Mbunge Joshua Nasari na Kangi Lugora wakitoa shukurani zake kanisani.
Gladness Mushi wa Full shwangwe -Arusha
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw Joshua Nassari leo amefanikiwa
kutoa sadaka ya shukurani katika kanisa la FPCT Kilinga wilayani meru
mara baada ya kuchaguliwa kama mbunge wa jimbo hilo
Akiongea na Mamia ya wananchi wa jimbo hilo katika kanisa hilo Bw
Nassari alisema kuwa ameamua kutoa sadaka maalumu ya kushukuru mungu
mara baada ya kumaliza vema uchaguzi huku wapiga kura wake wote wakiwa
salama tofauti na pale ambapo wengi waliadhimia
hata ivyo aliwataka viongozi wa vyama vingine kuhakikisha kuwa
wanakuwa mstari wa mbele kutetea maslahui ny6a wananchi na kuachananna
tofauti za kivyama ambazo kama zitaendelezwa basi zitachangia kwa
kiwango kikubwa sana umaskini wa Meru
Akiongea katika kanisa hilo kwa ajili ya ibada hiyo mchungaji Langaeli Kahaya naye
alisema kuwa wananchi wanapswa kuhakikisha kuwa kamwe hawamchagui
kiongozi yoyote kwa ajili ya maslahi ya Rushwa kwa kuwa wote wanaotoa
rushwa ndio wanaosababisha hata umaskini na umwagaji damu ndani ya nchi
Kutokana na hali hiyo alisema kuwa ni mwiko kwa wananchi wma Jimbo la Arumeru Mashariki
kujihusisha na Rushwa kwa vipindi vyote vya uchaguzi kwa kuwa mpaka
sasa Rushwa imeshaacha madhara makubwa sana ndani ya jimbo hilo na pia
Rushwa ni dhambi kubwa sana.
No comments:
Post a Comment