Pages

KAPIPI TV

Friday, September 7, 2012

MKURUGENZI HALMASHAURI YA WILAYA YA UYUI AKANUSHA

Na Hastin Liumba,Uyui

MKURUGENZI wa halmashauri ya wilaya ya Uyui,mkoani Tabora,Doroth
Rwiza,amekanusha madai ya kuwa ni fisadi,mbadhirifu,na mbabe kwa
watumishi,na kuwa madai hayo yamemdhalilisha,yeye,familia yake na
halmashauri kwa ujumla.

Rwiza alisema wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa
habari,ofisini kwake iliyopo makao makuu ya halmashauri hiyo,Isikizya.

Alisema tuhuma hizo zimetolewa na kwenye gazeti la Mtanzania la
jumanne,toleo namba 7066 la septemba 4,2012 kwa njia ya barua za
wasomaji yenye kichwa cha habari kisemacho,”Barua ya wazi kwa waziri
wa TAMISEMI”

Akizungumza maneno hayo,Rwiza alisema kuwa yeye anadaiwa kuwa anatumia
madaraka yake vibaya,kitu ambacho siyo kweli kwani katika kutekeleza
majukumu yake amekuwa akifuata taratibu,kanuni nasheria za utumishi wa
umma.

Rwiza alifafanua zaidi kuwa suala jingine amekuwa mkandamizaji kwa
baadhi ya watumishi wa halmashauri hiyo na kwamba suala hilo
lingekuwepo basi kungekuwa na malalamiko ya katika vikao vya baraza la
wafanyakazi ama chama cha wafanyakazi,na baraza la madiwani.

Kuhusu suala la yeye kutoa zabuni kwa upendeleo,nalo siyo kweli kwani
yeye haingii kwenye vikao vya zabuni na hajawahi kutengua maamuzi ya
bodi na wahusika hushindanishwa na kazi hiyo hufanywa kwa uwazi na
waombaji wote huridhika na maamuzi na hakuna malalamiko toka kwa
wazabuni.

Alisema kuhusu matumizi makubwa ya fedha yenye utata,nayo alikanusha
na kusema taarifa zote za ukaguzi hakuna sehemu inayoonyesha kuwepo
ubadhirifu,wizi,ama udanganyifu na badala yake halmashauri yake
imekuwa ikipata hati zinzoridhisha au safi.

Alisema taarifa zote za miradi ziko wazi ambapo madiwani kupitia
kamati zao hufanya ukaguzi kwa mujibu wa sheria na taratibu na hakuna
malalamiko yoyote ya miradi mibovu ama udanganyifu katika matumizi ya
fedha.

Kuhusu yeye kama mkurugenzi kuwapa fedha TAKUKURU,ili kudhoofisha
ukaguzi hazina ukweli wowote kwani hana uwezo ama ubavu kuwapa fedha
kukwamisha uchunguzi unaofanywa na vyombo vya serikali.

Alisema amekuwa akipandikiziwa chuki na majungu mengi na baadhi ya
wanasiasa wakishirikiana na watumishi kadhaa wa halmashauri yake ili
aonekane hafai mbele ya jamii.

Mkurugenzi huyo,alibainisha suala la ukandamizaji,vitisho na dhuluma
kuwa halipo na vyombo vya wafanyakazi vingekuwa na kesi nyingi za
namna hiyo na kila kitu kingekuwa wazi na badala yake sasa hakuna
mtumishi hata mmoja aliyejitokeza hadharani kuzungumzia vitendo hivyo
na kamayupo ajitokeze hadharani kuthibitisha.

Aliongeza kuwa anafahamu wapo wanasiasa na watumishi ambao bado
wanapinga suala la halmashauri kuhamia Isikizya na bado wamekuwa
wagumu kutekeleza agizo la serikali,huku akichukua hatua kwa watumishi
ambao wamekuwa wakikaidi utekelezaji huo.

Riwza alibainisha kuwa kuhusu malipo ya kiasi cha sh milioni 270
zinzodaiwa kutafunwa katika ujenzi wa daraja Mbangani,siyo kweli kwani
kuwa kuna vifusi viwili tu na kwamba nyaraka zote znzohusiana na mradi
huo zipo na kuna uwazi katika hilo kwa ukaguzi na hata PPRA na hivi
karibuni walizikagua.

Gazeti hili lilimtafuta mhandisi wa halmashauri hiyo,Injinia Lusekelo
Mwakyami apamoja na mweka hazina Angelo Mngongolo,kutoa ufafanuazi wa
sh milioni 270 zilizoandikwa kuwa zimetafunwa.

Injinia Mwakyami alisema madai hayo hayapo na kwamba mradi
unaozungumziwa ni unahusu barabar yenye urefu wa kilomita 6.0 kwa
kiwango cha changarawe na ujenzi wa daraja la moja la zege la
Mbanganilenye urefu wa mita 20.0.

Alibainisha kuwa mradi huo una gharama    ya sh milioni
269,996,000,ambazo ziko kwenye mkataba na hati mbili za malipo ambapo
hadi sasa malipo yaliyofanywa ni sh milioni 152,329,650 ambapo awamu
ya kwanza kiasi kilicholipwa ni sh 58,606,450 malipo ambayo
yalifanyika mwezi april 27,2012.

Aliongeza kuwa awamu ya malipo iliyofuata ilifanyika mwezi mei 15,2012
ya kiasi cha sh milioni 93,723,200 malipo ambayo yanahusu mradi huu
unaopigiwa kelele za ubadhirifu.

Aidha aliongeza kuwa haya yalihusu kazi za ukarabati wa barabara na
hakuna malipo mengine kwa sasa ambayo yamefanywa  kuhusiana na ujenzi
wa daraja la Mbangani na badala yake kazi ya ujenzi wa daraja hilo
unaendelea hadi sasa.

Naye mweka hazina wa halmashauri hiyo,Angelo Mngongolwa, alifafanua
kuwa katika fedha zinazodeaiwa kutafunwa siyo kweli kwani pamoja na
ufafanuazi huo kiasi cha sh milioni 117,66,360 bado kiko katika
akaunti benki na hakijatumika na matumizi yake yanasubiri utekelezaji
wa mradi huo.

Alisema katika ujenzi wa barabara ya Kigwa-Igalula kilomita 6.0
unaohusisha daraja la Mbangani lenye urefu wa mita 20.0 unapigiwa
kelele utekelezaji wake taarifa zake zimekuwa zikitolewa katika vikao
mbalimbali vya halmashauri na kamati ya fedha.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Said Ntahondi alisema taarifa
iliyotolewa  kwa njia ya barua za wasomaji katika gazeti la Mtanzania
la septemba 4,mwaka huu maneno hayo ni uzushi mtupu wenye lengo la
kuichafua halmashauri yake.

No comments: