Friday, July 18, 2014
SEMINA ELEKEZI AIRTEL RISING STARS KUFANYIKA DAR
Semina
elekezi ya michuano ya Airtel Rising Stars kwa mikoa sita inafanyika
kesho (Julai 19 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Washiriki wa semina hiyo ni
kutoka mikoa ya Mbeya (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Mwanza (Katibu
na mwakilishi wa wanawake), Morogoro (Katibu), Ilala (Katibu na
mwakilishi wa wanawake).
Temeke (Katibu na mwakilishi wa
wanawake), Kinondoni (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Dar es Salaam
(Mwenyekiti na Katibu), na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA)
kitakachowakilishwa na mwakilishi wa wanawake.
Washiriki wengine katika semina
hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine
ni wajumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana ya TFF.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA KUFANYA MAMBO JIMBO LA CHALINZE, SAFARI HII NI ZAMU YA JESHI LA POLISI
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akizungumza na uongozi wa polisi Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kipolisi ya Chalinze pamoja na wananchi waliojitokeza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali kwa jeshi hilo zikiwemo kompyuta, mifuko ya Saruji pamoja na fedha vilivyotolewa na mbunge huyo, Kwa ajili ya kutatua matatizo mbalimbali yanayolikabili jeshi la polisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya ulizni na usalama wa raia na mali zao. Pamoja na kukabidhi kompyuta hizo zitakazosaidia katika utunzaji wa kumbukumbu pia mbunge huyo ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi vya Mbwewe na Kiwangwa ambavyo thamani inafikia zaidi ya shilingi milioni 11, Kushoto kwake ni Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei, hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jana kwenye kituo kikuu cha polisi Chalinze.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-CHALINZE)
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete kompyuta Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Kamanda ACP Ulrich Onesphory Matei zilizokabidhiwa na mbunge huyo kwa ajili ya kuboresha shughuli za jeshi hilo jimbo la Chalinze katikati ni Mkuu wa kituo cha polisi Chalinze Afande J. S. Magomi.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kufungua ili kuonyesha kompyuta hizo huku viongozi wa jeshi hilo mkoani Pwani na jimbo la Chalinze wakishiriki shghuli hiyo.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimuonyesha moja ya kompyuta Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei wakati alipokuwa akitoa shukurani zake kwa niaba ya jeshi la polisi mkoani Pwani mara baada ya kukabidhiwa kompyuta hizo , katikati ni mkuu wa ituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimsikiliza Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Chalinze Mzee Bw. Kamis Kameza wakati alipokuwa akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa shule hiyo ambayo inajengwa na jeshi la kujenga taifa JKT kambi ya Ruvu.
Baadhi ya wanajeshi wa kambi ya JKT Ruvu wanaoshiriki katika ujenzi wa shule hiyo.
Moja ya madarasa ya shule hiyo ambayo yako katika hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wake.
Baadhi ya madarasa na maktaba ya shule hiyo yakiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi wake.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Chalinze Mzee wakati alipokagua ujenzi wa shule hiyo.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akiendelea kufanya ukaguzi wa ujenzi shuleni hapo kushoto ni Diwania wa kata ya Bwilingu Chalinze Bw. Ahmed Nasser.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikweteakikagua ujenzi wa Maktaba ya shule hiyo akiwa ameongozana na Diwani wa kata ya Bwilingu Ahmed Nasser mbele na Mwalimu mkuu wa shule hiyo Khamis Kameza.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria wakati wa hafla kukabidhi kompyuta kituo cha polisi Chalinze.
Diwani wa kata ya Bwilingu Chalinze Bw. Ahmed Nasser akizungumza wakati mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete alipolokabidhi jeshi la polisi kompyuta kwa ajili ya kuboresha shughuli za jeshi hilo.
WANANCHI WATAKA STAMICO IPEWE NGUVU KUSIMAMIA SEKTA YA MADINI NCHINI.
• Waunga mkono kauli ya Waziri wa Nishati na Madini
• Wataka wenye uwezo kuacha ubinafsi na ubepari
• Wataka raslimali za madini ziwanufaishe Watanzania wote
• Wataka wenye uwezo kuacha ubinafsi na ubepari
• Wataka raslimali za madini ziwanufaishe Watanzania wote
Na. Issa Mtuwa – STAMICO
Wananchi wameiomba serikali kuhakikisha rasilimali za Madini zinawanufahisha Watanzania wote na sio wachache wenye uwezo. Kauli ambayo imewahi kutolewa siku za hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati walipotembelea katika banda la Shirika la Madini la Taifa STAMICO katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (SABASABA) 2014, wananchi hao wamesema ili azma hiyo iweze kutimia ni vyema Serikali ikaijenga uwezo STAMICO kifedha na vitendea kazi ili iweze kutekeleza miradi ya uchorongaji na uchimbaji madini itakayowanufaisha wananchi.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake alioambatana nao katika banda la STAMICO, Mkazi wa mkoa wa Mara, Bw. Joel M.
Changarawe amesema katika kujenga uwezo wa kifedha wa Shirika hilo, Serikali haina budi kuendeleza azma yake ya kuikabidhi STAMICO migodi yote mikubwa ya Madini iweze kumiliki kwa niaba ya Watanzania na kuzalisha ili kuongeza tija kwa Taifa.
Jacqueline Aisaa akitoa maoni yake kuhusu sekta ya Madini wakati wa maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba 2014. Anae msikiliza ni Bw. Issa Mtuwa Afisa Uhusiano wa STAMICO.
“Nashauri Watanzania tuache ubinafsi na ubepari. Naishauri serikali Migodi yote ya Madini yenye RESERVE (akiba) kubwa imilikiwe na STAMICO kwa niaba ya Watanzania badala ya kukabidhi kwa Watanzania wachache wenye tamaa ya utajiri ambao wanamiliki vitalu vya madini kupitia migongo ya kampuni za kigeni” alisema Bwana Joel kwa kuandika kwenye kitabu maalum cha Maoni, ushauri na kero za Wananchi.
Naye Jacqueline Aisaa mkazi wa Masama-Moshi, ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Shahada ya kwanza katika Chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) alisema serikali iipe meno STAMICO ya usimamizi wa hisa zote za serikali kwenye migodi yote na usimamizi wa jumla katika sekta ya Madini ili Wananchi waweze kunufaika na raslimali hizo.
CHADEMA KIGOMA YAENDELEA KUPASUKA,VIGOGO WAHAMIA ACT
Aliyekuwa
Mwenyekiti na Katibu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mkoani
hapa,wamen`gatuka rasmi jana na kuhamia chama cha Alliance Conservative For
Transiparecy(ACT),kwa lengo la kukuza demokrasia ya chama hicho.
Hayo
yamebainika kigoma ujiji katika ofisi ya
chama cha wandishi wa habari mkoani humu(KGPC) ,ambapo viongozi hao walifika katika ofisi hiyo kwa dhima ya
kutangazia umma kuwa wao si wafuasi wa chama cha chadema.
Miongoni mwa
waliokuwa viongozi wa mkoa ni pamoja na
Mwenyekiti Jaffar Kasisiko,Katibu Msafiri Wamalwa sanjari na katibu wa baraza la
wanawake chadema Malunga Simba sambamba
na wanachama wawili waliokuwa chama hicho.
Jaffar
Kasisiko alisema kukihama chama hicho
hakina uhusiano na Mbunge wa jimbo la kigoma kaskazini Zitto Kabwe bali ni
kutokana na urasimu,ubinafsi na utashi wa viongozi wa chama hicho hasa
mwenyekiti wa chama husika.
“sijutii
kuachia ngazi ,najua watahisi namfuata Zitto,ukweli aliyenivuta kisiasa ni
Mwenyekiti wa ccm mkoa Dr.Kabourou enzi hiyo chadema ni taifa kubwa haswa ,sitaki
cheo napenda niwe mshauri wa chama hicho lengo kubadilisha fikra mpya” alibainisha
Kasisiko .
Ashauri
vyama vya siasa viepuke migogoro
isiyo na maslai ya umma na chama ,hali inayochangia kushindwa kushika hatamu katika chaguzi za kitaifa na kutaka viwajibishe
wanachama kwa katiba husika na si utashi.
Kwa
upande
wa Msafiri Wamalwa na Malunga Simba kwa nyakati tofauti walisema chama
hicho sawa na timu ya Brazili , hakina tija na umma bali kipo kwa masali
ya wachache.
Aidha Aprili,4,2014 Mlezi wa chadema mkoa Aidan Ndowa amekiri chama kipo katika wakati mgumu ambapo kati ya viongozi 209 walipo kigoma , viongozi 99 kutimkia chama cha ACT.
Ndowa
alisema hao waliojiengua leo(jana) ni
miongoni mwa hao 99 waliowabaini kwenye tathimini yao ya uhalisia wa
uhai wa chama,wakati huohuo chama cha ACT kimechukua kata 8 kati ya 11
zilizokuwa za chadema kati ya kata 19 zilizopo manispaa ya kigoma ujiji.
Juma
Ramadhan mratibu wa chama cha ACT anakiri chama hicho kina mvuto kwa
umma husika ambapo kwa sasa wana wananchama 7,000 na kudai
hitaji la kadi ni 10,000 kwa wakazi wa manispaa ya hiyo.
Thursday, July 17, 2014
ZIARA YA RAIS KUFUNGUA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU MKUZO, SONGEA
Rais
Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Saidi Mwambungu kulia ,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka (kushoto)
na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. David Shambwe wakikata
utepe kwa pamoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.
Rais
Dr. Jakaya Kikwete akipata taarifa ya mradi huo wa nyumba za gharama
nafuu kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw David
Shambwe
Rais Dr. Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo
Rais
Dr. Jakaya Kikwete akiwasili katika eneo la mradi wa nyumba za gharama
nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba (NHC) na kupokelewa na Ndg.
David Shambwe Kaimu Mkurungenzi Mkuu NHC na Mkurugenzi wa Uendelezaji
Biashara wakati alipokagua mradi huo uliopo katika wilaya ya Songea
mkoani Ruvuma akiwa katika ziara yake ya kikazi leo, Rais Dr. Jakaya
Kikwete anaendelea na ziara mkoani humo leo. (PICHA ZOTE KWA HISANI YA
KITENGO CHA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA JAMII CHA NHC)
Rais
jakaya Kikwete akipata maelezo ya kuhusu Mashine za kufyatulia matofali
ambazo zimegawiwa kwa kila wilaya za mkoa wa Ruvuma
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akizungumza katika hafla hiyo mchana huu
Akiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia
Vikundi vya nguma na burudani ikiburudisha katika tukio hilo mchana wa leo
"MBUNGE ADAIWA KUMPIGA BABA YAKE MZAZI"-KASULU
MBUNGE wa Jimbo la Kasulu mjini
Moses Machali anatuhumiwa kumtwanga baba yake mzazi Mzee Machali sambamba na kumfukuza nyumbani kwake,kutokana
na kitendo chake cha kulewa kupindukia ambayo imekuwa adha kwa mbunge huyo na
kupelekea mgogoro mkubwa baina yake na mzazi huyo .
Mbunge huyo
amefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na ulevi huo na kupelekea kumpa kichapo
kilichosababisha kuteguka kwa mkono sanjari na kumtupia nguo zake nje na
hatimaye mzee huyo kukimbilia kwa Balozi wa nyumba kumi Dickson Joaqim kwa msaada wa kisheria.
Awali
Julai ,15, 2014 usiku mzee alichelewa kurudi nyumbani na alipomgongea
mwanae afungue mlango ndipo akapata kichapo kutoka kwa mbunge huyo baada
ya kuona adha hiyo ni sugu kwa mzee wake.
Mwandishi wa KAPIPIJhabari.COM mkoani Kigoma amemuhoji mbunge huyo ambapo alisema mzazi wake anapenda kunywa pombe
kupindukia hali inayomfanya kila wakati wagombane juu ya tabia hiyo ambapo kwa
upande wa pili kisiasa inamuathiri katika uwajibikaji wake kwa wananchi.
Alisema baba yake anatumiwa na
chama cha ccm kwa lengo la kumdhoofisha kisiasa hasa katika
kipindi hiki cha majeruhi cha kuelekea uchaguzi mkuu mwakani na kumtaja balozi
wa mtaa wa mwilavya Dickson Joaqim ni
miongoni mwa watu wanaomshawishi mzee wake
kituo cha polisi kumshtaki.
“sijafikia hatua ya kumpiga mzee
wangu,najitambua ndio maana namsihi baba achane na pombe ambapo mimi najiskia
vibaya kuona analewa sasa tukiwekana
sawa baadhi ya watu wanadai nampangia sheria na ndo hivyo wanazusha ya kuzusha”
alibainisha Machali.
Alisema kwa kuthibitisha hilo umma kuwa hajampiga mzee wake na kwenye mkutano wa hadhara wilayani hapo, atakuwa
sambamba na mzee huyo na kukiri mzee wake amefuta kesi dhidi yake na kusisitiza
ccm watumie mbinu za ziada na kudai hawana
jipya.
Shuhuda
mmoja jina kapuni akiri kumuona mzee huyo akiwa na `PF3' akitembea kwa
shida huku mkono wake ukiwa umevimba akipatiwa matibabu katika moja ya
zahanati ya wilayani hapo
Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Frasser Kashai
alisema ni kweli mzee wake alifungua jalada la kumshataki mbunge huyo,pamoja na kupatiwa maelezo ya watu walioshuhudia tukio hilo ingawa Mbunge huyo nae alipatikana na kutoa maelezo.
Hata hivyo Kamanda Kashai alisema wakati Jeshi la Polisi likiandaa taratibu za kuwapeleka mahakamani,mlalamikaji Mzee Machali aliomba waende nyumbani wakafanye suluhu kifamilia hatua ambayo haikupingwa na Polisi.
"Baada ya Mzee wake kuamua hivyo sisi kama Jeshi la Polisi tuliona hatuna namna ya kufanya kwakuwa hatuwezi kumlazimisha mlalamikaji kwenda mahakamani wakati mwenyewe hataki na pia tuliangalia ukubwa wa tatizo,tukaona kuwa wamefanya uamuzi mzuri kuyamaliza kifamilia"alisema Kamanda Kashai.
TAARIFA RASMI KWA WAANDISHI WA HABARI KUTOKA CCM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Jana tarehe 16/07/2014 Kamati Kuu
ya Halmashauri Kuu ya CCM ilifanya kikao cha kawaida cha siku moja
mjini Dar es salaam. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete.
Pamoja na mambo mengine kikao
hicho kilipokea taarifa ya mazungumzo yanayoendelea kati ya CCM kwa
upande mmoja na CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi kwa upande wa pili.
Mazungumzo hayo yanayosimamiwa na
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi yana lengo la
kuangalia kwa kina ni kwa nini baadhi ya wajumbe wachache wa Bunge
Maalum la Katiba walisusia na kutoka nje katika awamu ya kwanza ya Bunge
hilo, na kuangalia namna watakavyorudi ili kukamilisha mchakato wa
mabadiliko ya Katiba nchini.
Kwa ujumla Kamati Kuu ya CCM
imeridhishwa na mwenendo wa mazungumzo hayo na kupongeza juhudi hizo
zilizofanywa na Msajili wa Vyama vya Siasa na Vyama husika. Kamati Kuu
inapenda kueleza imani yake kuwa mazungumzo hayo yatazaa matunda kwa
wajumbe wachache waliosusia Bunge Maalum la Katiba, kurejea Bungeni na
kumalizia sehemu ya mchakato uliobakia.
Kamati Kuu inayatakia kila la
kheri mazungumzo hayo.
Kamati Kuu pia ilipokea taarifa
za harakati za baadhi ya wanachama wa CCM walioonesha nia ya kuomba
ridhaa ya CCM kugombea Urais. Baada ya kutafakari kwa kina, Kamati Kuu
inapenda kuwakumbusha wote kuwa ili wasipoteze sifa za kugombea, ni
muhimu wakazingatia Katiba, Kanuni na taratibu za Chama zinazosimamia
masuala hayo.
Kuhusu wale waliopewa adhabu na
Kamati Kuu kutokana na kukiuka baadhi ya taratibu za Chama kwa suala
hili, Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama itafanya mapitio ya mwenendo
wao wa utekelezaji wa adhabu hiyo mwezi wa nane (Agosti 2014), na kama
itabainika kuwa hawatekelezi ipasavyo masharti ya adhabu zao,
itapendekeza kwa Kamati Kuu kuongezwa kwa adhabu kulingana na ukubwa wa
uvunjaji wa masharti ya adhabu husika.
Ni muhimu wanachama wote
wakakumbuka kuwa Chama ni pamoja na Katiba, Kanuni na taratibu zake,
hivyo kutoziheshimu na kuzifuata ni kukivuruga, jambo ambalo
halivumiliki.
Nia ya CCM kusimamia haya ni
kuhakikisha Chama kinakuwa na umoja na mshikamano ambao ni muhimu sana,
hasa tunapoelekea kukamilisha kazi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi
ya CCM ya 2010/2015 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
Aidha, Kamati Kuu imewatakia kheri na fanaka Watanzania wote wakati huu wanapomalizia mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Imetolewa na:-
Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
17/07/2014
MTOTO WA MIAKA MINANE ADAIWA KULAWITIWA NA MWENDESHA BODABODA,MZAZI ALALAMIKIA POLISI KUMPA DHAMANA MTUHUMIWA
WANANCHI WAKOMAA NA MANISPAA-KIGOMA UJIJI
TATIZO la mgogoro wa ardhi baina ya wananchi na mwekezaji katika eneo la kituo cha Afya cha Kakunku kata
ya Gungu Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani hapo,limebaki kuwa sintofahamu
kutokana na serikali kushindwa kuthibiti mgogoro huo.
Mgogoro huu wa kugombea ardhi baina yao na mwekezaji wa taasisi
ya kuhudumia makanisa mkoani Kigoma (JOY IN THE HARVEST) lipo kwa miongo
saba,ambapo imepelekea wananchi kuwa na
mashaka ya kuporwa eneo hilo ambalo kwa sasa kuna ujenzi wa uzio ili
kudhibiti vibaka wanaopora mali za watumishi na wagonjwa katika kituo hicho.
Pamoja na wananchi kutetea eneo hilo ,ambalo ni chachu ya kupunguza
vifo vya uzazi na umbali kwa kina mama
kufuata huduma hiyo katika hospitali ya mkoa maweni, ambapo kituo hicho kinatoa
huduma ya matibabu kwa zaidi ya kata tano.
Tukio la mwekezaji kutumia vyombo vya dola na kubomoa uzio wa
kituo hicho cha afya kimewapa wakati mgumu wananchi na kuomba manispaa kutatua
tatizo hilo ili wapate haki ya kutibiwa katika kituo hicho kilichokaribu na
wakazi wa kata hizo, ambapo Julai ,11,2014
mwenyekiti wa mtaa wa Kikunku na wajumbe wawili watupwa mahabusu kutokana na
mgogoro huo.
Bakari Genda,Ladslausi Mugabo,Hamis Paya,Crispian Daniel na
Chaila Richard ni kamati ya wafuatiliaji
wa sakata hilo watakiwa kumlipa fidia ya usumbufu kwa mwekezaji huyo kiasi cha sh.milioni 600 na kutoa maelezo
zaidi ya mara tano kituo cha polisi kati
mkoani hapo.
“Manispaa yenyewe inajichanganya awali walijenga kituo cha
wagonjwa wa kipindupindu katika eneo hilo pia wameweka eneo la mapumziko ya
wagonjwa katika eneo hilo na wanatarajia kufanya ujenzi wa wodi ya upasuaji kwa
kina mama,pia wameleta mkandarasi kwa ajili ya uzio na wakamuonyesha mipaka cha
ajabu baada ya ujenzi asubuhi tunakuta pamebomolewa yani hatuelewi kunanini
kati ya manispaa na mwekezaji huyo” walieleza wahanga hao.
Wakizungumzia hilo Hadija Issa,Christina Bugabo,Mnyonge Juma
na Sophia Issa washangaa serikali kuuza eneo ndani ya kituo cha afya na kukiri
uwepo wa kituo ni tija kwao kiafya na kiuchumi,awali walitozwa sh.20,000 za
usafiri kutoka eneo la gungu hadi katika hospitali ya rufaa ya Maweni kwa ajili
ya kujifungua .
Akifafanua hilo Mwenyekiti wa mtaa Manga Said ambaye pia ni
mwenyekiti wa bodi ya afya wa zahanati hiyo, akiri kuwepo kwa mgogoro huo
ambapo imeonekana kuwepo kwa utata baina ya wananchi na manispaa kutokuwa
wawazi katika mgogoro huo.
“wandishi semeni
uhalisia wa tukio ,kwa nini wakumbatie hili kwa miongo kadhaa,mwekezaji
aliuziwa pasipo jamii kujua, ije izungumze na raia wake aseme kweli
na si kupatiwa vitisho bali tukae chini na kutatua tatizo lililopo “
alisema Saidi.
Mujibu wa wakazi hao
na viongozi wanadai agizo la waziri wa tamisemi Hawa Ghasia limepuuzwa la
kuhakikisha mgogoro huo unatatuliwa ikiwa ni pamoja na kuweka uzio katika kituo
hicho cha afya.
Kwa upande wa mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ramadhani Maneno na
katibu wa chama cha NRA taifa Hamisi Kiswaga alitoa wito kwa manispaa kutatua mgogoro huo
kwa kuzungumza na mwekezaji huyo ikiwa ni pamoja na kumlipa fidia au kupatia
eneo mbadala ili eneo hilo libaki kuwa kituo cha afya kwa faida ya wananchi wa
eneo hilo.
Aidha mwekezaji wa eneo hilo, ameeleza kuwa eneo hilo
analimiliki kihalali kwa kwa mujibu wa sheria za manispaa kwa muda mrefu ambapo
hatua za ulipiaji wa eneo hilo risiti zipo na inatambuliwa kuwa eneo hilo lipo
chini ya taasisi hiyo ya kidini.
Hata hivyo afisa mipango miji manispaa ya Kigoma ujiji
alisema eneo hilo halina mgogoro, eneo la mwekezaji lipo na linajieleza pamoja
na eneo la zahanati tatizo lililopo ni manispaa kuweka ujenzi wa eneo la
kupumzikia katika eneo la mwekezaji huyo jambo ambalo litafanyiwa marekebisho.
WAZIRI MAKALLA ATOLEWA CHINI YA ULINZI WA POLISI BAADA YA MKUTANO WAKE KUFANYIWA VURUGU NA CHADEMA
Naibu Waziri wa Maji, Amos
Makalla (katikati), akiongozwa polisi kuingia kwenye gari baada ya
kutokea vurugu meza kuu, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya
Goba, Kinondoni Dar es Salaam, ambazo alidai zilipangwa kwa makusudi na
viongozi wa Chadema kwa lengo la kumvulugia ziara yake ya kuwaelezea
wananchi utekelezaji wa Ilani ya CCM katika suala la upatikanaji wa maji
ya uhakika jijini Dar es Salaam ifikapo Septemba, mwakani. PICHA ZOTE
NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Gari lililombeba Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, likilindwa na
polisi lililopokuwa linaondoka baada mkutano wa hadhara kuvunjika
kulikosababishwa na vurugu ambazo waziri alidai kuwa zilipangwa kwa
makusudi na wafuasi pamoja na viongozi wa Chadema waliokuwa wakirumbana
na viongozi wa CCM, katika Kata ya Goba, Kinondoni, Dar es Salaam.
Makalla alikuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji katika mikoa ya
Dar es Salaam na Pwani.
Makalla akijadiliana na maofisa wa CCM na Polisi kabla ya kwenda kupanda gari na kuondoka.
Poilisi wakiwadhibiti baadhi ya
wafuasi wa Chadema waliokuwa wakisababisha vurugu katika mkutano wa
hadhara uliofanyika Kata ya Makongo. Kinondoni.
Polisi wakimdhibiti mmoja wa
viongozi wa Chadema wakati wa mzozo uliotokea jukwaa kuu katika mkutano
wa Naibu Waziri wa Maji, Makalla na wananchi wa Kata ya Goba.
Kiongozi wa cHADEMA AKIZOZANA NA WA ccm jukwaani katika mkutano wa Makongo Juu.
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee akizoza jukwaani katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Goba na hatimaye kuvunjika
Polisi wakimdhibiti mfuasi wa Chadema asiendelee kufanya fujo katika mkutano wa Waziri na Wananchi wa Kata ya Goba
Askari wa FFU, akilinda doria
wakati waziri Makalla akikagua nyumba ambazo watu wamejiunganishia
isivyo halali eneo la Bonde la Msimbazi, Dar es Salaam.
Makalla na Mbunge wa Ubungo, John
Mnyika (kushoto) wakiangalia pampu zinazotumika kujazia maji kwenye
malori yanayonyonywa kutoka kwenye mabomba ya Dawasa. Pampu hizo
zilinaswa uani mwa nyumba katika eneo la Bonde la Mto Msimbazi Dar es
Salam
Waziri Makalla na viongozi
wengini wakishanga kuona tanki kubwa la maji lililojengwa chini ya moja
kati ya nyumba tano katika eneo hilo ambazo wamiliki wake
wamejiunganishia maji ya Dawasa isivyo halali
Naibu Waziri wa Maji, Amos
Makalla (kulia), akimhoji mchezaji wa zamani wa Simba, Dua Said ambaye
alikuwa miongoni mwa watu watano waliokamatwa kwa tuhuma za
kujiunganishia maji isivyo halali kutoka kwenye mabomba ya Mamlaka ya
Maji Safi na Taka (Dawasa), kwenye nyumba zao zilizopo Bonde la Mto
Msimbazi, Kigogo, Dar es Salaam. Makalla alikuwa kwenye ziara ya kukagua
miradi ya maji Dar es Salaam
Askari wakilinda doria katika eneo hilo
Moja ya malori yanayojazwa maji katika eneo hilo. Nalo liko chini ya ulinzi
Waziri Makalla akielezea athari
zinazotokana na wizi huo wa maji ambapo alisema kuwa katika nyumba hizo
tano kila siku wanaiba maji lita laki tatu, hivyo kila siku kuikoseasha
serikali mapato ambapo kwa mwezi yanafikia sh. bil 1.4.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John
Mnyika akielezea jinsi atakavyoshirikiana na Serikali katika mapambano
dhidi ya ufisadi wa maji jijini na kwamba atakuwa bega kwa bega
kuhakikisha mswada wa adhabu kubwa kwa wezi wa maji unapelekwa Bunge la
Novemba mwaka huu.
Mchaezaji wa zamani wa Simba, Dua
Said akielezea kwa wanahabari na mbele ya Waziri Makalla, jinsi
anavyoshirikiana na Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam
(DAWASCO), katika biashara ya kuuza maji. Dua Said alikuwa ni miongoni
mwa watu watano waliokamatwa kwa tuhuma za kujiunganishia maji ya
Dawasco isivyo halali katika eneo la Bonde la Msimbazi
Bomba jipya la maji likitandazwa
eneo la Makongo tayari kwa maandalizi ya kusafirisha maji kutoka Mtambo
wa Ruvu Chini ambao upanuzi wake umekamilika hivi karibuni.
Makalla akiuliza swali kwa
wakandarasi kuhusu utandazaji wa bomba hilo, wakati wa ziara yake ya
kukagua miradi ya maji Dar na Pwani.
Waziri Makalla akiwa na Mbunge wa
Jimbo la Kawe, Halima Mdee, Mwenyekiti wa CCM, Salum Madenge,
(KUSHOTO) Deusdedit Mtiro (kulia) walipokuwa wakimlaki alipowasili
kwenye mkutano katika Kata ya Makongo.
WAFUASI WA CHADEMA WAKISHANGILIA NA KUMTAKA WAZIRI AWAHAKIKISHIE UPATIKANAJI WA MAJI MAKONGO JUU
Chadema na CCM wakishangilia katika mkutano huo
Waziri Makalla akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Makongo
Moja wa wananchi akilalamika mbele ya waziri kuhusu adha kubwa wanaipata ya maji eneo la Makongo juu
Msafara wa viongozi wa Chadema na
CCM ukielekea kwenye mkutano wa wananchi katika Kata ya Goba ambao hata
hivyo ulivunjika baada ya kutokea vurugu
WanaCCM wakimshangilia Waziri Makalla alipokuwa akihutubia wananchi katika Kata ya Makongo
Chadema wakishangilia wakati Halima Mdee akihutubia Makongo Juu
Mfuasi wa Chadema akilalama
Mdee akizungumza na wanahabari baada ya mkutano wa Kata ya Goba kuvunjika
Wana CCM WAKISEREBUKA
MNYIKA AKIZUNGUMZA NA WAFUASI WA cHADEMA BAADA YA MKUTANO KUVUNJIKA