Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Omar Yussuf Mzee akizungumza na
Waandishi wa habari kuhusiana na saini iliotoliana Serekali ya Mapinduzi
Zanzibar na Serekali ya China hivi karibuni, mkutano huo umefanyika
katika Wizara ya Fedha Vuga.
Na Mohammed Mhina, Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeainisha mpango wa matumizi ya fedha shilingi Bilioni 14.8 zilizotolewa kama msaada na Serikali ya China kwa SMZ.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeainisha mpango wa matumizi ya fedha shilingi Bilioni 14.8 zilizotolewa kama msaada na Serikali ya China kwa SMZ.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari ofisini kwake leo mjini Zanzibar, Waziri wa
Fedha wa SMZ Mh. Omar Yusuf Mzee, amesema kuwa kipaumbele cha kwanza
katika fedha hizo itakuwa ni kuboresha huduma za Afya, Elimu na
miundombinu ya maji pamoja na uwekaji wa taa za sola kwenye baadhi ya
barabara za mji wa Zanzibar.
Akizungumzia
huduma za Afya, Waziori huyo wa fedha amesema kuwa sehemu ya fedha hizo
zitasaidia upanuzi na ujenzi wa Hospitali ya Mkoani Kisiwani Pemba na
kuifanya kuwa ya rufaa.
Waziri
Mzee amesema taratibu zote za ujenzi wa Hospitali hiyo imekamilika na
kwamba mara ujenzi huo utakapokamilika hakutakuwa na haja tena ya
wagonjwa mahututi kul;etwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi mmoja kwa vile
Hospitali hiyo itakuwa na kila aina ya vifaa na madawa ya tiba.
Amesema
fedha hizo pia zitasaidia kuwasomesha wataalamu wa afya, Walimu wa
masomo ya sayansi na kuboresha shule ya msingi ya Mwanakwerekwe kwa
kuongeza ujenzi wa vyumba 12 vya madarasa.
Mh.
Mzee amesema kuwa sambamba na hayo, fedha hizo pia zitasaidia kuweka
taa za sola katika kwenye baadhi ya barabara za mji wa Zanzibar na
kuboresha miundombinu ya maji mijini na Vijijini.
Amesema
visima virefu na vifupi vitachimbwa ili kuongeza rasilimali ya maji
katika maeneo mbalimbali ya visiwa vya Unguja na Pemba na kupunguza adha
ya upatikanaji wa maji mijini na Vijijini.
Amesema
fedha hizo zitasaidia kusomesha wataalamu wakiwemo Madaktari na
Wataalam wa fani mbalimbali wakiwemo wa masuala ya kilimo na ufugaji.
Katika
hatua nyingine Waziri Mzee pia amezungumzia suala la ununuzi wa Meli ya
Serikali itakayokidhi huduma za usafirishaji wa abiiria na mizigo kati
ya Kisiwa cha Unguja na Pemba.
Amesema Wizara yake inaendelea na mchakato wa ukusanyaji wa fedha shilingi Bilioni 17.6 kutoka katika vifungu 19 vya
bajeti ya ndani kupitia kwenye wizara mbalimbali ili kununulia Meli ya
Serikali itakayokidhi mahitaji ya usafiri wa abiria na mizigo kati ya
Zanzibar na Pemba.
Amesema
meli hiyo ambayo itagharimu zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 12,
itatengenezwa kwa muda wa miezi 18 na itasimamiwa na Kampuni ya Rowdies
ya nchini Uingereza.
Amesema
kuwa kinachofanyika sasa ni kuboresha michoro ya muundo wa meli hiyo
ili ikidhi vigezo na viwango vya usafiri katika ukanda huu wa Visiwa vya
Unguja na Pemba.
Waziri
Mzee amesema wakati Serikali ikiendelea na mchakato huo, kuna juhudi
zingine zinazochukuliwa na baadhi ya Makampuni ya usafiirishaji majini
ikiwemo ya Azam Marine za kutaka kuingiza nchini meli nyingine kubwa ili
kusaidia kupunguza adha ya usafiri wa abiria na mizigo kati ya Kisiwa
cha Unguja na Pemba.
No comments:
Post a Comment