Pages

KAPIPI TV

Friday, July 10, 2015

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YAWAFUTURISHA WAKAZI WA JIJI LA MBEYA , MKAPA HALL

 Baadhi ya wakina dada wakiwa wamejiweka sawa kuwapokea wageni mbalimbali ambao walifika Ukumbi wa Mkapa Jijini Mbeya kwa ajili ya Kufuturu
 Baadhi ya wadau wakiwa wanangoja muda wa kufuturu ufike 
 Bw. Francis Mwasamwene Meneja wa Mauzo Tigo Mkoa wa Mbeya ambaye pia alikuwa mratibu wa kufanikisha Shughuli hii ya Kuwafuturisha wakazi wa Mbeya akiongea Machache.
Meneja wa Tigo Pesa Kanda ya Njanda za Juu Kusini Thomas Meitaron akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya Tigo kwa wakazi wa Jiji la Mbeya bila kujali Dini kwa kujitokeza na kufuturu pamoja, alisema Tigo ni Sehemu ya Familia ya wanambeya na pia Waislam kwa ujumla ndio mana wafanyakazi na wananchi wa Mbeya wamejumuika Pamoja kufuturu, Mwisho alisisitiza kuwa sasa huduma za Tigo zimeboreshwa na zimemfikia kila mmoja.
Sheigh Ally Hassan Furukutu ambaye ni Katibu wa Bakwata Mkoa wa Mbeya , akiwashukuru Tigo kwa Moyo waliojitolea kuwafuurisha wakazi wa Jiji la Mbeya bila kujali Dini wala Kipao cha mtu, na aliahidi ushirikiano mzuri kati ya Tigo na Waislam, Mwisho alitoa Dua kwa wote.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi (wa kwanza kushoto) akipata futari pamoja na wegeni wengine walioalikwa kufuturu
Baadhi ya Wafanyakazi wa Tigo pamoja na wakazi mbalimbali kutoka jijini Mbeya wakichukua Futari ambayo iliandaliwa na kampuni la Tigo Tanzania.
Baadhi ya watu mbalimbali wakiwemo watumishi waserikali, wananchi na wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Tigo wakiendelea kupata Futari
 Baadhi ya wakina dada na akina mama wakiendelea kupata Futari iliyoandaliwa na Kampuni ya simu ya Tigo
 Wakiendelea kupata futari
 Picha ya Pamoja baada ya Kumaliza Kufuturu

Na Mbeya yetu

SHEREHE YA KUMUAGA (SEND OFF) TUMPALE JOHN MWAISANGO, YAFANA KATIKA UKUMBI WA MKAPA JIJINI MBEYA

Tumpale John Mwaisango(kulia) Bi. Harusi mtarajiwa akiwa pamoja na Mume wake Mtarajiwa Jeofrey Daniel Shipela (kushoto) katika nyuso za Furaha wakati wa sherehe za kumuaga .
Hivi ndivyo ukumbi ulivyo ulivyokuwa
Bibi Harusi Mtarajiwa Tumpale John Mwaisango akiwa anaingia ukumbini 
Bi Harusi mtarajiwa Tumpale John Mwaisango akimpa zawadi Mume wake Mtarajiwa Jeofrey Shipela wa kwanza kulia ni mpambe wa Bwana harusi mtarajiwa Venance Matinya
 Bi. Harusi Mtarajiwa Tumpale John Mwaisango (kushoto) Akikata keki kulia ni Mpambe wake Monica
 Bi. Harusi Mtarajiwa Tumpale John Mwaisango (kushoto) Akimlisha keki Mpambe wake Monica
Baba Mdogo wa Tumpale John Mwaisango akitoa neno kwa Binti yake na neno la Shukurani
Daniel Shipela (Kushoto) Baba Mzazi wa Bwana Harusi Mtarajiwa Jeofrey Shipela na Mama Mkubwa wake Elizabeth Njeje (kulia) wakitambulishwa
Mbele kwa Mbwembwe za aina yake na kwa umahili Mkubwa Bwana Charles Mwaipopo akifungua Shampeni , wakati wa Sherehe hiyo
Bibi Harusi Mtarajiwa akimrisha Chakula bwana Harusi Mtarajiwa 
Kutoka kulia ni Fredy Anthony Njeje, Grace Mwasote na Njuguna Karanja Marafiki wakubwa wa Joseph Mwaisango wakiwa katika Sherehe 
Baba Mchungaji ambaye ni Baba yake Mdogo wa Tumpale akimpa Mkono wa Pongezi 
Mbele ni Baadhi ya kaka zake na Bibi Harusi Mtarajiwa wamewakajeee...
Joseph Mwaisango kaka Mkubwa wa Tumpale John Mwaisango akimkabidhi zawadi mdogo wake Bibi Harusi Mtarajiwa , Fedha ambazo zitamsaidia ambapo anaenda kuanza Maisha na kumuaga rasmi.
Baadhi ya watu walikuwepo katika Sherehe hiyo
Huyo anaondoka baada ya kumaliza Sherehe
Bibi Harusi Mtarajiwa Tumpale John Mwaisango kuelekea katika Sendoff yake aliona bora asherekee pia na watoto yatima na waliokuwa wanaishi katika mazingira magumu cha Nuru hapa akiwapa zawadi
Baadhi ya Vitu ambavyo alipeleka katika kituo hicho
 Huko Nyumbani pia kulikuwa na Sherehe ya kumuaga Binti Tumpale Mwaisango, Hapa Baba Mdogo akitoa Neno la Shukurani
 Sherehe ikiendelea Nyumbani


NI NOMAAA....HUYU DEMU NI FAKE

Lulu kuja na Kitu kingine kipya Ni Nomaaaaaaaaaaa
Kaa Mkao wa Kula

WANAHABARI WAPEWA SEMINA KUHUSU WIKI YA USALAMA BARABARANI YA UMOJA WA MATAIFA DAR ES SALAAM

 Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mohamed Ally Mohamed (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua semina hiyo Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Maafa na Dharura, Dk.Elias Kwesi.
 Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Maafa na Dharura, Dk.Elias Kwesi (kulia), akizungumza katika semina hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mohamed Ally Mohamed kufungua semina hiyo. 

 Ofisa Mradi wa Usalama Barabarani wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Marry Kessy (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa mada kwenye semina hiyo.
 Mkaguzi wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Mossi Ndozero (kulia), akitoa mada kwenye semina hiyo.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Safe Speed Foundation, Henry
 Bantu akizungumza kwenye semina hiyo.
 Mkuu wa Kitengo cha Dharura na Maafa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mary Kitambi akitoa mada kuhusu sekta ya Afya inavyokabiliana na changamoto za utoaji huduma kwa wagonjwa wanaopata ajali.
 Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.
 Semina ikifunguliwa.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye 
semina hiyo.
 Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.


Dotto Mwaibale

WATOTO 1, 86, 300 wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na ajali za magari duniani hivyo kuwa changamoto kubwa ya usalama barabarani.

Hayo yalibainishwa na Ofisa Mradi wa Usalama Barabarani wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Marry Kessy wakati akitoa mada kwa wanahabari kwenye semina ya siku moja ya wiki ya umoja wa mataifa ya usalama barabarani iliyofanyika Dar es Salaam leo.

"Hii ni changamoto kubwa duniani na hapa nchini kwani kati ya watoto hao idadi kubwa ya wanaopoteza maisha katika ajali hizo ni watoto wa kiume" alisema Kessy.

Mkaguzi wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani, Mossi Ndozero alisema kumekuwa na changamoto nyingi zinazotokana na masuala ya usalama barabarani ikiwemo ukiukwaji wa sheria za barabarani unaosababishwa na binadamu.

Ndozero aliwataka watumiaji wa vyombo vya moto kuwa makini wawapo barabarani na kufuata sheria jambo litakalo saidia kupunguza changamoto hiyo ya ajali kama sio kuisha kabisa.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Safe Speed Foundation, Henry Bantu alisema maendeleo ya dunia yamesababisha ongezeko la magari barabarani hususan nchini Tanzania hivyo kuongeza ajali za barabarani.

Bantu aliwataka watanzania kujenga utamaduni wa usalama barabara ambao hatuna jambo litakalo saidia kupunguza ajali kwa kusaidiana na wadau wengine.


Mkuu wa Kitengo cha Dharura na Maafa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mary Kitambi alisema ajali zinazotokea nchini zimechangia kuwepo kwa ongezeko kubwa la wagonjwa hivyo kuwa changamoto katika hospitali mbalimbali nchini kutokana na wodi kutokidhi ongezeko la wagonjwa na vifaa tiba.

Alisema kilele cha maadhimisho ya wiki ya umoja wa mataifa ya usalama barabarani yatafanyika Julai 15 mwezi huu Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko jijini Dar es Salaam.

Thursday, July 9, 2015

BODI YA UTALII TANZANIA (TTB), YAANDAA ONESHO LA SITES KUFANYIKA UKUMBI WA MLIMANI CITY OKTOBA MOSI JIJINI DAR ES SALAAM

Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji Bodi ya Utalii Tanzania, Devotha Mdachi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu Onesho la Sites litakalofanyika Oktoba Mosi hadi 3, 2015 Ukumbi wa Mlimani City. Kushoto ni Ofisa Mauzo Mkuu wa Shirika la Ndege la Ethiopia, Lima Dsilva na  Meneja Huduma wa Shirika la Ndege la Ethiopia, Dawit Mekonnen. 

 Meneja Huduma za Utalii wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Philip Sebastian (wa pili kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni   Ofisa Mauzo Mkuu wa Shirika la Ndege la Ethiopia, Lima Dsilva na  Meneja Huduma wa Shirika la Ndege la Ethiopia, Dawit Mekonnen, Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi na Ofisa Uhusiano Mkuu wa TTB, Geofrey Tengeneza.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.



Na Dotto Mwaibale

KAIMU Mkurugenzi Mwendeshaji, bodi ya Utalii nchini, Devotha Mdachi, alisema ufinyu wa bajeti ya matangazo katika sekta ya utalii unasababisha  sekta hiyo, kutofanya vizuri ukilinganisha na nchi nyingine.

Mdachi aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akitolea
ufafanuzi wa onesho la utalii nchini, linalotarajia kufanyika Oktoba mosi hadi 3 mwaka huu linalojulikana kama Sites.

Kaimu mkurugenzi huyo alisema kuwa bajeti finyu iliyotengwa na Serikali katika kutoa matangazo ya utalii wa ndani ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine zinavyojitangaza duniani.

Pia, alisema kutokuwa na ofisi za bodi ya utalii katika kila mkoa
na kutokuwa na Shirika la Ndege la Taifa kusababisha utalii wa ndani kuwa mdogo.

“Wenzetu wa Kenya bajeti yao ya matangazo ya utalii ni kubwa
ukilinganisha na sisi kwani wao wametenga bilioni 36 katika
matangazo, lakini sisi bajeti yetu ya matangazo ni finyu sana ambapo ni bilioni 2.3,” alisema Mdachi

Kwa upande wake, Meneja huduma za utalii nchini ambaye
pia ni Mratibu Mkuu bodi hiyo, Sebastian Philip alisema onesho hilo litakutanisha wafanyabishara wa hapa nchini kutoka kwenye masoko ya utalii, hivyo ni vema watanzania kutumia fursa hiyo kuhakikisha kunaleta soko kubwa la utalii nchini.(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)