Pages

KAPIPI TV

Friday, June 8, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA MAJAJI WAWILI NA MAKAMISHNA JIJINI DAR-ES-SALAAM

Rais Dk. Jakaya Kikwete akimwapisha Mh. Semistocles Kaijage (kulia) kuwa jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kabla ya uteuzi huo Mh. Semistocles Kaijage alikuwa jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akifuarahia Jambo na kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Edward Rutakangwa (wa tatu kutoka kulia)  mara baada ya kumwapisha leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Jaji wa mahakama ya Rufani Mussa Kipenka na Jaji  Semistocles Kaijage (wa kwanza kushoto).
Mh. Rufani Mussa Kipenka akipongezwa na baadhi ya ndugu waliohudhuria hafla fupi ya kuapishwa kwake kuwa jaji wa mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Mhe. Edward Rutakangwa kuwa kamishna  wa Tume ya Utumishi wa Mahakama katika hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu jijini Dares salaam.
Jaji wa mahakama ya Rufaa Mh. Semistocles Kaijage akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amesema atahakikisha kuwaanatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria,kupunguza mlundikano wa kesi na kuhakikisha kuwa maamuzi yanatolewa kwa haki.
Jaji wamahakama ya Rufani Mh. Mussa Kipenka akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa na Rais  Dkt. Jakaya kikwete leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni jaji mkuu wa Tanzania Mohammed Chande Othman.

No comments: