Kampuni
ya Clouds Media International leo imetangaza kuwa imepewa leseni ya
kurusha matangazo katika nchi za umoja wa falme za kiarabu (UAE).
Akielezea
kuhusu leseni hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bwana Joseph
Kusaga, amesema sasa kituo cha Clouds TV kimataifa kitakuwa
kikishuhudiwa na watu wa mataifa mbalimbali.
Clouds
TV kimataifa ni mwendelezo wa televisheni maarufu sana kwa vijana
nchini Tanzania, hata hivyo sehemu kubwa ya maudhui yatakayokuwemo
kwenye Clouds TV kimataifa itakuwa na mpangilio mpana wa vipindi kwa
watazamaji vitakavyorushwa kwa lugha za Kiingereza na Kifaransa.
Akieleza
zaidi Kusaga amesema “Leo ni siku ya kihistoria na alama ya hatua moja
katika mpango wetu wa kina wa kupeleka maudhui ya Clouds TV kimataifa
kupitia matangazo kwa njia ya mitandao’’.
Clouds
TV kimataifa haitotoa tu burudani, lakini pia itakuwa kiunganishi kwa
waafrika waishio katika umoja wa nchi za falme za kiarabu pamoja na
kuwapa fursa za kutangaza bidhaa zao na kuimarisha uhusiano baina yao.
Vituo
vya televisheni katika Umoja wa falme za kiarabu vipo vingi na vyenye
ushindani mkubwa, lakini Clouds TV kimataifa imebahatika kupata nafasi
ya kurusha matangazo yatakayowafikia walengwa katika chaneli yenye uwezo
wa kuwahudumia zaidi ya watazamaji takribani milioni 3.5 kutoka katika
nchi za Afrika.
Kwa sasa hakuna kituo kinachotoa huduma hii na hivyo kuwa fursa muhimu kwa watazamaji.
Clouds
TV kimataifa itarusha vipindi vya burudani, tamthilia, maigizo,
ucheshi, na muziki, vyote vitakavyo kuwa vimeandaliwa kutoka nchi za
mashariki, magharibi na kusini mwa bara la afrika na itapatikana kwa
watazamaji walio katika Umoja wa falme za kiarabu kupitia huduma ya IPTV
inayotolewa na Etisalat na Du.
Clouds
TV kimataifa itarushwa kupitia mamlaka ya Abu Dhabi ijulikanayo kama
twofour54, ikiungana na vituo kama FOX na CNN. Clouds TV kimataifa
itaanza kurusha matangazo ya majaribio katika wiki chache zijazo kabla
ya tarehe 15 mwezi June mwaka huu.
No comments:
Post a Comment