Pages

KAPIPI TV

Saturday, September 1, 2012

WAZIRI MLENDA ACHAGULIWA KUWA NAIBU MEYA WA MANISPAA YA TABORA

 Kutoka kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Ghulam Dewij akimpongeza Naibu Meya Waziri Mlenda baada ya kuchaguliwa na baraza la Madiwani kushika wadhifa huo kwa muda wa mwaka mmoja.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Tabora Waziri Mlenda akizungumza katika kikao cha baraza la Madiwani muda mfupi mara baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo,Mlenda ambaye pia ni diwani wa kata ya Ipuli amechukuwa nafasi hiyo baada ya diwani Kulwa kumaliza muda wake.
 Mkuu wa Wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya na mbunge wa jimbo la Tabora mjini Ismail Aden Rage wakihesabu kura katika uchaguzi wa Naibu Meya wa Manispaa ya Tabora,pembeni ni Waziri Mlenda akishuhudia wakati viongozi hawa wakihesabu kura hizo ambapo Waziri Mlenda alipata jumla ya kura 32 za ndiyo kati ya kura 32 zilizopigwa.

No comments: