Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimwelekeza Mkurugenzi wa kampuni ya Events World, Dimo Debwe Mitiki, jinsi ya kuwasilisha maoni yake kuhusiana na kazi za Umoja wa Mataifa na nini angependa Umoja huo ufanye zaidi kwa ajili ya watanzania kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”. (Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimwelekeza mmoja wa wananchi aliyetembelea la Umoja huo jinsi ya kuwasilisha maoni yake kuhusiana na kazi za Umoja wa Mataifa na nini angependa Umoja huo ufanye zaidi kwa ajili ya watanzania.
Laurean Kiiza (kushoto) kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), akimsimia Meneja mwendeshaji wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige kuwasilisha maoni (GeoPoll) yake moja kwa moja kwenye simu ya kiganjani, alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya sabasaba yanayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam.
Mdau wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Lemmy Hipolite (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi na Meneja mradi wa TUBEGA ART ambaye ni mtaalamu wa sanaa za uchoraji, Amos Mtambala, jinsi alivyowezeshwa na Umoja huo kupitia Shirika la Kazi Duniani (ILO) kupata elimu inayomwezesha kuwa mjasiriamali kwa kuuza michoro hiyo ndani ya banda la Umoja wa Mataifa.
Mkurugenzi na Meneja mradi wa TUBEGA ART ambaye ni mtaalamu wa sanaa za uchoraji, Amos Mtambala, akionyesha baadhi ya kazi zake kwa wananchi waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akitoa maelezo ya maeneo mbalimbali yaliyofanikiwa katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDAP) kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa na kutaka kufahamu shughuli mbalimbali za UN Tanzania.
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimkabidhi makabrasha na vipeperushi mbalimbali vya Umoja Mataifa, Mwandishi wa Michuzi blog, Chalila Kibuda aliyetembelea banda hilo kwenye maonyesha ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Sophia Mataro (wapili kushoto) kutoka Shirika la UNESCO Tanzania, akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini kwa mmoja wa wananchi alitembelea banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”.
Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na kituo cha Televisheni cha Channel Ten kilichotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba yanaoendelea kutimua vumbi jijini Dar es Salaam.
Timu ya wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa "Delivering as One" wanaotoa huduma kwenye banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara kimataifa maarufu kama “Sabasaba” yanayoendelea kurindima jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa nje wa banda la Umoja wa Mataifa lililopo Karume Hall katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.
Na Modewji blog team
Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania limetoa nafasi ya kipekee kwa watanzania kutoa maoni yao wakati wa kipindi hiki cha maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam, yaliyoanza kurindima Juni 28, huku wakikusanya maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi juu ya utendaji wake kwa wanaotembelea kwenye maonyesho hayo kila siku.
Aidha, katika kupokea maoni hayo, UN imeweka utaratibu wa moja kwa moja kwa wananchi kufika kwenye banda lao na kutoa maoni yao, ambayo yanaenda moja kwa moja kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Nchini Alvaro Rodriguez.
Njia nyingine ya kuwasilisha maoni ya moja kwa moja ni kupitia mtandao wa (Online) kwa kuingia http://gpl.cc/UN2
Kupitia linki hiyo, mtumiaji anaweza kutumia simu yake ya smartphone, laptop na vifaa vingine vya kielektroniki.
Njia nyingine ni ya kutumia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055.
Na kwa njia ya tatu ni kuwasilisha namba ya simu na majina na ujumbe unaotaka na UN wataufanyia kazi.
Aidha, maoni hayo yatakuwa yakipokelewa kwa kipindi chote cha SabaSaba, hivyo wananachi wameombwa kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao ya nini UN wakifanye nchini pamoja na mambo mengine.