Pages

KAPIPI TV

Saturday, August 25, 2012

HALMASHAURI YA MANISPAA YA TABORA INAKOELEKEA SASA

Na Hastin Liumba,Tabora

KUWEPO makundi mawili yanayosigana katika baraza la madiwani wa
halmashauri ya manispaa Tabora,kunasababisha wakuu wa idara kushindwa
kuwajibika,na kuwepo kwa taarifa potofu za miradi ya
maendeleo.Imegundulika.

Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu kwa siku kadhaa,baada ya kuibuka
upya kwa makundi mawili ndani ya baraza la madiwani kulikosababisha baadhi yao eti kutaka mstahiki meya wa manispaa hiyo,Bw. Ghulam Dewji Remtulah kuachia ngazi pasipo kuweka bayana msingi wa kumtaka kufanya hivyo.

Aidha uchunguzi huo umebaini kuwa hata kelele za madiwani hao,kuwa

kuna miradi ambayo hairidhishi  kunatokana na makundi hayo mawili
kukomoana  na kuifanya manispaa hiyo kuonekana kana kwamba imekumbwa na mgawanyiko.

Uchunguzi unaonyesha kuwa miradi ya maendeleo hukaguliwa na kamati ya

fedha na uongozi sanjari na mhandisi wa majengo wa manispaa na mkuu wa
wilaya,huku kamati hiyo  ikiongozwa na mstahiki meya wa manispaa ya
Tabora Ghullam Dewji.

Aidha kutokana na miradi mingi ya maendeleo kupigiwa kelele na

madiwani hao kumetokana na kutokupatikana kwa taarifa za miradi hiyo kwa wakati na
taarifa zilizokamilika.

"Makundi haya mawili ya madiwani waliogawanyika yanatokana na kamati
hiyo kushindwa kuweka bayana jinsi miradi hiyo ya maendeleo inavyotekelezwa." alisema mmoja wa madiwani ambaye hakutaka kuweka bayana yupo kundi lipi.

Alisema anashangazwa sana na taarifa za miradi zilizopo kwani miradi
hiyo inayolalamikiwa ilikaguliwa na kamati ya madiwani hao,kamati inayoitwa ni kamati fedha na uongozi ikiongozwa na mstahiki meya.

Aidha aliongeza kuwa miradi hiyo huenda imekuwa haina taarifa za
kutosha kuweza kuwatosheleza madiwani hao kuamini kile ambacho wamekuwa wakipewa katika taarifa kimaandishi.

Mtumishi mmoja wa manispaa ya Tabora aliuambia mtandao huu kuwa

mpasuko uiliopo kiasi cha madiwani hao kumuomba mkuu wa mkoa wa Tabora
Fama Mwassa, kuunda tume huru kuchunguza utendaji kazi na kuwepo
ubadhirifu ni madiwani hao kushindwa kuelewana katika makundi mawili tofauti.

Aliongeza kuwa kinachoondelea hapa ni kuundwa tume huru itakayomaliza
ubishi japo kasoro haziwezi kuepukika.
 

"Miradi wanakagua wenyewe kupitia kamati ya fedha na uongozi tena akiwemo mkuu wa wilaya....leo hii inaonekana kuna uchakachuaji na iundwe tume huru, hao waliokuwa kwenye ukaguzi walienda kufanya nini katika ziara hiyo." alisema mmoja wa watumishi wa manispaa hiyo.

Alisema kinachoonekana hapa ni kutaka manispaa hii ni kuwanufaisha
wachache ikiwemo wakuu wa idara kutolewa kafara hapa baadhi ya madiwani hasa waliowengi walitaka meya aondoke sasa tume huru inaundwa muda siyo mrefu itabainika na ukweli utawekwa hadharani.

Alisema kibaya zaidi kinatokana na kuwa na uwakilishi wa kisiasa zaidi kuliko uhai na usimamaizi mzuri ili manispaa Tabora isonge mbele.

Hivi karibuni chama cha mapinduzi kilifanya uchaguzi na kupitisha jina
la naibu meya ambaye ni diwani wa kata ya Ipuli,Waziri Mlenda
aliyepata kura 24 na mpinzani wake Juma Makala alipata kura 8 huku
kura zilizopigwa ni 32.

Hali hiyo inaonyesha Waziri mlenda anaungwa mkono na madiwani huku

baadhi ya madiwani wakisema mstahiki meya Remtulah, alikuwa akimuunga
mkono Juma Makala.

Mkurugenzi wa halmashauri ya mansipaa Tabora,Hadija Makuwani mara

kadhaa amekuwa akisisitiza hawezi kukubali manispaa hiyo igeuke uwanja
wa visasi na kwamba atajitahidi kurejesha mshikamano ili kazi na
miradi mbalimbali isewe na malalamiko.


No comments: