Pages

KAPIPI TV

Wednesday, May 30, 2012

WAZIRI ABOOD AMEKUTANA NA MAASKOFU LEO ZANZIBAR

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud Mohamed akifafanua jambo alipozungumza na Maaskofu mbalimbali kufuatia vurugu zilizotokea Zanzibar za kuchomwa Moto kwa Makanisa mbalimbali,huko katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
  Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Askofu Mkuu wa Anglican Tanzania Dk Valentine Mokiwa katika mazungumzo ya pamojakuhusu vurugu zilizojitokeza Zanzibar.
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud Mohamed wa kwanza kushoto akisalimiana na Askofu Mkuu wa Anglican Tanzania Dk Valentine Mokiwa baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao pamoja na Maaskofu mbalimbali,huko katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Askofu Mkuu  wa Anglican Tanzania Dk Valentine Mokiwa akifanya mahojiano na Mwandishi wa BBC kuhusiana na  matatizo yaliotokezea Zanzibar ya kuchomwa Moto kwa Makanisa mbalimbali,huko katika Ukumbi wa Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

No comments: