Pages

KAPIPI TV

Saturday, September 1, 2012

RAGE ATOA MSAADA VIFAA VYA MICHEZO ZAIDI YA SHILINGI MIL.KUMI NA MBILI

 Mkuu wa wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya akikabidhi msaada wa vifaa vya michezo jezi pamoja na mipira kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Ghulam Dewij baada ya mkuu huyo kukabidhiwa seti 25 za jezi thamani ya sh.mil.7,250,000 na mipira 50 thamani ya sh.1,500,000.kwa ajili ya maandalizi ya Ligi ya Rage Cup itakayozishirikisha timu za kata za manispaa ya Tabora.
Mstahiki Meya Ghulam Dewij akikabidhi mipira kwa madiwani wa kata mbalimbali kwa ajili ya maandalizi ya Rage Cup itakayoanza hivi karibuni.

Na Juma Kapipi,Tabora mjini.
 
Mbunge wa jimbo la Tabora mijini Ismail Rage ametoa msaada ya vifaa vya michezo kwa kata 25 za manispaa ya Tabora vyenye thamani ya shilingi mil.8,250,000 kwa ajili ya maandalizi ya Ligi ya Rage Cup itakayoanza kutimua vumbi hivi karibuni mjini Tabora.

Akizungumza wakati wa kutoa msaada wa vifaa hivyo ambavyo ni jezi seti 25 na mipira 50 Mbunge huyo Ismail Rage alisema huo ni mkakati alioupanga katika kusukuma mbele jitihada za kuinua soka kwa vijana wa manispaa ya Tabora.

Rage alisema katika mashindano hayo yatakayochezwa kwa mtindo wa Ligi ya mtoano kwa timu zote za kata hadi vijijini,mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shilingi mil.moja wakati mshindi wa pili atajipatia kiasi cha shilingi laki tano taslimu huku akiweka wazi kuwa huenda zawadi hizo zikaongezeka kulingana na baadhi ya wadau ambao wameahidi kumuunga mkono kuchangia katika mashindano hayo akimtaja makamu mwenyekiti wa timu ya Simba wekundu wa Msimbazi.

Aidha Rage katika kuhakikisha Ligi hiyo inaendeshwa bila kikwazo ameahidi kukipatia shilingi laki tano Chama cha Mpira wa miguu Manispaa ya Tabora Tufa,ili kiweze kuendesha mashindano hayo bila wasiwasi.    

No comments: