Pages

KAPIPI TV

Friday, September 7, 2012

WAKUU WA MAJESHI YA POLISI WAKUBALIANA KUDHIBITI UHALIFU WA KIMATAIFA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini Inspekta Jenerali, Said Mwema, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa mkutano mjini Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Shiirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Bara la Afrika SARPCCO)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akijumuika kuimba wimbo wa Taifa na wakuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Generali, Said Mwema (wa pili kushoto) wakati alipofika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo Sept 05, 2012 kwa ajili ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini Inspekta Jenerali, Said Mwema, akizungumza mara baada ya kukabidhiwa uwenyekiti wa Shirikisho la SARPCCO.
  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Plisi hapa nchini Inspekta Jenarali, Saidi Mwema. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Afrika ya Kusini, Kamishna Jenerali Bi. Mangwashi Phiyega
Picha ya pamoja ya Wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi za SADC na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Mohammed Gharib Bilali.

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar

Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SARPCCO chini ya kivuli cha SADC, wamekubaliana kuimarisha nguvu za pamoja na kukabili uhalifu wa Kimataifa.

Wakuu hao wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi 12 kati ya 14 wanachama wa Shirikisho hilo, walifikia uwamuzi huo wakati wa mkutano wao wa siku tatu uliomalizika jana mjini Zanzibar.

Katika mkutano huo ambao ulitanguliwa na mikutano mingine ya kamati tendaji za Majeshi hayo walikubaliana pia kubadilishana taarifa za wahalifu na kuhakikisha kuwa Magenge ya watu wanaojihusisha na uhalifu wa kimataifa wanabainika na kutiwa nguvuni.

Miongoni mwa makosa yaliyojadiliwa kwa undani na kupatiwa ufumbuzi wa jinsi ya kuyakabili ni ugaidi, uharamia, usafirishaji na uuzaji wa dawa za kulevya pamoja na usafirishaji na biashara haramu wa binadamu.

Wakizungumzia biashara haramu ya dawa za kulevya, Wakuu hao wamesema biashara hiyo imekuwa ikileta madhara makubwa kwa vijana walio wengi na hivyo mbali ya kudhoofisha afya kwa watumiaji, lakini pia dawa hizo zimekuwa zikithoofisha huduma za kiuchumi kwa nchi masikini.

Wamesema kutokana na ukweli huo, kuna haja ya kila nchi kuhakikisha kuwa wanapata taarifa na kuwakamata wale wote wanaojihusisha na usafirishaji, usambazaji na uuzaji wa dawa hizo.

Wakizungumzia uharamia, Wakuu hao wamesema kuwa watahakikisha kuwa usalama unaimarisha katika huba za bahari ya hindi kama hatua ya kudhoofisha nguvu za wavamizi na watekaji wa meli za bizigo baharini.

Kuhusu uhalifu unaovuka mipaka, Wakuu hao wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za SADC wamekubaliana pia kufuatilia nyendo za watuhumiwa wakiwemo wale wanajihusisha na wizi na usafirishaji wa magari na mifugo ya wizi kutoka nchi moja kwenda nyingine kwa magendo.

Wakati wa Mkutano huo, Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, alichaghuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi zilizo Kusini mwa Bara la Afrika.

Nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Afrika ya Kusini Kamishna Jenerali Bi. Mangwashi Phiyega.

Awali akifungua mkutano huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilali, aliwataka Wakuu hao wa Majeshi ya Polisi kuhakikisha kuwa wanabuni mbinu za kisasa zitakazosaidia kukomesha uhalifu wa kimaifa ukiwemo ule wa biashara haramu ya dawa za kulevya.

No comments: