TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kutokana na ratiba ya uchaguzi mkuu ndani ya Chama cha Mapinduzi mkoani Tabora,tarehe 22/08/2012 wanachama wa CCM wataanza kuchukua fomu za kuomba kugombea Uongozi ngazi za Wilaya na Mkoa kwa kuzingatia ratiba hiyo.
Baadhi ya waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Tabora wapatao 22 ambao wanaongozwa na Mwenyekiti wao diwani wa kata ya Tambukareli Mh.Salumu Luzila wamewachangia fedha za kuchukulia fomu Viongozi wao wa wilaya na mkoa,kwa maana ya Mwenyekiti wa CCM mkoa Bw.Hassan Mohammed Wakasuvi na Mwenyekiti wa CCM wilaya Tabora mjini Bw.Moshi Omari Abdurhamani(maarufu Konkota).
Madiwani hao wamefanya hivyo kwa madhumuni ya kuwaunga mkono Wenyeviti hao ili waweze kuendelea tena kuongoza.Ili watekeleze na kuendeleza heshima iliyopo ya Chama chetu mkoani kwa ujumla.
Pia yale waliyoyaanzisha ili waweze kuyakamilisha.Zaidi ya hayo ni viongozi wenye kuleta umoja ndani ya CCM katika mkoa wetu wa Tabora.
Tunawatakia kila la heri katika mchakato ili waweze kuchaguliwa kwa kishindo.
Taarifa hii imetayarishwa na IDD KAPAMA Katibu wa siasa na uenezi CCM Mkoa wa Tabora.

No comments:
Post a Comment