Pages

KAPIPI TV

Thursday, August 2, 2012

POLISI TABORA YAFUNGUA MASHINDANO YA KOMBE LA POLISI JAMII

 Afisa mnadhimu Jeshi la Polisi mkoani Tabora John Kauga akisalimiana na wachezaji wa Timu za kata ya Ng'ambo na Gongoni wakati wa mashindano ya Kombe la Polisi Jamii ambayo yamefunguliwa jioni hii katika Uwanja wa kumbukumbu ya Vita mjini Tabora ambapo timu kumi na mbili zinashiriki mashindano hayo.
 Wachezaji wa timu za kata ya Gongoni na Ng'ambo katika mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo ya Kombe la Polisi Jamii.
Afisa mnadhimu Jeshi la Polisi Tabora John Kauga akitoa nasaha kwa wachezaji katika ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Polisi Jamii.
 Muamuzi Maulid Mwikalo akiwatambulisha wasaidizi wake kwa Afisa mnadhimu John Kauga wakati akikagua timu zilizoshiriki katika ufunguzi wa mashindano ya Kombe la Polisi Jamii.

Na Juma Kapipi-Tabora
Katika kufikia lengo la kutaka kupunguza au kuondosha kabisa vitendo vya uharifu mkoani Tabora,Jeshi la Polisi mkoani humo limeanzisha mashindano ya Kombe la Polisi Jamii ambayo yameshirikisha timu 12 za kata mbalimbali.

Akifungua mashindano hayo katika uwanja wa kumbukumbu ya Vita mjini humo, Afisa mnadhimu wa Jeshi la Polisi mkoani Tabora John Kauga amesema lengo la michuano hiyo ni kujenga mahusiano mazuri baina ya Polisi na raia hatua ambayo itasaidia katika kupambana na vitendo vya kiharifu.

Aidha amesema msimamo wa Jeshi la Polisi ni kushirikiana na raia katika ulinzi shirikishi Jamii ili kuhakikisha matokeo mazuri katika kupambana na vitendo vya uharifu ambapo pia dhana ya Utii bila Shuruti inapata mafanikio makubwa kwa Jamii. 

Katika michuano hiyo ya Kombe la Polisi Jamii imezikutanisha zaidi ya timu 12 za kata mbalimbali za Manispaa ya Tabora.

 

No comments: