Pages

KAPIPI TV

Tuesday, June 30, 2015

MKUU WA MAJESHI MSTAAFU JENERARI SARAKIKYA APEWA TUZO YA HESHIMA NA TANAPA KWA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO MARA 38

????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu aki mkabidhi tuzo maalum ya heshima Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerari Sarakikya akiwa na mkewe kwa kupanda mlima Kilimanjaro mara 38, Jenerari Sarakikya pia amepewa Kadi maalum ya kuingia mbuga zozote za TANAPA Bure yeye pamoja na familia yake lakini ambapo katika hatua nyingine atalipiwa gharama zote za kushiriki mkutano wa masuala ya utalii kuhusu milima mirefu zaidi duniani yeye pamoja na mke wake huko nchini Marekani, Katika mkutano huo Jenerari Sarakikya anatarajiwa kutoa mada kuhusu mlima Kilimanjaro.
Jenerari Mrisho Sarakikya amekabidhiwa tuzo hiyo katika hafla ya utoaji wa tuzo za TANAPA za waandishi wa habari za utalii iliyofanyika kwenye hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo ambapo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wamepewa tuzo hizo.
Katika picha kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi za mbuga za Taifa TANAPA.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MWANZA)
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo za TANAPA za waandishi wa habari kwenye hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu katikati, Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi wa TANAPA na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Mwanza kwenye hoteli ya Gold Crest.
????????????????????????????????????
Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi wa TANAPA akizungumza katika hafla hiyo.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu wa pili kutoka kulia akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru wa tatu kutoka kulia, Kutoka kushoto ni Devotha Mdachi Kaimu Mkurugenzi wa (TTB), Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Ndugu Baraka Konisaga na Kushoto ni Mkurugenzi wa TANAPA Dr. Allan Kijazi.
????????????????????????????????????
Theophil Makunga Mhariri Tendaji wa Jambo Leo akisoma jina la mmoja wa washindi katika hafla hiyo, Kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga na Mkurugenzi wa TTB Bi. Devotha Mdachi.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Humphrey Mganga mwandishi bora wa habari za utalii katika magazeti katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Fredy Sikagonamo mwandishi bora wa habari za utalii vipindi vya redio katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Magessa Maggesa mwandishi bora wa habari za utalii kwa vipindi vya Televisheni kutoka Stars TV katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Jimmy Mengere kutoka Chanel Ten Morogoro mwandishi bora wa habari za utalii kwa habari za Utalii aliyeandika kuhusu wanyama wanavyouwawa kwa ajali katika mbuga ya Mikumi.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Kasilda Mrimila Mwandishi bora wa habari za utalii za Televisheni kutoka Star TV Morogoro kwa kuandika kukauka kwa mto Ruaha Mkuu , kulia ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Jackson Kalindimya Mwandishi bora wa habari za Utalii Magazeti katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru na kushoto ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akikabidhi tuzo kwa Frank Leonard
????????????????????????????????????
Baadhi ya wakuu wa vitengo wa mamlaka ya hifadhi za taifa TANAPA wakiwa katika hafla hiyo kulia ni Mkuu wa Mawasiliano Pascal Shelutete na na wa pili ni Ibrahim Mussa Mkurugenzi wa Masoko na Utalii TANAPA.
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu katikati akiwa na viongozi wengine katika hafla hiyo kulia ni Dr. Allan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA , kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga na katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru.
????????????????????????????????????
Meneja wa Mawasiliano TANAPA Bw. Pascal Shelutete akitoa utaratibu wa utoaji wa tuzo hizo.
????????????????????????????????????
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru akitambulishwa katika hafla hiyo.
????????????????????????????????????
Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerari Mrisho Sarakikya na mkewe wakitambulishwa katika hafla hiyo.
????????????????????????????????????
Mwimbaji Mariam akitumbuiza katika hafla hiyo
????????????????????????????????????
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga akizungumza katika hafla hiyo
????????????????????????????????????
Jaji mkuu wa tuzo hizo Dkt. Ayoub Rioba akitambulisha majaji wenzake waliofanya kazi ya kutafuta washindi wa tuzo hizo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Wanenguaji wa bendi ya Utalii wakitumbuiza katika hafla hiyo
????????????????????????????????????
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akipiga picha ya pmaoja na washindi.

KONGAMANO LA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WANAWAKE TANZANIA (TANZANIA BUSINESS ENTREPRENEURS) LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Tanzania Business Entrepreneurs for Women,  Haika Lawere akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Mbezi Guarden Dar es Salaam.
 
 Wadau wa kongamano hilo wakiwa wamejipanga kisawasawa. Kutoka Kulia ni Getrude Kilyabusebu, Haika Lawere, Hilda Mgaja na  Julieth Mjale.
 Mwezeshaji wa Kongamano hilo, James Mwang'amba 
akitoa mada.
 Muwezeshaji wa kongamano hilo, Chriss Rupia (kulia), akitoa maelezo juu ya namna ya kuanzisha Kampuni na hatua mbalimbali ambazo mtu anatakiwa azifuata wakati wa kufungua kampuni hasa binafsi.
 Mwenyekiti wa Tanzania Business Entrepreneurs for Women Haika Lawere (wa kwanza kulia) pamoja na wadau wengine wakiangalia bidhaa mbalimbali wakati wa kongamano hilo. 
 Mmoja wa majaji akiangalia bidhaa mbalimbali zilizopangwa kwenye meza zilizotokana na ubunifu wa wanawake waliohudhuria kongamano hilo.
Kongamano likiendelea
Baadhi ya wajasiriamali na wadau mbalimbali wakiwa katika Kongamano hilo.
Mmoja wa waratibu wa kongamano hilo Getrude Kilyabusebu (Kulia) akiweka sawa  kumbukumbu ya wadau waliofika katika kongamano hilo.
Bidhaa mbalimbali zikioneshwa.
Maonyesho ya bidhaa mbalimbali yakiendelea.

Baadhi ya wajasiriamali wakionesha kazi zao.
  Wadau mbalimbali wakitizama bidhaa mbalimbali katika Kongamano hilo.

Na Dotto Mwaibale

WAJASIRIAMALI wanawake nchini wametakiwa kuwa na moyo wa uthubutu ili kupiga hatua ya maisha na kiuchumi badala ya kuwa waoga.

Mwito huo umetolewa na Mratibu wa Kongamano la Jumuia ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, Julieti Mjale wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Mbezi Garden Dar es Salaam jana.

"Uthubutu katika jambo lolote ni muhimu kwani unamfanya muhusika kupiga hatua ya maendeleo" alisema Mjale

Alisema wajasiriamali waliowengi wamekuwa na mipango mizuri ya kubuni biashara fulani lakini wanakuwa na hofu ya kupoteza fedha zao na hiyo inatokana na kushindwa kuthubutu au kuchukua maamuzi magumu ya kuanza kufanya biashara waliyoikusudia.

Akijitolea mfano yeye alisema alithubutu kwa kuanza kufanya biashara za chini lakini leo hii ana nyumba za kupangisha na kufikia hatua ya kufanya biashara za kwenda nje ya nchi na kuandaa makongamana ya namna hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya biashara.

Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Haika Lawere alisema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wajasiriamali wanawake ili kupeana uzoefu wa biashara na kujua changamoto walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kupanua wigo wa shughuli zao na kutafuta masoko mapya ya bidhaa zao.

Katibu wa Jumuia hiyo, Hilda Ngaja, alisema changamoto kubwa waliyonayo wajasiriamali wanawake ni kutokuwa na uelewa mkubwa wa kufanyabiashara zao na kujikuta wakirudi nyuma kimaendeleo na ndio maana wamekuwa wakitumia fursa za semina na makongamano kwa ajili ya kuelimishana.
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba-0712-727062)



MWILI WA MKE WA MWANAHABARI THOBIAS MWANAKATWE WA KAMPUNI YA THE GUARDIAN ALIYEFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI NJE YA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM KUZIKWA KARATU MKOANI ARUSHA

 Mhariri wa Gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu (kushoto), na waombolezaji wengine wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mke wa mwanahabari wa Kampuni ya The Guardian, Thobias Mwanakatwe, Levina Genda wakati wakilipekeka kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Karatu mkoani Arusha kwa mazishi yatakayofanyika kesho.
 Mwanahabari wa Kampuni ya The Guardin Ltd, Thobias Mwanakatwe akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa mke wake, Levina Genda wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika Hospatali ya Amana Dar es Salaam leo a. Mke wa Mwanakatwe alifariki kwa kugongwa na gari maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mwishoni mwa wiki.
 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada ya kumuaga Levina Genda, iliyofanyika Hospitali ya Amana Ilala Dar es Salaam leo asubuhi.
 Hapa ni huzuni umetawala.
 Wafanyakazi wenzake na Thobias Mwanakatwe wa Kampuni ya The Guardian wakiwa wamejiinamia kwa huzuni.
 Thobias Mwanakatwe (katikati), akiwa na wafanyakazi wenzake waliofika kumfariji.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Levina na waombolezaji wengine wakiwa kwenye ibada ya kumuaga mpendwa wao.
 Kiongozi wa dini kutoka kanisa la Katoliki akiongoza ibada ya kumuombea marehemu.
 Ibada ikiendelea.
 Mwakilishi wa wanahabari kutoka mkoani Mbeya ambako Mwanakatwe alikuwa akifanyakazi kabla ya kuhamia Dar es Salaam, Patrick Kosima akitoa akizungumza katika ibada hiyo kabla ya kutoa rambirambi ya sh.220,000.
 Mhariri wa Gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu (katikati), akizungumza katika ibada hiyo wakati akiwasilisha salamu za rambirambi za Kampuni ya The Guardian.
 Mdau Fabiola Bula wa Karatu, akitoa heshima za mwisho kwa marehemu. 
 Heshima za mwisho kwa marehemu zikiendelea.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya The Guardian wakitoa heshima za mwisho kwa wifi yao, Levina Genda. 'Hakika ni huzuni tupu'
Jeneza likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Karatu kwa mazishi.
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba -0712-727062)

Monday, June 29, 2015

TAASISI YA KIISLAM YADAIWA KUNYANYASA NA KUWAFANYIA UKATILI WATOTO MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Mmoja kati ya Wanafunzi wa Shule ya Arba Light akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu adha wanayofanyiwa na Uongozi wa Kutayba Saccos ikiwa ni pamoja na kufungiwa huduma za choo wakati wakiwa shuleni hapo jambo ambalo limetafsilika kuwa ni manyanyaso na ukatili wa hali ya juu.
Bi.Fatuma Kidori mkazi wa Kanyenye akizungumzia Ukatili huo wa kuzuia Watoto wasipate elimu katika Shule hiyo kwa zaidi ya siku tano baada ya kuwafungia Mageti kitendo kilichofanywa na Uongozi wa Kutayba Saccos taasisi inayomilikiwa na Baraza kuu la Jumuiya ya Taasisi za Kiislam nchini.
Mwalimu Dolla Fungameza mkuu wa Shule hiyo ya Arba Light akizungumza masikitiko yake kufuatia kitendo hicho cha kikatili dhidi ya watoto kilichofanywa na Uongozi wa Kutayba Saccos
Baadhi ya watoto Chekechea wanaosoma katika Shule ya Arba Light iliyopo kata ya Kanyenye Manispaa ya Tabora wakiwa wamekaa nje ya Shule yao baada ya mmoja kati ya viongozi wa Taasisi ya Kutayba Saccos kufunga mageti akizuia watoto hao wasipate haki yao ya msingi ya elimu kufuatia mgogoro uliopo baina ya Uongozi wa Kutayba Saccos na Wamiliki wa majengo ya shule hiyo.
Geti likiwa limefungwa na Uongozi wa Kutayba Saccos wakizuia Watoto na walimu wao wasiingie madarasani jambo ambalo ni kinyume na haki za binadamu.Hata hivyo mtandao huu ulitaka kuhoji hatua ya Uongozi wa Kutayba Saccos kuzuia watoto hao lakini viongozi hawakuwa tayari na hivyo waliamua kujifungia milango ofisini kwao.