Pages

KAPIPI TV

Friday, June 8, 2012

MWANAMKE AJERUHIWA KWA RISASI NA KUPORWA MIL.2.5"Wananchi Tabora mjini hasa wafanyabiashara wahofia usalama wa maisha na mali zao"

 Mwanamke anayefahamika kwa jina la Demita Marco(37)mkazi wa Aly Hassan Mwinyi akiwa amelazwa Hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete kufuatia kujeruhiwa na risasi wakati alipovamiwa na majambazi dukani kwake barabara ya Kitete manispaa ya Tabora.
 Demita akiwa amelala kitandani katika hospitali ya Kitete.
Majeraha katika mguu wa kulia wa Demita kufuatia tukio la kupigwa risasi na majambazi wakati walipomvaia dukani kwake.

Na mwandishi wetu Tabora.

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Demita Marco mkazi wa Aly Hassan Mwinyi amejeruhiwa vibaya kwa risasi katika mguu wake wa kulia kufuatia tukio la kuvamiwa na majambazi usiku akiwa dukani kwake eneo la barabara ya Kitete manispaa ya Tabora.

Akizungumza na mtandao huu wa kijamii Demita ambaye amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete alisema watu wawili kati ya watano walifika katika mlango wa duka lake na kumtaka atoke dukani huku wakimuonesha bastola kwa lengo la kutaka kumpora.

Demita ameeleza kuwa alipokaidi kutii amri hiyo ya majambazi hayo,yalimvuta na kumtoa nje kwa nguvu hatua ambayo iliambatana na kumfyatulia risasi iliyompata mguu wake wa kulia na kuanguka chini.

"Wakati nikiwa chini nimeanguka huku nikipiga kelele ya kuomba msaada majambazi hayo yaliingia dukani na kuchukua shilingi milioni mbili na nusu pamoja na vocha za shilingi laki moja"alisema Demita huku akidai kuwa wakati huo wote akipiga kelele majirani zake walishindwa kutokea kwakuwa majambazi hayo yaliendelea kufyatua risasi hewani wakati yalipomaliza kuchukua pesa hizo.

Hata hivyo hilo likiwa ni tukio la pili kubwa ndani ya siku tatu, juzi majambzi yalivamia duka lililoko Miti mitatu maeneo ya National Housing nakupora fedha, juzi hiyo hiyo yalivamia duka la M-Pesa lililopo barabara ya sikonge wakapora fedha na kumjeruhi mtoa huduma kwa risasi ambaye kwasasa amepelekwa Hospitali ya Nkinga kwa matibabu zaidi kwa upande mwingine majambazi hayo  pia walivamia duka jingine la M-pesa maeneo ya isevya.

No comments: