Pages

KAPIPI TV

Friday, September 7, 2012

HUSSEIN BASHE - SALAAM ZANGU KWA WANA UVCCM HASA WAGOMBEA



Ndg zangu awali ya yote niwapongeze Nyote Mliojitokeza na kushiriki Chaguzi za Ngazi ya wilaya na Kuwapa Hongera Mliochaguliwa na Kuwataka ambao hamkupata nafasi msivunjike Moyo kuendelea kutimiza wajibu wenu kama wanachama.Pia mliochaguliwa niwaombe kufanya jitihada kufikia matarajio ya waliowachagua.

Pili Niwatakie kila la kheri waliojitokeza kugombea nafasi za Ngazi ya Mkoa na Taifa ambao wengine mtakua na Safari kuelekea Dodoma kwenye Usaili ninawaombea kila la kheri huko muendeko na kuwapa Moyo Siasa ndani ya CCM zinahitaji Uvumilivu wa hali ya juu niwatake na kuwaomba kuonyesha Uvumilivu katika kipindi hiki cha uchaguzi.


Ndg zangu jambo la msingi ninalowaomba huu ni mwaka wa uchaguzi niwatake mtumie mapungufu mlioyoyaona ktk kipindi chetu iwe fursa zenu kurekebisha na kujenga jumuiya Imara zaidi,Mtumie fursa hii ya uchaguzi kujenga msingi Imara wa Umoja na Msikamano jambo ambalo sisi kaka zenu hatukufanikiwa kulijenga.


Mtumie uchaguzi huu kurejesha Umoja Na Mshikamano Mtumie Fursa hii kuungana na si kugawanyika zaidi,Mtumie fursa hii kutowapa Nafasi Maadui wa UVCCM ambao kwao hufaidika na Mgawanyiko wa JUMUIYA yetu,mtumie uchaguzi huu kurejesha Historia na Msingi mkuu wa Uwepo wa Jumuiya hii kusimamia maslahi ya wengi na maslaha mapana ya Taifa hili.


Nitumie fursa hii kuwaomba msivunjike moyo kama hautachaguliwa ama hautateuliwa,Nimatamanio yangu kuona vijana wote wenye sifa za kikanuni kurudishwa majina yao na bila kuwakata ili kujenga taswira ya jumuiya kuwa ni sehem yenye kutoa fursa kwa vijana wote wa chama cha mapinduzi na siku ya mwisho wapiga kura wapate fursa ya kuwa na wigo mpana wa kuchagua kwa kuwa na wagombea wengi ili kujenga utamaduni kushindanisha uwezo na kutoruhusu wachache kuwaamulia wengi.


Mwisho niwatakie kila la kheri wagombea wote na mungu awasaidie kuwapa moyo wa uvumilivu na kuwatayari kitimiza wajibu wenu.


Najua mtauliza MABASTOLA NZG niweke rikodi sawa sawa sikutoa Bastola,Sijawahi kumiliki Bastola,Sikuanzisha Vurugu,Sikulala Mahabusu,Sikufikishwa Mahakamani,Sikushiriki kuvunja Taratibu zozote za Chama ,Sikuchelewa kurudisha Fomu nilirudisha ktk wakati Muafaka yaliyotokea ni matokea ya Kuficha Maradhi na Kukumbatia Maovu ndani ya Chama Chetu niwaombe mkipata nafasi msiwe sehemu ya kukumbatia maovu kwani huleta athari kama za nzg.


Wasallaam kila la kheri ndg zangu

No comments: