Pages

KAPIPI TV

Saturday, September 8, 2012

SERENGETI FIESTA YAFUNIKA TABORA,HAIJAWAHI KUTOKEA

Mmoja wa wasanii mahiri katika miondoko ya hip hop hapa nchini,Mwana FA akiwaimbisha wakazi wa mji wa Tabora wimbo wake wa Yalaiti,usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Ally Hassan Mwinyi,ambapo wakazi wa mji huo walijitokeza kwa wingi.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mabeste akikamua kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,ambapo katika tamasha hilo wakazi wa mji wa Tabora walijitokeza kwa wingi na kujishuhudia vipaji mbalimbali vya muziki.
 Wakazi wa Tabora walioamua kujiachia kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 wakishangwaka vilivyo usiku wa kuamkia leo,tamasha hilo limefanyika jana katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,aidha tamasha hilo siku ya jumapili litakuwa linarindima ndani ya Singida Motel,mkoani humo.
 Nikki Mbishi akishusha mistari yake mbele ya wakazi wa mji wa Tabora. 
Pichani kulia ni Shaffih Dauda Dauda akiwa na wadau mbalimbali
 Namna wakazi wa mji wa Tabora wakiwa ndani ya uwanja wa Ally Hassan Mwinyi wakati tamasha la Serengeti Fiesa lilipokuwa linaondoka.
 Dj Zero kutoka Clouds FM akikamua katika moja ya mashine za kisasa akikonga nyoyo za wakazi waliofulika ndani ya uwanja wa Ally Hassan Mwinyi,na kulia kwake ni Hamza Balla,
 Moja wa zao la Serengeti Fiesta 2012,Supa Nyota Ney Lee akitumbuiza jukwaani.
Msanii Recho akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani akisindikizwa madensa wake.
 Palikuwa hapatoshi ndani ya Tabora usiku wa kuamkia leo.
 Rich Mavoko akiliongoza skwadi lake kusakata kiduku
 Mbunge wa Tabora Mjini,Mh Ismail Adeni Rage akisoma moja ya namba ya aliyebahatika kuibuka na bajaji,kulia kwake ni Mkuu wa utafiti wa Clouds .TV,Ruge Mutahaba.
 NI full mzuka mwanzo mwisho kwa mashabiki wa Fiesta Tabora.
Sir Juma Nature akikamua usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012

Hamza Balla na marafiki zake wakiwa wamepozi ndani ya tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo.

No comments: