Pages

KAPIPI TV

Saturday, June 2, 2012

UZINDUZI WA TAMASHA LA MTEMI MILAMBO MKOANI TABORA

 Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa akifyatua mshale ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Tamasha la Mtemi Milambo lililofanyika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Uyui mjini Tabora.
Mkurugenzi mtendaji wa Chief Promotion, Amon Mkonga akiwa katika vazi rasmi la kijadi lenye asili ya wenyeji wa mkoa wa Tabora kabila la Wanyamwezi wakati wa Uzinduzi wa Tamasha la Mtemi Milambo lililoandaliwa na Kampuni ya Chief Promotion.

 Kutoka kushoto ni Msanii maarufu wa vichekesho nchini, Bambo akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Fatma Mwassa wakati wa Uzinduzi huo.
 Msanii maarufu nchini wa fani ya kucheza na Nyoka,Aly Mango akicheza na Joka kubwa,pichani akionekana amemeza kicha cha Joka hilo. 
 Mmoja kati ya watumishi wa Serikali Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora (kulia) akiwa amebebeshwa nyoka katika Tamasha hilo.
 Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa akikagua maonesho ya bidhaa za asili ya Wenyeji wa Tabora kabila la Wanyamwezi .
 Baadhi vikundi vya Ngoma za jadi za mkoa wa Tabora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa.
 Mtoto Pamela Adam(10) ambaye anasoma darasa la nne Shule ya Msingi Mwenge akiwa amebebeshwa nyoka mkubwa aina ya Sawaka ikiwa ni sehemu ya shamlashamla za Uzinduzi huo. 
Bambo akiwaburudisha baadhi ya wakazi wa mjini Tabora waliohudhuria Uzinduzi wa Tamasha la Mtemi Milambo,Bambo aliamua kuweka kuvua koti la Suti yake na kuanza kusakata muziki katika viwanja wa Shule ya Sekondari ya Uyui mjini Tabora. 

No comments: