Pages

KAPIPI TV

Thursday, July 16, 2015

MAGUFULI ATAMBULISHWA KWA WANA CCM ZANZIBAR

 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa kwenye gari la wazi pamoja na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan kwenye mitaa ya Michenzani Zanzibar. Mhe. Magufuli aliwasili Zanzibar kwa lengo la kutambulishwa kwa wanachama wa CCM Zanzibar akiongozana na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan ambapo wote kwa pamoja walipata kuwasalimia wananchi wa Zanzibar kwenye viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar. Maelfu ya watu wakiufuata msafara wa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Mhe. John Pombe Magufuli aliyeongozana na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassn.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akihutubia wakazi wa Zanzibar waliojitokeza kwa wingi kushuhudia sherehe fupi za kutambulishwa kwa wagombea wa nafasi ya Urais kwa kupitia CCM kwenye viwanja vya Afisi Kuu. Mgombea mwenza wa nafasi ya Urais Mhe. Hassan Suluhu Hassan akizungumza kwenye sherehe fupi za utambulisho nje ya Afisi kuu ya CCM Zanzibar. Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli akiwasalimu wakazi wa Zanzibar waliojitokeza kwa wingi kwenye sherehe za kumtambulisha yeye na mgombea mweza kwenye viwanja vya Afisi Kuu Zanzibar. Wakazi wa Zanzibar wakimsikiliza mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Magufuli kwenye viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar. Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na mgombea wa ueais kwa kupitia CCM Dk.John Magufuli. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TTCL YATOA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI KATIKA SHULE YA SEKONDARI LUSWISI ILEJE MBEYA.

 Meneja wa TTCL Mkoa wa Mbeya, James Mlaguzi akisoma taarifa ya msaada uliotolewa na kampuni hiyo katika shule ya Sekondari Luswisi.
 Mbunge wa Ileje aliyemaliza muda wake,Aliko Kibona akitoa shukrani kwa niaba ya  wananchi wa Kata ya Luswisi kwa kampuni ya TTCL kutokana na msaada waliopokea.
 Mbunge Aliko Kibona pamoja na Meneja wa TTCL wakikabidhiana mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu.
 Mbunge na Meneja wakipongezana baada ya kukabidhiana Saruji na Mbao.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Luswisi wakifurahia msaada uliotolewa na TTCL.

 Wanafunzi wakisaidia kushusha mifuko ya saruji iliyotolewa na kampuni ya TTCL.
 Watumishi wa TTCL Mbeya wakijadiliana jambo kabla ya kuanza makabidhiano ya msaada wa saruji na mbao katika shule ya sekondari Luswisi.
 Baadhi ya wanakijiji waliojitokeza kupokea msaada huo.
 Watumishi wa TTCL Mbeya wakimsikiliza Mbunge alipokuwa akitoa shukrani kwa  niaba ya wananchi.

  Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Luswisi, Mseven Ndangalaakielezea furaha yake baada ya kupokea msaada wa saruji na mbao kutoka TTCL.
 Ngoma za asili zikiendelea kutoa burudani katika hafla ya kukabidhiana msaada wa saruji na Mbao. 

KAMPUNI ya simu ya TTCL imetoa msaada wa saruji na mbao katika Shule ya Sekondari ya Luswisi iliyopo Kata ya Luswisi Wilaya ya Ileje mkoani Mbeya kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mbili za Walimu na chumba kimoja cha darasa.

Kampuni hiyo ilitoa msaada wa mifuko 100 ya saruji na mbao vyenye thamani ya shilingi Milioni tatu ikiwa ni kupunguza changamoto inayowakabili Walimu wa Shule hiyo ambayo inawalimu 22 huku ikiwa na Nyumba moja iliyokamilika ambayo anaishi Mkuu wa Shule.

Wakizungumza baada ya kupokea msaada huo baadhi ya Walimu hao wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Shule, Mseven Ndangala, alisema Walimu wanaishi katika wakati mgumu kwani asilimia kubwa wamepangishwa na wanakijiji sehemu ambayo ni mbali na eneo la shule.

Alisema Walimu wengi wamepanga umbali wa kilomita 7 kutoka shuleni hivyo hulazimika kukodi pikipiki kuwapeleka na kuwarudisha shule kwa gharama ya shilingi 6000 kwa siku hali inayowarudisha kwenye umaskini na kupunguza ari ya kufundisha kutokana na kutumia gharama kubwa kwenye usafiri.

Aliongeza kuwa hivi sasa kuna walimu wapya watano ambao kwa mazingira yalivyo hawataweza kupanga kutokana na ukosefu wa fedha na kuwalazimu kuishi walimu wote watano kwenye chumba kimoja hali inayoonesha kuwakatisha tama kuendelea kufundisha shuleni hapo.

Awali akikabidhi msaada huo, Meneja wa TTCL Mkoa wa Mbeya, James Mlaguzi, alisema Kampuni ilipata maombi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Ileje, Aliko Kibona kwa ajili ya kusaidia kupunguza adha hiyo jambo ambalo lilikubaliwa na hatimaye kuwafikishia.

Alisema kampuni imejipanga kuhakikisha mwishoni mwa mwaka huu inapeleka huduma za mawasiliano vijijini ili kuwawezesha wakulima kutafuta masoko ya mazao yao kwa njia za mtandao.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ileje aliyemaliza muda wake, Aliko Kibona aliwashukuru kampuni ya TTCL Hususani Afisa mtendaji Mkuu Dk. Kazaula Kamugisha kwa kumkubalia ombi lake ili kuhakikisha walimu wanakuwa na mazingira mazuri ya kufundishia kwa kuwajengea nyumba nzuri.

Aidha alitoa wito kwa Watendaji wa vijijini na Kata kuhakikisha wanasimamia vizuri msaada huo kwa kuhakikisha unafanya kazi zilizokusudiwa ili kuwaridhisha waliotoa misaada na hivyo kuwafanya wawe na moyo wa kujitolea katika kipindi kingine.

Aliongeza kuwa ni wajibu wa Wabunge, wadau na wananchi kuhakikisha wanatumia kila njia wanatengeneza mazingira mazuri ya Walimu kuwa na ari kubwa ya kufundisha kuliko kuitegemea Serikali kwa kila kitu.

WAKILI ELIAS NAWERA ACHUKUA FOMU ZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KAWE JIJINI DAR ES SALAAM

Wakili Elias Nawera akionyesha alama ya dole baada ya kukabidhiwa fomu hizo. Kulia ni mgombea ubunge mkoa wa Dar es Salaam kupitia Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Lilian Mkosani.
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe (kushoto), akimkabidhi fomu ya kugombea ubunge jimbo la Kawe, kada wa chama hicho, Wakili Elias Nawera (katikati), Dar es Salaam leo mchana. Kulia ni mgombea ubunge mkoa wa Dar es Salaam kupitia Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Lilian Mkosani
 Wakili Nawera (kulia), akiandika jambo kabla ya kulipa sh. 100,000  ya kuchukulia fomu.
 Hapa akimshukuru Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe baada ya kuchukua fomu hizo.
 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe (kushoto), akimuelekeza Wakili Elias Nawera mambo ambayo anapaswa kuyafuata baada ya kukabidhiwa fomu hizo.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni ambaye anamaliza muda wake Iddi Azani akimpongeza Wakili Nawera baada ya kuchukua fomu hizo. Azan alifika katika ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni kwa ajili ya kuchukua fomu ya kutetea nafasi yake ya ubunge katika Jimbo hilo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

"NATOSHA KUVAA VIATU VYA UBUNGE WA DEWJI SINGIDA MJINI"- HASAN MAZALA

fomu
Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM Manispaa ya Singida, Hasan Mazala akionesha vijana fomu yake ya kuwania ubunge Jimbo la Singida Mjini jana kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM Mkoani Singida.
kwa nguvu
Mazala akiwaasa vijana kufanya kazi kwa nguvu katika jimbo hilo.
nimenyooka
Mkinipa nafasi ya kuwatumikia mambo yatanyooka namna hii.
ninao uwezo
tuko imara
Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Singida Mjini Hassan Philipo Mazala akisistiza jambo kwa vijana waliomsindikiza kuchukua fomu.
pamoja
vijana
Baadhi ya vijana wakiwa katika picha ya pamoja na Hassan Mazala nje ya jengo la makao makuu ya CCM Mkoa wa singida mara baada ya kuchukua fomu.(PICHA ZOTE NA HILLARY SHOO).

Na Hillary Shoo, SINGIDA
MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa (MNEC) Manispaa ya Singida,Hassan Mazala amechukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Singida Mjini ..

Akizungumza na kundi la Vijana wa CCM kwenye ukumbi mdogo jana, Mazala amesema kuwa amefungua ukurasa mpya wa maisha yake kwa kuwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Mohammed Dewji aliyestaafu.

‘Nimejipima nikaona ninaweza kuvaa viatu vilivyoachwa wazi na Dewji kwani katika kipindi chote alichukuwa Mbunge nilishirikiana nae katika kuyatekeleza yale yote aliyonituma kama msaidizi wake wa karibu.” Alisema Mazala.

“Nimekuwa Kiongozi kwa muda mrefu katika ngazi mbalimbali kuanzia kwenye vijiji ,Kata, Wilaya, Mkoa na sasa Taifa, hivyo nina uwezo wa kutosha na nimekomaa kisiasa katika kufanya kazi hii ya Ubunge bila wasiwasi wowote pale alipoachia Dewji” Alisisitiza.

Aidha alisema anazifahamu changamoto zinazolikabili Jimbo hilo kwani ametembea kona zote na kujionea hali halisi ya wananchi wanavyojishigulisha na shughuli za kijamii.

“Nina Moyo wa dhati kabisa wa kuwatumikia, ninaombeni mnibebe, najua yamesemwa mengi sana juu yangu katika kipindi ambachio nimlikuwa nafanya kazi na MO, lakini yapuuzeni hayo kwani hayana ukuweli wowote ni chuki binafsi tu.” 
Alisema huku akishangiliwa na kundi la vijana linalojiita team Mazala.

Hata hivyo Mazala ambaye ana uwezo mkubwa wa kutawa jukwaa alisema kamwe hatawaanguisha wananchi wa Jimbo hilo huku akitumia misamiati Zimwi likujualo, Usiache mbachao na mwokoto kuni porini huota moto pamoja.

Akitangaza kutogombea tena Ubunge mapema Julai 08 mwaka huu mjini Singida Dewji alimsifu Mazala kwa kusema kuwa ni mchapa kazi, mwaminifu, mwadilifu na ana moyo wa kujitolea kwani aliweza kusimamia kazi zake zote bila ya matatizo yoyote.

“Na pia ninapenda kumshukuru kipekee mtu mmoja ambaye bila yeye mafanikio yangu ya kiuongozi niyoyopata hapa Singida yasingeweza kufanikiwa vizuri bila ya yeye.” Alisema Dewji katika taarifa yake hivi karibuni.

JUMAA MHINA 'PIJEI' ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KAWE, ATAJA VIPAUMBELE VYAKE

Hapa ikionesha fomu baada ya kukabidhiwa.
 Kada wa CCM Jumaa Mhina 'Pijei' (katikati), akipokea fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam, kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe leo mchana. Anaye shuhudia kulia ni Kada wa chama hicho anayewania ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia CCM, Ramadhan Ndanga 'Potipoti'.
 Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe (kushoto), akimpa maelezo ya kufuata baada ya kukabidhiwa fomu hizo.
Waandishi wa habari wakimuhoji nini atawafanyia wananchi wa Jimbo la Kawe iwapo atachaguliwa.

Na Mwandishi Wetu

MUWANIA nafasi ya Ubunge Jimbo la Kawe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jumaa Mhina 'Pijei' amesema akipata nafasi hiyo atashirikiana na wananchi wa jimbo hilo katika kutatua changamoto zilizopo.


Hayo aliyasema wakati akichukua fomu ya kugombea nafasi hiyo Dar es Salaam leo mchana na utaja vipaumbele vyake vya maendeleo atakayofanya.

Alisema mwaka 2010 aligombea lakini katika kura za maoni ya ccm hazikutosha, mwaka huu anaamini zitatosha na kulikomboa jimbo lililo mikononi mwa wapinzani.

Alisema kipaumbele chake ni ajira kwa vijana, elimu, miundimbinu ya barabara na umeme na kuwa mafanikio hayo yatakuja iwapo atashirikiana kwa karibu na wananchi hivyo aliomba wananchi kuto muangusha wakati ukifika.

Alisema tayari ametoa ajira kwa vijana kwa kuwapa bodaboda ambazo zimepunguza tatizo la ajira na vitendo vya uhalifu katika jimbo hilo.

Mhina alisema kipaumbele kingine atakacho kitoa ni kuhakikisha anatumia uzoefu wake wa ujasiriamali kwa kuwajengea uwezo wanawake na vijana kwa kuwapa elimu na kuwawezesha kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuinua mitaji yao.

Wednesday, July 15, 2015

MC PILIPILI NA TAASISI YA MEDO WASAINI MKATABA WA KUSAIDIA ELIMU MKOANI MOROGORO

 Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Morogoro (MEDO), James Mbuligwe (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kabla ya MC Pilipili kutiliana saini na taasisi hiyo ya kusaidia elimu. Kutoka kulia ni Meneja Mradi, Bertha Gama, Emmanuel Elias 'MC' Pilipili na Makamu Mwenyekiti wa Medo, Seluwa Amin.
 MC Pilipili (katikati), akizungumza kabla ya kutia saini.
 Makamu Mwenyekiti wa Medo, Seluwa Amin (kushoto), akiangalia mkataba huo kabla ya kusainiwa.
 MC Pili pili (katikati), akisaini mkataba huo.
 Makamu Mwenyekiti wa Medo, Seluwa Amin (kushoto), akimkabidhi mkataba huo MC Pilipili. Kulia ni Meneja Mradi Medo, Bertha Gama.


Na Dotto Mwaibale

MSANII na mshereheshaji wa shughuli mbali mbali, Emmanuel Elias 'MC' Pili pili ameingia mkataba na Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Morogoro (Medo), kwa ajili ya kusaidia elimu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kabla ya kusaini mkataba wa kusaidia watoto walio katika mradi wa elimu kwa watoto unaoendeshwa na Medo, Pilipili alisema ni wakati muafaka kwa watanzania kwa ujumla kujenga tabia ya kusaidia shughuli za maendeleo hasa katika elimu.

Alisema bila ya kuwa na elimu hakuna kinachoweza kufanyika katika mambo mbalimbali pamoja na uongozi hivyo kila mtu eneo alipo anapaswa kusaidia elimu kupitia taasisi hiyo ya Medo ili iweze kuwasaidia watoto wengi zaidi.

"Napenda kuwasapoti watoto hawa waliochini ya mradi 
unaoendeshwa na Medo kwa kuwasaidia mahitaji mbalimbali hivyo naomba watanzania wanisapoti wakiwemaniio wasanii wenzangu" alisema Pilipili.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Taasisi ya Maendeleo ya Elimu Mkoa wa Morogoro, James Mbuligwe alisema taasisi yake kuingia mkataba na MC Pili pili kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao ni hatua nzuri ya mafanikio kwao.

Alisema  taasisi hiyo imezindua kampeni maalumu ya 'Nisaidie 500 Yatosha kunipa elimu ambapo balozi wa mradi huo ni Msanii Wastara Sajuki" alisema Mbuligwe.

Meneja wa Mradi huo, Bertha Gama alisema hadi hivi sasa kuna watoto 35 wanaopata elimu ya Sekondari katika shule za Kauzeni, Kihonda, Mwembesongwe na Mzinga na kuwa mwaka huu wanafunzi wanne waliochini ya mradi huo wanategemewa kuhitimu kidato cha nne.



Alisema lengo la taasisi hiyo ni kufikisha huduma zao nchi nzima ambapo kwa awamu ya kwanza wameanzia mkoani Morogoro na kupitia chini ya mradi huo watoto 100 watanufaika na kwa awamu ya pili wanatarajia kuifanya mikoa ya Kanda ya Ziwa. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

THE NORWEGIAN EMBASSY GRANTS UN TANZANIA 3.1 MILLION US DOLLARS

IMG_2156_1
Ambassador of Norway, H.E Hanne-Marie Kaarstad, (left) and UN Resident Coordinator, Mr. Alvaro Rodriguez, signing agreement of USD 3.1 million for Grants to support the UN’s Refugees response, governance initiatives, and UN Partnership Building in Zanzibar as well as on Human Rights, at the ceremony which was held at the UN offices in Dar es Salaam.
*Refugees and Governance programs among key areas of support

The Norwegian Embassy today has signed an agreement with One UN Tanzania to release USD 3.1 million (approximately 6.9 billion Tshs).The signing ceremony was held at the UN offices in Dar es Salaam between the Ambassador of Norway H.E Hanne-Marie Kaarstad and the UN Resident Coordinator Mr. Alvaro Rodriguez. The contribution will focus on providing support to the UN’s refugee response, governance initiatives, and UN partnership building in Zanzibar as well as on human rights.

Emphasizing on the Embassy support to the One UN, Ambassador of Norway H.E Hanne-Marie Kaarstad stated that Tanzania has set a good example of UN Agencies working together with coherence, efficiency and effectiveness. She added; “The UN has always been a vital and highly valued partner for Norway. The implementation of the new Sustainable Development Goals, which we hope will be adopted by the UN General Assembly in September, will require hard work. It is not business as usual and requires concerted efforts from us all. 

We wish to support the UN in assisting the people and the Government of United Republic of Tanzania in their effort to achieve these goals and fulfil their international obligations, including giving a voice to the most marginalised and vulnerable.”
IMG_2163
Ambassador of Norway, H.E Hanne-Marie Kaarstad, (left) and UN Resident Coordinator, Mr. Alvaro Rodriguez, shake hands after affirming their signatures on the agreement.
Thanking the government and people of the Kingdom of Norway for their continued support, the UN Resident Coordinator, Mr. Alvaro Rodriguez, stated that Norway has been a supportive and constructive partner of One UN and Tanzania for decades. “The contribution of USD 3.1 Million will be used to strengthen partnerships, enhance democratic governance interventions by UN agencies and provide urgent relief to Burundian refugees in Tanzania”. He added that the One UN looks forward to a continued collaboration with Norway in the years to come.
Norway has been a major supporter of the UN reform agenda and the upcoming Sustainable Development Goals (SDGs) and with other development partners, is committed to the development vision of the government and the people of Tanzania.
Ballot-box
Ballot box.
DSC_0170
Nyarugusu Refugee's camp in Kigoma.

MTANGAZAJI WA RADIO FREE AFRICA, WILLIAM BUNDALA ATANGAZA RASMI KUWANIA UBUNGE

1525677_749904191774263_4961655255847640040_n
Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” katika pozi.
SAM_2530
Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha Bibi K” akiwa amebebwa juu na wakazi wa Ushetu wakati wa mkutano wake wa kutangaza nia kuwania ubunge katika jimbo jipya la Ushetu wilayani Kahama.
SAM_2529 (1)
Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha Bibi K” akiwa amebebwa juu na wakazi wa Ushetu wakati wa mkutano wake wa kutangaza nia kuwania ubunge katika jimbo jipya la Ushetu wilayani Kahama.
SAM_2477 (2)
Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” akitangaza nia kuwania ubunge katika jimbo jipya la Ushetu wilayani Kahama.
SAM_2480 (1) 11-40-46
Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha Bibi K” akizungumza na wakazi wa Ushetu wakati wa mkutano wake wa kutangaza nia kuwania ubunge katika jimbo jipya la Ushetu wilayani Kahama.
KIJU 2
Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha Bibi K” akiwajibika katika kazi yake ya uandishi wa habari.
KIJUUU
Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa, William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha Bibi K” akiwa katika moja ya mikutano muhimu.

Na Mwandishi wetu
Siku moja tu baada ya Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania kutangaza majimbo mapya ya Uchaguzi,Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “Kijukuu cha Bibi K” ametangaza rasmi kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Ubunge katika Jimbo la jipya la Ushetu katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga,kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Bundala ametangaza kuingia kwenye mchakato wa kugombea kuteuliwa na Chama ili aweze kupeperusha bendara ya Chadema/UKAWA katika uchaguzi mkuu ujao katika mkutano wake wa kutangaza nia uliofanyika katika Kijiji cha Bogomba “B” kata ya Ubagwe wilayani Kahama.

Mtia nia huyo alisema endapo Chama chake kitampitisha na hatimaye kushinda Ubunge katika Jimbo hilo atahakikisha anasukuma kasi ya maendeleo katika jimbo hilo jipya lenye Rasimali nyingi kupitia nafasi yake na wajibu kama anavyotakiwa Mbunge Kufanya.

Alisema kuwa dhamira yake imemsuta kwenda kuwatumikia wananchi wa wilaya hiyo ambayo yeye ni mzawa na kuwa atahakikisha anapigania maendeleo ya wananchi kwa kasi huku akiondoa uonevu kwa waandishi wa habari na watumishi wengine serikalini na katika halmashauri za wilaya.

Sambamba na hayo amesema kuwa sababu nyingine iliyomsukuma ni kuona wagombea wengine wanaolitaka jimbo hilo hawako kwa ajili ya ukombozi wa jimbo hilo bali wako kwa ajili ya maslahi binafsi kutokana na asilimia kubwa ya wagombea hao si wakazi wa eneo hilo na kwamba hawafahamu matatizo ya wana ushetu kama anavyoyafahamu yeye.

Aliongeza kuwa akifanikiwa kuukwaa Ubunge pia atasimamia kuhakikisha Jimbo hilo jipya linapata Chuo cha ufundi kwa ajili ya vijana wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne kupata elimu jambo lilatalopunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana.

Bundala alisema kipaumbele kingine atakachoshughulikia ni pamoja na kusimamia na kutoa elimu ya Sheria kupitia wanasheria ambao watazunguka katika kata kutoa elimu hiyo hususan katika maswala ya umiliki wa Ardhi,Mirathi,haki za wakulima na wafugaji pamoja na haki za raia na mali zao kwa ujumla.

Akizungumzia kuhusu suala la michezo katika jimbo hilo, Bundala alisema kuwa kupitia Kijukuu Cup atahakikisha anashirikiana na halmashauri na wadau wa michezo kuhakikisha halmashauri ya ushetu inapata timu ya kucheza ligi kuu Tanzania Bara.

Awali Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CHADEMA (BAVICHA) Halmashauri ya Ushetu Emmanuel Magema aliwataka vijana wote kuungana ili kumuunga mkono kijana mwenzao aliyejitokeza na kuonesha nia ya kutaka kuongoza akiwa Mbunge wa jimbo hilo.

Wilaya ya Kahama kwa sasa ina halmashauri za wilaya tatu za Msalala,halmashauri ya mji wa Kahama na halmashauri mpya ya Ushetu na kufanya majimbo ya uchaguzi kuwa matatu.

Katika kinyang’anyiro cha Ubunge katika jimbo jipya la Ushetu kuna watu zaidi ya watano wanaotajwa kulimendea jimbo huku wagombea wa CHADEMA wakionekana kuungwa mkono na makundi mengi hususan vijana.