Pages

KAPIPI TV

Friday, August 10, 2012

RAIA WANNE WA KONGO WALIONUSURIKA KATIKA AJALI YA BASI LA SABENA WAKOSA HATI HALALI ZA KUSAFIRIA.

 Vijana wanne raia wa Kongo ambao walinusurika katika ajali ya basi la Sabena iliyotokea katika eneo la Kitunda wilayani Sikonge mkoani Tabora,kutoka kushoto ni Shukuru Samwel(20)au Lyongola,Amani Yoshuwa(21),Jumaine Hamsini(18)  na Malega Juma(19) ambapo mwanmke mmoja  Asia Ngamia ambaye walidai kuwa ndiye aliyekuwa akiwasafirisha kutoka Burundi kwenda Malawi alifariki dunia katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu 17 na majeruhi 78.
 Vijana hao raia wa Kongo baada ya kubainika kuwa walikuwa wakisafirishwa isivyohalali walilazimika kurudishwa mjini Tabora umbali wa kilomita zaidi ya 350 kutoka eneo ilikotokea ajali kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Hii ni hati ya kusafiria ambayo alikuwa akiitumia mwanamke huyo ambaye kwasasa ni marehemu Asia Ngamia ambaye ni raia wa Kongo.

No comments: