Pages

KAPIPI TV

Saturday, May 19, 2012

WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI LOLANGULU WAUNGANISHWA NA WANAFUNZI WA NEW CANAAN MAREKANI

 Baadhi ya wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari ya Lolangulu muda mfupi mara baada ya kutoka kuzungumza na wenzao New Canaan Country School ya Marekani kupitia Program ya Connect to Learn.
 Mratibu na kiongozi wa mradi wa Milenia Mbola Dk.Gerson Nyadzi akizungumza na wanafunzi hao wakati wanafunzi hao wakifanya Program hiyo ya Connect to Learn inayoratibiwa na Mradi wa vijiji vya Milenia Mbola kwa ufadhili wa msanii maarufu ulimwenguni Lady Madonna.
 Mwalimu na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Lolangulu wakati wakijibu na kuulizana maswali na wanafunzi wa New Canaan Country School kupitia mtandao wa Skyper.
 Wanafunzi wa Lolangulu wakijaribu kuwasikiliza wenzao wa New Canaan Country School.
 Maafisa Mradi wa Vijiji vya Milenia Mbola (MVP)kutoka kushoto Happy ni mratibu wa Maendeleo ya jamii,katikati Dk.Gerson Nyadzi ni mratibu na kiongozi wa MVP na Kim ni mratibu wa kitengo cha Teknolojia na mawasiliano.
Mmoja kati ya walimu wa Shule ya Lolangulu akiwaonesha wanafunzi wa New Canaan kwa njia ya mtanadao.

Na Juma Kapipi-Mbola
Mratibu na kiongozi wa mradi wa vijiji vya Milenia Mbola(MVP) Dk.Gerson Nyadzi amesema kupitia Program ya Connect to Learn,mradi unakusudia kuendeleza programu hiyo kwa wanafunzi walioko eneo la mradi ambapo watakuwa wakifanya mahojiano kwa njia ya mtandao na wanafunzi wa shule za Sekondari zilizopo mjini Tabora kwa lengo la kuwapatia uzoefu kupitia Teknolojia hiyo. 

Dk.Nyadzi ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na mtandao huu muda mfupi mara baada ya wanafunzi hao wa shule za msingi na Sekondari Lolangulu kumaliza program ya Connect to Learn na wanafunzi wa New Canaan ya marekani ambapo wanafunzi hao waliunganishwa mazungumzo yao kupitia mtandao wa Skyper kwa zaidi saa mbili.

Amesema hatua ya kutaka wanafunzi hao wa Lolangulu kuunganishwa na wenzao wa Tabora mjini kupitia mitandao ya kuonana ana kwa ana itawajengea uzoefu wa kuwasiliana kwa mtandao wakati watakapo kuwa wakitaka kuwasiliana na wenzao wengine kutoka nchi nyingine duniani.

Pamoja na mafanikio makubwa yanayojionesha katika Progaram hiyo ya Connect to Learn,Dk.Nyadzi amesema bado kuna changamoto hasa kwa wanafunzi kutojua Lugha fasaha ya kiingereza kwa wanafunzi wa Lolangulu na kutojua kiswahili  kwa wanafunzi hao wa Marekani.

Aidha kupitia Program hiyo ya Connect to Laern wanafunzi wa Lolangulu walipata fursa ya kuulizana maswali na wanafunzi wa New Canaan hatua ambayo pia ililenga kwa wanafunzi hawa kufahamiana na kutambua viongozi wa nchi zao,rasilimali na mazingira wanayoishi.

Kwaupande wake mratibu wa maendeleo ya jamii Happiness Mgaya alisema ni mra ya tatu sasa kwa wanafunzi hwa kuunganishwa na wenzao wa marekani na huku akibainisha kuwa ni hatua muhimu itakayosaidia kuwajengea uwezo na kuwaondolea hofu ya kutumia dhana za teknolojia ya habari na mawasiliano wanafunzi  hao wa Lolangulu. 




No comments: