Pages

KAPIPI TV

Thursday, July 9, 2015

SHIRIKA LA GLOBAL PEACE FOUNDATION (GPF) LAANDAA KONGAMANO KUBWA LA VIJANA LA KUJADILI AMANI, KUFANYIKA ZANZIBAR KUANZIA JULAI 12, 2015

  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation (GPF), Arnold Kashembe.
 Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation (GPF), Arnold Kashembe (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kongamano kubwa la vijana  litakalofanyika Zanzibar kwa kipindi cha mwezi mzima kuanzia Julai 12 mwaka huu. Kongamano hilo litahudhuriwa na marais wastafu na viongozi maarufu. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa GPF nchini, Martha Nghambi na Mratibu wa kongamano hilo, Antu Mandosa
 Mwakilishi Mkazi wa GPF nchini, Martha Nghambi  (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Balozi wa Amani, Risasi Mwaulanga na  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation (GPF), Arnold Kashembe.
 Balozi wa Amani, Risasi Mwaulanga  akizungumza katika mkutano huo.
 Mratibu wa kongamano hilo, Antu Mandosa akizungumza kuhusu kongamano hilo.
Mkutano ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

SHIRIKA la Global Peace Foundation limewataka Watanzania kudumisha amani iliyopo ili nchi yetu isije ikakumbwa na machafuko kama nchi za jirani.

Akizungumza leo jijini  Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Global Peace Foundation na Mshauri wa Amani Afrika , Arnold Kashembe alisema Shirika hilo limeandaa mkutano wa kujadili mkakati wa kudumisha amani utakao jumuisha nchi za Afrika Mashariki (EAC).

"Shirika la GPF limeandaa mkutano wa kujadili mkakati wa kudumisha amani utakao jumuisha nchi za Afrika Mashariki (EAC) ambao utafanyika Zanzibar kuanzia Julai 21- 24," alisema Kashembe.

Kashembe alisema mkutano huo wa kipekee utawakutanisha maraisi wastaafu nane akiwemo Keneth Kaunda na Amani Karume, viongozi wa dini, wafanyabiashara na viongozi wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki na nchi jirani.

Aidha Global Peace Leadership Conference (GPLC) 2015 itatoa mafunzo na nyenzo ili kuhimiza ushirikiano katika ukanda wa Afrika Mashariki na kujaribu kupunguza tofauti na matatizo yanayowakumba.

Mada nyingine ni kuwapongeza vijana 400 kutoka Afrika Mashariki wanaotarajiwa kushiriki kuongeza nguvu katika mbinu za ujasiriamali na kuwa mfano wa wanafunzi wa wengine huko watokapo.

Kujenga mikakati imara ya kudumisha ukaribu na kusaidiana mbinu za kupambana na umaskini, tatizo la ajira, HIV, Malaria na kuwezesha na kuzindua misheni Maendeleo ya Afrika kama lengo kuu na kiini cha mabadiliko kupitia Amani, Uongozi bora, na Uimara wa maendeleo kiuchumi.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

MDAHALO WA TAASISI YA MWALIMU NYERERE WATAKA AMANI,WAPINGA RUSHWA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015

 Mtoa mada Awadh Ali Said, akitoa mada kuhusu muungano na umuhimu wa kuzingatia misingi ya amani katika mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ambao ulifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo.
 Mtoa mada Dk. Humphrey Polepole akitoa mada kuhusu kuzingatia misingi ya amani na umoja wa taifa letu kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akitoa majumuisho ya jumla juu ya dhima ya mdahalo huo, ambapo aliwataka watanzania kuendelea kupiga vita rushwa na kusisitiza kutowachagua watoa rushwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku (kushoto), akiteta jambo na watoa mada katika kongamano hilo, Jaji mstaafu Joseph Warioba na Dk.Humphrey Polepole (katikati)
 Jaji mstaafu Joseph Warioba, akimuonesha Dk. Humphrey Polepole ujumbe mfupi aliotumiwa kwenye simu yake .
Jaji mstaafu Joseph Warioba akisalimiana na washiriki wa mdahalo huo baada ya kumalizika. Mdahalo huo uliorushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha ITV.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
 Jaji mstaafu Joseph Warioba (kulia), akiwaaga washiriki wa mdahalo huo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii. com-simu namba 0712-727062)


MO, DIAMOND PLATNUMZ KUTIKISA SINGIDA MJINI MCHANA HUU

IMG_7330
Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akishuka kwenye ndege mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Singida.
IMG_7331
Mh. Mohammed Dewji akilakiwa na Mjumbe wa halmashauri kuu CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida, Hassan Mazala mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Singida mjini kwa ajili kuhutubia Mkutano mkubwa ambao atawasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya mwaka 2005/2010 na 2010/2015 ambapo Mwanamuziki wa kimataifa Nassib Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz atatumbuiza wanaSingida. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya Singida, Jumanne Hamis Nguli.
IMG_7333
Mh. Mohammed Dewji akisalimiana na Katibu wa CCM wilaya ya Singida mjini, Magdalena Ndweta.
IMG_7334
Mh. Mohammed Dewji akisalimiana na Katibu ambaye pia ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya Singida mjini, Duda Juma.
IMG_7336
Mwanamuziki wa kimataifa nchini, Diamond Platnumz akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya Singida, Jumanne Hamis Nguli.
IMG_7341
Mh. Mohammed Dewji akionekana mwenye furaha na tabasamu bashasha akiongoza na Mwenyekiti wa CCM wilaya Singida, Jumanne Hamis Nguli kusalimiana watoto na wananchi waliojitokeza kumlaki katika uwanja wa ndege wa Singida mjini.
IMG_7343
Umati wa watoto wanaoishi karibu na maeneo ya uwanja wa ndege wa Singida mjini wakiwa wamefurika kwenye uwanja huo kumpokea mbunge wao.
IMG_7344
Pichani juu na chini watoto na vijana wakimfurahia Mbunge wao Mh. Mohammed Dewji.
IMG_7345
IMG_7347
IMG_7351
Diamond Platnumz akigombaniwa na wakazi wa Singida mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Singida.
IMG_7352
Mwanamuziki wa kimataifa Diamond Platnumz, Rommy Jones pamoja na mlinzi wake wakielekea kwenye gari maalum mara tu baada ya kuwasili.
IMG_7353
Wananchi wa Singida mjini wakimsindikiza Mbunge wao Mh. Mohammed Dewji.
IMG_7356
IMG_7357
CCM Oyeeeeeeee!!!

SABASABA WINDHOEK LUNCH PARTY ILIVYOJUMUISHA WADAU WA VIP WAKITAIFA NA KIMATAIFA KATIKA UKUMBI WA DANKEN HOUSE MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM

Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited James Rugemalira akitangaza nia na kuwakaribisha wageni mbalimbali katika hafla hiyo ya Sabasaba Windhoek Lunch Party.
 Bwana Rugemalira (kulia) akimweleza jambo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kansa kutoka nchini India Profesa. Antony Pais walipokutana katika hafla hiyo.
 Bwana James Rugemalira (kulia), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Ukanda Maalumu wa Kiuchumi Mkoa wa Tanga, Chris Incheul Chae ambaye pia hakukosa kuhudhuria hafla hiyo.
 Bwana Rugemalira (kulia ) akisalimiana na Mwanyekiti wa Kamati ya Mahusiano na Umma wa Kampuni ya Mabibo Beer wines and Spirits Limited, Anic Kashasha.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited,  Secelela Balisidya naye alikuwepo kuhakikisha mambo yanaenda sawa.    
 Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Alice Marco (kulia) naye alikuwepo kuhakikisha kila mgeni anapata vinywaji vya Windhoek vya kutosha. Hakuwa na mzaha katika swala hilo.
 Mdau Faustine Kapama (kushoto) na mawakili Paschal Kamala na Sosten Mbedule walikuwepo kufurahia kinywaji murua cha Windhoek.
 Ni wageni wengi walikuwepo kuhudhuria hafla hiyo.
 Unaona mambo yanavyochangamsha? ni Windhoek tu kwa kwenda mbele.
 Huwezi kuamini ilikuwa furaha kila kona.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Benedicta Rugemalira (kushoto) na mwanasheria wa kampuni hiyo, Respicius Didace (kulia) wakiwa na wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi walipohudhuria hafla hiyo.
Dk. Dee (kulia),  akiwa na madaktari wengine katika hafla hiyo.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

Tuesday, July 7, 2015

NASSAR APATA AJALI MBAYA YA HELKOPTA,AKIMBIZWA HOSPITALI YA SELIAN ARUSHA KWA MATIBABU

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar amepata ajali mbaya ya Helkopta na sasa amekimbizwa hospitali ya Selian Arusha kwa ajili ya kupatiwa matibabu pamoja na Rubani ya ndege hiyo.

MTANGAZA NIA UBUNGE LUDEWA AANGUKIA PUA NAFASI YA NEC ,ASEMA HATAKI TENA KUGOMBEA

Aliyeshindwa ujumbe wa NEC Ludewa Injinia Zephania Chaula  akiangana na mbunge  Deo  Filikunjombe baada ya  kushindwa katika nafasi  hiyo ,Chaula alikuwa ni mmoja wa wana CCM waliokuwa  wakitaka kuwania ubunge jimbo la Ludewa

 Mkuu  wa wilaya ya  Ludewa Antonia Choya akimkabidhi  hati ya  shukrani mbunge wa Ludewa  Deo Filikunjombe (kushoto)
 Mjumbe  wa  mkutano huo Bw  Choya  akipiga  kura.
 Wajumbe  wakishiriki  kupiga  kura.
 Wajumbe  wakishiriki  kupiga kura
 Mgombe  Chaula  akishukuru kwa  kushindwa
 Injinia  Chaula  akimpongeza mshindi mzee Nkwera.
Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  akipiga  kura  kumchangua mjumbe wa NEC Ludewa

Na MatukiodaimaBlog
 
MBIO za  ubunge jimbo la  Ludewa  mkoani  Njombe zimeishia hewani  kwa
mtangaza  nia wa  wanafasi  hiyo Injinia  Zephania  Chaula  baada ya
kuambilia  kura 11 pekee katika nafasi ya mjumbe  wa Halmashauri  kuu (
NEC) Taifa kutoka  wilaya ya Ludewa  aliyokuwa akiwania dhidi ya katibu
msaidizi  wa mbunge wa  jimbo la Ludewa  Hilaly  Nkwera  aliyeibuka
mshindi kwa  kupata  kura 138 kati ya  kura  zote halali 151 zilizopigwa .

Huku mgombea  huyo aliyeshindwa katika nafasi hiyo ya Ujumbe wa NEC Injinia Chaula  akiapa  kutogombea tena nafasi hiyo kwa
madai kuwa ni mara ya pili sasa anashindwa  vibaya  katika  mchakato 
wa  kuwania nafasi hiyo ambapo awali alishindwa mgombea  wa darasa  la 
saba marehemu Elizabeth Haule .

Uchaguzi
huo  mdogo  wa  kuziba nafasi ya  mjumbe  wa  NEC  iliyoachwa  wazi na
aliyekuwa  mjumbe wa nafasi hiyo Elizabeth Haule  aliyefariki  dunia
mapema mwaka  huu ,ulifanyika  mwishoni mwa  wiki  hii kwa
kuwashirikisha  wagombea  hao  wawili kabla ya mgombea  mwingine ambae
ni mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo  Filikunjombe  kuandika barua ya
kujitoa katika  kinyang’anyiro  hicho akiwapisha wagombea  hao
wachuane  kutokana na yeye  kudai  kuwa atachukua fomu ya kugombea tena
ubunge  wa  jimbo  hilo la Ludewa .

Akitangaza
matokeo  hayo ya  uchaguzi msimamizi  mkuu  wa uchaguzi huo  Lucas
Nyanda  ambae ni katibu  wa  jumuiya  ya  wazizi wa CCM mkoa  wa Njombe
,alisema  kuwa  jumla ya  wajumbe  waliopaswa  kushiriki katika
uchaguzi  huo ni 164 ila   wajumbe  halali  walioshiriki ni 151 na kati
ya  wajumbe  hao kura 2  ziliharibika  huku Injinia Chaula akipata  kura
11 na mshindi wa nafasi hiyo Bw  Nkwera  akipata  kura 138
 
Awali
mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Bw  Filikunjombe  ambae alikuwa ni mmoja
kati ya  wana CCM watatu  ambao majina  yao yalirejeshwa  kuwania
nafasai hiyo alisema  kuwa analazimika  kujitoa katika  nafasi hiyo
ili  kupisha wanachama  hao wawili  ambao wamemzidi  umri  ili  kuweza
kupambana  na  yeye ataendelea  kuwa kuwatumikia  wananchi  wa Ludewa
katika nafasi ya  ubunge pekee.


Akiwashukuru wajumbe
kwa ushindi  huo  wa nafasi ya ujumbe wa NEC Bw  Nkwera ambae
kitaaluma ni mwalimu na pia amepata  kuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Ludewa na mwenyekiti wa madiwani wa mkoa wa Njombe na Iringa
alisema kuwa
amefurahishwa na imani  kubwa ambayo wana CCM wameionyesha  kwake  kwa
kumchagua  kuwa mwakilishi wao katika vikao  vya  kitaifa .

Bw
Nkwera  alisema wana CCM Ludewa waamini  kuwa nafasi hiyo hawajakosea
kumpa na kamwe  hatawaangusha kwani atahakikisha anawatumikia  vema
katika vikao  vya  juu kwa kuanza na  safari ya  kumpata mgombea wa
nafasi ya  Urais wa CCM ambae atakuwa ni chaguo la  wana CCM wote wa
Ludewa .
Huku
Chaula mbali ya  kuwashukuru kwa  kura  11 alizopata bado  alisema
kuwa hatakuwa tayari  kuendelea  kugombea tena kwani yawezekana kabisa
Mungu hajapenda  yeye  kuwa  kiongozi wa kisiasa bali ametaka  aendelee
kuwa mtaalam .
“Nasema haya
kutoka moyoni mimi ni mwanachama hai wa chama cha mapinduzi na nakipenda chama change
hivyo naahidi sitagombea tena katika maisha yangu nafasi hii ya UNEC  kutokana
na ukweli kuwa nahisi siasa inanikataa maana kila nikigombea nashindwa hivyo
ngoja nifanye kazi nyingine pia nampongeza  sana mshindi Mzee  Nkwera katika
utendaji wake ndani ya chama”,alisema Mhandisi Chaula

Wakati
huo  huo serikali  ya  mkoa  wa Njombe kupitia mkuu wa mkoa wa Njombe
Dr  Rehema Nchimbi imempongeza kwa  kumpa hati ya shukrani  mbunge  wa
jimbo la Ludewa  Bw  Filikunjombe kwa  ushiriki  wake  mkubwa katika
kufanikisha  mbio  za mwenge katika  mkoa  huo kwa kuwa mbunge  pekee
kushiriki  mbio  za mwenge na kuchangia vizuri .
 
Akikabidhi hadi  hiyo mbele ya  wajumbe wa mkutano wa Halmashauri  kuu , mkuu wa
wilaya ya Ludewa Bw.Anatory Choya aliweza kumtunuku hati hiyo ya  heshima mbunge wa
jimbo la Ludewa  Filikunjombe kwa kushiriki kimamirifu katika mbio za
mwenge wa Uhuru ndani ya mkoa wa Njombe.
Akitoa chetihicho Bw.Choya alisema kuwa kutokana na ushiriki alioufanya mh.Filikunjombe
katika mbio cha mwenge wa Uhuru mkuu wa mkoa wa Njombe na ofisi yake wameona
wampatie cheti cha heshima Filikunjombe kwani ni mbunge pekee aliyeshiriki
katika mbio hizo za Mwenge katika mkoa wa Njombe.

DIAMOND PLATNUMZ KUPAMBA MKUTANO MKUBWA WA JIMBO LA SINGIDA MJINI VIWANJA VYA PEOPLE'S CLUB

11101348_827429087339981_3431616584413911623_n