Pages

KAPIPI TV

Friday, September 7, 2012

UCHAGUZI WA CCM NAFASI YA UENYEKITI MKOA WA TABORA BADO NGOMA NZITO!!!

Na Hastin Liumba,Tabora

Chama cha mapinuduzi,(CCM),mkoa wa Tabora,kitaingia kwenye historia
ambayo inaweza ikajirudia ya mwaka 2007, ya uchaguzi wa nafasi
mwenyekiti wa chama hicho mkoa.

Hatua hiyo inakuja kufuatia mwenyekiti wa sasa anayemalizia muda wake
Hassan Wakasuvi kuchukua fomu huku hasimu wake wa kisiasa Juma Samweli
Nkumba,naye kavuta fomu kukabiliana naye.

Mahasimu hawa ndiyo waliopambana na kuchukuana vikali katika uchaguzi
wa mwaka 2007 ambapo,mshindi wa uchaguzi ule alikuwa ni mwwenyekiti wa
sasa Hassan Wakasuvi aliyepata kura 422,huku Juma Samweli Nkumba
akipata kura 400.

Idadi ya kura hizo ilivuta hisia za wanachama na wafuatiliaji wa
masuala ya kiasi kiasi cha wadadisi hao safari hii wakisema historia
inaweza kujirudia kwani Juma Samweli Nkumba,bado anaonekana kuwa na
nguvu.

Aidha kinyang`anyiro hicho pia wapo waliochukua fomu ambao kijana
machachari toka kata ya Goweko wilayani Uyui Haji Kiyanga Baggio,na
Mwamba Zuberi.

Wagombea hao wanne wanatarajiwa kuwa katika mvutano mkubwa kwani
safari hii fomu za uongozi zimechukuliwa na vijana wadogo.

Hatua ya mwenyekiti wa zamani wa chama hicho,mkoa ambaye alishindwa
katika uchaguzi uliofanyika ukumbi wa chuo cha utumishi kampasi ya
Tabora,imedaiwa ni maombi ya wafuasi wake ambao wanasema chama
kimepoteza mvuto chini ya mwenyekti wa sasa,Hassan Wakasuvi.

Mmoja wa wanachama ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini,alisema
watu wanaweza wakashangaa sana na matokeo ambayo yanaweza kumuweka
Juma Samweli Nkumba kukalia kiti hicho tena kabla ya kuanguka kwenye
uchaguzi wa mwaka 2007.

“Sikiliza ndugu yangu yule mzee bado ana nguvu na wafuasi wengi
wanachama na wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa wanaweza kupigwa na
butwaa endapo atashinda kwani chama mkoa wa Tabora sasa nidhamu
imeshuka.” Alisema.

Hata hivyo baadhi ya wanachama kadhaa walionesha kushangazwa na hatua
ya Juma Samweli Nkumba, ya kuchukua fomu baada ya mzee huyo katika
kauli zake za mara kwa mara kuwa hana nia ya kuomba tena uenyekiti wa
CCM mkoa wa Tabora.

Wakati uenyekiti CCM mkoa wa Tabora,hali ikiwa hivyo,CCM wilaya moja
ambayo inaonyesha kutakuwa na mvutano mkali,wilaya ya Uyui,ambayo
mchuano huo kwa waliochukua fomu ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo
la Igalula,Tatu Ntimizi,Musa Ntimizi.

Wengine waliovuta fomu ni Hamis Bundala ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Uyui,na Abdalah Kazwika.

Wilaya hii inatarajiwa kuwa ya vuta nikuvute kwani katika uchaguzi
huu,Hamis Bundala na mwenyekiti wa sasa anayemalizia muda wake Abdalah
Kaziwka wanaodaiwa kuwa uadui wa kiasiasa kwa muda sasa.

Mahasimu hawa waliaza uhasama katika uchaguzi wa nafasi ya mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Uyui,baada ya Hamis Bundala kuangushwa na
naibu wake ambaye kwa sasa ni marehemu Mashaka Kalyuba.

Kutokana na uchaguzi huo wa mwenyekiti wa halmashauri,Hamis Bundala
aliwahi tamka kuwa aliyemuhujumu hadi akaanguka ni mwenyekiti wa sasa
wa CCM wilaya ya Uyui,Abdalah Kazwika.

Toka hapo uadui wao kiasisa uliendelea na katika moja ya mikutano ya
chama hicho kupitia kamati ya madiwani wa CCM uliwahi kuzuka mvutano
wa kurushiana maneno kati ya wawili hao,huku Hamis Bundala akimwambia
kwa maneno ya ukali mwenyekiti wa CCM wa sasa Abdalah Kazwika kuwa
atachukua fomu kupambana naye.

Hatua hiyo ya Hamis Bundala inaonyesha ni ya kutaka kulipiza kisasi
cha kushindwa kwenye uchaguzi wa halmashauri kwa kile alichoamini
aliyemwangushwa ni Abdalah Kazwika.

Wakati hayo yakijiri kwenye nafasi ya mkoa na wilaya ya Uyui,wilaya
nyingine za Sikonge,Tabora mjini,Igunga,Urambo na Nzega bado hali ya
mivutano haijapamba moto licha ya wilaya za Nzega na Urambo kuwa na
misuguano ya chini kwa chini.

No comments: