Pages

KAPIPI TV

Saturday, August 13, 2016

WARSHA YA KIMATAIFA KUHUSU MPANGO WA TAKWIMU ZA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk. Aziz Ponary Mlima akihutubia kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi wakati akifungua warsha ya kimataifa kuhusu mpango wa takwimu za malengo ya maendeleo endelevu uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Alibina Chuwa (kushoto), akihutubia katika warsha hiyo.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaban (katikati), akipitia nyaraka kwenye warsha hiyo. Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. 
Warsha ikiendelea.
Wadau wa maendeleo wakiwa kwenye mkutano huo.

Wadau wakifuatilia mada kwenye warsha hiyo.

Wanahabari wakiwa kwenye warsha hiyo.
Warsha ikiendelea.
Taswira ya meza kuu kwenye warsha hiyo. Kutoka kulia Dk. Verena Knippel, Mratibu wa Shirika la Global Partinership, Sanjeev Khagram, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk.Alubina Chuwa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk. Aziz Ponary Mlima, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaban, na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. 

Thursday, August 11, 2016

SHULE ZA FEZA HAZITAFUNGWA

                                                          Na Dotto Mwaibale

UONGOZI wa  Shule za Feza nchini umeibuka na kukanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii,  kuwa wao  hawana uhusiano na  Fethullah Gulen wala serikali ya Uturuki  kwa vile   hawajawahi kupokea misaada toka pande hizo mbili za uendeshaji na kuwa shule hizo hazitafungwa.

Kauli hiyo imetolewa baada ya hivi karibuni kuenea kwa uvumi kuwa shule za Feza  zipo hatarini kufungwa kwa madai kuwa  mmiliki wake ni yule aliyejihusisha na jaribio la kuipindua serikani nchini Uturuki.

Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hizo, Habibu Miradji aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanahabari Kawe jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Alisema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa Shule za Feza ni kama asasi  zingine zilizosajiliwa kishera na serikali, hivyo ni mali ya watanzania.

“Shule za Feza zitabaki kuwa kiwanda  cha kuzalisha wazalendo wa kitanzania  na raia bora wa duniani, hivyo wazazi wanapaswa kuondoa hofu,” alisema.

Alisema toka mwaka 1995 shule hiyo imepata mafanikio ya kujenga shule za awali tatu, shule za msingi mbili, sekondari tatu na shule ya kimataifa moja.

Aliongeza kuwa  huo ni uwekezaji  wenye mchango katika kukuza pato la taifa, kutoka awamu ya pili, tatu, nne hadi awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.
\Alisema shule ya Feza ni hazina kwa Tanzania kwani shule zake zimekuwa zikishika nafasi ya 10 bora toka mwaka 2004 hadi leo.

Alisema  wanatoa  wito kwa wazazi  kuwasiliana na uongozi wa shule hiyo  kujua kinachoendelea kwenye shule husika kwa manufaa ya wanafunzi wetu na taifa bila kusikiliza uvumi huo unaoenezwa na watu wasiopenda maendeleo ya shule hizo.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

UHARIBIFU KATIKA VITUO VYA MABASI YA MWENDO KASI JIJINI DAR WAENDELEA KUFANYIKA KILA SIKU

Ikiwa ni Takribani miezi michache kupita tangu mabasi ya mwendo kasi yaanze kufanya kazi kwa ufanisi mzuri, kumekuwa na mambo kadha wa kadha yakiendelea ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa miundombinu ya vituo hivyo vya mabasi hayo.

Hili limeonekana bila chenga Morogoro Road ambapo kipande cha kutokea Jangwani mpaka Manzese kikionesha wazi  vifaa vya kuhifadhia taka vimeharibika, huku vingine vikionekana kuchomolewa, kupinda, na kulegea. 

 Swali la kujiuliza hapa ni kwamba kwa jinsi miundombinu hii ilivyo kaa  ni ngumu sana hata mtu kugonga kwa mguu sasa inakuwaje inaharibika kiasi hiki?
Hapa upande wa kulia ukionekana kuwa kifaa cha kuhifadhia taka kilisha chomolewa na kubakiza mfuniko tuu na papo hivi kwa zaidi ya mwezi sasa.
Hapa Kifaa cha kuhifadhia taka taka kikiwa kimepinda haijulikani kiligongwa au kuna watu walikuwa wanataka chomoa.
Hiki kikiwa kimelegea kabisa amambapo muda wowote litachomoka
Hapa mfuniko ndio ulisha potea tena
Hili nalo tayari linaelekea kudondoshwa chini
Hii hapa ndio funga kazi kabisa yani wamesha chomoa muundo mbinu wote wa kushoto 

Picha na Fredy Njeje

VIJANA NCHINI WAPEWA ELIMU KUHUSU KUJIHUSISHA NA SHUGHULI ZA MAENDELEO.



Kuelekea kilele cha siku ya vijana duniani, vijana mbalimbali nchini wamekutanishwa kwa pamoja na kupewa elimu jinsi wanavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha pamoja na kukamilisha Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs).

Akizungumza katika kongamano hilo mgeni rasmi ambaye ni Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA), Christine Mwanukuzi-Kwayu, aliwataka vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kusaidia kubadilisha maisha yao binafsi na kwa taifa.
Mgeni rsmi katika kongamano hilo Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA), Christine Mwanukuzi-Kwayu akizungumza na vijana.

Alisema vijana wengi wamekuwa hawajihusishi na mambo ya maendeleo na hivyo ni wasaa sasa na wao waanze kujihusisha ili waweze kuchangia kuleta maendeleo katika taifa kwani hata takwimu kwa sasa zinaonyesha vijana wanashiriki kwa kiasi kidogo kutokana na wengi wao kutokuwa na ujuzi.

"Vijana hivi mnajua kama nyie ndiyo mnatarajiwa kuongoza taifa lakini bado mmelala hata katika uchunguzi uliofanyika unaonyesha vijana asilimia nne ndiyo wanajihusisha kwa karibu na shughuli za maendeleo kwa nchi yetu ila wengi mnakuwa hmajui," alisema Mwanukuzi-Kwayu.

Nae Meneja Miradi wa Shirika la Restless Development Bw. Oscar Kimaro amesema kuwa matatizo wanayoyapata vijana duniani yanatokana na kutokua na ushirikishwaji wa vijana katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika nchi.
Meneja Miradi wa Shirika la Restless Development Bw. Oscar Kimaro akiwapa vijana njia za kupata mafanikio na kuwaeleza mambo ambayo yanachangia wao kushindwa kufikia malengo.

“Changamoto zinazomkabili kijana nchini Tanzania ndio hizo hizo zinazoweza kumkabili kijana nchi nyingine, lakini haya yote hutokana na kutoshirikishwa kwa vijana katika sekta mbalimbali za uzaliashji na za kimaendeleo chini,” alisema Oscar

Na Hashimu Ibrahim
Mtendaji Mkuu wa Chama cha Vijana wa Shirika la Umoja wa Mataifa (YUNA), Arafat Bakar akitoa burudani kwa vijana waliohudhuria kongamano hilo.
Baadhi ya vijana waliohudhuria kongamano hilo.

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

WADHAMINI WARUDISHA HADHI YA SHINDANO LA MISS TANGA 2016


 Miss Tanga 2016, Eligiva Mwasha akiwapungia mikono wananchi waliojitokeza kushuhudia shindano hilo mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi
 Miss Tanga 2016, Eligiva Mwasha akiwapungia mikono watazamaji waliojitokeza akiwa na mshindi wa pili na tatu katika Shindano hilo ambalo liliandaliwa na Radio Tanga Kunani (TK) na Hotel ya Tanga Beach Resort.
Warembo walioingia tano bora wakiwa jukwaani

Kamati ya Miss Tanzania nao walikuwepo wakifuatilia shindano hilo ambalo lilifanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort mjini Tanga.

 Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akizungu mza wakati wa shindano hilo
Msanii Nevy Kenzo akitumbuiza wakati wa shindano la kumtafuta mlimbwende wa mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016)lililofanyika hivi karibuni kwenye hotel ya Tanga Beach Resort
WAKATI shindano la kumsaka malkia wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016)likifanyika mwishoni mwa wiki na hatimaye mrembo Eligiva Mwasha kuibuka na ushindi kwenye kinyang’anyiro hicho dhidi ya washiriki wengine 10.
 

Shindano hilo ambalo lilisimama kwa muda baada ya serikali
kulisimamisha lile la Taifa msimu huu lilionekana kuwa na msisimuko wa hali ya juu kuanzia wapenzi,wadau na washiriki iliyochangiwa na waratibu wa shindano hilo Radio ya Tanga Kunani FM (TK) wakishirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort.

 

Ushindani wa washiriki hao ulianza kuonekana tokea wakati warembo hao wakiwa kwenye kambi yao ambayo ilifanyika kwenye hotel hiyo ambapo kila mmoja alionekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kuondoka na taji hilo.
 

Hali iliendelea kuwa ya mvutano zaidi baada ya baadhi ya washiriki
kuaga mashindano hayo na kutoa fursa yaw engine kuingia nafasi ya tano bora katika kinyanganyiro hicho ambacho kilihudhuriwa na wapenzi wengi kuliko kawaida.

 

Kitendo hicho kinaonekana kinawezesha kurudisha hamasa na heshima ya shindano hilo ambalo hufanyika kila mwaka mkoani hapa lakini pia kuhamasisha hasa vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki msimu ujao.
 

Katika shindano hilo nafasi ya pili ilichukuliwa na Aisha Ally huku
nafasi ya tatu ikitwaliwa na Rukaiya Hassani katika shindano hilo
ambalo lilikuwa na ushindani mkubwa kutokana na kusheheni warembo wakali.

 

Halikadhalika nafasi ya mrembo kwenye kipaji katika shindano hilo
ilinyakuliwa na Edna Chisabo ambapo kinyang’anyiro hicho kilifanyika siku moja kabla ya onyesho la kumsaka mrembo wa mkoa huu  kwenye ukumbi wa Tanga City Lounge uliopo mjini hapa.

 

Licha ya kufanyika shindano hilo lakini yapo mambo ambayo kimsingi yameweza kuleta msisimuko na kulifanya kuonekana kuwa na ubora wa hali ya juu.
 

Mambo hayo ndio yamechangia kwa asilimia kubwa kupelekea shindano hilo kuwa na mvuto mkubwa kuliko mashindano mengine ambaye yalikwisha kufanyika mkoani hapa lakini pia uwepo wa  watazamaji wengi.
 

La kwanza ni eneo ambapo onyesho hilo limefanyika,moja kati ya mambo ambayo yalichangia kuonekana kuwa na mvuta mkubwa ilitokana na shindano hilo msimu huu kufanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort.
 

Tunasema hivyo kwa sababu kila mtu anapokwenda kuangalia burudani ya aina yoyote lazima aangalia ulinzi na uimara wa eneo husika hasa ukizingatia wapo baadhi yao huenda na vyombo vyao vya usafiri.
 

Kama ujuavyo ulinzi wa mahali husika ndio huwafanya watu kwenda kupata burudani lakini pia ni eneo tulivu ambalowatu wanaweza kufanya mambo yao kila kupata usumbufu wa aina yoyote.
 

Jambo hilo limesababisha baadhi wa watu kuacha kwenda kwenye maeneo yaliyopo karibu nao na kwenda maeneo mengine ya mbali kwa ajili yakusaka utulivu lakini pia ulinzi.
 

Jambo jingine ambalo lilisababisha onyesho hilo kuwa bora ni uwepo wa warembo makini na wenye muonekana bomba na hivyo kupelekea wapenzi na wadau wao kujitokeza kwa wingi kushuhudia mtanange huo ambao ulikuwa wa aina yake.
 

Kilicholifanya shindano hilo kuendelea kuvutia wapenzi na mashabiki ambao walijitokeza  ni wasanii ambao walikuwa wakitumbuiza kabla ya kuanza.
 

Wasanii wanaounda kundi la Nevy Kenzo wazee wa Kamati Chini ilikuwa ni kichocheo kikubwa cha umati mkubwa wa wadau wa tasnia ya urembo na burudani kujitokeza kwa wingi kushuhudia shindano .
 

Nevy Kenzo ambao walipanda jukwaani kutumbuiza walisababisha ukumbi mzima kulipuka kwa shangwe na nderemo huku baadhi yao wakiimba nyimbo zao ikionyesha namna wanavyokubalika.
 

Nevy Kenzo wakati akiimba ilifikia wakati mpaka wapenzi na mashabiki wa tasnia ya urembo waliviona viti vyao vya moto na kulazimika kupanda jukwaani kucheza sambamba na wasanii hao.
 

Haikuishia hapo lakini wasanii ambao walipanda jukwaani kabla ya Nevy Kenzo kutumbuiza wa Kundi la Wazenji Classic lenye makazi yake mjini Tanga walikuwa na moto na kusababisha shangwe  kila mahali.
 

Shangwe hizo zinaonyesha namna kundi hilo lilivyoweza kujizolea
umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanga hasa kwa kipindi kifupi kutokana na aina ya mziki ambao wanaufanya staili ya mduara na bongo fleva.

 

Sababu kubwa ya kuona kundi hilo kuonekana litakuwa hatari ni namna wanayoweza kulitawala jukwaa wanapokuwa stejini na kuonekana kuinua mara kwa mara wapenzi na mashabiki wao
 

Suala jingine ambalo lilikuwa kivutio kikubwa ni namna warembo
walivyokuwa wakipanda jukwaani na kuanza kujitambulisha na kujielezea kwa watazamaji.

 

Hali hiyo ilisababisha wakati mwengine baadhi ya warembo kupanda jukwaani kwa madoido makubwa kwa lengo la kuonyesha umahiri wao ili kuwashawisha majaji kuwapa alama nzuri.
 

Mbunge wa Jimbo la Tanga atinga Miss Tanga. 
Kitendo cha Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF)Mussa Mbaruku kuhudhuria shindano la kumsaka mlimbwende wa mkoa wa Tanga mwaka huu kilionyesha namna alivyokuwa kiongozi mpenda michezo na kuithamini.

Mbunge huyo ambaye alikuwa kwenye shughuli zake za kikazi lakini alilazimika kuungana na wakazi wa jimbo lake kumshuhudia mrembo ambaye anapatikana.

Akizungumza mara kabla ya kutangaza mshindi wa Taji la Miss Tanga 2016,Mbunge Mussa alisema tasnia ya urembo imekuwa ikiwapa vijana maisha mazuri lakini pia imekuwa ni daraja la wao kupata mafanikio

Alisema lazima watanzania ikiwemo wazazi kubadilika na kuondokana na dhana ya kuwa  ya kuwa urembo ni suala la uhuni kwani imekuwa ikisaidia vijana wengi kupata maendeleo.
 
 "Ndugu zangu lazima tubadilike na kuishi kutokana na utandawazi
uliopo ile dhana ya kuwa urembo ni uhuni mimi nadhani imepitwa na wakati na uhuni mtu anaweza kuwa nao hata asiposhiriki mashindano hayo hivyo wazazi na walezi ruhusuni watoto wenu washiri kwenye mashindano haya "Alisema.

Mussa alisema kuwa anaamini washindi wa shindano hilo wataweza
kuuwakilisha vema mkoa wa Tanga kwenye mashindano ya Kitaifa na kuweza kushinda kama walivyofanya kwenye onyesho hilo.
  
“Ninaimani kubwa na washindi ambao wamepatikana kwenye shindano hilo wanaweza kuwa chachu ya mabadiliko kwenye tasnia ya urembo mkoa huu kwani wanaweza hata kuleta taji la Miss Tanzania msimu huu “Alisema.

"Neno la Mshindi wa taji la Miss Tanga 2016 Eligiva Mwasha" Alisema kuwa kwanza anawashukuru wakazi wa Mkoa wa Tanga  kwa ujumla kwa sapoti yao walionyesha katika  fainali za miss tanga 2016 na yeye kupata fursa ya  kunyakua taji hilo

Licha ya kuibuka na ushindi lakini niwaombe niombea kwani kwa sasa safari aliokua nayo bado kubwa sana kwani anamtihani  wakwenda kuiwakilisha Tanga katika fainali za Miss Kanda  na  badae kulekea Katika fainali za miss Tanzania baadae mwaka huu.

MGODI WA BUZWAGI WAKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 700 KWA HALMASHAURI YA KAHAMA.

  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya mji wa Kahama, hafla hiyo ilifanyika baada ya kukamilika kwa hafla ya kukabidhi madarasa ya shule ya msingi Budushi na nyumba za walimu Mwime.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakishuhudia wakati wa hafla ya makabidhiano ya hundi
Mbunge wa Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kishimba akihutubia wananchi wa Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 700
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Asa Mwaipopo akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu wakati wa makabidhiano ya hundi ya malipo ya huduma. 
  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akihutubia wananchi wa Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma
Baadhi ya wananchi katika wilaya ya Kahama wakishuhudia makabidhiano hayo.

Na Dixo Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.


Mgodi wa Buzwagi umekabidhi wa halmashauri ya mji wa Kahama hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia saba na kumi na saba (717,276,055/=) ikiwa ni sehemu ya malipo ya kodi ya huduma(service levy) ambayo hulipwa kwa halmashauri hiyo.
 
Akizungumzia malipo hayo ya hundi Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo amesema kiasi hicho ni malipo ya kuanzia mwezi januari hadi juni mwaka huu.
Mwaipopo ameongeza kuwa licha ya Kampuni yake kulipa kodi mbalimbali na kujishughulisha katika kufadhili miradi ya Maendeleo, amesema ipo haja ya Jamii kuilinda na kuitunza miradi hiyo ili iwe na manufaa kwa Jamii nzima.
“Acacia kupitia Mgodi wetu wa Buzwagi tunajivunia kuwa wadau muhimu wa maendeleo wa halmashauli ya mji wa Kahama na serikali kwa ujumla, na tunafarijika sana kwa ushirikiano ambao tumekuwa tukiupata, ombi letu kwa Jamii zinazonufaika na miradi yetu kuilinda na kuitunza kwa manufaa ya Jamii nzima.”
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Fadhili Nkurlu aliyepokea hundi ya kodi ya huduma kutoka kwa uongozi wa Mgodi wa Buzwagi na baadae kuikabidhi kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika kutekeleza miradi ya Maendeleo”
Akizungumza kwa niaba ya halmashauri ya mji wa Kahama Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Abel Shija ameupongeza uongozi wa Mgodi na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuiletea Jamii Maendeleo.

Wednesday, August 10, 2016

VIJANA WAENDESHA MDAHALO KUJADILI CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOWAKABILI KUELEKEA SIKU YA KIJANA DUNIANI, KARIMJEE JIJINI DAR

Mwakilishi Mkazi msaidizi kutoka UNFPA Bi. Christine Mwanukuzi akifungua mdahalo huo, kuwashukuru vijana kwa kujumuika pamoja na kuwapongeza kwa kufanikisha mdahalo huo kuelekea katika siku ya vijana duniani siku ya tarehe 12.08.2016
Bw. Badru Juma Rajabu akielezea historia ya siku ya vijana ilipoanzia na kusisitiza kuwa vijana wanatakiwa kutambulika na wasisahau kuchukua fursa pale wanapowezeshwa

Oscar Kimario muwezeshaji kutoka Restless Development akielezea baadhi ya ripoti juu ya vijana na kuwasihi vijana kuwa ndio watakuwa mstari wa mbele katika maendeleo endelevu hivyo wanapaswa kujituma na kufanya kazi kwa bidii

Vijana wakiendelea kufuatilia mdahalo huo kwa makini
Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa ILO Nancy Lazaro akizungumzia ajira zenye staha ,alisema kuwa vijana wengi wameajiriwa lakini katika ajira zisizo na staha na kusisitiza ifike kipindi sasa vijana waajiliwe na kazi zenye Staha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Msichana Initiatives Rebeca Gyumi akijibu maswali mbalimbali ambayo waliuliza vijana waliofika katika kongamano hilo na kusema kwamba sio kweli kwamba wanafunzi waliomaliza elimu ya vyuo ni vilaza
Vijana wakiendelea kufuatilia wajibu maswali wakijibu yale waliyo yauliza

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St.Josephs Veronica Shayo kidato cha tano akisisitiza vijana kuwa na tabia za kuweka akiba kwa kile wanachopata ili kije kuwasaidia pindi watakapo kuwa wakubwa.
Muwezeshaji wakati wa kongamano hilo la vijana ambalo kauli mbiu yake inasema Sepesha Umasikini kwa Michongo Endelevu na yenye tija Bw. Lawrence Ambokile akiendelea kutoa mwongozo 
Noreen Toroka akijibu baadhi ya maswali lakini pamoja na hayo amewasisitiza vijana kuto kutumia kipato wanacho kipata bila tija na wawe na utaratibu wa kuhifadhi kwa ajili ya maendeleo baadae, pia aliongeza kuwa vijana wasilazie damu fursa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili yao

Baadhi ya vijana kutoka Restless Development na wanafunzi pamoja na wadau wakendelea kufuatilia mdahalo

Mwanzilishi wa Malkia Investment Bi. Jenipher Shigoli akichangia  jambo katika mdahalo huo

Albert Kutoka ILO akichangia na kujibu maswali ya vijana mbalimbali katika mdahalo huo ambapo alisisitiza vijana kujituma
 Mwanzilishi wa Charity Movement Sophia Mbeyela akitoa ushuhuda wake wa jinsi alivyo anza ujasiliamali tangia akiwa mdogo na kusisitiza kwamba vijana haijalishi ni mzima au ana ulemavu wa viungo vya mwili wake wote wanatakiwa kujumuika pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo ya Taifa

Kijana Onesmo akiwaeleza vijana wenzake kuwa kama wao walemavu wavioungo wanaweza kufanya mambo makubwa iwaje vijana wazima wasiweze hii ilikuwa ni changamoto

Picha ya pamoja ya Baadhi ya Washiriki wa Mdahalo huo

Picha na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa



YONO YASHINDA TUZO YA KIMATAIFA YA UBORA WA KAZI

Mwenyekiti wa  Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart, Yono Kevela, akionesha tuzo za kimataifa ya ufanisi bora wa kazi baada ya kukabidhiwa.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Udalali ya Yono Auction Mart, imekabidhiwa tuzo ya Mshindi wa Kimataifa ya Ufanisi na Ubora wa Kazi, baada ya kushindanishwa na kampuni nyingine 49 za nchi tofauti duniani hatua iliyotokana na utendaji wake katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza Jijini Dar es salaam jana, Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Yono Kevela, alisema ushindi huo unatokana na ufanisi wao wa kazi zikiwepo za ukusanyaji madeni ya kodi kutoka kwa wadaiwa sugu wa serikali .

Kevela alisema baadhi ya kazi walizofanya baada ya kupata zabuni ya kukusanya madeni ya wadaiwa ni za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wizara mbalimbali, taasisi za fedha na wakala wa serikali pamoja na wadau wengine.

Alisema ushindi wa tuzo hiyo ni faida ya ufanisi wa kazi zao katika kukusanya kodi za serikali huku akiahidi kutobweteka katika jukumu hilo alilopewa na Serikali hadi kushinda tuzo hiyo na badala yake atazidi kuongeza juhudi ili kampuni hiyo izidi kufanya vizuri.

“Tunashukuru kazi na huduma zetu kutambuliwa kimataifa, tumekuwa mabalozi wazuri wa Tanzania, tumetumia fursa hiyo kuitangaza nchi na kuwahimiza wawekezaji kuja kuwekeza “, alisema. Kevela

Alisema Tuzo hiyo ilitolewa Ufaransa na sherehe za kukabidhi washindi tuzo hizo zilifanywa Juni 25, mwaka huu Rome Italia ambako kampuni hiyo imeshinda ikitoka sekta binafsi, huku upande wa serikali ukishinda sekta ya Utalii kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Kampuni hiyo ya Yono imejizolea umaharufu hivi karibuni bada ya kupewa kazi ya kukusanya madeni ya wadaiwa 24 wa TRA, yenye thamani ya Sh bilioni 18.95 baada ya wadeni hao kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam mwishoni mwa mwaka jana.

Hata hivyo baada ya kampuni hiyo kuanza kazi, baadhi ya wadaiwa walifanikiwa kulipa madeni yao huku wengine wakilipa kiasi na wengine mali zao walikubali zikamatwe na kuuzwa ili kulipa madeni hayo, ambapo hadi sasa zaidi ya Sh bilioni saba zimeshakusanywa.

Maeneo mengine ambayo kampuni hiyo inafanya kazi ya kukusanya madeni dhidi ya wadaiwa mbalimbali ni pamoja na maeneo ya ardhi, mahakama, mabenki na taasisi zingine.