Pages

KAPIPI TV

Thursday, August 30, 2012

MWANAFUNZI APOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA NZEGA


Na Hastin Liumba,Nzega 
Jackson Josephat kulia,akiwa na baba yake Josphat Mwita,na
baadhi ya dada zake na mdogo wake

MWANAFUNZI wa darasa kwanza,shule ya msingi Kitongo wilayani Nzega,mkoani
Tabora,Jackson Josephat,(11),amepotea katika mazingira ya kutatanisha.

Akizungumza na KAPIPIJhabari.COM wilayani Nzega,baba mzazi wa mtoto
huyo,Josephat Mwita,(37),alisema mwanaye alipotea katika mazingira ya
utata mnamo mwezi machi 18,mwaka huu.

Mwita alisema mtoto wake alipotea akiwa matembezini nyumbani kwa baba
yake mdogo Amos Mwita, mtaa wa Samora wilayani hapa,majira ya saa nane
mchana.

Mwita alisema alijaribu kmtafuta bila ya mafanikio na alitoa taarifa
kituo cha polisi wilaya ya Nzega,lakini kwa bahati mabya RB namba ya
tukio hilo amepoteza.

Aidha amesema licha ya kutoa taarifa kituo cha polisi Nzega,pia ametoa
taarifa stendi ya mabasi,kanisa katoliki Nzega na kituo cha radia
Victoria mkoani Mara.

Alisema baada ya kupotea amekuwa akisikia kwa watu kuwa mtoto wake
amekuwa akionekana katika baadhi ya mitaa wilayani hapa lakini kila
afanyapo juhudi za kumtafuta imekuwa ni vigumu.

"Nasikia uchungu sana kupotelewa na mtoto wangu tena alikuwa ameanza
darasa la kwanza mwaka huu......wasamaria wema kama watafanikiwa
kumuona wanisaidie ili aweze kuendelea na masomo yake." alisema.

Alisema na imani mtoto wake atakuwa katika mazingira ya wilayani
Nzega,lakini cha kushangaza hata mtu anayekaa naye anashindwa kuelewa
ni vipi akaye na mtoto ambaye siyo wake.

Anabainisha kuwa licha kutoamini imani za kishirikina,bado ataendelea
kumuomba mwenyezi Mungu ili mtoto wake aweze kupatikaa na aendelee na
masomo yake.

Mwita alitoa wito kwa jamii itayomuona atoe taarifa kituo cha polisi
ama apige simu namba 0787-052690,0754-838465,au 0686-570850. au kituo
cha taxi stendi ya mabsi Nzega,eneo ambalo baba yake nafanya kazi zake
kama dereva taxi.



.

No comments: