Pages

KAPIPI TV

Saturday, June 27, 2015

CHADEMA MOSHI VIJIJINI WARUDISHA FOMU ZA KUWANIA UBUNGE NA UDIWANI.

Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Moshi vijijini,Godlisen Maramia akipokea fomu kutoka kwa Deogratius Mushi ya kuwania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi vijijini wakati aliporudisha katika ofisi za chama hicho zilizopo Majengo.
Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Moshi vijijini ,Godlisen Maramia akimpongeza mtia nia Deuogratius Mushi kwa uamuzi wa kuingia katika kinya'ng'anyiri cha kuwania nafasi hiyo.
Mushi akipongezwa na makada wengine wa Chadema waliofika kumsindikiza ofisnini hapo.
Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Moshi vijijini,Godlisen Maramia akipokea fomu toka kwa Tally Kisesa ya kuwania Ubunge wa viti maalumu katika jimbola Moshi vijijini.
Mtia nia wa nafasi ya Udiwani katika kata ya Kindi,kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Michael Kirawira akirejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo katika ofisi ya Chadema kata ya Kindi.
Wananchi wa kata ya Kibosho Magharibi wakimlaki Mgombea wa nafasi ya Ubunge Deo Mushi ambaye pia ametangaza kuwania nafasi ya Udiwani katika kata hiyo.
Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi vijijini,Deogratius Mushi,akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuasili katika kata hiyo.
Deo Mushi ambaye pia ni mwenezi wa Chadema wilaya ya Moshi vijijini ,akizungumza na baadhi ya wananchi katika kata ya Kibosho Magharibi .
Baadhi ya wananchi waliohudhuria kikao hicho.
Deo Mushi akizungumza.
Mbali na kuwania nafasi ya Ubunge ,Deogratisu Mushi pia amerudisha fomu ya kuwania nafasi ya udiwani katika kata ya Kibosho Magharibi  na hapa akikabidhi kwa Mwenyekiti wa Chadema katika kata hiyo Kikas Mmasi.
Mwenyekiti wa Chadema katika kata ya Kibosho Magharibi Kikas Mmasi akizungumza katika kikao hicho mara baada ya kupokea fomu ya Deo Mushi.

Thursday, June 25, 2015

ADHA YA USAFIRI BARABARANI LEO HII

Gari lenye namba za usajili T 607 CVL likiwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara baada ya kuharibika
Leo hii asubuhi nikitokea Singida kwenda Dar kwa basi la Shabiby Line, lenye nambari za usajili T607 CVL iliondoka stendi ya Misuna Singida mnaomo saa 12.48(moja kasoro 12) za asubuhi. Safari ilikuwa nzuri mpaka gari ilipofika nje kidogo ya Manyoni kuelekea Dodoma mnamo saa 2.30 kwa muda wa sekunde chache mpaka dkk moja hivi ulisikika mlio usio wa kawaida ingawa dereva wa gari hilo aliendelea na safari huku nikijiuliza mlio huo ulikuwa wa kitu gani ghafla ukasikika mlio mkubwa sana kiasi cha kupelekea taharuki ndogo miongoni mwa abiria, hapo ndipo dereva akaanza kupunguza mwendo na hatimaye kusimama. Dereva na wahudumu wawili wa gari hilo wakateremka kwenda fuatilia kilichotokea. Lakini hawakurudi garini mpaka abiria wakaanza kuteremka toka garini ili kujua kulikoni. Nikiwa miongoni mwa abiria walioteremka hapo nje ya gari hatukukuta mtu yeyote baadaye dereva na wahudumu wakaonekana kama mita 500 kutoka ilipo gari wakiwa wamesimama. Baada ya kulikagua gari uvunguni ikaonesha kipande cha propela shaft kinakosekana. Hivyo tukaelewa kuwa hilo ndilo lililotokea, lakini mimi na abiria wenzangu tuliendelea kusimama pale nje ya gari kwa muda upatao nusu saa hivi bila dereva na wenziwake kurudi ilipo gari kuondoa sintofahamu hiyo. 

Waliendelea kubaki kule mpaka baadhi ya abiria walipoamua kuwafuata walipo. Ndipo wakatoa maelezo kuwa propela shafti ilichomoka na wameshawasiliana na ofisi zao za Dodoma na kuwa gari imetumwa kuja tufaulisha. 

