiki, Kompyuta na Samani za ofisini kwa ajili ya kusaidia shughuli za utendaji za Jeshi la Polisi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia). Misaada hiyo imetolewa na Serikali ya China. Naibu Waziri Silima aliishukuru China kwa misaada hiyo iliyotolewa kwa ajili ya kulisaidia Jeshi la Polisi.
PIX 3Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing akizungumza kabla ya kumkabidhi misaada ya Pikipiki, Kompyuta na Samani za ofisini kwa ajili ya kusaidia shughuli za utendaji za Jeshi la Polisi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (kulia). Misaada hiyo imetolewa na Serikali ya China. Naibu Waziri Silima aliishukuru China kwa misaada hiyo iliyotolewa kwa ajili ya kulisaidia Jeshi la Polisi.
PIX 4Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akiiwasha moja ya pikipiki zilizotolewa na Serikali ya China kwa ajili ya kulisadia Jeshi la Polisi. Jumla ya pikipiki 50 zilitolewa na China ikiwa ni misaada yao ya mara kwa mara kwa ajili ya kulisadia jeshi hilo kwa lengo la kukabiliana na uhalifu nchini. Hata hivyo, Naibu Waziri Silima aliishukuru Serikali ya China kupitia Balozi wake nchini, Lu Youqing (wapili kushoto).
PIX 6Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (katikati-waliokaa), Balozi wa China nchini, Lu Youqing (wapili kulia), Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Abdulrahman Omar Juma Kaniki (wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Serikali

MAELFU YA WANANCHI WAMLAKI RAIS KIKWETE GAIRO, KATIKA ZIARA YAKE YA MKOA WA MOROGORO

ga10 Rais Kikwete akihutubia umati wa maelfu ya wananchi waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014
ga14Rais Kikwete akiagana na baadhi ya wananchi  waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014 ga11 Rais Kikwete akihutubia umati wa maelfu ya wananchi waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014 ga12Rais Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na wazee wa mji wa gairo waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014
ga13  Rais Kikwete akiagana na baadhi ya wananchi  waliojitokeza  kumsikiliza  kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014ga7 Sehemu ya maelfu ya wananchi waliofurika kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  kumsikiliza Rais Kikwete alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014 ga6 Mmoja wa wananchi waliofurika kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro akichukua kumbukumbu wakati wa  kumsikiliza Rais Kikwete alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014 ga5 Sehemu ya maelfu ya wananchi waliofurika kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  kumsikiliza Rais Kikwete alipowahutubia kwenye mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014 ga4Mbunge wa Gairo Mhe. Ahmed Mabhut Shabiby akimkaribisha Rais Kikwete kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014 ga3 ga1 Rais Jakaya Kikwete akilakiwa na maelfu ya wananchi alipowasili kwenye uwanja wa mkutano wa mji wa Gairo mkoani Morogoro  kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti 26, 2014

WATOTO 984 WAOZESHWA KWA NGUVU TARIME,1628 WAKEKETWA


Baadhi ya washiriki katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es Salaam.
Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akishangilia baada ya kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu za viganjani kwa simu zote zilizosajiliwa nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya uzinduzi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akishangilia baada ya kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu za viganjani kwa simu zote zilizosajiliwa nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya uzinduzi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Mjane wa Hayati Nelson Mandela na Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akimbusu mmoja ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara kuonesha ishara ya upendo katika uzinduzi huo.
Mjane wa Hayati Nelson Mandela na Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akimbusu mmoja ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara kuonesha ishara ya upendo katika uzinduzi huo.
Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akisalimiana na baadhi ya viongozi mbalimbali kutoka mkoani Mara.
Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akisalimiana na baadhi ya viongozi mbalimbali kutoka mkoani Mara.
Baadhi ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara wakizungumzia namna walivyonusurika kufanyiwa vitendo vya kikatili (kukeketwa). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka akiwasikiliza.
Baadhi ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara wakizungumzia namna walivyonusurika kufanyiwa vitendo vya kikatili (kukeketwa). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka akiwasikiliza.
Viongozi mbalimbali wastaafu wa Serikali, viongozi wa dini Mkoa wa Mara, wawakilishi wa wanafunzi Mkoa wa Mara wakiwa katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Viongozi mbalimbali wastaafu wa Serikali, viongozi wa dini Mkoa wa Mara, wawakilishi wa wanafunzi Mkoa wa Mara wakiwa katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Baadhi ya viongozi wa mashirika mbalimbali walioshiriki hafla ya uzinduzi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa mashirika mbalimbali walioshiriki hafla ya uzinduzi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es Salaam.
Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akizungumza kabla ya kuzindua rasmi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akizungumza kabla ya kuzindua rasmi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Baadhi ya wanafunzi wakiangalia ujumbe mfupi uliotumwa kwa simu zote zilizosajiliwa kwa njia ya simu za kiganjani na Mjane wa Hayati Nelson Mandela, Bi. Graca Michel kwa kushirikiana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Bi. Sophia Simba kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Baadhi ya wanafunzi wakiangalia ujumbe mfupi uliotumwa kwa simu zote zilizosajiliwa kwa njia ya simu za kiganjani na Mjane wa Hayati Nelson Mandela, Bi. Graca Michel kwa kushirikiana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Bi. Sophia Simba kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Baadhi ya wanafunzi wakitumbuiza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Baadhi ya wanafunzi wakitumbuiza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Moja ya kikundi cha maigizo kikionesha igizo namna mtoto wa kike anavyokabiliana na changamoto za unyanyasaji kutoka kwa jamii katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike
Moja ya kikundi cha maigizo kikionesha igizo namna mtoto wa kike anavyokabiliana na changamoto za unyanyasaji kutoka kwa jamii katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike

JUMLA ya wasichana wenye umri mdogo wapatao 984 wameolewa na kukatishwa masomo huku wasichana wengine 1,628 wakikeketwa wilayani Tarime, Mkoa wa Mara ikiwa ni miongoni mwa vitendo vya kikatili ambavyo amekuwa akifanyiwa mtoto wa kike baadhi ya maeneo nchini Tanzania.

Takwimu hizo za vitendo vya kikatili dhidi ya mtoto wa kike wilayani Tarime zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele kwa niaba ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.

Akizungumza kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo, Henjewele alisema takwimu hizo zavitendo vya kikatili Mkoani Mara ni za kuanzia mwaka 2013 hadi Juni 2014. Alisema baadhi ya familia eneo hilo wanamchukulia mtoto wa kike kama kitega uchumi hivyo wamekuwa wakiwaozesha mapema ili kupata mali (yaani ng’ombe) jambo ambalo bado uongozi wa mkoa huo kwa kushirikiana na wadau anuai wamekuwa wakipinga na kupambana na ukatili huo.

“…Matukio ya vitendo vya unyanyasaji kwa mtoto wa kike kwa mwaka 2013 hadi Juni 2014 ni kama ifuatavyo; watoto wa kike wapatao 984 waliozeshwa, wasichana 1,628 walikeketwa, jumla ya wanafunzi wa kike 4,134 walipewa mimba na kukatishwa masomo yao huku wasichana 1,912 wakifanyiwa ukatili wa vipigo kwenye familia ama kwenye ndoa na jumla ya watoto 11 walibakwa…,” alisema Henjewele.

Aidha alisema vitendo hivyo vya kikatili kwa mtoto wa kike vinachangiwa na baadhi ya jamii mkoani humo kuendeleza mila na desturi zilizopitwa na wakati, migogoro ya koo, mwamko duni wa elimu kwa jamii na usiri mkubwa wa kutokubali mabadiliko dhidi ya vitendo vya kikatili kwa jamii hiyo. Akizungumzia jitihada zinazofanywa na viongozi wilayani hapo kukabiliana na vitendo hivyo, alisema wamekuwa wakiendesha semina na vikao mbalimbali na wazee wa kimila, mangariba na jamii kwa ujumla kwa lengo la kutokomeza vitendo vya Ukatili wa kijinsia, ukeketaji pamoja na mila na desturi zilizopitwa na wakati.

Kwa Upande wake mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel akizungumza kabla ya kuzindua rasmi kapeni hizo alisema viongozi kwa kushirikiana na wanajamii mkoani Mara wakiamua kwa dhati wanaweza kukabiliana na ndoa za utotoni na vitendo vingine vya kikatili eneo hilo.

Akizungumzia kwa ujumla alisema jamii nyingi ya kiafrika bado zinamthamini mtoto wa kiume zaidi ya yule wa kike ilhali watoto wote wanapaswa kuwa na haki sawa. Aliwataka wazazi wenye mawazo kama hayo kubadilika na kutoa haki sawa kwa watoto bila ubaguzi. Alishauri suala la uamuzi dhidi ya maisha ya mtoto lifanywe kwa ushirikiano kwa familia nzima pamoja na kushirikishwa mtoto.

“…Lazima tukubali kubadilika, umefika wakati suala la uamuzi wa wakati gani wa kuolewa kwa mtoto wa kike ufanywe kwa ushirikiano kati ya wazazi wote pamoja na mtoto mwenyewe tena kwa wakati muafaka…lazima turejeshe maamuzi pia kwa mtoto mwenyewe si kutumia nguvu kwa kila kitu,” alisema Bi. Michel.

Aliongeza hata hivyo ipo haja ya kuwa na asasi za ushauri ngazi ya familia ambazo zitakuwa zikitoa ushauri juu ya masuala ya familia kwa kuzingatia sheria na taratibu zinazotambulika. Alisisitiza katika kampeni za sasa juhudi na elimu ya kutosha itolewe kwa jamii mkoani Mara ili baadaye ifanyike tathmini kwa eneo hilo jambo ambalo linaweza kusaidia mapambano maeneo mengine hapo baadaye.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka akifafanua juu ya shughuli za kampeni hizo alibainisha kuwa zitaambatana na utoaji elimu kwa makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, watendaji wa vyombo vinavyosimamia sheria, viongozi wa jamii na jamii kwa ujumla juu ya mapambano ya kampeni hizo. Kampeni hizo baadaye zitaendelea katika maeneo mengine ya Tanzania.

Programu ya kampeni hiyo imefanikishwa kwa kushirikiana na Serikali, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Shirika lisilo la Kiserikali la Children’s Dignity Forum (CDF), Graca Machel Trust (GMT), asasi za mkoani Mara na uongozi wa mkoa. *Imeandaliwa na www.thehabari.com