Baada ya kukaa mpaka saa 5.30 bila gari kutokea toka Dodoma kutufaulisha, kitu kilichoanza kuleta jazba kwa abiria ambao walimweka kiti moto dereva ambaye alipata wakati mgumu sana kujibu maswali ya abiria wengi wakimshutumu kwa uzembe wa kutosikia mlio usio wa kawaida katika gari muda mfupi kabla ya kuharibika. 

Kabla ya dereva kuwekwa kiti moto baadhi ya abiria walijaribu kupiga simu katika moja ya namba iliyosemekana ni ya meneja wa kampuni hiyo ya Shabiby Line lakini hawakupata majibu ya kuridhisha kitu kilichopelekea jazba miongoni mwa abiria.

Hali iliendelea kuwa ya sintofahamu mpaka saa  6 mchana dereva wa gari hiyo alipokuja na kusema kuwa hakuna gari toka Dar itakayofika pale porini ila kuna Hiace na Coaster zimekodiwa kutusogeza Dodoma ambako tumea ahidiwa gari itatuchukua kuendelea na safari ya Dare es Salaam, ambako badala ya kufika saa 9 mchana sasa tutafika Dar saa 3 usiku. 

Kibaya zaidi kuna watu ambao mwisho wa safari zao si Dar tu bali pamoja na Zanzibar, Bagamoyo na kwingineko ambao sasa hawatoweza kwenda leo. 

Adha hiyo pia imenikuta mimi mwandishi wa habari hii ambaye kwenda kwangu Dar es Salaam ni kuipokea familia yangu inayowasili leo toka nchini Uingereza ambao sijaonana nao tangu mwaka 2010, kwa bahati mbaya kwangu nilimwahdi mwanangu mdogo Ndisha kuwa ningekuwepo Airport kuwapokea hili sasa halitowezekana kwani ndege iawasili Dar saa 3 usiku muda ambao unatarajiwa basi tutakalopanda lifike Ubungo.

Maoni ya abiria wengi wameilaumu kampuni hiyo kubwa ya usafiri wa abiria kwa kutokuwa na mipango mizuri hasa katika mawasiliano na abiria hasa gari linapoharibika. 

Leo iliwachukua staff wa gari hilo nusu saa kuwaeleza abiria tatizo liliotokea na mipango ya kujikwamua toka porini kukiwa hakuna huduma yeyote na gari likiwa na abiria watoto na mchanga mmoja. 

Ni juu ya utawala wa Kampuni ya Shabiby kuelimisha wafanaykazi wake kuwa na lugha za ki staarabu kwa wateja wao.

Baadhi ya abiria wakiwa wamelala juu ya mawe bila shaka kwa njaa.
Dereva wa gari hilo katikati akiwa kajiegesha katika jiwe 
Baadhi ya familia zenye watoto katika msafara huo uliokwama Sukamahela
Tumekwama! abiria wakijadiliana la kufanya!
Hapa ndipo kipande cha nyuma cha proprla shafti kilipochomoka
Ubovu kama huu inaelekea si wa siku moja, bila shaka gari hii haijafanyiwa uangalizi kwa kipindi kirefu jambo ambalo ni hatari kwa abiria na waliomo garini.
Tukifaulishwa.

Ndani ya Hiace

Basi la Shabiby likwa tupu baada ya abiria kufaulishwa baada ya masaa mengi ya sintofahamu

Picha na habari na Mkala Fundikira Dodoma

DR.KIGWANGALLAH APATA WADHAMINI TABORA MJINI NA NZEGA AWATAKA WANANCHI KUKUBALI MABADILIKO

Mbunge wa Jimbo la Nzega Dr.Hamisi Kigwangallah akizungumza na baadhi ya wakazi wa Tabora mjini wakati wa kutafuta wadhamini kuomba ridhaa kwa Chama chake CCM kumteua kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika Uchaguzi mkuu wa mwaka huu
Dr.Kigwangallah akisaini vitabu vya wageni ofisi ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini muda mfupi mara baada ya kuwasili na kupokea Sahihi na majina ya wanachama wa CCM waliojitokeza kumdhamini.

Dr.Kigwangallah akionesha fomu ya majina ya watu waliojitokeza kumdhamini kwa ajili ya kuomba ridhaa kwa CCM imteue kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baadhi ya viongozi wa CCM Tabora ngazi ya wilaya na mkoa

Moja kati ya vikundi vya wasanii ambavyo ambavyo vilifanya onesho wakati wa mkutano wa Dr.Kigwangallah alipokuwa akizungumza na wananchi katika ofisi za CCM  Tabora mjini.

Dr.Kigwangallah akicheza ngoma ya asili ya Waswezi
Dr.Kigwangallah akisalimiana na wananchi waliokuwa wamemzunguuka ambapo wananchi hao walijawa na shauku angalau ya kumsalimia kwa kumshika mkono







TANGAZO LA MSIBA TANZANIA NA MAREKANI

DR. ALI MZIGE wa Mikocheni, Dar es salaam anasikitika kutangaza kifo cha Dada yake MRS MARIAMU -MWAJUMA MUSISA (NEE MZIGE) kilichotokea Raleigh, North Carolina Marekani tarehe 21-06-2015. Mwili wa marehemu utaletwa Tanzania kwa ajili ya mazishi.
Tutatoa taarifa zaidi mwili utakapowasili. Kwa mawasiliano tafadhali mpigie Yussuf Mhiro 0754-609-338 / 0714-979-014.Usoma taarifa hii tafadhali wajulishe ndugu jamaa na marafiki wa Ukoo wa Humbi Ziota na Musisa. Au Kaka wa Marehemu DR. ALI A. MZIGE 0713 410 531, 0754 495 998.
Inna Lillahi, wa inna ilaihi ra'ajiun.

Wednesday, June 24, 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU UKUMBI WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM LEO


Rais Jakaya Kikwete akihutubia wakati akifungua Kongamano la nne la Kimataifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam leo asubuhi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi inayojishughulisha na Utafiti wa Sayansi ya Jamii (REPOA), Profesa Samuel Wangwe akitoa hutuba  mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa kongamano hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, (COSTECH), Dk.Hassan Mshinda akizungumza katika uzinduzi huo.
Rais Jakaya Kikwete (katikati), akiwa meza kuu na viongozi wengine. Kulia ni Waziri wa Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbawara na Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Kanali mstaafu Joseph Simbakalia.
Wadau wa masuala ya sayansi wakiwa kwenye kongamano hilo.
Wadau wa masuala ya sayansi wakiwa kwenye kongamano hilo.


Wanahabari wakiwa kwenye kongamano hilo la kimataifa.

Kongamano likiendelea

Na Dotto Mwaibale

RAIS Jakaya Kikwete amesema Serikali itaendelea kuwekeza kwenye watafiti na wabunifu ili kuliletea taifa maendeleo na kuleta mapinduzi ya viwanda ili kufikia uchumi wa kati ulioimara ifikapo mwaka 2025.

Pia imeelezwa kuwa utafiti unanafasi kubwa sana katika kulinufaisha taifa kwasababu kama hakuna ubunifi na utafiti hakuna sekta itakayoendelea nchini.

Rais  Jakaya Kikwete ameyasema hayo Dar es Salaam leo asubuhi wakati akifungua kongamano la nne la watafiti na wabunifu wa sayansi na teknolojia .

Kikwete alisema hakuna nchi yoyote duniani ile iliyoendelea bila kuwa na watafiti pamoja na wabunifu katika masuala ya sayansi na teknolojia kuiwekeza kwe watafiti kunalipa.

''Tunapozungumza mapinduzi ya viwanda ambayo yanatupeleka kwenye uchumi wa viwanda ulioimara mwaka 2025 ni lazima tufikirie kuwa na wataalamu na wanataaluma ambao ni watafiti na wabunifu ili kujenga miondombinu ya viwanda''alisema.

Alifafanua kuwa viwanda ambavyo vinaanzishwa na kuendelezwa katika karine hii ni viwanda vya kisasa ambavyo vinahitaji teknolojia na ubunifu wa kiwango cha juu na kama hakuna wataalamu itakuwa ni kazi bure.

Kikwete alisema anashukuru kufanya maamuzi mazito katika kipindi chake cha uongozi kwa kuhahakikisha anaendeleza sekta ya sayansi na teknolojia kwa kuongeza bajeti ya fedha katika kitengo cha utafiti.

''Naamini Rais atakayenibadili ataendeleza juhudi hizi na kuweza kujenga nchi yenye uchumi imara kwa kuhakikisha watafiti wanaendelezwa kwajili ya mapinduzi ya viwanda nchini kwasababu hatuendelea kwa kununua kwa wenzetu lazima na sisi tutengeneze na tuuze nje ili kuingiza mapato''alisema.

Alifafanua kuwa kwa kipindi cha miaka ya 2010 hadi 2005 kitengo cha utafiti kilikuwa kinapangiwa bajeti ya  shilingi milioni 35 ambazo zilikuwa hazikidhi mahitaji.

''Nilivyona hivyo niliangiza waziri husika kupandisha kiwango hicho ili kuwapa watafiti nafasi ya kufanya kazi zao kwa umakini na sasa kitengo kinapewa bilioni 10''alisema.

Kikwete alisema matokeo ya jitihada za kuwaendeleza watafiki zimeshaanza kuonekana huku akimtolea mfano mtafiki aliye gundua dawa ya ugonjwa wa kuku wa mdondo kwamba yeye peke yake ameweza kuliingizia taifa sh. bilioni 186.


''Mbali na hilo alisema hadi sasa watu wapatao 517 wamenufaika kwa kufadhiriwa na kusoma masomo ya sayansi ya utafiti kwa ngazi ya shahada ya udhamivu watu 344 na phd watu 175'' alisema.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba-0712-727062)

DENMARK YAIMARISHA SEKTA YA UTAMADUNI NA UBUNIFU TANZANIA.

PROGRAMU mpya za utamaduni na ubunifu zinatoa fursa kubwa ya uanzishaji  wa shughuli za kitamaduni zenye kuimarisha sekta ya ubunifu wenye mwelekeo kiuchumi.
Balozi wa Denmark nchini Tanzania,Bw. Johnny Flentoe akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa program mpya ya CKU.
 
Kwa mujibu wa balozi wa Denmark nchini Tanzania,Bw. Johnny Flentoe, amesema kwamba Tanzania inautajiri mkubwa wa kiutamaduni ambao unaweza kutumiwa kuchangia pato la taifa GDP.

 “Bado tasnia ya sanaa na ubunifu ambayo ingeliweza kuchangia katika uchumi na kuwapatia kazi vijana haijatumika ipasavyo. Kutokana na hilo kipaumbele cha programu hii mpya ni kuwezesha vijana kutumia sanaa na ubunifu kukuza ajira,” anasema balozi Johnny Flentoe.
Mshairi Jasper Sabuni akifanya kazi ya 'spoken words' wakati wa uzinduzi wa program mpya ya CKU.

Juni 5, 2015, Ubalozi wa Denmark ukishirikiana na Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Denmark (CKU) umezindua program mpya ya utamaduni na  maendeleo Tanzania ( Tanzania Culture and Development Programme ).

Programu hiyo imelenga kutengeneza fursa za kiuchumi kupitia jukwaa la sanaa na ubunifu ambapo watanzania watajipambanua kupitia kushiriki shughuli mbalimbali za kitamaduni na kujipatia kipato.
Baadhi ya wadau waliofika kwenye uzinduzi wa program mpya ya CKU Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja
CKU inatekeleza program hiyo kupitia kwa washirika wake likwemo Tamasha la Kimataifa la Filamu (Zanzibar International Film Festival (ZIFF), kupitia mradi wao wa Village Panorama ambao unalenga kuonyesha filamu za kuelimisha maeneo ya vijijini huko Zanzibar.

Taasisi nyingine ni Culture and Development in East Africa (CDEA), ambao watafanya utafiti wa namba sanaa ya muziki na filamu inavyochangia katika pato la taifa, wakati taasisi ya Soma Book Café ikiindesha mashindano ya uandishi na usomaji wa vitabu.

Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wao watanufaika na program hiyo kwa kupatiwa vifaa vya muziki vya kufundishia huku Nafasi Art Space ambacho ni kituo cha sanaa kikiboreshwa na kupata uwezo wa kutumika kama kituo kikubwa cha sanaa za maonesho.  
Meneja wa CKU Afrika Mashariki, Christoph Lodemann akitoa maelezo mafupi juu ya program mpya ya Tanzania




“Sanaa ina uwezo mkubwa wa kuwezesha majadiliano na kupaza sauti ya umma. Ndio maana Denmark inawezesha kuwapo kwa jukwaa ili wananchi waweze kujieleza wenyewe kupitia sanaa. Kwa kukuza vipaji vya wasanii wapya nchini Tanzania, Denmark inatoa mchango wake mkubwa kwa wasanii na wabunifu,”  anasema meneja wa CKU Afrika Mashariki Christoph Lodemann.

Denmark inawezesha shughuli za sanaa,utamaduni  na ubunifu wa kisanii nchini Tanzania kama mchango wake katika juhudi za kukuza uchumi wa taifa hili.